Huyu mbunge, mh!

Nashauri kabla ya hiyo mechi mazoezi wayafanyie Tarime kuwakakamaza zaidi.Mechi ipigwe uwanja wa ugenini Darfur International Stadium baina ya Tanzania Army na Al-Shabab refarii atoke Taliban washika vibendera watoke Alqueda na kamisaa Mpalestina na Stars wakishinda hiyo mechi wazawadiwe kinu cha nyuklia cha kisasa kabisa.Onyo hakuna kukimbia mpaka mwisho wa mchezo vinginevyo ni faini kali ikiambatana sambamba na kufungiwa maisha kushiriki michuano hiyo na shirikisho la vita vya kirafiki ulimwenguni.Nawasilisha.....!!!!
 
mkuu kimicho umetokea baraza la wawakilishi? Nimejenga picha akilini juu ya mazingira ya hiyo mechi nikachoka
 
Mh. Madam speaker, kwa kuwa serikali yetu inaajiri wanajeshi kila mwaka, na kwa kuwa hakuna kitu wafanyacho zaidi ya kula na kukimbizana na raia. Na kwa kuwa serikali yetu inanunua silaha kila mwaka na silaha hizo hazitumiki ipasavyo na kwa wakati na hatimaye kuharibika na kudhuru raia kama ilivyotokea Mbagala na G'mboto. Je serikali haioni umuhimu wa kukodisha wanajesh wetu ili tupate nyongeza ya pato la kigeni? Na je, serikali haioni umuhimu wa kuomba vita vya kirafiki na jirani zetu ili kuchangamsha wanajeshi wetu na kutumia silaha ili zisilipuke ovyo?
Mkuu nimecheka sana ngoja nikugongee Li- Sekis
 
Wabunge wetu wa VITI MAALUM ndio wenye akili kama hizi!
 
Tukiomba mechi ya kirafiki na Israel na Jei Wii ikashinda, siku Marekani ikiomba mechi ya kirafiki na Tized, nadhan kuanzia ombaomba Matonya mpaka wale wala bata wa kila watakimbia kusevu roho, Marekani kwa mabomu ya maana hawajambo, Jei Wii mabomu yanakwenda kotekote!
 
Back
Top Bottom