Huyu mgonjwa wa mguu makutano ya Ubungo anajimaliza mwenyewe

Achana naye huyo. Hana kidonda wala usaha. Huwa kuna materials fulani wanazungushia mguuni au mkononi na mguu au huo mkono huonekana kama una kidonda kikubwa au usaha mwingi.
Hu ungekua usaha hata yeye asingepata nguvu ya kwenda kuzurula barabarani. Usaha usikie hivihivi tu.
Hana kidonda wala jeraha. Anajifunga kipande cha nyama anakipaka manini sijui ndio kile kipande cha nyama kinaonekana kina usaha. Kama huamini siku moja jaribu kumchukua umpeleke hospitali uone matusi yake.
............Ila wakuu huo mguu si umevimba?au ni mimi naona vibaya?!
 
Watanzania tukoje?

Jama ile tu kuleta hii post jf ni kamsaidia vya kutosha..Mimi mwezi wa tisa nilimpa huyo jamaa Tshs.5000 baada ya kuuona kwa mbali mguu wake huo nikamsogelea nakumpa..

Hivyo kama una uwezo wa kumsaidia msidie ila usihoji jamaa kuleta hii post jf.
Ulitapeliwa hicho kidonda sio kidonda original ni nyama ya ng'ombe ameibandika kwa ustadi wa hali ya juu huwezi kugundua kirahisi
 
Kimsingi kama ni Mtumiaji Mzuri wa Stendi ya Ubungo huyo Jamaa atakuwa sio Mgeni Machoni kwako.
Hatukatai kweli wapo Matapeli ambao wanambinu mbali mbali za kukuhadaa hadi uamini kweli huyo MTU ni Mgonjwa na anahitaji Msaada, ila kwa huyo Jamaa hapo kwenye Picha hicho ni Kidonda na kweli alishawahi kufungwa bandage kikawa kinaelekea kupona lakini ndo hivyo tena huyo ni Teja hivyo hajali chochote kuhusu huo Mguu zaidi ya hizo Mia mbili za Unga.
Magari anayopendelea kuomba ni ile Column ya kwanza ukingia Stendi hususani Gari za Shabiby.., na siku hizi pale Shabiby Wanamfukuza asikae kwa kuwa huo Mguu unatoa harufu Kali kiasi cha kuwakera abiria na yeye lazima akuoneshe hicho Kidonda ili umuonee huruma hivyo ni Kweli hilo ni Donda Ndugu!!!
 
Tatizo ni hayo macho yako @avator, alivyoyaona akajua akienda hispital ndio sababu ya wew kumchukua msukule
 
Kwa hiyo boss na huo mguu kuvimba pia ni sababu ya nini
Atakuwa na matende

Kaa ukijua mtu aliyetumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu huwa wanavimba miguu kutokana na figo kuwa zimechoshwa kutokana na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa muda mrefu

Kuhusu hilo la kidonda ni usanii mtupu hpo ni kipande cha nyama ya ng'ombe ndyo kimehusika na sio kidonda km anavyotaka kuaminisha watu
 
Hicho kitu cheupe kwenye mguu sio kwamba kitu kimefungwa bali ni usaa uliotanda kuzunguka eneo hilo

Kila nimipita Ubungo kurejea nyumbani muda ya jioni mara nyingi namuona kijana huyu akiwa na kidonda kikubwa sana kwenye mguu wake wa kushoto

Muda wote anazunguka kutoka gari moja kwenda jingi akipata fedha kidogo anazozitumia kwaajili ya chakula

Kwasasa mguu wake umefikia hatua nzito zaidi kuliko hapo mwanzo ambapo alikuwa na nafuu sana

View attachment 958722

Najiuliza kwanini asichukue uamuzi wa kwenda Hospitali?

Niliwahi kumshauri hivyo lakini nikabaini anatumia kidonda chake kujiingizia kipato

Kifupi hajali uhai na afya yake, nilimwambia hata akienda Muhimbili hakuna wa kumfukuza hata kama hana fedha

Licha ya kuendelea kuharibu mguu wake lakini anawaumiza sana mioyo wapita njia
Fid Q Quote " Kuna Masikini na Omba omba wanao geuza kidonda Mtaji"
Akienda Hospitali anaweza kupona lakn hakipona hatakua tena Mtaji wa kumfanya Aendelee kuishi Mjin. Cdhan kama hakuna Mataji,Madaktari na Viongozi wasiopita Ubungo. Unadhan wamesgindwa kumsaidia....? Watu kama hao wengi wanakimbia Hospitalini
 
ushaambiwa kaweka kipande cha nyama ...
Ndiyo kipande cha nyama ndiyo ila kwanini huo mguu umevimba?hili ndo swali!

