Huwezi kupanda mlima hadi juu kileleni bila kuponda baadhi ya mimea kwa miguu yako

Street brain

JF-Expert Member
Oct 24, 2022
486
606
Wazee wanasema: huwezi kupanda mlima hadi juu kileleni bila kuponda baadhi ya mimea kwa miguu yako. Aliye kileleni ni vyema akumbuke maumivu aliyosababisha wakati wa safari ya kupanda mlima.

Hakuna aliyepata mafanikio bila kusababisha maumivu kwa wengine. Baadhi ya ndoto za dada, kaka na wadogo zako zilizimwa ili upate kuendelea mbele. Ukishafika juu, usifikiri kwamba dada, kaka au wadogo zako hawakuwa na bidii au akili.

Labda ndugu zako wapo chini kwa sababu walikubali kukanyagwa ili wewe upite. Fikiri kabla ya kuwasema kwamba ni wavivu. ©️Pd. PK
 
Back
Top Bottom