Huyu mwanajeshi mwizi unamjua?

Huyu mwanajeshi mwizi unamjua?

....bongo nouuma...! watu wamepiga kontena kadhaa na bado wanadunda na vyeo wanapewa,mshikaji kajino kamoja tu anampelekea mzee akachukue kamisheni, wamemdaka...daaahhh...!!
 
Kumbe wanajeshi kuua tembo wanaanza toka jeshini.Sasa naelewa kwanini yule mtendaji mkuu mstaafu wa jeshi mwenye cheo kikubwa ni fundi wa kung'oa meno ya tembo.
 
kesi yake inaendeleaje au watasema tena wanasubiri upelelezi ukamilike?
huyu kesi yake ni kuhamishiwa lugalo, huko labda ataiba meno ya kuku... teh teh...adhabu za kubongo ni kuhamishiwa kambi tu..!!
 
Ila siku hizi naona JWTZ inapelekwa sawa sawa na polisi kwani angekamatwa polisi ungesikia ametoroka chini ya ulinzi mkali!Polisi hata ukiwakamata na fuso ya bangi kama ilivyokuwa kule Kilimanjaro watatoroka tu!Wajeda wengi tu wako jela kwa kuua lakini wanapouwa polisi utashuhudia tume za uchunguzi au utasikia mtuhumiwa amefanikiwa kutoroka chini ya ulinzi mkali wa polisi!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Sheria dhaifu ndio zimetufikisha hapa. Hiyu jamaa inaonekana ni mzoefu. Kabla hajakamatwa je ni tembo wangapi wameteketea. je ni kazi ngapi amefanikisha. waliomtuma ni lina nani na wapo wapi. Lazima tujiulize maswali mengi. Ingekuwa china huyu jamaa kushnehi
 
JUL122013


[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
jangili1.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mwanajeshi anayesadikiwa kukutwa na jino la Tembo akiwa chini ya ulinzi pamoja na kidhibiti chake, huyu alitegemewa kuilinda Nchi lakini .
(Picha na maktaba)

Alitaka kuingia Malawi, apandishwa kizimbani

OFISA Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Suleiman Chesana, anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni nne, amepandishwa tena kizimbani baada ya kukutwa na meno mengine ya tembo kilo 781 yenye thamani ya Sh bilioni 9.3.

Mshtakiwa huyo, alipandishwa tena kizimbani jana kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, mbele mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kusomewa mashtaka na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka.

Kweka alidai kosa la kwanza ni la kujishughulisha na nyara za Serikali bila kibali, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Ilidaiwa Mei 23, mwaka huu, katika mpaka wa Malawi na Tanzania, mtuhumiwa alikamatwa akisafirisha isivyo halali nyara zenye thamani ya Sh bilioni 9.3, zikiwa zimefichwa katika mifuko ya saruji, wakidai wanasafirisha saruji.




[/TD]
[/TR]
[/TABLE]






 

Je ni kweli ni hili moja tu? Huyo tembo alikuwa kibogoyo? Au mengine wameshachukua wamebakisha ushahidi hilo moja

Sen from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Huyu sio wa Serengeti alikuwa na vx?
 
Back
Top Bottom