STORY: Jesus Freak

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,921
14,820
ENGLISH: JESUS FREAK
SWAHILI: KITUKO WA YESU

NA-DEDICATE STORI HII KWA WATU WOTE WANAOMPENDA MUNGU HUKU DUNIANI.

SIKO HAPA KUKOSOA IMANI ZA WATU WALA DHEHEBU ZA WATU ILA KATIKA KIPINDI HIKI TUNACHOJIANDAA KWENDA MBINGUNI, KABLA YA UNYAKUO WA KANISA, KUNA VITUKO VINGI SANA VIMETOKEA AMBAVYO VINATENGENEZA HADITHI NYINGI TU.

VINGINE VINAHUZUNISHA, VINACHEKESHA,VINALIZA, VINAUMIZA, VINAFURAHISHA, MWISHO WA SIKU IMANI YETU NI MOJA TU KWA YESU KRISTO AMBAE TULIMPENDA NA TUNAMPENDA SANA KIASI CHA KUONEKANA AU KUJULIKANA KAMA VITUKO WA YESU(JESUS FREAKS!).
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

CAUTION/ TAHADHARI:

MPENZI MSOMAJI USOMAPO STORI HII JUA KUWA HII NI STORI TU KAMA STORI ZINGINE – NI MOJA KATI YA BURUDANI ZILIZOPO DUNIANI

TAFADHALI USICHUKULIE BINAFSI (DON’T TAKE IT PERSONAL)

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

SEHEMU YA 1
A. NJIA ILE NI NYEMBAMBA IENDAYO UZIMANI

MWAKA 2018:

Natembea duka moja hadi jingine naangalia vitu vya kununua (zawadi) za kupeleka nyumbani kwa familia yangu mitaa ya New York City Mjini Marekani, baada ya masaa mengi ya kuzura na kuchoka nikaamua kwenda kwenye mgahawa nipate kituliza tumbo.

Nikafika, nikakaa, akaja mhudumu nikaagiza nachohitaji nikaendelea kusubiria huku natumia simu yangu kuangalia mitandao ya kijamii kilichojiri huko Instagram, Facebook, Snapchat, Whatsapp, Twitter na Tumblr… nilipochoka nikaanza kujipiga selfie ili ni-upload picha Instagram, si unajua tena sisi watoto wa mitandaoni kila sehemu unataka kupiga picha na wewe uonekane umo.

Katika ku-edit picha nilizojipiga nikaona kwenye picha mtu amekaa kiti cha tatu nyuma yangu kama namfahamu. Kugeuka na kuangalia nyuma kweli ni yeye, sikuamini, yeye hakuniona ila mimi nilimuona, sikuamini nakwambia huyu mtu mimi namfahamu miaka mingi tena kuliko maelezo, amefikaje New York Mjini sikuelewa, kweli?

Nikaondoka kwenye kiti changu nikamfuata nikakaa mbele yake maana alikuwa amekaa mwenyewe anasoma kitabu cha hadithi, akageuka kuangalia huyu ni nani amekuja kukaa mbele yangu, kuniangalia hakuamini,
“Heeee! Wewe? Upooo? Unafanya nini huku New York?”
Huyu Mtu alikuwa anaitwa Azonto, ndio Azonto ndio jina lake,la kuzaliwa, la shuleni, la Kanisani kila sehemu ni Azonto labda awe amebadilisha miaka hii lakini anaitwa Azonto.

NAOMBA NIKUELEZE AZONTO NI NANI;
MWAKA 2000

Azonto nilisoma nae shule ya Sekondari Tambaza, jijini Dar es Salaam, tulisoma Darasa moja form 5 na 6…Baada ya hapo tukaenda wote kusoma IFM hapo Posta ya Zamani.

Azonto aliokokaga tulipokuwaga form 5 bwana, aliokokokea kule kwenye vipindi vya dini, wakati walimu wa dini wakiwa wanakuja kila jumatano kuhubiri sikumoja injili ikamnasa kama umeme, akaingia line akampa Yesu Kristo Maisha yake kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yake kama wanavyosema wenyewe wanaoenda Mbinguni!

Safari ya Kwenda Mbinguni ya Azonto ikaanza hapo form5, aliokokea UKWATA (Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania)… unajua pale shuleni Tambaza kulikuwa na walokole wa aina mbili, wale wa waliookoka wa dhehebu la Lutheran walijiita UKWATA, wale wa madhehebu ya walokole walijiita JUWAKWATA lakini Azonto alikuwa UKWATA, akakaa kaa UKWATA weee alipoona kiu na njaa ya haki inazidi kujaa ndani yake akaona UKWATA hapamtoshi akaamua kuhamia JUWAKWATA,akawa anasali huko…

Nikisema Kiu na njaa ya Haki namaanisha hivi, “unapookoka ukiwa bado mchanga kiimani, unatamani mambo ya Yesu uyajue yote ingawa inachukua muda kuyajua yote ya Ufalme wa Mbinguni lakini ndani yako unakuwa na kiu fulani ya kujua mambo ya haki ya ufalme wa Mungu wa Mbinguni, yaani mambo ya Yesu Kristo”
Na hakuna watu wanaojua kuyaelezea hayo mambo ya Ufalme wa Mungu kama walokole!

Injili ya Yesu Kristo ikamkolea huko JUWAKWATA, akakaribishwa sasa kwenye makanisa ya kilokole, mwanzo alisitasita ila tulipoingia form 6 Azonto alihamia makanisa ya walokole ingawa yeye alikuwa Mlutheri!

Nilipomwuliza kwanini unahama dhehebu lako ulilolelewa na wazazi wako, akanijibu Biblia imesema; “Tokeni Mkatengwe nao – 2 Korintho 6:17”

Nilipomwuliza kwanini unataka kutengwa na watu waliokulea tangu huna akili mpaka sasa, akanijibu “Mambo ya Ufalme wa Mungu ni magumu kuyaelewa ukiwa kimwili, unahitaji imani kama mtoto mdogo kuyaelewa lakini ni marahisi sana kama utajaliwa Neema ya Mungu”

Mimi nikanyamaza, shule ikaendelea Azonto akaanza kuhubiri sana pale shuleni, shule nzima ikamjua wakawa wanamwita Mchungaji Azonto maana alikuwa mwanaume.

Test tukifanya anafaulu ila sio saaana kama ambavyo alikuwa hajaokokaga, kabla hajaokoka Azonto alikuwa na akili mnooo, alikuwa anapataga A akifeli sana B

Alipookoka akaanza kuchezea kwenye C na D, tukamkalisha chini tukamsihi Azonto naona kama unasahau wajibu wako wa sasa, unasahau shule unashikamana na mambo ya kuhubiri unaonaje umalize kwanza form 6 alafu matokeo yakitoka ukasomee Uchungaji?

Azonto hakuelewa, akaendelea na kupiga Gombo (Gombo – Neno la Mungu).

Shule ikamalizika, ikaisha kila mtu akarudi makwao kusubiria matokea ya form 6 yatoke tuanze chuo, majibu ya form 6..

Majibu ya form 6 yalipotoka mimi binafsi nilikuwa nataka kujua Azonto kapata divisheni ngapi? Maana yale mahubiri yake bwana ukiyasikiliza unaweza kuona kama maisha ni marahisi hasa ya Kimasomo ila kwenye uhalisia doh unaweza ukaangukia pabaya!

Sikunyingine anakwambia hasomi masomo kabisa Mungu anamuonyesha kwenye maono majibu, sikunyingine anasema Malaika kamtokea anamfundisha anakuja anafanya mitihani akiwa hajasoma kabisa, siku nyingine anasema palepale kwenye mitihani Malaika wanakujaga wanampaga majibu anajaza,ila matokeo yakija tunashangaa anapataje C wakati watenda dhambi wengine kama mimi tunapiga A za kufa mtu

Nikikueleza mimi na Azonto tulikuwa tunaakili darasani tunashindana kufaulu, tunashindana kupata A nyingi nadhani utanielewa kuwa Azonto alikuwa mshikaji wangu sana… ndio alijaribu kunivuta kwenye dhehebu lake lakini sikuona haja ya kuhamia, hata mimi nampenda sana Yesu lakini shule ni shule bwana asikwambie mtu!

Sikunyingine analala mkesha ijumaa Kanisani kwao alafu jumatatu kuna Mitihani ya Mock, hapo hajasoma, majibu yakitoka anapata D. ukimwuliza mbona unashuka sana Azonto anakwambia ni majaribu, shetani ananipima imani yangu..

Sasa kwenye mitihani ya Taifa bwana huwezi amini, Azonto alishinda kanisani, ijumaa,jumamosi, jumapili kafunga siku 3 kavu hali, hanywi anasali tu, hapo jumatatu ni Mtihani wa Taifa! Doh Imani kama ya Azonto sikuwahi kuiona nadhani mwara ya mwisho niliisomakwa Mtume Petro, Yohana kwenye Ufunuo wa Yohana na Yesu Kristo Mwenyewe!

Jumapili jioni akarudi kwao akanywa uji, akalala akaamka saa 3 akaanza kusoma!

Hapo kesho yake kuna mtihani wa taifa saa 2 kamili asubuhi, alipokuja kunieleza baada ya kumaliza mitihani sikuamini!

Na mitihani yote aliifanya na aliwahi darasani kila mtihani na tukamaliza pamoja

Siku ya kumaliza pepa kila mwanafunzi alikuwa anasheherekea kivyake pale shuleni, wengine wanavunja chupa, wengine wanatukana, wengine wanaimba, wengine wanakatika bolingo, wengine wanasifu na kuabudu,
Azonto alianguka kifudifudi anasujudu na kuabudu kwa machozi, yani kama ingekuwa enzi za simu za smart mbona mitandao ya kijamii kama whatsapp wangeinjoy video za kufowadi!

Sasa matokeo yametoka, nikaenda mpaka shuleni nikakuta matokeo bado hawajabandika wakaniambia niende baraza la mitihani wameshabandika, nikaondoka mdogo mdogo mpaka pale bamaga baraza la mitihani.

Nakutana na watoto wa Tambaza kibao wamekuja kuangalia matokeo, wengine wanalia wamepata divishen 0, wengine 4, wengine 3 wengine wamefaulu wana divishen 2 wengine wana divishen 1, doh hali ilikuwa mbaya sana, nikaingiwa na hofu kubwa, hata kumwangalia Azonto nikashindwa nikaanza kuangalia matokeo yangu … kuchungulia matokeo yangu nina divishen 1 ya mwishooo, doh nilisalije mieee! Roho ilipumua puuuuuuu! Huku najipepea nikasema afadhali sasa naingia chuo, nikiwa katika kufurahi nikamkumbuka Azonto bwana, kuangalia eh ana divishen 4 ya mwisho anaangukia kwenye divishen 0 yani nilimhurumia jamaani, Azonto, mtu wa kupata Divishen 1 ya kwanza leo anaangukia pua inakuwaje?

Nikaondoka nimesononeka juu yake badala ya kufurahia juu yangu ufaulu wangu, nikamuwazia ataenda wapi huenda ataenda uchungaji jamani, doh Azonto maskini wee!

Sikumwonaga tena Azonto mpaka nilipoenda kusoma Chuo Cha IFM, akaja na yeye akaanza kusoma Certificate, akawa anafaulu, alipomaliza Certificate akaanza mwaka wa 1, anaendelea vile vile na mambo yake ya kuhubiri, kuombea watu, kuwatia moyo, na pale IFM wakaanza kumjua wakawa wanamwita Pastor Azonto!

Kwenye ibada za kusali alikuwa anasali CASFETA, yeye ndio muhubiri, sikufichi Azonto alikuwa muhubiri mzuri sana, unaweza ukaokoka hapo hapo, alikuwa anaombaaaaa, ohoooo! Akianza kuomba hapa unadhani Mungu anafungua Mbingu anashukaaa!

Watu wanalipukaje mapepo, akiombea watu wanaponaaaa!
Ila shule yetu ile ya IFM usiposoma tu jiandae kufeli, kila mwaka Azonto alikuwa anakula Supplimentary, doh Azonto kweli hakutaka kujifunza kwenye makosa ya Form 6.

Shule yangu ya IFM ikaisha nikamuacha bado anasoma, nikaingia kazini nikafanya miaka 2 Benki, sikumoja nikiwa nawasiadia wateja na yeye akaja ana shida ya kibenki, tukaongea sana nikaamua kumtoa lanchi maana alikuja mida ya lunch time, nikamwuliza maendeleo yake maana alikuwa amechokaaa mbayaa yani ukimwangalia utamnunulia chakual cha mwezi mzima, akaniambia shule alidisko mwaka wa mwisho, akaondoka akaenda kusomea uchungaji na sasa ameshapewa Kanisa huko kwa walokole amekuwa Mchungaji msaidizi, nikakaribishwa Kanisani kwake nikamshukuru nikimuahidi nakuja lakini mpaka leo mwaka wa 18 sijafikaga Kanisani kwake…

Sasa leo baada ya miaka 18, nakutana nae hapa New York Mjini Marekani nikashangaa sana, nikataka kujua kilichomleta Marekani ni Uchungaji ule ule au? Maana sio kwa kile kitabu alichokuwa anasoma kilichoandikwa Why Men Love Bitches alafu alikuwa anakunywa wine!

AZONTO: “Heeee! Wewe? Upooo? Unafanya nini huku New York?”
Lisa ni wewe au naota? Oh Mungu wangu wee! Huku anacheka akainuka anikumbatie, tukakumbatiana!

LISA: nipo Azonto jamaani miaka 18 sijakuona Mchungaji

AZONTO: akacheka sana, mchungaji tena?

LISA: Ndio Mchungaji, mara ya mwisho tuliongea… (kabla hajamalizia sentensi yangu akanistopisha)

AZONTO: Hapana mimi sio Mchungaji tena

LISA: kweli? Imekuwaje?

AZONTO: Mambo mengi yametokea nikaona niachane na Uchungaji

LISA: Na Yesu je? Maana kabla haujawa Mchungaji ulimpata kwanza Yesu

AZONTO: akanyamaza

LISA: vipi mbona kimya? Sikuelewi Marekani umekuja kufanyaje? Na mbona unakunywa wine, na kusoma vitabu vya wahuni? Au unataka kuoa?

AZONTO: Hapana sitaki kuoa, mambo mengi yametokea Lisa ndugu yangu, naona na wewe umependeza kweli, umeshaolewa? Marekani umekuja kufanyaje Lisa

LISA: Nimeletwa kikazi

AZONTO: Bado unafanya kazi Benki?

LISA: Ndio ila ile banki nilishahama nimehamia benki nyingine, sasa nimekuwa Benki meneja

AZONTO: Hongera sana, Mungu amekubarikia sana, una watoto wangapi Lisa?

LISA: Nina watoto wakike mapacha 2 na mmoja wa kiume… Mke wa Mume Mmoja

AZONTO: Doh, akaanza kulia hapo hapo wazungu wanashangaa,

LISA: vipi tena Azonto mbona unalia tena kuna nini? Nyamaza tafadhali watu wanatushangaa plz nyamaza ndugu yangu, tukaamua kuhama kile kijiwe tukaenda Kukaa Park… tumekaa Azonto haongei, machozi yanamtoka masikini, muda kweli ulikuwa unaenda sana, ikabidi nianze kumwuliza shida nini maana muda unaenda na mimi kesho yake nasafiri kurudi Bongo… ndio Azonto akaanza kufunguka

AZONTO: Kusema kweli inauma, mambo niliofanyiwa Kanisani yanaumiza mno, najua mara ya mwisho tulionana nikamwambia nimekuwa Mchungaji Msaidizi

LISA: ndio, sasa shida ikawaje!?

AZONTO: Mchungaji Kiongozi niliekuwa namsaidia kazi alinizunguka sana, nilikuja kupata msichana niliependana nae nje ya lile Kanisa lake lakini ni Mlutheri akanikatalia akasema huyu sio wa imani yetu atakusumbua akamkataa.

Nikaja nikampata mwingine wa pale kanisani akanikatalia,kila nikipata msichana wa kuoana nae ananikatalia

Mikaja kugundua kuwa kumbe wale wanawake wa pale Kanisani aliokuwa ananikatalia walikuwa wanawake wake anatembea nao kwa siri na huku na mke na watoto pale pale Kanisani

Alikuwa anatembea na wajane pale kanisani, mabinti wasioolewa sikujua saa ngapi, mabinti wengi pale wametoa mimba zake.

Upande wa Shekeli (Sadaka) sasa zote alikuwa anachukua yeye mimi nnalipwa laki 2 kwa mwezi yeye anakusanya million 5 sadaka kwa mwezi.
Kukiwa na ujenzi wa Kanisa hela zote anazichukua yeye!

LISA: kwahiyo umemuacha Yesu kwasababu ya Sadaka upewi nyingi au kwasababu Mchungaji ametembea na wanawake wote Kanisani?

AZONTO: Sio kweli usemayo,

LISA: Kwani aliekuokoa ni Yesu au Mchungaji?

AZONTO: Yesu

LISA: sasa kwanini umemwacha Yesu? Mimi nakujua unampenda sana Yesu, sasa kwanini upendo wako kwa Mungu utengwe na Sadaka za Kanisani na Mademu wa Mchungaji Kiongozi?

AZONTO: Ngoja basi nikueleze Mama au niache?

LISA: Endelea!

AZONTO: Siku moja Mchungaji kiongozi akaniita ofisini, akaniambia kuna binti amemwona ambae ananifaa, ameshamchunguza sana ameona anaweza kulea huduma yangu ya kichungaji!

Akamleta binti, alikuwa mdogo wa miaka 25 na mimi nina miaka 33, kweli ukimwangalia ni binti mzuri sana anavutia, kwa maelezo ya Mchungaji Kiongozi ameokoka msomi mwenzangu alisoma CBE, ameajiriwa Benki miaka 3 kazini, akaniambia huyu Binti anakufaa sana .

Nilipomwuliza amemtoa wapi akasema ni mtoto wa shangazi yake kijijini kwahiyo sikuwa na neno.

Kweli baada ya ule utambulisho ndani ya miezi 2 tukaoana, Mchungaji akanibadilishia mshahara nikawa nalipwa milioni 2 na nyumba ya kupanga nalipiwa kila mwezi na usafiri nikapewa, nikaona Baraka ndio hizi Mungu ameniangushia.

LISA: ah Hongera sana kumbe ulikuwa unalipwa kama Meneja wa benki ee?

AZONTO: Ngoja niendelee kwanza

LISA: Enhe endelea nakusikiliza

AZONTO: Maisha ya ndoa yakaendelea, mwezi wa 1, mwezi wa 2, mwezi wa 3 mke wangu akapata Mimba

LISA: Oh jamani kwahiyo mna mtoto?

AZONTO: si bora ningekuwa na mtoto sasa,

LISA: Heee imekuwaje tena?

AZONTO: unajua tangu nimuoe Yule binti kila tukiwa tunaingia kwenye unyumba, anakataa anasingizia tumbo, sikuelewa ile mimba aliipata wapi?
Nilipoanza kuuliza ameipata wapi akawa mkali sana, siku inayofuata nikaitwa na Mchungaji Kiongozi

LISA: Enhe?

AZONTO: Akanieleza kuhusu ugomvi wangu na mke wangu akaanza kunitia moyo tusigombane na mambo ya kichungaji ya kufanya councelling kibao, lakini ujue Lisa mimi sio mlevi, nikitaka kumjua mke wangu najua hapa nimemjua kwahiyo nilikuwa na uhakika kabisa kuwa ile mimba sio yangu, ila kwasababu boss kasema nivumilie nikavumilia

LISA: Uuuwi! Enhe?

AZONTO: Basi baada ya yale maongezi nikarudi nyumbani nikaendelea kulea mimba mpaka mtoto alipozaliwa, akazaliwa mtoto mwanaume, lakini hafanani name kabisa, nikasema huenda ni mchanga akikua atanifanania na unajua watoto wa kiume hufanana na mama zao

LISA: Enhe?

AZONTO: Basi mtoto akakua alipofika mwaka mmoja, mchungaji Kiongozi akatuita na mke wangu, tukajua anatuitia habari ya kubariki mtoto si unajua walokole hatunaga ubatizo wa watoto wadogo tunawabariki tu kama Yesu!

LISA: Sawa, Enhe?

AZONTO: Kwenda kumsikilizza akasema namtaka mumlete mtoto leo usiku hapa kanisani, saa 5 nanusu usiku.

Sisi tutakubali, kweli usiku yake tukampeleka tukijua labda ni maombi, kufika hamna mlinzi hamna nini, akasema mleteni mtoto mara nikaona panga pembeni, nikauliza panga la nini.

Mchungaji Kiongozi akasema huyu mtoto lazima tumtoe kafara
Nikauliza kwanini?

Akasema tumekosea masharti huyu mtoto hakuwa wa kwangu alikuwa wake, na huyu mke wangu alikuwa ni mpenzi wake wa miaka mingi alimpeleka kijijini baada ya kuoa akamjengea na nyumba akawa anakaa huko, baada ya kuona anataka kuja mjini wakaelewana aolewe na mimi ili wao kuwa karibu zaidi hapa Dar

Nilipouliza masharti gani tumekosea akasema tumelala pamoja baada ya kujifungua mtoto, masharti yetu hayaruhusu hivyo

Kuulizia masharti gani, akampa mtoto mke wangu akaenda kufungua pale kwenye maji ya ubatizo, akaniambia hapa ndio tunatoaga watoto kafara, watu wakibatizwa tunanasa hatima zao, tunakuwa tunacheza nazo, ndio unaona walokole wengi wanateseka hawasogei mbele wanakaa hapo miaka na miaka mpaka watakapotii masharti kama hayo nayotaka kukuambia!

Nilipouliza masharti gani akasema yeye ni mchawi, na kwenye kikao chao cha uchawi mke wangu ni malkia msaidizi na hii ni zamu yake ya kutoa kafara mwane, kwahiyo lazima usiku huu ifanyike la sivyo kanisa litakosa waumini watapungua sana.

Akasema ndio mimi ni Mchungaji mwenye upako mkubwa unadhani upako nautoa wapi? Kwa shetani kuzimu, shetani ndio anajaza kanisa, jina la Yesu tunalitumia tu kama kivuli lakini ushindi ni kwa shetani.

Si unajua kuwa Mungu huwa anachelewa na mimi ninataka nifanikiwa sasa!

Nilichoka Lisa, sikuamini, nguvu zikaniisha nikazimia hapo hapo, kuja kuzinduka nipo hospital na mke wangu pembeni, nilipomwuliza mtoto yuko wapi akaniuliza mtoto gani?

Nikamwambia tumezaa watoto akanijibu umechanganyikiwa hatuna mtoto hatujawahi kupata mtoto. Niliporudi nyumbani nikakuta nyumba imebadilika sana makochi mapya, pasafi Tv mpya, nikashangaa vimewekwa saa ngapi

Nikaingia kulala kwanza nilipoamka mke wangu akaniletea supu, kuiangalia supu kuna kidole cha mtoto!

Nikasikia kutapika ghafla nikatapikia kile chakula, mke wangu akakimbia kuondoa chakula, akasafisha akarudi jikoni mimi nikaenda kukaa sebuleni, nikawaza sana nafanyaje, nikisema niende kwenye sheria sina uthibitisho nafanyaje?

Nikawaza na kuwazua, nikampigia simu dada yangu aje haraka pale nyumbani, akaja nikamwongelesha kilugha maana mkewangu sio wa lugha yangu akanielewa, akalala pale pale, asubuhi mke wangu alipoenda kazini nikapaki mizigo yangu yote nikampa dada, akaondoka nayo mpaka kwake, nikaiangalie ile nyumba nikaomba Mungu anisamehe
Nikaingia kwenye kabati nikaanza kumpekua mke wangu, nikakuta ameweka pesa nyingi sana thamani ya million 10 sikuelewa alipozitoa ila nilikuwa nakumbuka kuwa majuzi mtoto alitolewa kafara pale Kanisani.. nikachukua Milion 10 nikaondoka mpaka Kanisani nikammkuta Mchungaji Kiongozi hayupo, nikamwachia secretary ampe mchungaji kiongozi funguo yangu nikaondoka kurudi kwa dada.

Dada akanitoa pale kwake maana mke wangu alikuwa anapajua kwa dada yangu lakini sio kwa mke wangu, akanipeleka kwa mdogo wangu wa mwisho Kiluvya, kuishi huko, akaniambia kesho kutwa uende Ubalozi wa Marekani nimekuandalia documents nimeshazipeleka wanakusubiria ufanye interview, kweli Kesho Kutwa nikaenda nikafanya Interview, wakaniuliza naenda kusomea nini nikawaambia uchungaji wakanigongea visa wakaniambia siku fulani nenda ofisi fulani ya DHL ukachukue Visa yako itakuwa tayari…

kweli siku nilioenda nikachukua Visa, mdogowangu akampigia Dada, Dada akamwambia mwambie Azonto kesho saa 2 usiku aje Airport nitamtuma Dereva wa ofisini kwangu ampelekee tiketi Airport maana mimi nikiondoka hapa nitafuatiliwa

Maana ameshakuja mke wake Azonto na mchungaji wake kumwulizia, namtakia safari njema na masomo mema tutawasiliana akifika New York.

LISA: Doh pole sana Azonto, sasa ukasafiri salama?

AZONTO: Ndio nilisafiri salama sikuwaona Mchungaji wala mke wake na zile hela milioni 10 niliondoka nazo ndio nikaja nazo kuanza maisha huku maana sister ndio analipia nusu Ada si unajua uchungaji tunapewa ufadhili?

LISA: ndio, kwahiyo hapa New York wewe ni Mgeni?

AZONTO: Nimeshakaa Miaka 3 hapa New York

LISA: Unasoma Uchungaji kweli au ilikuwa geresha?

AZONTO: Uchungaji nilishamaliza mwaka 1, nikaaa kufanya kazi kwenye hizi NGO za Kanisani wakanipenda ndio wakaniajiri so nina work permit ilionifanya nibaki Marekani na kuongezewa Visa!

LISA: Jamaa pole sana

AZONTO: Asante Lisa

LISA: Najua sasa hautatamani kuoa tena

AZONTO: Hapana nimeshaoa, Mmarekani Mweusi mwaka jana na tuna watoto 2 wakike na kiume

LISA: Oh! Hongera Mno rafiki yangu, Yule Mchungaji Free Mason na Mkeo wa Bongo wanaendeleaje?

AZONTO: Sijawasikia tena, ila mke wangu alishakufaga, aligongwa na gari akiwa anavuka barabara alinieleza sister, lakini mimi nilijua kafara ya Mchungaji Kiongozi imetembea

LISA: Jamaan jamaan jamaan, Azonto nakufahamu ulikuwa unampenda Mungu sana, kwanini umeacha?

AZONTO: Nachukua likizo kwa walokole, ila Mungu sijamuacha nampenda sana ila mimi sio mchungaji kabisa ingawa nimesomea na nafanya kazi kwenye Taasisi moja yapo ya Kanisa huku New York

LISA: Doh jamani jamani jamani pole mno! Mwisho wa siku Mungu amekubarikia maisha yanaenda umeshaoa na una watoto 2

AZONTO: Ni kweli tangu Nimekanyaga Marekani sijawahi tena kuhangaika kimaisha mambo yangu yanaenda kama miujiza, mateso yooote nilioyapata Nyumbani huku siyaoni tena, nikigusa kitu kinaenda, popote napoweka mkono wangu kufanya jambo kinafanikiwa mara 100, sasa hivi nimefungua restaurant na mke wangu ndio pale ulipokuja ukanikuta nakunywa wine!

LISA: Oh jamaan! Lakini kwanini unakunywa pombe? Pombe si dhambi au?

AZONTO: Nimekwambia nimechukua likizo kwa Walokole lakini sio kwa Yesu, Yesu ninaemjua aligeuza maji kuwa wine

LISA: sio wine ni mvinyo kama soda, juice

AZONTO: My dia, wine ni wine, Yesu angegeuza kuwa juice ingeandikwa juice lakini wakaandika wine
Mtume Paulo kwenye agano Jipya alimshauri Timotheo anywe mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake
Mimi sinywi pombe kabisa, lakini nakunywa wine
Hiki kitabu nakisoma kwasababu kuna mtu namfanyia councelling anapenda sana Malaya ndio nikakiona hiki kitabu hapo book shop juzi nikaamua kukinunua, nikisome nione!

LISA: Bado unampenda Yesu Kweli?

AZONTO: Kwa moyo wangu wote, akili zangu zote, mawazo yangu yote na kila kitu nmilicho nacho, sisali tena kwa walokole nasali Lutherani kwangu kwa zamani walipokuwa wanasali wazazi wangu!

LISA: How are you lakini?

AZONTO: Am very fine Lisa, am very Happy Lisa, nimeshaingia kwenye Promise Land yangu, Mungu akipenda mwakani naweza kupewa Green Card ndio nafuatilia Process zake!

LISA: Kweli ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu na wenye nguvu ndio wewe, watu wangepitia maisha yako wangeshamuacha Mungu na Yesu Muda sana!
AZONTO: Lakini sio mimi, mimi niliamua tangu nikiwa mdogo form 5 na namshukuru Mungu nimepitia maisha niliopitia sawa na neno la Mungu linalosema, Marko 10: 25, “ Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu”
Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Mathayo 7:14
Yesu niliemchagua Form 5 ni wa Kwangu, ninampenda sana na sita muacha milele yote mpaka kufa. Kuhubiri sijaacha naendelea kumtangaza mpaka pumzi yangu ya mwisho!

LISA: Nikamwangalia Azonto nikampenda, kweli watakatifu Duniani bado wapo, Azonto alikuwa amenenepa, amependezaaa, amenawiri na rangi yake imebadilika anaung’aa, amevaa Tshirt lake limeandikwa
JESUS FREAK!

ITAENDELEA IJUMAA KUU HII TAR 19 APRIL 2019 SAA 5 ASUBUHI YA TANZANIA
 
Naliona tatizo kwenye hii simulizi! Hamna pahala popote na Ubalozi wowote wa U.S unatoa VISA kwa DHL saa ingine mujipange wa TZ sio mazuzu
ENGLISH: JESUS FREAK
SWAHILI: KITUKO WA YESU

SEHEMU YA 1
A. NJIA ILE NI NYEMBAMBA IENDAYO UZIMANI

MWAKA 2018:
Natembea duka moja hadi jingine naangalia vitu vya kununua (zawadi) za kupeleka nyumbani kwa familia yangu mitaa ya New York City Mjini Marekani, baada ya masaa mengi ya kuzura na kuchoka nikaamua kwenda kwenye mgahawa nipate kituliza tumbo.

Nikafika, nikakaa, akaja mhudumu nikaagiza nachohitaji nikaendelea kusubiria huku natumia simu yangu kuangalia mitandao ya kijamii kilichojiri huko Instagram, Facebook, Snapchat, Whatsapp, Twitter na Tumblr… nilipochoka nikaanza kujipiga selfie ili ni-upload picha Instagram, si unajua tena sisi watoto wa mitandaoni kila sehemu unataka kupiga picha na wewe uonekane umo.

Katika ku-edit picha nilizojipiga nikaona kwenye picha mtu amekaa kiti cha tatu nyuma yangu kama namfahamu. Kugeuka na kuangalia nyuma kweli ni yeye, sikuamini, yeye hakuniona ila mimi nilimuona, sikuamini nakwambia huyu mtu mimi namfahamu miaka mingi tena kuliko maelezo, amefikaje New York Mjini sikuelewa, kweli?

Nikaondoka kwenye kiti changu nikamfuata nikakaa mbele yake maana alikuwa amekaa mwenyewe anasoma kitabu cha hadithi, akageuka kuangalia huyu ni nani amekuja kukaa mbele yangu, kuniangalia hakuamini,
“Heeee! Wewe? Upooo? Unafanya nini huku New York?”
Huyu Mtu alikuwa anaitwa Azonto, ndio Azonto ndio jina lake,la kuzaliwa, la shuleni, la Kanisani kila sehemu ni Azonto labda awe amebadilisha miaka hii lakini anaitwa Azonto.

NAOMBA NIKUELEZE AZONTO NI NANI;
MWAKA 2000
Azonto nilisoma nae shule ya Sekondari Tambaza, jijini Dar es Salaam, tulisoma Darasa moja form 5 na 6…Baada ya hapo tukaenda wote kusoma IFM hapo Posta ya Zamani.

Azonto aliokokaga tulipokuwaga form 5 bwana, aliokokokea kule kwenye vipindi vya dini, wakati walimu wa dini wakiwa wanakuja kila jumatano kuhubiri sikumoja injili ikamnasa kama umeme, akaingia line akampa Yesu Kristo Maisha yake kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yake kama wanavyosema wenyewe wanaoenda Mbinguni!

Safari ya Kwenda Mbinguni ya Azonto ikaanza hapo form5, aliokokea UKWATA (Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania)… unajua pale shuleni Tambaza kulikuwa na walokole wa aina mbili, wale wa waliookoka wa dhehebu la Lutheran walijiita UKWATA, wale wa madhehebu ya walokole walijiita JUWAKWATA lakini Azonto alikuwa UKWATA, akakaa kaa UKWATA weee alipoona kiu na njaa ya haki inazidi kujaa ndani yake akaona UKWATA hapamtoshi akaamua kuhamia JUWAKWATA,akawa anasali huko…

Nikisema Kiu na njaa ya Haki namaanisha hivi, “unapookoka ukiwa bado mchanga kiimani, unatamani mambo ya Yesu uyajue yote ingawa inachukua muda kuyajua yote ya Ufalme wa Mbinguni lakini ndani yako unakuwa na kiu fulani ya kujua mambo ya haki ya ufalme wa Mungu wa Mbinguni, yaani mambo ya Yesu Kristo”
Na hakuna watu wanaojua kuyaelezea hayo mambo ya Ufalme wa Mungu kama walokole!

Injili ya Yesu Kristo ikamkolea huko JUWAKWATA, akakaribishwa sasa kwenye makanisa ya kilokole, mwanzo alisitasita ila tulipoingia form 6 Azonto alihamia makanisa ya walokole ingawa yeye alikuwa Mlutheri!

Nilipomwuliza kwanini unahama dhehebu lako ulilolelewa na wazazi wako, akanijibu Biblia imesema; “Tokeni Mkatengwe nao – 2 Korintho 6:17”

Nilipomwuliza kwanini unataka kutengwa na watu waliokulea tangu huna akili mpaka sasa, akanijibu “Mambo ya Ufalme wa Mungu ni magumu kuyaelewa ukiwa kimwili, unahitaji imani kama mtoto mdogo kuyaelewa lakini ni marahisi sana kama utajaliwa Neema ya Mungu”

Mimi nikanyamaza, shule ikaendelea Azonto akaanza kuhubiri sana pale shuleni, shule nzima ikamjua wakawa wanamwita Mchungaji Azonto maana alikuwa mwanaume.

Test tukifanya anafaulu ila sio saaana kama ambavyo alikuwa hajaokokaga, kabla hajaokoka Azonto alikuwa na akili mnooo, alikuwa anapataga A akifeli sana B

Alipookoka akaanza kuchezea kwenye C na D, tukamkalisha chini tukamsihi Azonto naona kama unasahau wajibu wako wa sasa, unasahau shule unashikamana na mambo ya kuhubiri unaonaje umalize kwanza form 6 alafu matokeo yakitoka ukasomee Uchungaji?

Azonto hakuelewa, akaendelea na kupiga Gombo (Gombo – Neno la Mungu).

Shule ikamalizika, ikaisha kila mtu akarudi makwao kusubiria matokea ya form 6 yatoke tuanze chuo, majibu ya form 6..

Majibu ya form 6 yalipotoka mimi binafsi nilikuwa nataka kujua Azonto kapata divisheni ngapi? Maana yale mahubiri yake bwana ukiyasikiliza unaweza kuona kama maisha ni marahisi hasa ya Kimasomo ila kwenye uhalisia doh unaweza ukaangukia pabaya!

Sikunyingine anakwambia hasomi masomo kabisa Mungu anamuonyesha kwenye maono majibu, sikunyingine anasema Malaika kamtokea anamfundisha anakuja anafanya mitihani akiwa hajasoma kabisa, siku nyingine anasema palepale kwenye mitihani Malaika wanakujaga wanampaga majibu anajaza,ila matokeo yakija tunashangaa anapataje C wakati watenda dhambi wengine kama mimi tunapiga A za kufa mtu

Nikikueleza mimi na Azonto tulikuwa tunaakili darasani tunashindana kufaulu, tunashindana kupata A nyingi nadhani utanielewa kuwa Azonto alikuwa mshikaji wangu sana… ndio alijaribu kunivuta kwenye dhehebu lake lakini sikuona haja ya kuhamia, hata mimi nampenda sana Yesu lakini shule ni shule bwana asikwambie mtu!

Sikunyingine analala mkesha ijumaa Kanisani kwao alafu jumatatu kuna Mitihani ya Mock, hapo hajasoma, majibu yakitoka anapata D. ukimwuliza mbona unashuka sana Azonto anakwambia ni majaribu, shetani ananipima imani yangu..

Sasa kwenye mitihani ya Taifa bwana huwezi amini, Azonto alishinda kanisani, ijumaa,jumamosi, jumapili kafunga siku 3 kavu hali, hanywi anasali tu, hapo jumatatu ni Mtihani wa Taifa! Doh Imani kama ya Azonto sikuwahi kuiona nadhani mwara ya mwisho niliisomakwa Mtume Petro, Yohana kwenye Ufunuo wa Yohana na Yesu Kristo Mwenyewe!
Jumapili jioni akarudi kwao akanywa uji, akalala akaamka saa 3 akaanza kusoma!
Hapo kesho yake kuna mtihani wa taifa saa 2 kamili asubuhi, alipokuja kunieleza baada ya kumaliza mitihani sikuamini!
Na mitihani yote aliifanya na aliwahi darasani kila mtihani na tukamaliza pamoja

Siku ya kumaliza pepa kila mwanafunzi alikuwa anasheherekea kivyake pale shuleni, wengine wanavunja chupa, wengine wanatukana, wengine wanaimba, wengine wanakatika bolingo, wengine wanasifu na kuabudu,
Azonto alianguka kifudifudi anasujudu na kuabudu kwa machozi, yani kama ingekuwa enzi za simu za smart mbona mitandao ya kijamii kama whatsapp wangeinjoy video za kufowadi!

Sasa matokeo yametoka, nikaenda mpaka shuleni nikakuta matokeo bado hawajabandika wakaniambia niende baraza la mitihani wameshabandika, nikaondoka mdogo mdogo mpaka pale bamaga baraza la mitihani.

Nakutana na watoto wa Tambaza kibao wamekuja kuangalia matokeo, wengine wanalia wamepata divishen 0, wengine 4, wengine 3 wengine wamefaulu wana divishen 2 wengine wana divishen 1, doh hali ilikuwa mbaya sana, nikaingiwa na hofu kubwa, hata kumwangalia Azonto nikashindwa nikaanza kuangalia matokeo yangu … kuchungulia matokeo yangu nina divishen 1 ya mwishooo, doh nilisalije mieee! Roho ilipumua puuuuuuu! Huku najipepea nikasema afadhali sasa naingia chuo, nikiwa katika kufurahi nikamkumbuka Azonto bwana, kuangalia eh ana divishen 4 ya mwisho anaangukia kwenye divishen 0 yani nilimhurumia jamaani, Azonto, mtu wa kupata Divishen 1 ya kwanza leo anaangukia pua inakuwaje?

Nikaondoka nimesononeka juu yake badala ya kufurahia juu yangu ufaulu wangu, nikamuwazia ataenda wapi huenda ataenda uchungaji jamani, doh Azonto maskini wee!

Sikumwonaga tena Azonto mpaka nilipoenda kusoma Chuo Cha IFM, akaja na yeye akaanza kusoma Certificate, akawa anafaulu, alipomaliza Certificate akaanza mwaka wa 1, anaendelea vile vile na mambo yake ya kuhubiri, kuombea watu, kuwatia moyo, na pale IFM wakaanza kumjua wakawa wanamwita Pastor Azonto!
Kwenye ibada za kusali alikuwa anasali CASFETA, yeye ndio muhubiri, sikufichi Azonto alikuwa muhubiri mzuri sana, unaweza ukaokoka hapo hapo, alikuwa anaombaaaaa, ohoooo! Akianza kuomba hapa unadhani Mungu anafungua Mbingu anashukaaa!
Watu wanalipukaje mapepo, akiombea watu wanaponaaaa!
Ila shule yetu ile ya IFM usiposoma tu jiandae kufeli, kila mwaka Azonto alikuwa anakula Supplimentary, doh Azonto kweli hakutaka kujifunza kwenye makosa ya Form 6…

Shule yangu ya IFM ikaisha nikamuacha bado anasoma, nikaingia kazini nikafanya miaka 2 Benki, sikumoja nikiwa nawasiadia wateja na yeye akaja ana shida ya kibenki, tukaongea sana nikaamua kumtoa lanchi maana alikuja mida ya lunch time, nikamwuliza maendeleo yake maana alikuwa amechokaaa mbayaa yani ukimwangalia utamnunulia chakual cha mwezi mzima, akaniambia shule alidisko mwaka wa mwisho, akaondoka akaenda kusomea uchungaji na sasa ameshapewa Kanisa huko kwa walokole amekuwa Mchungaji msaidizi, nikakaribishwa Kanisani kwake nikamshukuru nikimuahidi nakuja lakini mpaka leo mwaka wa 18 sijafikaga Kanisani kwake…

Sasa leo baada ya miaka 18, nakutana nae hapa New York Mjini Marekani nikashangaa sana, nikataka kujua kilichomleta Marekani ni Uchungaji ule ule au? Maana sio kwa kile kitabu alichokuwa anasoma kilichoandikwa Why Men Love Bitches alafu alikuwa anakunywa wine!

AZONTO: “Heeee! Wewe? Upooo? Unafanya nini huku New York?”
Lisa ni wewe au naota? Oh Mungu wangu wee! Huku anacheka akainuka anikumbatie, tukakumbatiana!

LISA: nipo Azonto jamaani miaka 18 sijakuona Mchungaji

AZONTO: akacheka sana, mchungaji tena?
LISA: Ndio Mchungaji, mara ya mwisho tuliongea… (kabla hajamalizia sentensi yangu akanistopisha)
AZONTO: Hapana mimi sio Mchungaji tena
LISA: kweli? Imekuwaje?
AZONTO: Mambo mengi yametokea nikaona niachane na Uchungaji
LISA: Na Yesu je? Maana kabla haujawa Mchungaji ulimpata kwanza Yesu
AZONTO: akanyamaza
LISA: vipi mbona kimya? Sikuelewi Marekani umekuja kufanyaje? Na mbona unakunywa wine, na kusoma vitabu vya wahuni? Au unataka kuoa?
AZONTO: Hapana sitaki kuoa, mambo mengi yametokea Lisa ndugu yangu, naona na wewe umependeza kweli, umeshaolewa? Marekani umekuja kufanyaje Lisa
LISA: Nimeletwa kikazi
AZONTO: Bado unafanya kazi Benki?
LISA: Ndio ila ile banki nilishahama nimehamia benki nyingine, sasa nimekuwa Benki meneja
AZONTO: Hongera sana, Mungu amekubarikia sana, una watoto wangapi Lisa?
LISA: Nina watoto wakike mapacha 2 na mmoja wa kiume… Mke wa Mume Mmoja
AZONTO: Doh, akaanza kulia hapo hapo wazungu wanashangaa,
LISA: vipi tena Azonto mbona unalia tena kuna nini? Nyamaza tafadhali watu wanatushangaa plz nyamaza ndugu yangu, tukaamua kuhama kile kijiwe tukaenda Kukaa Park… tumekaa Azonto haongei, machozi yanamtoka masikini, muda kweli ulikuwa unaenda sana, ikabidi nianze kumwuliza shida nini maana muda unaenda na mimi kesho yake nasafiri kurudi Bongo… ndio Azonto akaanza kufunguka
AZONTO: Kusema kweli inauma, mambo niliofanyiwa Kanisani yanaumiza mno, najua mara ya mwisho tulionana nikamwambia nimekuwa Mchungaji Msaidizi
LISA: ndio, sasa shida ikawaje!?
AZONTO: Mchungaji Kiongozi niliekuwa namsaidia kazi alinizunguka sana, nilikuja kupata msichana niliependana nae nje ya lile Kanisa lake lakini ni Mlutheri akanikatalia akasema huyu sio wa imani yetu atakusumbua akamkataa,
Nikaja nikampata mwingine wa pale kanisani akanikatalia,kila nikipata msichana wa kuoana nae ananikatalia

Mikaja kugundua kuwa kumbe wale wanawake wa pale Kanisani aliokuwa ananikatalia walikuwa wanawake wake anatembea nao kwa siri na huku na mke na watoto pale pale Kanisani

Alikuwa anatembea na wajane pale kanisani, mabinti wasioolewa sikujua saa ngapi, mabinti wengi pale wametoa mimba zake
Upande wa Shekeli (Sadaka) sasa zote alikuwa anachukua yeye mimi nnalipwa laki 2 kwa mwezi yeye anakusanya million 5 sadaka kwa mwezi.
Kukiwa na ujenzi wa Kanisa hela zote anazichukua yeye!
LISA: kwahiyo umemuacha Yesu kwasababu ya Sadaka upewi nyingi au kwasababu Mchungaji ametembea na wanawake wote Kanisani?
AZONTO: Sio kweli usemayo,
LISA: Kwani aliekuokoa ni Yesu au Mchungaji?
AZONTO: Yesu
LISA: sasa kwanini umemwacha Yesu? Mimi nakujua unampenda sana Yesu, sasa kwanini upendo wako kwa Mungu utengwe na Sadaka za Kanisani na Mademu wa Mchungaji Kiongozi?
AZONTO: Ngoja basi nikueleze Mama au niache?
LISA: Endelea!
AZONTO: Siku moja Mchungaji kiongozi akaniita ofisini, akaniambia kuna binti amemwona ambae ananifaa, ameshamchunguza sana ameona anaweza kulea huduma yangu ya kichungaji!
Akamleta binti, alikuwa mdogo wa miaka 25 na mimi nina miaka 33, kweli ukimwangalia ni binti mzuri sana anavutia, kwa maelezo ya Mchungaji Kiongozi ameokoka msomi mwenzangu alisoma CBE, ameajiriwa Benki miaka 3 kazini, akaniambia huyu Binti anakufaa sana
Nilipomwuliza amemtoa wapi akasema ni mtoto wa shangazi yake kijijini kwahiyo sikuwa na neno..
Kweli baada ya ule utambulisho ndani ya miezi 2 tukaoana, Mchungaji akanibadilishia mshahara nikawa nalipwa milioni 2 na nyumba ya kupanga nalipiwa kila mwezi na usafiri nikapewa, nikaona Baraka ndio hizi Mungu ameniangushia.
LISA: ah Hongera sana kumbe ulikuwa unalipwa kama Meneja wa benki ee?
AZONTO: Ngoja niendelee kwanza
LISA: Enhe endelea nakusikiliza
AZONTO: Maisha ya ndoa yakaendelea, mwezi wa 1, mwezi wa 2, mwezi wa 3 mke wangu akapata Mimba
LISA: Oh jamani kwahiyo mna mtoto?
AZONTO: si bora ningekuwa na mtoto sasa,
LISA: Heee imekuwaje tena?
AZONTO: unajua tangu nimuoe Yule binti kila tukiwa tunaingia kwenye unyumba, anakataa anasingizia tumbo, sikuelewa ile mimba aliipata wapi?
Nilipoanza kuuliza ameipata wapi akawa mkali sana, siku inayofuata nikaitwa na Mchungaji Kiongozi
LISA: Enhe?
AZONTO: Akanieleza kuhusu ugomvi wangu na mke wangu akaanza kunitia moyo tusigombane na mambo ya kichungaji ya kufanya councelling kibao, lakini ujue Lisa mimi sio mlevi, nikitaka kumjua mke wangu najua hapa nimemjua kwahiyo nilikuwa na uhakika kabisa kuwa ile mimba sio yangu, ila kwasababu boss kasema nivumilie nikavumilia
LISA: Uuuwi! Enhe?
AZONTO: Basi baada ya yale maongezi nikarudi nyumbani nikaendelea kulea mimba mpaka mtoto alipozaliwa, akazaliwa mtoto mwanaume, lakini hafanani name kabisa, nikasema huenda ni mchanga akikua atanifanania na unajua watoto wa kiume hufanana na mama zao
LISA: Enhe?
AZONTO: Basi mtoto akakua alipofika mwaka mmoja, mchungaji Kiongozi akatuita na mke wangu, tukajua anatuitia habari ya kubariki mtoto si unajua walokole hatunaga ubatizo wa watoto wadogo tunawabariki tu kama Yesu!
LISA: Sawa, Enhe?
AZONTO: Kwenda kumsikilizza akasema namtaka mumlete mtoto leo usiku hapa kanisani, saa 5 nanusu usiku
Sisi tutakubali, kweli usiku yake tukampeleka tukijua labda ni maombi, kufika hamna mlinzi hamna nini, akasema mleteni mtoto mara nikaona panga pembeni, nikauliza panga la nini
Mchungaji Kiongozi akasema huyu mtoto lazima tumtoe kafara
Nikauliza kwanini?
Akasema tumekosea masharti huyu mtoto hakuwa wa kwangu alikuwa wake, na huyu mke wangu alikuwa ni mpenzi wake wa miaka mingi alimpeleka kijijini baada ya kuoa akamjengea na nyumba akawa anakaa huko, baada ya kuona anataka kuja mjini wakaelewana aolewe na mimi ili wao kuwa karibu zaidi hapa Dar

Nilipouliza masharti gani tumekosea akasema tumelala pamoja baada ya kujifungua mtoto, masharti yetu hayaruhusu hivyo

