Huyu mwanajeshi mwizi unamjua?

Huyu mwanajeshi mwizi unamjua?

NAPITA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
5,077
Reaction score
2,248
jangili1.jpg

Mwanajeshi aliekukutwa na jino la Tembo akiwa chini ya ulinzi pamoja na kidhibiti chake.


JUL122013


[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
jangili1.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mwanajeshi anayesadikiwa kukutwa na jino la Tembo akiwa chini ya ulinzi pamoja na kidhibiti chake, huyu alitegemewa kuilinda Nchi lakini .
(Picha na maktaba)

Alitaka kuingia Malawi, apandishwa kizimbani

OFISA Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Suleiman Chesana, anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni nne, amepandishwa tena kizimbani baada ya kukutwa na meno mengine ya tembo kilo 781 yenye thamani ya Sh bilioni 9.3.

Mshtakiwa huyo, alipandishwa tena kizimbani jana kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, mbele mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kusomewa mashtaka na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka.

Kweka alidai kosa la kwanza ni la kujishughulisha na nyara za Serikali bila kibali, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Ilidaiwa Mei 23, mwaka huu, katika mpaka wa Malawi na Tanzania, mtuhumiwa alikamatwa akisafirisha isivyo halali nyara zenye thamani ya Sh bilioni 9.3, zikiwa zimefichwa katika mifuko ya saruji, wakidai wanasafirisha saruji.




[/TD]
[/TR]
[/TABLE]








 

Attachments

  • zawadi.jpeg
    zawadi.jpeg
    24.1 KB · Views: 633
Yesu njoo mara ya pili uchukue walio wako maana sasa hakuna wa kumuamini kabisa.
 
dah...pingu inaheshimika, katuliaaa, kumbe hata mbwa wako mwenyewe anaweza kukung'ata!
 
Back
Top Bottom