Nawaza labda kuna namna ameufunga huo mguu ndani ya hiko kipande cha nyama ili damu isitembee kwa uhuru na kusababisha ganzi inayosababisha mguu kuvimba?
 
Unaambiwa mguu haujavimba ule, ile n Sanaa kama sanaa zingine
 
Jamaa kabugi hapo kwenye kikaptula. Huo mguu cjui unapigwa ganzi ili utune. Ila asaidiwe jamani shida n shida tuu hata kama sio ulemavu.
Hicho kitu cheupe kwenye mguu sio kwamba kitu kimefungwa bali ni usaa uliotanda kuzunguka eneo hilo

Kila nimipita Ubungo kurejea nyumbani muda ya jioni mara nyingi namuona kijana huyu akiwa na kidonda kikubwa sana kwenye mguu wake wa kushoto

Muda wote anazunguka kutoka gari moja kwenda jingi akipata fedha kidogo anazozitumia kwaajili ya chakula

Kwasasa mguu wake umefikia hatua nzito zaidi kuliko hapo mwanzo ambapo alikuwa na nafuu sana

View attachment 958722

Najiuliza kwanini asichukue uamuzi wa kwenda Hospitali?

Niliwahi kumshauri hivyo lakini nikabaini anatumia kidonda chake kujiingizia kipato

Kifupi hajali uhai na afya yake, nilimwambia hata akienda Muhimbili hakuna wa kumfukuza hata kama hana fedha

Licha ya kuendelea kuharibu mguu wake lakini anawaumiza sana mioyo wapita njia
 
Kaka umedanganyika na ukaamini. Huo mguu hauna kidonda sisi tushawahi kumkamata huyo jamaa na kumfungua hiyo bandeji alikuwa analia kama anachinjwa. Kumaliza kumfungua rapurapu la nyama likadondoka puuh. Akaishia kusema washkaji kausheni basi maisha magumu. Na aliyetushtua kuwa anajifunga nyama ni dada mmoja mfanyakazi wa clouds. Hatukuamini kama wewe usivyoamini.
Huyu jamaa kweli ni mgonjwa, anakidonda kikubwa sana ila ni mteja, hospital alishauriwa ukatwe akagoma, unamtesa sana, sema uteja kauweka mbele.Maskan yake ubungo maziwa bondeni kule
 
Ndugu yangu hawa watu ni wasanii sana kuna mmoja tulishawahi kumchukua hapo kariakoo na tulienda kumkagua pale mgulani mle ndani tulichokiona sio chenyewe hawa ni waigizaji wakubwa
 
Huyu jamaa anaendaga hospital. Siku nyingine unamkuta kidonda kisafi. Na alivyo ziro ananyanyua mguu ili kula mtu auone. In short dar kuna wasanii na wengine hutumia shida ndogo kama njia ya kipato. Kuna mmoja pale mbezi aliondolewa na Tanroad wakati wa ujenzi lakini akakataa na akawa na taka kumpa rushwa ya 5000 ili aachwe afanye kazi ya kuomba.
Mwingine kimara darajani kama unateremka polisi slope ya mwisho. Yeye hukaa na mtoto mdogo, yule mama hana tatizo lolote lile, juzi nimemkuta anauza chenchi kwa wapiga debe....

Mwengine mateja walimfukuza asikae darajani kwa sababu anajifanya hana mkono mmoja kumbe anauficha kwa ndani.
 
Mkuu kama nibzingaombwe basi hata mimi nineingia king na kuivesha. Lakini jamaa guu limevimba lote. Na makonda husema ni kweli kidonda ila jamaa ninmteja
Achana naye huyo. Hana kidonda wala usaha. Huwa kuna materials fulani wanazungushia mguuni au mkononi na mguu au huo mkono huonekana kama una kidonda kikubwa au usaha mwingi.
Hu ungekua usaha hata yeye asingepata nguvu ya kwenda kuzurula barabarani. Usaha usikie hivihivi tu.
 
Shukrani kwa mtoa uzi,nimejaribu kupitia comment za wadau humu nimegundua kwamba ni usanii wa kujibandika nyama,ngozi etc
Lengo la hao wanaofanya hivyo only money,sitatoa msaada tena bila kujiridhisha pumbavuuuuu maisha magumu ni kwa wote!!!!
Mimi nilishaga acha kuwapa waombaomba msaada wa aina yyte coz nikigundua ni wasanii hatari wanafanya usanii ili wapate kipato we utashangaa mtu anaomba miaka yote wala haachi... Nmeshawashitukia kitambo kila wakija oficin kwangu wanapita kama 2 kwa siku ila wqnaambulia kuambiwa leo sina njoo ck ingine kila siku wimbo ni huo huo leo sina njoo siku nyingine mpka wanakata tamaa hawaji ovyo ovyo... We ni nikupe hera yangu wakat nami nina ndugu wanaohitaji msaada kama ww au hata zaidi yako si ni bora nimtumia mama angu kijijin ahemee chakula ale nipate baraka kuliko kuwapa hao vibaka na wajanja wa mjini wengi wao wana miradi na biashara za maana kama nyumba za kipangisha na za kuishi nk.
 
Kimsingi kama ni Mtumiaji Mzuri wa Stendi ya Ubungo huyo Jamaa atakuwa sio Mgeni Machoni kwako.
Hatukatai kweli wapo Matapeli ambao wanambinu mbali mbali za kukuhadaa hadi uamini kweli huyo MTU ni Mgonjwa na anahitaji Msaada, ila kwa huyo Jamaa hapo kwenye Picha hicho ni Kidonda na kweli alishawahi kufungwa bandage kikawa kinaelekea kupona lakini ndo hivyo tena huyo ni Teja hivyo hajali chochote kuhusu huo Mguu zaidi ya hizo Mia mbili za Unga.
Magari anayopendelea kuomba ni ile Column ya kwanza ukingia Stendi hususani Gari za Shabiby.., na siku hizi pale Shabiby Wanamfukuza asikae kwa kuwa huo Mguu unatoa harufu Kali kiasi cha kuwakera abiria na yeye lazima akuoneshe hicho Kidonda ili umuonee huruma hivyo ni Kweli hilo ni Donda Ndugu!!!
Utaibiwa Sana wewe na ubishi wako mwambie unampeleka hosipitali alafu ulete mrejesho hapa!!!??
 
Achana naye huyo. Hana kidonda wala usaha. Huwa kuna materials fulani wanazungushia mguuni au mkononi na mguu au huo mkono huonekana kama una kidonda kikubwa au usaha mwingi.
Hu ungekua usaha hata yeye asingepata nguvu ya kwenda kuzurula barabarani. Usaha usikie hivihivi tu.
Kweli kabisa...usaha mwingi hivo nafikiri asingeweza hata kugeuza huo mguu...mtu unaweza pata kajipu huo usumbufu wake mwili wote unauma .sembuse usaha wote huo kweli?
 
Kimsingi kama ni Mtumiaji Mzuri wa Stendi ya Ubungo huyo Jamaa atakuwa sio Mgeni Machoni kwako.
Hatukatai kweli wapo Matapeli ambao wanambinu mbali mbali za kukuhadaa hadi uamini kweli huyo MTU ni Mgonjwa na anahitaji Msaada, ila kwa huyo Jamaa hapo kwenye Picha hicho ni Kidonda na kweli alishawahi kufungwa bandage kikawa kinaelekea kupona lakini ndo hivyo tena huyo ni Teja hivyo hajali chochote kuhusu huo Mguu zaidi ya hizo Mia mbili za Unga.
Magari anayopendelea kuomba ni ile Column ya kwanza ukingia Stendi hususani Gari za Shabiby.., na siku hizi pale Shabiby Wanamfukuza asikae kwa kuwa huo Mguu unatoa harufu Kali kiasi cha kuwakera abiria na yeye lazima akuoneshe hicho Kidonda ili umuonee huruma hivyo ni Kweli hilo ni Donda Ndugu!!!
Mkui we ni ndugu yake nn mbona wote hapa wamekataa kuwa sio mjonjwa bali ni ujanja huwa mnagawana mapato nn
 
Kaka umedanganyika na ukaamini. Huo mguu hauna kidonda sisi tushawahi kumkamata huyo jamaa na kumfungua hiyo bandeji alikuwa analia kama anachinjwa. Kumaliza kumfungua rapurapu la nyama likadondoka puuh. Akaishia kusema washkaji kausheni basi maisha magumu. Na aliyetushtua kuwa anajifunga nyama ni dada mmoja mfanyakazi wa clouds. Hatukuamini kama wewe usivyoamini.
Sasa huo mguu inakuwaje manake unaonekana mguu wote umevimba sasa hapo anatumia mbinu gani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom