Huyu mama anaendesha basi la kampuni gani Mbeya-Dar?

Huyu mama anaendesha basi la kampuni gani Mbeya-Dar?

2014 nilikuwa natoka Dom nakuja Dar kufika chalinze tukakutana na basi fulani hivi ilikuwa mpya mpya kimuonekano jina limenitoka

Yule dereva wa lile basi alitoka spidi na kutu overtake kwa spidi ya ajabu kufika mbele uso kwa uso na scania dereva wetu ikabidi asogee kando kumpisha alivyofanikiwa kupita pita kama vile panya anavyopenya penya na kukoswa bado akawa anaendelea kulikimbiza gari na kuovertake huko mbele mie nilimuona yule driver ni mwansmke ila abiria wengine hawakutambua,basi zima lilipigwa na butwaa na mshangao na minongono kibao

Bahati nzuri lile basi tukafanikiwa kulikuta mile 1 stand ndipo walipomuona yule driver ni mwanamke wacha watu waanze kucheka ,wenye kuongea lake ,watu walishangaa saaana

Popote alipo yule dereva mwanamke heshima kwake ase nampa salute

Alivaa uniform sketi ya blue ,shati jeupe huku akibadilisha gear tu na kuover take mijibaba yenye ndevu alikuwa na fujo sana barabarani

Nimekumbuka hili tukio
Huyu hapa

images-20.jpeg
 
Asee sipandi basi la mikoani linaloendeshwa na mwanamke I don't trust them ila inaonekana ni raha kundeshwa nao
 
Back
Top Bottom