Huu wizi kupitia Tigopesa, naomba Tigopesa mnisaidie majibu hapa

Kaibiwa kizembe
Jibu kama simu zako zilishikwa na hao matapeli, leo au days before...

Kama walizishika tafuta mtu anaitwa TIGOPESA kwa phonebook yako ukimkuta, liaaaaaa... Kisha endelea na bness, chukulia kuwa umelipa ada ya mafunzo as hutaibiwa tena na hakuna mtu atagusa yo phone again!
 
Aliyemuibia ni mtu wake wa karibu
Mchezo uliofanyiwa hapo ni huu,
Kuna mtu alishika simu yako, akasave namba zake kwa jina la tigopesa.
Kisha akakutumia msg ya kawaida na ikaja kwa jina la tigopesa ambalo limesaviwa kwenye simu.
Huyo mtu aliangalia Salio lako kwenye msg za tigopesa. Hivo akawa anatuma msg akiongeza hizo amounts.

Umeibiwa kwa staili hiyo bila shaka
 
252 real
HIZICODE YA MARANGU KISAMBIO
Screenshot_20200611-184241.png
 
Hapa niseme neno, kuna baadhi ya watoa huduma za fedha kuepuka usumbufu wa kuingiza namba isiyosahihi, huamua kumpa mteja simu na kumwambia ingiza namba. Yule mteja kama si mwema, anacancel kwanza kisha anasave kwenye simu yako namba ambayo atakuja kukupiga nayo mwenzake hapo baadae au hata kesho yake, namba anaisave kwa herufi kubwa TIGOPESA au MPESA. Kisha anakwambia hebu rudia kuniwekea ile sehemu ya kuweka namba, anakupa simu, unabofya tena, unampa simu, anaingiza namba sahihi, unamrushia hiyo buku mbili yake, anasepa.

Kesho yake, anakuja mtu na mazungumzo yenu yanakuwa kama hivii
Mteja: niingizie milioni mbili. (Anatoa burungutu lamilioni mbili kweli)
Wakala: salio halitoshi bosi
Mteja: dah, una kiasi gani?
Wakala: ngoja nicheki
Mteja:..............................
Wakala: laki mbili na nusu
Mteja: Anahesabu laki mbili na nusu, anampatia wakala."Niingizie hiyo hiyo"
Wakala: Anapokea hela na kukamilisha muamala.
Mteja anatembea zake huku anajua kwenye float uko kapu.

Baada ya dk 3 anakuja mteja wa kutoa
Mteja: nataka nitoe laki tano
Wakala: Toa
Mteja: Anabonyeza bonyeza, kisha anakufowadia messeji ambayo wakala hupokea pindi mteja atoapo pesa, namba ya huyu mteja anaekutumia meseji ilishaseviwa kwako kwa jina la TIGOPESA. So meseji ikiingiza itaonekana kweli imetoka TIGOPESA, lakini fake.
Wakala: Unatoa laki tano keshi.

Baada ya dk 3 tena anakuja mteja wa kutoa
Mteja: nataka nitoe laki nne
Wakala: Toa
Mteja: Anabonyeza bonyeza, kisha anakufowadia messeji ambayo wakala hupokea pindi mteja atoapo pesa, namba ya huyu mteja anaekutumia meseji ilishaseviwa kwako kwa jina la MPESA. So meseji ikiingiza itaonekana kweli imetoka MPESA, lakini fake.
Wakala: Unatoa laki nne keshi.

Ukiangalia salio halisi, umeliwaaaaaaaa.
 
Salio lililokuepo mwanzo limeongezeka vizuri tu... angekuwa kasave namba angejuaje salio lililopo kabla yeye hajatoa? Lazima salio lingepishana tu
ngoja nikupe mpango mji unavyofanyika.kuna mtu wa tigopesa anahusika hapo ingawa siyo moja kwa moja,mpango unakuwa wa muda mrefu kidogo unaanza kwa mtu kusave namba yake kwako kwa jina la TIGOPESA or whatever,kisha anatulia kisha hapo anachokisubiri ni taarifa za salio lako la kwenye simu na mkononi,hapo ndo mtu wa tigopesa anapohusika kutoa taarifa za akaunti yako,na ndio maana uliona salio limeongezeka,kwamba walijua una shilingi ngapi kwenye simu wakajumlisha na kile kiasi walichokihitaji kutoka kwako.pole sana
 
Wizi huu umekuwa mwingi, asilimia kubwa Ni kivuli cha tigopesa... Tingo Kuna Nini hasa

Sent using Jamii Forums mobile app

Huu wizi uko siku nyingi ni kutochunga simu yako unayofanyia miamala

Akiishika mtu anaandika namba yake anasev jina TIGOPESA

Akija pale hatoi chochote anashika shika simu anakufowadia hilo limeseji aliloliandaa we ukiangalia unaona ni ya TIGOPESA unampa Cash anakuswaga na jingine fasta unatoa tena mpaka kuja kushtula wamemaliza droo washasepa
 
Huu wizi uko siku nyingi ni kutochunga simu yako unayofanyia miamala

Akiishika mtu anaandika namba yake anasev jina TIGOPESA

Akija pale hatoi chochote anashika shika simu anakufowadia hilo limeseji aliloliandaa we ukiangalia unaona ni ya TIGOPESA unampa Cash anakuswaga na jingine fasta unatoa tena mpaka kuja kushtula wamemaliza droo washasepa
Ile balance ya mwanzo anaijuaje?
 
Ile balance ya mwanzo anaijuaje?
Yaaan huu wizi ni wakitambo ndugu yangu kama nnavyokwambia hakuna kosa kubwa kwa wakala kama kutoa simu yake anayofanyia miamala kwa mtu mwingine. Hata kwenye semina si kila siku mnakatazwa?

Wizi wowote wa muamala wa kielectronic lazima kuna sehem mtoa huduma/ aliyeaminiwa kuwa na PIN kafanya uzembe au wizi.

Kama mdau hapo juu alivyoshauri nenda kwenye Phonebook ukikuta kuna jamaako anaitwa TIGOPESA lia sana halaf shukuru Mungu
 
Huu mchezo huwa anahusishwa na mtu wa IT huko tigo na ndiyo anayetuma message ya uongo ya salio lako ambayo ndio unaona salio limeongezeka kumbe ni message hewa, mtu wa kwanza anapofanya muamala nia ni kupata jina la wakala na kumtajia huyo mtu wa IT huko Tigo ili kumuwezesha kuangalia details zako na ndiyo ataangalia salio lako kwenye Tigopesa ndio atakutumia message yenye kuonesha salio limeongezeka.

Kinga ni kuuliza salio kuhakiki salio baada kupokea message.
 
Huu mchezo huwa anahusishwa na mtu wa IT huko tigo na ndiyo anayetuma message ya uongo ya salio lako ambayo ndio unaona salio limeongezeka kumbe ni message hewa, mtu wa kwanza anapofanya muamala nia ni kupata namba yako na kumtajia huyo mtu wa IT huko Tigo ili kumuwezesha kuangalia details zako na ndiyo ataangalia salio lako kwenye Tigopesa ndio atskutumia message yenye kuonesha salio limeongezeka.

Kinga ni kuuliza salio kuhakiki salio baada kupokea message.
Dah aisee bado nafuatilia comments ili nijifunze
 
Back
Top Bottom