aseeee!
Juzi kati hapa, majira ya saa6 kasoro usiku nikiwa nimetoka kwenye banda la mpira kuangalia usiku wa mabingwa a.k.a UEFA champions league, wakati narudi njiani kwenye kichochoro kimoja hivi nikakutana na vibaka wawili (Nyumbani dstv ipo lakini napenda zile amsha amsha za kibanda umiza).
eebbanaaae! kibaka mmoja akawa kwa mbele ananisubiria ameshika kitu kama bisibisi mkononi, nilimuona kwakua kulikua na mbalamwezi kiaina! duh! nikasena nifanyaje hapa, kushoto na kulia ni ukuta yani ni chochoro zile za ukuTa huku na huku duh!! nikasema ngoja nirudi nilipotoka, aseeee! nageuka hivi kubabake zao kumbe kuna mwingine yupo nyuma yangu nimewekwa mtu kati wanataka wanipige mande!
mfukoni nina iphone 7, nikasema hapa lazima nijitetee asee kwa laifu hili hii simu haiwezi kwenda hivi hivi bora hata damu imwagike!
yule Mmoja akasema "oya mwana, chojoa vyote ulivyokua navyo!"
nikawaambia sawa, nikatoa simu nikampa yule mmojawapo, nikawaambia "ngoja niwavulie na raba hii wanangu bora mniache mweupe lakini msiniue!"
wakati nimeinama nafungua kamba za viatu kuna jiwe nililiona pembeni pale, na lengo langu la kuinama kuvua viatu ni ili niliokote nimkandamize nalo yule niliempa simu!, nikalitaimu lile jiwe pembeni ya mguu wangu nikaliokota bila wao kujua.
asee! niliamka nalo fasta Kama kipanga nilimkandamiza na jiwe kichwani yule niliempa simu ukatoka mlio "kwaaaaaa!!!" akakata moto akaanguka chini anagalagala analia!, yule mmoja akasema "wewe boya umempiga mshkaji na jiwe kichwani nakuchoma na bisibisi!"
nikamwambia "ni ngumi hiyo, sio jiwe" duh! alivyosikia hivyo akakurupuka akakimbia!
nikachukua simu yangu kwa yule alieanguka chini baada ya kumkandamiza na jiwe kichwani, namimi nikamsachi mfukoni kwake alikua na wallet namimi nikaone nisepe nayo, undava! undava! nikamwacha anaugulia maumivu hapo
nkafika home nikatulia kidogo nalitafakari lile tukio, nikasema ngoja niifungue ile pochi ya yule kibaka aseee! duh! nikakuta shilingi 15,000/=, kadi ya bank, passport size zake mbili, leseni na kilichonishangaza zaidi ni kitambulisho chake cha chuo fulani kikubwa hapa mjini aseee!!
ikabidi nicheke mazee, Nikijiuliza kumbe kuna wanachuo manyamera hivi!!??
WEWE MWANACHUO, NAJUA WEWE NI KIBAKA MSOMI LAZIMA UTAKUA UNAPITA MAENEO HAYA, UKIONA HII NICHEKI NIKUPE POCHI YAKO, ILA ACHA WIZI UTAKUJA KUFA BWEGE WEWE!