Huyu mgonjwa wa mguu makutano ya Ubungo anajimaliza mwenyewe

Huyu jamaa anaendaga hospital. Siku nyingine unamkuta kidonda kisafi. Na alivyo ziro ananyanyua mguu ili kula mtu auone. In short dar kuna wasanii na wengine hutumia shida ndogo kama njia ya kipato. Kuna mmoja pale mbezi aliondolewa na Tanroad wakati wa ujenzi lakini akakataa na akawa na taka kumpa rushwa ya 5000 ili aachwe afanye kazi ya kuomba.
Mwingine kimara darajani kama unateremka polisi slope ya mwisho. Yeye hukaa na mtoto mdogo, yule mama hana tatizo lolote lile, juzi nimemkuta anauza chenchi kwa wapiga debe....

Mwengine mateja walimfukuza asikae darajani kwa sababu anajifanya hana mkono mmoja kumbe anauficha kwa ndani.
Siku moja nikiwa pale Mwenge mataa nasubiri daladala ya Makumbusho, tuko abiria wengi...mara akaja mzee mmoja akiwa na box fulani hivi analitumia kujilaza chini aonekane ni ombaomba.

Akafika pale stendi, akalitandika lile box...akatafuta pozi zuri akajilaza, akaanza kuomba wapita njia. Alipoona hapati, akaamka akakunja box lake, daladala ilivyokuja na yeye akapanda kama abiria.

Nikajisemea moyoni mjini shule...babu mjanja. Mjini kumejaa waongo wa namna nyingi kiasi kwamba wale wenye shida kweli kweli inakuwa ngumu kusaidiwa.
 
Jamani Dunia ina mengi kuna watu wanatengeneza haya madonda; wewe unaona donda lina usaa kumbe hamna kitu; mwenzako ndiyo duka lake hilo kujipatia kipato.

Huwezi ukawa na donda kubwa hivyo eti ukapata nguvu ya kuomba barabarani wee hayo maumivu ni hatari.
 
KAKA MTOA MADA UNAFAHAMU KUWA WENGINE WAZIMA HUWA WANABANDIKA NYAMA MBICHI?
HIi ni Dar.
 
Akamatwe na wanausalama. Achunguzwe kama ni tapeli, sheria ifuate mkondo. Asiachwe aendelee kutapeli watu.

Ikiwa kweli ni mgonjwa asaidiwe matibabu.
Kwa ukubwa wa hicho kidonda lazima angepata homa.
Halafu na paja lingevimba pia, na isingewezekana kuunyanyua mguu sababu ya maumivu makali.
 
Sina uhakika kuhusu afya ya huyo jamaa, so sitomjudge.. Ila ninawafahamu vizuri walaghai watatu wanaoomba misaada kupitia maradhi feki..

1. Kiuno.. Aisee huyu mwamba ukikutana nae hata kama ulibaki na hela ya nauli utampa kisha utembee kwa miguu na kuimba haleluya.. Bwege anatembea kama nyoka anayejaribu kusimama dede.. Kiuno spring zinanyongorota kabisa na anatumia fimbo kupata balance.. Ukimwona utadhani mgonjwa kweli kumbe tapeli..

2. Bubu Kiziwi.. Huyu ni mzee kijana anajifanya chokambaya na hana kauli.. Ana kidaftari chake cha harambee za ujenzi wa choo chake mwaka wa 8 huu hajamakimaliza.. Anatembea na picha mkononi ya familia yake duni inayomtegemea.. Mrongo!

3. Safari.. Huyu jamaa ni chapombe mbwa.. Yeye afya yake unaweza kudhani alipata ajali mbaya maana kababuka mwili mzima ana michubuko kisa ulevi ila yuko road daily anaomba hela akatibiwe kifua na vidonda.. Cover story yake ni mabomu ya kule Mbagala ya 2009.. Chenga sana huyu jamaa na hata jina la Safari limetokana na kilevi akipendacho.. Safari lager..

Karibuni sana Jijini Daslaam watu wangu wa mikoani!
 
Mwacheni ndio maisha aliyochagua..kuwa mgonjwa upate hela za kusukuma siku au uwe mzima uwe huna hela ya kula ufe! Chaguo ni lako
 
Siku moja nikiwa pale Mwenge mataa nasubiri daladala ya Makumbusho, tuko abiria wengi...mara akaja mzee mmoja akiwa na box fulani hivi analitumia kujilaza chini aonekane ni ombaomba.

Akafika pale stendi, akalitandika lile box...akatafuta pozi zuri akajilaza, akaanza kuomba wapita njia. Alipoona hapati, akaamka akakunja box lake, daladala ilivyokuja na yeye akapanda kama abiria.

Nikajisemea moyoni mjini shule...babu mjanja. Mjini kumejaa waongo wa namna nyingi kiasi kwamba wale wenye shida kweli kweli inakuwa ngumu kusaidiwa.

Hahaaa hahaaaa mkuu umenichekesha sana,alipoona hapati Akaamua kuondoka,doh
 
Ndio maana unaambiwa kosa vyote ila usikose AKILI... kwake yeye anaona huo ndio mtaji wa kupata mia mbili mia mbili na haombei kabisa apone maana atazikosa hizo mia mbili mia mbili
Heroine ni shida
 
Msaidie. Mchukue mpeleke hospitali, sasa kuja kumuanika humu JF itasaidia nini?
Kama anaweza kutembea kote huko katika kuomba...ikiwa ataweza kutibiwa bila shida anashindwaje kwenda hospitali?


Mara nyingine ni Ujinga tu.
 

Similar Discussions

21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom