Huyu Baba Kiboko..

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,945
12,576
Nyumba ni ya familia na wanaishi pamoja na wapangaji. Binti kamaliza elimu yake ya juu na kufanikiwa kupata kazi, ili aweze kuwa huru kaamua kuhama nyumbani na kutafuta nyumba ya kupanga. Baba yake kamwambia badala ya kwenda kumpa pesa ya kodi mtu mwingine ni bora abaki palepale nyumbani, ila kile chumba anachoishi akilipie na mahitaji mengine ajitegemee kama vile chakula n.k. Baba anadai hawezi kuacha binti yake akampe mtu mwingine kodi ya nyumba wakati yeye ndie kamsomesha. Binti anaishi kwao kama mpangaji mwingine tu...
Hivi wakuu hii imekaaje?? Inakubalika??

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,785
6,614

sio mbaya, anachangia uchumi wa familia kiivyo

daughter

JF-Expert Member
Jun 22, 2009
1,275
739
Huyo mzee anamatatizo,
itafika time binti atataka kununua kiwanja atasema 'badala ya kumpelekea mtu mwingine iyo ela nipe mimi nikukatie kaeneo huku uwani!'
Balaa iyo. Lakini kwani ni kabila gani (am just asking!)

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
18,833
11,689
Mwisho atamwambia kuliko kwenda kumfaidisha mwanaume mwingine ni bora amuoe yeye,maana ye ndie kamsomesha.

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
790
Huyo dingi mkoloni! Kwa kuwa lengo la binti ilikua ni kupata uhuru, namshauri akae humo humo tena kwa uhuru wote, just like watanzania wengine!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,945
12,576
Huyo mzee anamatatizo,itafika time binti atataka kununua kiwanja atasema 'badala ya kumpelekea mtu mwingine iyo ela nipe mimi nikukatie kaeneo huku uwani!'Balaa iyo. Lakini kwani ni kabila gani (am just asking!)
Ni wa kaskazini..

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,945
12,576
Kwa upande mwingine sio vibaya...kama kuna chumba ambacho mpangaji yeyote angekaa, why not binti yake??
sawa lakini kuna uhuru fulani ambao binti atakosa...... Lakini kali kuliko ni pale ambapo binti anaishi kama wapangaji wengine tu....hii haijatulia.

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,435
Nunua bidhaa za Tanzania uijenge Tanzania. Napita tuu ngoja nikatafakari kabla sijachangia

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,207
8,689
Sijajua uhuru tunouzungumzia hapa ni wa vipi!
Lakini nijuavyo mimi ni kuwa ishu si baba kupata senti za upangaji tu!
Binti kwenda mbali kujitegemea ni zaidi ya kodi!
Actually kuwa mbali na nyumbani inamwezesha mtu ku'interact na jamii kwa mapana zaidi! Kuna kero za upangaji ambazo tuliopata kupanga wote tunazifahamu, ambapo kwa kukaa nyumbani atazisikia redioni!, na kwa hali hiyo binti hatajengeka ipasavyo!
Kuna watu watakuwa Limited kufika pale nyumbani kwake, kisa ni kwa baba-mtu...hata kama anaishi kwa kupanga watu hawatajua hilo, watajua anaishi chini ya wazazi, hivyo umakini fulani unahitajika kuingia nyumbani kwake!

Hivyo kumshauri binti apange kwa babaye ni kosa kubwa, aidha ni kuvuruga saikolojia ya binti...Huyu mzee atakujaona vituko ambavyo hakutarajia, na atapata presha bure!

pinochet

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
345
96
Huyu mzee gangwe kweli,issue hapa ana hisi binti akikaa nje ya home atamegwa,duu mzee ana wivu mbaya na bintiye. Kwani akiweka mpangaji siatapata tu fedha? Huo ni ukoloni mamboleo.

daughter

JF-Expert Member
Jun 22, 2009
1,275
739
Sijajua uhuru tunouzungumzia hapa ni wa vipi!

Lakini nijuavyo mimi ni kuwa ishu si baba kupata senti za upangaji tu!

Binti kwenda mbali kujitegemea ni zaidi ya kodi!

Actually kuwa mbali na nyumbani inamwezesha mtu ku'interact na jamii kwa mapana zaidi! Kuna kero za upangaji ambazo tuliopata kupanga wote tunazifahamu, ambapo kwa kukaa nyumbani atazisikia redioni!, na kwa hali hiyo binti hatajengeka ipasavyo!

Kuna watu watakuwa Limited kufika pale nyumbani kwake, kisa ni kwa baba-mtu...hata kama anaishi kwa kupanga watu hawatajua hilo, watajua anaishi chini ya wazazi, hivyo umakini fulani unahitajika kuingia nyumbani kwake!

Hivyo kumshauri binti apange kwa babaye ni kosa kubwa, aidha ni kuvuruga saikolojia ya binti...Huyu mzee atakujaona vituko ambavyo hakutarajia, na atapata presha bure!

well said PJ,huyo binti hawezi jua maisha hukunje yako vipi,hatakutana na changamoto za kitaa.cio poa hata kidogo

0 Reactions
Reply
Top Bottom