Kuulizia masharti gani, akampa mtoto mke wangu akaenda kufungua pale kwenye maji ya ubatizo, akaniambia hapa ndio tunatoaga watoto kafara, watu wakibatizwa tunanasa hatima zao, tunakuwa tunacheza nazo, ndio unaona walokole wengi wanateseka hawasogei mbele wanakaa hapo miaka na miaka mpaka watakapotii masharti kama hayo nayotaka kukuambia!
Nilipouliza masharti gani akasema yeye ni mchawi, na kwenye kikao chao cha uchawi mke wangu ni malkia msaidizi na hii ni zamu yake ya kutoa kafara mwane, kwahiyo lazima usiku huu ifanyike la sivyo kanisa litakosa waumini watapungua sana
Akasema ndio mimi ni Mchungaji mwenye upako mkubwa unadhani upako nautoa wapi? Kwa shetani kuzimu, shetani ndio anajaza kanisa, jina la Yesu tunalitumia tu kama kivuli lakini ushindi ni kwa shetani.
Si unajua kuwa Mungu huwa anachelewa na mimi ninataka nifanikiwa sasa!
Nilichoka Lisa, sikuamini, nguvu zikaniisha nikazimia hapo hapo, kuja kuzinduka nipo hospital na mke wangu pembeni, nilipomwuliza mtoto yuko wapi akaniuliza mtoto gani?
Nikamwambia tumezaa watoto akanijibu umechanganyikiwa hatuna mtoto hatujawahi kupata mtoto. Niliporudi nyumbani nikakuta nyumba imebadilika sana makochi mapya, pasafi Tv mpya, nikashangaa vimewekwa saa ngapi
Nikaingia kulala kwanza nilipoamka mke wangu akaniletea supu, kuiangalia supu kuna kidole cha mtoto!
Nikasikia kutapika ghafla nikatapikia kile chakula, mke wangu akakimbia kuondoa chakula, akasafisha akarudi jikoni mimi nikaenda kukaa sebuleni, nikawaza sana nafanyaje, nikisema niende kwenye sheria sina uthibitisho nafanyaje?
Nikawaza na kuwazua, nikampigia simu dada yangu aje haraka pale nyumbani, akaja nikamwongelesha kilugha maana mkewangu sio wa lugha yangu akanielewa, akalala pale pale, asubuhi mke wangu alipoenda kazini nikapaki mizigo yangu yote nikampa dada, akaondoka nayo mpaka kwake, nikaiangalie ile nyumba nikaomba Mungu anisamehe
Nikaingia kwenye kabati nikaanza kumpekua mke wangu, nikakuta ameweka pesa nyingi sana thamani ya million 10 sikuelewa alipozitoa ila nilikuwa nakumbuka kuwa majuzi mtoto alitolewa kafara pale Kanisani.. nikachukua Milion 10 nikaondoka mpaka Kanisani nikammkuta Mchungaji Kiongozi hayupo, nikamwachia secretary ampe mchungaji kiongozi funguo yangu nikaondoka kurudi kwa dada.
Dada akanitoa pale kwake maana mke wangu alikuwa anapajua kwa dada yangu lakini sio kwa mke wangu, akanipeleka kwa mdogo wangu wa mwisho Kiluvya, kuishi huko, akaniambia kesho kutwa uende Ubalozi wa Marekani nimekuandalia documents nimeshazipeleka wanakusubiria ufanye interview, kweli Kesho Kutwa nikaenda nikafanya Interview, wakaniuliza naenda kusomea nini nikawaambia uchungaji wakanigongea visa wakaniambia siku fulani nenda ofisi fulani ya DHL ukachukue Visa yako itakuwa tayari… kweli siku nilioenda nikachukua Visa, mdogowangu akampigia Dada, Dada akamwambia mwambie Azonto kesho saa 2 usiku aje Airport nitamtuma Dereva wa ofisini kwangu ampelekee tiketi Airport maana mimi nikiondoka hapa nitafuatiliwa
Maana ameshakuja mke wake Azonto na mchungaji wake kumwulizia, namtakia safari njema na masomo mema tutawasiliana akifika New York.
LISA: Doh pole sana Azonto, sasa ukasafiri salama?
AZONTO: Ndio nilisafiri salama sikuwaona Mchungaji wala mke wake na zile hela milioni 10 niliondoka nazo ndio nikaja nazo kuanza maisha huku maana sister ndio analipia nusu Ada si unajua uchungaji tunapewa ufadhili?
LISA: ndio, kwahiyo hapa New York wewe ni Mgeni?
AZONTO: Nimeshakaa Miaka 3 hapa New York
LISA: Unasoma Uchungaji kweli au ilikuwa geresha?
AZONTO: Uchungaji nilishamaliza mwaka 1, nikaaa kufanya kazi kwenye hizi NGO za Kanisani wakanipenda ndio wakaniajiri so nina work permit ilionifanya nibaki Marekani na kuongezewa Visa!
LISA: Jamaa pole sana
AZONTO: Asante Lisa
LISA: Najua sasa hautatamani kuoa tena
AZONTO: Hapana nimeshaoa, Mmarekani Mweusi mwaka jana na tuna watoto 2 wakike na kiume
LISA: Oh! Hongera Mno rafiki yangu, Yule Mchungaji Free Mason na Mkeo wa Bongo wanaendeleaje?
AZONTO: Sijawasikia tena, ila mke wangu alishakufaga, aligongwa na gari akiwa anavuka barabara alinieleza sister, lakini mimi nilijua kafara ya Mchungaji Kiongozi imetembea
LISA: Jamaan jamaan jamaan, Azonto nakufahamu ulikuwa unampenda Mungu sana, kwanini umeacha?
AZONTO: Nachukua likizo kwa walokole, ila Mungu sijamuacha nampenda sana ila mimi sio mchungaji kabisa ingawa nimesomea na nafanya kazi kwenye Taasisi moja yapo ya Kanisa huku New York
LISA: Doh jamani jamani jamani pole mno! Mwisho wa siku Mungu amekubarikia maisha yanaenda umeshaoa na una watoto 2
AZONTO: Ni kweli tangu Nimekanyaga Marekani sijawahi tena kuhangaika kimaisha mambo yangu yanaenda kama miujiza, mateso yooote nilioyapata Nyumbani huku siyaoni tena, nikigusa kitu kinaenda, popote napoweka mkono wangu kufanya jambo kinafanikiwa mara 100, sasa hivi nimefungua restaurant na mke wangu ndio pale ulipokuja ukanikuta nakunywa wine!
LISA: Oh jamaan! Lakini kwanini unakunywa pombe? Pombe si dhambi au?
AZONTO: Nimekwambia nimechukua likizo kwa Walokole lakini sio kwa Yesu, Yesu ninaemjua aligeuza maji kuwa wine
LISA: sio wine ni mvinyo kama soda, juice
AZONTO: My dia, wine ni wine, Yesu angegeuza kuwa juice ingeandikwa juice lakini wakaandika wine
Mtume Paulo kwenye agano Jipya alimshauri Timotheo anywe mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake
Mimi sinywi pombe kabisa, lakini nakunywa wine
Hiki kitabu nakisoma kwasababu kuna mtu namfanyia councelling anapenda sana Malaya ndio nikakiona hiki kitabu hapo book shop juzi nikaamua kukinunua, nikisome nione!
LISA: Bado unampenda Yesu Kweli?
AZONTO: Kwa moyo wangu wote, akili zangu zote, mawazo yangu yote na kila kitu nmilicho nacho, sisali tena kwa walokole nasali Lutherani kwangu kwa zamani walipokuwa wanasali wazazi wangu!
LISA: How are you lakini?
AZONTO: Am very fine Lisa, am very Happy Lisa, nimeshaingia kwenye Promise Land yangu, Mungu akipenda mwakani naweza kupewa Green Card ndio nafuatilia Process zake!
LISA: Kweli ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu na wenye nguvu ndio wewe, watu wangepitia maisha yako wangeshamuacha Mungu na Yesu Muda sana!
AZONTO: Lakini sio mimi, mimi niliamua tangu nikiwa mdogo form 5 na namshukuru Mungu nimepitia maisha niliopitia sawa na neno la Mungu linalosema, Marko 10: 25, “ Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu”
Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Mathayo 7:14
Yesu niliemchagua Form 5 ni wa Kwangu, ninampenda sana na sita muacha milele yote mpaka kufa. Kuhubiri sijaacha naendelea kumtangaza mpaka pumzi yangu ya mwisho!

LISA: Nikamwangalia Azonto nikampenda, kweli watakatifu Duniani bado wapo, Azonto alikuwa amenenepa, amependezaaa, amenawiri na rangi yake imebadilika anaung’aa, amevaa Tshirt lake limeandikwa JESUS FREAK!

ITAENDELEA IJUMAA KUU HII TAR 19 APRIL 2019 SAA 1 JIONI YA TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom