Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,644
- 860,861
Naomba tujadili kwa weledi ili tuweze kuelimikaWuiii uuuruuuu wiyooo ni huzuni na maumivu. Jana tu tulikuwa na furaha Chief Godlove kafulia baada ya habari kusambaa mitandaoni magari yake yakichukuliw.
Vijiwe vya umbea na vibaraza vilichangamka balaa. Tukajuwa mwana wote tuko sawa. Hadi tulimshukuru mungu kwa faraja ya kipekee.
Lakini furaha yote imetoweka kumbe yale magari bado ni yake yalikuwa yanapelekwa Nairobi alipo sasa hivi.
Ni pigo kubwa sana kwa maskin.
Mungu tusaidie tena kuwa na furaha hata mfanye tu Elon Musk ashuke hadi dollars billion 15.
Jana usiku tulilala na furaha with out empty stomachs happy leo tutalala na huzuni with our still empty stomachs.
MODS please mtufariji watu wenu asee.
View attachment 3529828
1.Je unajua kwanini zilibwebwa kwenye breakdown all the way to Kenya? Kumbuka gari ya breakdown ni sawa na ambulance gari la kubebea wagonjwa.. Breakdown ni ambulance ya Magari mabovu( yanayoumwa)
Japo hawezi kukubali huu ukweli hayo yamepekwa hospital Nairobi kwakuwa wenzetu wanetuacha mbali kidogo
2. Unajua ni kwanini zimepigwa picha juu ya ambulance zikiwa zimewashwa double hazard? Hi yo ni kwa ajili ya kuonesha kwamba zinawaka.. Lakini kiuhalisia zinaumwq hazitembei mwendo mrefu
3. Hizo gari kuzitembeza Tz mpaka Kenya kwenye breakdown tena ya wazi zimeongezewa tatizo maanq zimekula vumbi la kutosha na jua na mvua.. Ziko highly sensitive na vumbi kwenye sensor zake
4. Unajua kwanini hajapendq kukodi madereva waziendeshe?
Tuchukulie hazina shida. Lakini zisingefika Kenya zikiwa hai kutokana na miundombinu na mafuta yetu
Kingine no kuogopa kilometers.. Hata kama mafuta yangekuwa sawa lakini zingekula kilometers za kutosha na service yake asingemudu asilani ama hakuna wataalam wa service zake
5. Vipi kuhusu gharama? Kawalisha watu matango pori kwamba katumia zaidi ya usd 20,000 kuzipeleka huko Kenya! Huu ni uongo uliopitiliza
Ukweli ni kwamba alikosa pesa za kukodi container moja ya forty feet ama 2 za twenty feet akazipakia humo ambapo zingekuwa salama zaidi na zingefika kama zilivyo bila kuchafuka na vumbi la njia nzima ama la angezikodia ndege ya mizigo
Container moja forty feet Dar to Nairobi haizidi usd 4000.. Kale ka breakdown kakubebea nagari magonjwa hakazidi usd 2000
6. Mzee Ruge na Davis Mosha waliwahi kuagiza Rolls roys ambazo zilikuja na cargo plane .. Raha yake ni kwamba zinapofika hupigwa picha na kuchukuliwa video zikifunguliwa na kuendeshwa kutoka kwenye ndege.. Hata wanaolipia Container maalum kwa gari zao watu huziona zikitolewa kisha kuendeshwa mpaka kwenye parking huku zikiwa zimewashwa taa zote ama double hazard
Hizi zinazigojeka tumeziona zikiwa juu ya ambulance halafu tukapakiwa kejeli matusi na kashfa za kutosha
Hatutaziona zikishushwa kwakuwa si vizuri kumpiga picha mgonjaa anayepelekwa wodini toka kwenye ambulance
7. Hizo gari zina engine kubwa sana nadhani ni V8 na V12 na ni petrol.. Na ni gari za kuchomoka hazitaki slow speed. Hizo hazinywi mafuta bali zinabwia. Kwa barabara zetu hizi za vibao vya 50 na 120 sijui zingekula full tank ngapi
Kiuhalisia hizo gari ni mzigo usiobebeka na bei anazotaja si halisi maana kanunua mitumba.
Zina spare zake maalum
Zina mafuta yake maalum
Zina lubricants zake maalum
Na zinachagua sana njia
Kama Range rover ya 2015 service ya kawaida inaenda mpaka usd 3000 hayo madude je?
Kuna sababu nyingi za kumfanya mtu asafiri nje ya nchi na mojawapo ni ugonjwa na maradhi.. Usiondoke na ambulance halafu useme unaenda vacation!
LA mwisho mshaurini mwana.. Pesa hazitaki kelele wala kubwatukabatuka.. Ndio maana wenye hela zao huwa na timu professionals za
Wasemaji
Mavazi
Vyakula
Afya
Ulinzi nknk