Huyu kaka ana jinsia gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu kaka ana jinsia gani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MadameX, Aug 3, 2012.

 1. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Habari zenu wakuu, nina mtu wangu wa karibu hali yake inanipa utata. Yeye yuko late 30's amelelewa kilokole na pia hivyo nyumbani kulikuwa na maadili mazuri yaani it was very strict family, mambo ya ujana kwao yalikuwa hayana sehemu, kwahiyo mambo ya watoto wa mjini kwake yalikuwa hakuna.


  Sasa yeye ni mtu mzima, mamake na nduguze wamepiga dau la kuoa wamechoka maana kihali na mali inamruhusu (anaishi peke yake). Kitu cha kushangaza huyu mtu hajawahi kuwa wala kuonekana na GF kama kawaida ya wanaume. Hana hata mtoto wa kusingiziwa, yaani urafiki na wanawake hana hata ule wa platonic hakuna zaidi ya sisi jamaa zake. Nimejaribu kumconnect na sister fulani hivi poa, kwa kuhisi labda atakuwa domo zege nalo halikufaa maana ni muda wako pamoja lakini mazungumzo hayaendi next level.

  Kuwa ni mlokole si mlokole...jamani kuna jinsia gani zaidi kwa mwanaume kama mtu si gay or straight kuna 3rd option?
   
 2. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,205
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hakunaga Third option ila kila binadamu ana tabia zake kuna watu wengine huwa kusoma hawajui na hata ukimwonyesha picha ndio unamchanganya kabisa hivyo basi kama ni mtu wako wa karibu zungumza naye very friend in order kujua tatizo lake ni nini then utajua ni wapi unaweza kumsaidia kama usipofanya hivyo hata umlete wadada 20 is equal to zero.
   
 3. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,959
  Likes Received: 20,296
  Trophy Points: 280
  Huyo uliyemuunganisha naye, fanya wakutane usiku, wengine wana aibu zao bhana
   
 4. Double K

  Double K JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 908
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Wazazi wameonge wameshindwa, basi mtafutieni mtu ajifanye housegirl na mumpe somo kuwa kazi yake ni kumtega mpaka kieleweke, atumie every woman power she has kuhakikisha anampata au anajua tatizo ni nini, labda haifanyi kazi na mnazidi kumpa stress na kusema hawezi.
   
 5. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Dah hii kesi ngumu kweli MadameX, lakini nitajitahidi kudig in kidogo kadri nitakavyoweza

  Kiafrika mahusiano huanzishwa na mwanaume so yeye ndio huwa anatakiwa ainitiate hayo mahusiano kwa msichana. Sasa tabu inakuja pale kwenye kuanzisha mahusiano, kunahitaji mambo mengi sana lakini kikubwa kabisa ni confidence kwamba yes i can get this person to talk to me and accept what i am gonna tell her. Sasa hali hii hujengwa tangu ukiwa mtoto na inajengwa na mazingira hasa unayokulia. Ntakupa mfano, wakati mi nikiwa mdogo ulikuwa ukiniweka na msichana pamoja ni kama roho ilikuwa inataka kunitoka kwa uwoga (hasa kama huyo msichana mwenyewe nilikuwa na hisia zozote kwake)

  Kuwa karibu na wasichana na kuwazoea kukanifanya nikaondoa ule uwoga niliokuwa nao enzi hizo. Sasa kwa kesi ya ndugu yako ni kwamba malezi aliyolelewa yamemfanya awe na hali kama niliyokuwa nayo mimi nilivyokuwa mtoto, kutokuwajiamini na kuwa na woga. Na believe me if this is the case hata ukimwekea mwanamke ndani akiwa mtupu he will never do anything maana uwezo wa kufanya tendo hilo kwa mwanaume unahusisha kwa kiasi kikubwa sana akili yake ambayo kama hajiamini then hawezi kufanya kitu.

  Kwahiyo cha kufanya, ni lazima aanze kuwa karibu na wanawake as friends ili awazoee, believe me kuna wakati itamlazimu kwenda beyond ulokole wake ili kujenga hiyo confidence inayohitajika ili kuondoa maswali mengi yanayomsumbua kama, Can i?, Will she?, How do i? na kadhalika....

  Hebu ngoja niendelee kufikiria mengine then ntarudi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  huyo dada uliyemuunganisha naye ndiye anaweza kusaidia kutoa 'clue' ya status ya jamaa kimahusiano... e.g huwa wanaongea nini wakiwa pamoja: vitambulisho vya taifa, sensa, kutekwa kwa dr ulimboka au mambo ya mahusiano and probably how the guy feels towards her....
   
 7. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,572
  Likes Received: 923
  Trophy Points: 280
  MadameX,
  Kuna watu wapo hivyo,mimi nina kaka yangu wa kuzaliwa na sasa ana 50yrs (kazaliwa 1962)...ana kazi nzuri and everything in life ila hana GF wala hajawahi kuwa naye. Wala usiendelee kumlengesha kwa wanawake sanasana atakuchukia tu na uhusiano wenu utaharibika kabisa....coz anaonekana HAPENDI mahusiano na wanawake.
  Izoeeni tu hiyo hali yake kama sisi tulivyoizoea hali ya ndugu yetu na maisha yanasonga.
   
 8. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,897
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Huyo hana tatizo lolote kwa jinsi ulivyoeleza ni mazingira ya ukuaji wake yaliyosababisha hali hiyo ambapo inapaswa kuwasifu wazazi wake.Lakini naona wazi kuna kosa linalofanyika hapa nalo ni kumpa pressure ya kuoa na hiyo ni hatari sana kwani inaweza kusababisha kijana wa watu akafungulia kuonyesha urijali wake na kuishia kwenye magonjwa.Ni vyema kwenda naye taratibu kwa kumkutanisha na wasichana tofauti mpaka atakapokutana na chaguo lake na kila kitu kitakuwa sawa.Kuna mtu alikuwa kama huyo na alishafikia mpaka kukutanishwana wasichana chumbani na nguo wakamvulia lakini wala hakushtuka lakini leo ameoa na anaishi kwa amani na mkewe hivyo huyo naye ni kumpa muda zaidi kwani kwa mwanaume miaka 30 ndio kwanza kunakucha....
   
 9. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni akili tu imejengeka kuona tendo hilo au kuwa na wanawke ni kosa, njia rahisi ya kuondoa hilo ni awe na watu ambao watakuwa wako wazi kwenye kuzungumzia hilo jambo, nashauri mtafutie mwanamke chakaramu ambaye kila neno linalomtoka mdomoni ni tusi atazoea tu, mwanamke aliye decent kwa jamaa yako huyo atamuaribu zaidi!!
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Kwani mwanamme hawezi kujiamulia kukaa peke yake bila mwanamke?

  Kama mtu mwanamme hana interest na wanawake, kashaangalia kaona magonjwa na michosho mingine tu, anataka kufanya mambo yake bila usumbufu wa familia na watoto, atakuwa si mwanamme?

  Haya matatizo ya kufuatilia watu walioamua kuishi maisha yao tofauti na tunavyojua kawaida yapo nchi zisizoendelea ambapo watu wanachofikiria kinazunguka mule mule tu, kuzaliwa, kuoa,kuzaa,kufa.

  Unajuaje kama mtu anatafuta dawa ya kansa huko (au anataka kufanya kingine chochote ambacho ni muhimu kwake) anaona GF au mke na watoto watamzingua tu.

  Atakuwa na makosa gani?
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unafikiri hilo linahitaji kuondolewa kama mtu kaamua mwenyewe maisha yake kuishi hivyo?
   
 12. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hata wanawake wa Tanga wameshindwa kumtega!!
   
 13. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kuna rafiki yake husband pia yupo hivyo, yaani siyo gay wala straight, na kuna kipindi tulimlengeshea mdada ikashindikana, then husband akaamua kumwendea na kuzungumza naye kama kamati, jamaa akajidai hawezi kuwatokea wadada. sasa akamwambia poa, mimi nitaongea na mdada na nitamalizana naye kabisaaaaaaaaaaaaaa, nikimleta kwako ujue ashakubali kila kitu uendelee tu.
  tukaongea na rafiki yangu, tukamwambia kila kitu na kwa vile yeye ni mjanja akakubali, tulipompeleka mbona tulipata aibu...... aliongea naye usiku kucha mpaka dada wa watu akasinzia na yeye akalala, asubuhi kaamka mapema. tumeamua kumwacha
   
 14. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 848
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hivi makaka ​huwa wana jinsia gani?
   
 15. by default

  by default JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  jaribu kupretend umechanganyikiwa ukalale kwake siku moja then utarudi na jibu la hapo kwenye red
   
 16. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  umeshasema kaka halafu unaulizia jinsia....:A S confused:
   
 17. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kweli aisee.... hasa kama ni khanithi
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Jamii maskini zimejikita katika kufuatilia mambo yasiyo muhimu kama haya, nani khanithi nani rijali. Nani ana mke mmoja nani ana wake wanne na upuuzi mwingine kama huo.

  Wakati wenzetu wanatafuta dawa za UKIMWI na kansa, wanapeleka vyombo Mars, wanasolve Poincare's conjecture.

  I bet Grigori Perelman angekuwa Mtanzania watu wangemsema khanithi.
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kwani mnaishi kijiji gani? Miaka 30 kwa kijana wa kiume sio mingi. Kuna watu wako reserved na mambo yao tu, ila ni ma-heartbreaker wazoefu! Nani alitoa uzi wa maswali ya kukera ya 'unaoa ama unaolewa lini?'
   
 20. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kweli aisee, tunapenda kufuatilia watu... hasa makhanisi
   
Loading...