Huyu mama anaendesha basi la kampuni gani Mbeya-Dar?

Huyu mama anaendesha basi la kampuni gani Mbeya-Dar?

Lakini ni muda sana, kwani mpaka sasa anaendesha,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, NDENJELA EXPLESS (mbeya - -Dar)
 
Shishi baby nae yupo chang'ombe anasomea u driver wa mabasi makubwa siku si nyingi mtamuona mabasi ya mikoani
 
2014 nilikuwa natoka Dom nakuja Dar kufika chalinze tukakutana na basi fulani hivi ilikuwa mpya mpya kimuonekano jina limenitoka

Yule dereva wa lile basi alitoka spidi na kutu overtake kwa spidi ya ajabu kufika mbele uso kwa uso na scania dereva wetu ikabidi asogee kando kumpisha alivyofanikiwa kupita pita kama vile panya anavyopenya penya na kukoswa bado akawa anaendelea kulikimbiza gari na kuovertake huko mbele mie nilimuona yule driver ni mwansmke ila abiria wengine hawakutambua,basi zima lilipigwa na butwaa na mshangao na minongono kibao

Bahati nzuri lile basi tukafanikiwa kulikuta mile 1 stand ndipo walipomuona yule driver ni mwanamke wacha watu waanze kucheka ,wenye kuongea lake ,watu walishangaa saaana

Popote alipo yule dereva mwanamke heshima kwake ase nampa salute

Alivaa uniform sketi ya blue ,shati jeupe huku akibadilisha gear tu na kuover take mijibaba yenye ndevu alikuwa na fujo sana barabarani

Nimekumbuka hili tukio
Pamoja na ajali zote zinazotokea barabarani,vifo,majeraha na madhara mengine yanayotokana na ujinga huu wa madereva bado Kuna watu kama wewe na wenzako mnaona Ni mambo ya kusupport.
Kweli akili Ni nywele..watanzania tuache uvivu wa kufikiri kabla hujapost ujinga tafari kwanza,iwe mwanamke Au mwanamme umakini na maamuzi sahihi barabarani Ni lazima...
 
Binafsi siwezi kupanda basi linaloendeshwa na mwanamke au chombo cha moto cha cha cha masafa marefu........najua kuna watu hawatanielewa lakini wenye elimu ya maumbile watanielewa.......

Samahani kama nimemkwaza mtu na maoni yangu....
 
Na kuna mwingine yupo Has ana tank pia nilikutana nae Zambia
 
wanakuaga na ndoa mbilimbili, kufuatana na route, atakapofikia analiwa
 
Alafu huyu atakuwa ni mchaga, wachaga hawapendi ujinga....wanasukuma hadi gogo. Truck za kubeba tani 30, huyo ni wa njia ya Tanga.....safi sana.. Hivi miwani haimsumbui? Maana hapo anaona vioo viwili kwa wakati mmoja
Ni njia ya Tanga na kampuni ni Tashriff
 
K
Mkuu, hebu fafanua vizuri tuone kosa lake, kwani kuovateki malori manne kama mbele kweupe ni kosa?...
Hatulipiti gari kwa sababu tu mbele hakuna gari, tunalipita gari kwa kuzingatia kanuni za barabarani na muongozo uliopo barababarani kv mistari nk na hali ya barabara...huyo mama eneo aliloovateki halikuwa salama na mstari ulikuwa hauruhusu, pia mbele palikuwa na kona....JIELIMISHE ZAIDI KWA SEHEMU HII YA KANUNI ZA BARABARANI

Kulipita gari jingine

Kabla ya kulipita gari jingine LAZIMA uhakikishe kuwa:
• barabara haina vikwazo vyovyote
• gari lililo nyuma halijaanza kulipita gari lako
• gari la mbele halijaanza kulipita gari jingine
• kuna upenyo mkubwa wa kutosha mbele ya gari unalotaka kulipita.

Usilipite gari jingine isipokuwa kama una uhakika unaweza kufanya hivyo
bila ya kusababisha hatari kwa watumiaji wengine wa barabara au kwako
mwenyewe. Iwapo una shaka usilipite gari jingine.

Usilipite gari linalotembea au lililoegeshwa:
• iwapo gari linakaribia kutoka upande mwingine – isipokuwa kama
una uhakika unaweza kufanya hivyo bila ya kulilazimisha gari hilo
kupunguza mwendo au kupinda ghafl a ili kukuepuka
• pale gari linalopitwa linaashiria kupinda kulia
• pale ambapo huwezi kuona umbali wa kutosha mbele, mfano kwenye
kona au karibu ya kilele cha kilima
• kwenye makutano
• kwenye alama za pundamilia au karibu na alama hizo au mahali
pengine wanapovuka watembea kwa miguu
• kwenye reli au karibu na reli
• ambapo unatakiwa kuingia kwenye njia iliyo maalum kwa mabasi au
waendesha baiskeli
• ambapo unatakiwa kupita kwenye eneo lenye mistari ya mshazari au
ya umbo la V.
= ambapo kulipita gari jingine hakuruhusiwi kwa alama ya “Hakuna
kulipita gari jingine” au michoro ya barabarani.

NAAMINI MAELEKEZO HAYA YATAKUFAA,YAMO KTK KANUNI ZA BARABARANI.Mwabeja
 
Simwamini mwanamke katika safari nzito kama hiyo. ......hachelewi kukwepa NYOKA mkaingia porini.
 
Back
Top Bottom