Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Nimemsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga sakata la ajali ya Costa iliyoua watu 17. Kwa kumsikiliza Tu unagundua Hana maarifa. Kama si zao la awamu ya tano basi ana vimelea vya Wakuu wa Mikoa wa awamu ya tano. Walikuwa wakuu wa Mikoa wa kukamata, kufunga ,weka maabusu nk
Hospitali zetu zinajulikana hazina magari yakutosha ya wagonjwa; tunaelewa kwamba Madaktari wa wilaya na Mikoa awaendi kwenye ajali wanasubiri waletewe majerui hospitalini, tunaelewa wazi kwamba usiku Madaktari wanakuwa wachache hospitalini na polisi wanakuwa wengi barabarani wakiwa na magari ya Doria. Nini kosa ya mganga mkuu wa wilaya na Mkoa?
Lakini pia kutokana na uchache wa wataalamu yawezekana hawa waliosimamishwa kazi ndio wataalamu wabobezi wanaotakiwa kuwahudumia hao wagonjwa na wagonjwa wengine kwenye maeneo Yao. Leo kuna watu wanakosa huduma zao hospitali Kwa Sababu wapo nybani wanasubiri uchunguzi kwanini walichelewa kwenda eneo la ajali.
Hebu tujiulize mkuu wa Wilaya alikuwa wapi wakati ajali inatokea? Tujiulize polisi walikuwa wapi? Mkuu wa mkoa na mganga mkuu wote wapo Tanga mjini, yeye alikuwa wapi hakuwahi kwenda kutoa huduma ya Kwanza? Kwanini kama yeye alishindwa kufika Kwa wakati anaamini Mganga mkuu angeweza kufika kwa wakati? Nani mwenye usafiri wa kuwahi eneo la tukio Kati ya mkuu wa mkoa na mganga mkuu?
Kama tunataka kuokoa maisha ya watu uchunguzi uendelee wakati hao wahusika wakiwa wanaendelea kutoa huduma. Tunaweza kutumia akili ndogo kwenye taaluma tukawapokonya uhai wagonjwa wengi.
Ilipotokea ajali ya ndege mwanza mafmdaktari mabingwa walikwenda kuokoa au walikaa kwenye vyumba vyao wakiwa na vifaa kutoa huduma?
Mkuu wa mkoa unataka kutuambia Mganga mkuu ana mobile hospital? Kwamba anaweza kwenda eneo la ajali na vifaa vya hospitali?
Nimetafakari Sana nikajiuliza wanaofanya kazi chini yake wapo salama? Ndio maana mkoa haupati maendeleo.