Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,055
- 79,399
Hamjambo!
1. Ni sawa uoe/kuolewa alafu useme nikijipenda inatosha, au akinipenda Mama inatosha. Mkeo au mumeo asipokupenda tafsiri yake hakuna ndoa hapo.
2. Uongozi unatokana na mapenzi. Kupendwa. Ndio maana watu wanachagua viongozi wanaowapenda.
3. Na huwezi kuongoza watu wasiokupenda. Kwa sababu msingi mkuu wa kuongoza ni lazima upendwe. Chochote unachokifanya bila kupendwa hakiwezi kuthaminiwa. Huwezi kupewa sifa na utukufu.
4. Mwanaume ni kichwa cha nyumba kama kuna upendo yaani kama mkewe anampenda.
Lakini kama mke hampendi mumewe hakuna kichwa tena hapo. Kanuni ni ileile. Huwezi muongoza mtu asiyekupenda. Huwezi.
5. Ndio maana Mkeo kama hakupendi hata umfanyie nini bado haoni kama umefanya Jambo lolote. Atakulaumu Kila Siku. Ataona hufanyi lolote. Ataona wanaume wengine ni Bora kuliko. Atasifia wanaume wengine.
6. Katika Saikolojia ya Uongozi. Popote pale Mapenzi na kupendwa ni nguzo na ustawi wa uongozi wa eneo hilo.
7. Upendo unazungumzia watu. Na Uongozi ni watu. Mioyo ya watu ikiwa juu yako wewe ni kiongozi.
Ndio maana Iran pamoja ni taifa dogo mbele ya Marekani lakini moja y strength za Iran ni wananchi wengi wanampenda Ayatollah na uongozi wake. Hivyo sio Rahisi Marekani kumshinda Muiran kwenye ground battle.
8. Kuongoza watu wasiokupenda ni stress Sana. Ni kama mwanaume aliyeoa mwanamke asiyempenda. Yaani ni mateso. Utajipendekeza wee. Utatafuta attentions utajifaraguza, utajichekesha, utaleta drama lakini haibadili kitu kama hupendwi ni hupendwi.
9. Biblia inakisa cha Mfalme Sauli na Kijana Daudi.
Baada ya Goliath kuangushwa na Daudi. Waisrael moyo wao ulianguka kwa Daudi. Wanawake na vijana walimpenda Kijana Saudi.
10. Jambo hilo lilimuumiza Sana Mfalme Sauli kwa sababi anajua maana ya upendo kwenye ufalme wake. Hapo ndipo Mfalme sauli anawaambia washauri zake " kama watu wanaimba na kumsifu Daudi hivyo, Daudi amekosa nini tena zaidi ya huu ufalme"
11. Kwamba kupendwa ndio ufalme wenyewe. Ndio utawala wenyewe. Ndio uongozi wenyewe.
12. Unapopendwa hutumii nguvu kubwa kutumikia watu. Kwani watu wanakusaidia kuongoza. Wanajitoa kwaajili yako. Nawe unajitoa kwaaajili yao.
13. Kwenye amri za Mungu. amri ya Kwanza ni Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote, na Akili zako zote.
14. Hiyo ni Kanuni ya kwanza katika Ufalme. Mungu anajua kwamba huwezi kuwa Mfalme Bila kupendwa na watu unaowaongoza. Na ndivyo ilivyo.
15. Ni kama Mzazi usipendwe na watoto. Yaani hata uwe tajiri unayemiliki dunia. Bado itakuuma tuu.
Kufikia hapa sina la ziada.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam