Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 41,983
- 12,702
Nyumba ni ya familia na wanaishi pamoja na wapangaji. Binti kamaliza elimu yake ya juu na kufanikiwa kupata kazi, ili aweze kuwa huru kaamua kuhama nyumbani na kutafuta nyumba ya kupanga. Baba yake kamwambia badala ya kwenda kumpa pesa ya kodi mtu mwingine ni bora abaki palepale nyumbani, ila kile chumba anachoishi akilipie na mahitaji mengine ajitegemee kama vile chakula n.k. Baba anadai hawezi kuacha binti yake akampe mtu mwingine kodi ya nyumba wakati yeye ndie kamsomesha. Binti anaishi kwao kama mpangaji mwingine tu...
Hivi wakuu hii imekaaje?? Inakubalika??
Hivi wakuu hii imekaaje?? Inakubalika??