Nataka nikufundishe maisha wakati nasoma advance diploma katika chuo kimoja kipo hapa dar maeoneo ya town kuna mwl alinifanyia kitu mbaya sana, kunishitaki kuwa nilikuwa namsaidia mwanafunzi mwenzangu ktk mtihani, kwa hiyo nikapewa disco cheating. Nikaanza chuo upya, mwaka juzi mkewe wakati anarudi home maeneo ya surrender bridge kwenye foleni jamaa alipasua kioo akachukua begi ndani pakiwemo na doc za kusafiria siku inayofuata, wakati nipo mitaa ya home mara nikamuona mtoto wake wa kike akiwa na mama yake (mke wa yule mwl) nikamuuliza vipi mbona huku kinondoni akaniambia mama ameibiwa Leo mchana, ila tumeambiwa tukipata mtu anayekaa huku itakuwa rahisi kupata hata doc. Nilitafuta wahuni wote ninao wajua mpaka tukapata doc zilipotupwa hiyo ilikuwa saa tano usiku. Dogo haya ni maisha.