Huyu, HANAGA Mpinzani BONGO NZIMA

Nikimuona nakumbuka unga wa ngano, nakuvaa nguo za viraka pamoja ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari. Huyu Mwl alitawala kundi la wajinga toka mwaka 1960 wananchi wake walikuwa hawajawahi kuona TV wala kufanya mijadala kama hivi. Enzi zake ukikutwa na dola 50 utajuta lazima uende jela.
Eti nini? Anhaaaa kumbe ritz!!!
 
Wote wanao beza wamezali enzi hizi za JK na william! Habari zake wanazisikia kutoka kwa wahuni tu.

Wewe uliezaliwa umri mmoja nae, hebu weka mazuri yake ili tuyajadili. Hebu tuone hizo kauli zetu wahuni na zenu wasafi!
 
Nikimuona nakumbuka unga wa ngano, nakuvaa nguo za viraka pamoja ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari. Huyu Mwl alitawala kundi la wajinga toka mwaka 1960 wananchi wake walikuwa hawajawahi kuona TV wala kufanya mijadala kama hivi. Enzi zake ukikutwa na dola 50 utajuta lazima uende jela.

TV inakusaidia nini? comedy?

wajinga ? WEWE unajiona umeelimika? unafahamu tofauti ya literacy level ya miaka ya 70 na sasa?

tanzania ilipata tunzo ngapi kipindi cha nyerere kwenye suala la elimu?
 
Yaani kuna watu wanamuona huyu kama mungu wao,eti bila yeye tz sijui ingekuwaje,tokeni hapa hata kama asingekuwepo tz ingepata uhuru na maisha yangekuwa bora kuliko yeye,kuna nchi gani leo duniani haina uhuru?huyu ndio chanzo cha ujinga wetu,vp kenya wametuzidi na uganda kwa elimu?sababu ni huyu,na huyu ndio rais pekEe hapa tz aliekuwa na uchu na madaraka,miaka 24 ikulu,kaja kukimbia ikulu baada ya kuifilisi nchi kwa kutaka sifa za kukomboa kila nchi,leo hii wanatucheka hao tuliokuwa na kiherehere cha kuwakomboa,jamaa huyu ndio alietufikisha hapa tulipo,
 
TV inakusaidia nini? comedy?

wajinga ? WEWE unajiona umeelimika? unafahamu tofauti ya literacy level ya miaka ya 70 na sasa?

tanzania ilipata tunzo ngapi kipindi cha nyerere kwenye suala la elimu?
Asante sana ndugu yangu. Kuna watu humu kazi yao ni kubwabwaja tu. Hawajui thamani ya Mwl katika nchi hii. Eti TV, ptuuuuuuuu, TV yenyewe ndiyo hiyo miziki ya Diamond na filamu za akina naniiii.... Upuuzi tu.
 
Sie watu wa pwani ndo tulomfunda huyu mzee wenu kuvaa kistaarab (sarawili + kikoi), yy alikua mtu wa makaputura na masulupwete..pichani dhahiri ni baada ya kuoneshwa jinsi ya kuketi wakti ukialikwa ustaarabuni. najua wabara mtapinga/
 
Ukimaanisha tungekuwa bado tunakula lile dona la farasi?



Halafu lile dona tamu jamani, yaani umenifanya nikumbuke mazuri mengi ya miaka ile kama foleni za kununua viwembe na mafuta ya koroboi. If I could only turn back time, ningependa nipate lile dona pamoja na mchele kitumbo for this x-mas!
 
Msingi wa uchumi mbovu huyu ndo aliyeutengeneza.Halafu leo mnamsifia kweli hamnazo.Ila yako mazuri amefanya ila ni machache sana ukifananisha na uharibifu aliofanya
 
Nakubaliana nawewe kabisa kwani Tanzania ya leo si ya wajinga kama aliowaongoza yeye. Pia sasa kuna demokrasi hakuna tena alama ya ndio na hapana kuwa wagombea urais.

Ndugu juzi tu ccm wepiga kura ya ndio na hapana kuchagua mwenyekiti, kaa kimya usije kukosa majibu kwa ushabiki.
 
Nyerereism bado inawasumbua! Hata wakijitahidi wanashindwa kwani bado wako wengi wanadanganywa na utakatifu wa nyerere hivyo si rahisi kuuacha hata kwa mdomo tu na nyuma ukimpinga kwa vitendo!
 
Hakuna binadamu asiyekuwa na mapungufu yake, na Mwalimu hakuwa malaika ila pale alipofanya vizuri ni vema asifiwe

Enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna matabaka ya waliokuwa nacho na wasiokuwa nacho kama sasa, kulikuwa hakuna rushwa kama ilivyo sasa,

Alikuwa anaudhubutu wa kukemea maovu na kuadibisha waliokosea.
 
Back
Top Bottom