T Kaiza-Boshe

Member
May 27, 2013
20
39
Wote tunakubaliana kuwa ujangili ni mbaya, na ni kosa la jinai; na kwamba sawa kuadhibiwa kisheria!

Na tunazo sheria za Uhifadhi wa Wanyamapori zinazotumika kulinda Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na sheria Na. 383 kama zilivyorekebishwa 2023 zinazotuhusu watu wote; wananchi, na wageni pia.

Kisichoeleweka na pia kutokuballika ni sheria hizo hizo kutumika kumuonea mwanamke wa Kitanzania na kumpendelea mwanamke wa Kichina kwa namna ya kutisha.

Inakuwaje mama wa Kitanzania ahukumiwe miaka 22 jela kwa kukutwa na vipande vya swala vyenye thamani ya shilingi za Kitanzania 900,000/=, wakati mama wa Kichina aliyekutwa na hatia ya ujangili wa meno ya ndovu yenye thamani ya dola za Kimarekani MILIONI 6 alihukumiwa miaka 17 (ikapunguzwa ikawa miaka 15, kuondoa muda aliokaa jela)?

Cha kushangaza zaidi swala siyo mnyama aliye kwenye hatari ya kutoweka, yaani hayuko kwenye IUCN- Red Book, na hivyo hajaorodheshwa na CITES kuwa hatarini kutoweka na kuhitaji ulinzi zaidi.

Isitoshe swala hajawahi kuwa "national game" (mnyama mwenye hadhi mahsusi). Hivyo mama wa Kitanzania kukutwa na vipande vya swala ni ujangili wa kawaida.

Tofauti na swala, tembo yuko kwenye orodha ya wanyama wanaokabiliwa na athari za kutoweka (threatened). Ameorodheshwa na IUCN na CITES hivyo. Isitoshe ujangili wa tembo ni UHUJUMU UCHUMI.

Iweje, sasa, huyu mama wa Kichina apewe adhabu ndogo kuliko wa Kitanzania aliyefanya ujangili wa kawaida, tena wa thamani ndogo sana.

#Mawakili
#TanganyikaLaw Society
#TAWLA
#AWLAE

Msaidieni huyu mama wa Kitanzania akate rufaa probono atendewe haki.

Ndimi Theonestina Kaiza-Boshe,
Mwanataaluma wa Wanyamapori na Maendeleo Endelevu

Email address: tkaiza@gmail.com

Screenshot_20231107-152250_WhatsApp.jpg
Screenshot_20231107-152054_MP4 Video Downloader Free.jpg
 
Back
Top Bottom