K
Hatulipiti gari kwa sababu tu mbele hakuna gari, tunalipita gari kwa kuzingatia kanuni za barabarani na muongozo uliopo barababarani kv mistari nk na hali ya barabara...huyo mama eneo aliloovateki halikuwa salama na mstari ulikuwa hauruhusu, pia mbele palikuwa na kona....JIELIMISHE ZAIDI KWA SEHEMU HII YA KANUNI ZA BARABARANI
Kulipita gari jingine
Kabla ya kulipita gari jingine LAZIMA uhakikishe kuwa:
• barabara haina vikwazo vyovyote
• gari lililo nyuma halijaanza kulipita gari lako
• gari la mbele halijaanza kulipita gari jingine
• kuna upenyo mkubwa wa kutosha mbele ya gari unalotaka kulipita.
Usilipite gari jingine isipokuwa kama una uhakika unaweza kufanya hivyo
bila ya kusababisha hatari kwa watumiaji wengine wa barabara au kwako
mwenyewe. Iwapo una shaka usilipite gari jingine.
Usilipite gari linalotembea au lililoegeshwa:
• iwapo gari linakaribia kutoka upande mwingine – isipokuwa kama
una uhakika unaweza kufanya hivyo bila ya kulilazimisha gari hilo
kupunguza mwendo au kupinda ghafl a ili kukuepuka
• pale gari linalopitwa linaashiria kupinda kulia
• pale ambapo huwezi kuona umbali wa kutosha mbele, mfano kwenye
kona au karibu ya kilele cha kilima
• kwenye makutano
• kwenye alama za pundamilia au karibu na alama hizo au mahali
pengine wanapovuka watembea kwa miguu
• kwenye reli au karibu na reli
• ambapo unatakiwa kuingia kwenye njia iliyo maalum kwa mabasi au
waendesha baiskeli
• ambapo unatakiwa kupita kwenye eneo lenye mistari ya mshazari au
ya umbo la V.
= ambapo kulipita gari jingine hakuruhusiwi kwa alama ya “Hakuna
kulipita gari jingine” au michoro ya barabarani.
NAAMINI MAELEKEZO HAYA YATAKUFAA,YAMO KTK KANUNI ZA BARABARANI.Mwabeja