Shahidi alivyotoa majibu ya kufikirisha kesi ya mjane wa Bilionea Msuya

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
1687238829299.png

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara (RPC), George Katabazi ni miongoni mwa mashahidi katika kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu na tajiri wa madini Mirerani, mkoani Arusha, Erasto Msuya, maarufu kama Bilionea Msuya.

Leo Jumatatu Juni 19, 2023 amehitimisha ushahidi wake aliouanza Ijumaa iliyopita, baada ya kuhojiwa maswali ya dodoso kutoka kwa mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, Peter Kibatala na Nehemia Nkoko, kuhusiana na ushahid wake mkuu alioutoa wakati akiongozwa na mwendesha mashtaka.

Hata hivyo katika mahojiano hayo, shahidi huyo Kachero mwenye cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), alikuwa na majibu ya kufikirisha baada ya kujibu maswali mengi kuwa hakumbuki taratibu zinazomuongoza kutekeleza majukumu yake ndani ya jeshi hilo wala nyenzo za kazi zikiwemo nyaraka muhimu.

Katika kesi hiyo namba namba 103 ya mwaka 2018, mjane huyo wa marehemu Bilionea Msuya,Miriam Mrita anatuhumiwa kumuua wifi yake, Aneth Msuya; yeye na mwenzake, mfanyabiashara Revocatus Muyella maarufu kama Ray.

Aneth aliuawa kwa kuchinjwa, Mei 25, 2016 kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, miaka mitatu tangu kuuawa kwa kaka yake Bilionea Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Agosti 7, 2013.

Ushahidi mkuu
Katika ushahidi wake akiongozwa na mwendesha Mashtaka, wakili wa Serikali, Marietha Maguta, RPC Katabazi mwenye cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) alisema kuwa ndiye aliyekamata gari la mshtakiwa Miriam, linalodaiwa kuhusika katika mauaji hayo.

ACP Katabazi aliieleza mahakama kuwa wakati wa mauaji hayo alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Arusha, akiwa na cheo cha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP).

Alieleza kuwa Agosti 5, 2016 asubuhi, alipigiwa simu na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, akamwelekeza kukamata mali zinazodaiwa kuhusika katika tukio la mauaji, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

ACP Katabazi alidai kuwa mali hizo zilikuwa ni magari mawili yaliyodaiwa kumilikiwa na mshatakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Miriam na kwamba alifuatilia na Agosti 10 alikamata gari moja katika hotel ya SG ya mshtakiwa huyo iliyoko eneo la Sakina.

Alidai aliipekua gari hiyo aina ya Range Rover, rangi ya fedha yenye namba ya usajili T 429 BYY ndani yake walikuta nyaraka mbalimbali zikiwemo za usimamizi wa mirathi ya Erasto Msuya, barua ya mauziano ya shamba na nyaraka za benki.

Alidai kuwa baada ya upekuzi alijaza mali hizo, gari na nyaraka hizo zilizokuwemo ndani yake kwenye fomu ya ukamataji mali mbele ya mashahidi huru, akasaini pamoja na mashahidi hao.

Shahidi huyo alieleza kuwa baada ya hapo aliwapa maafisa wawili wa Polisi, Ditektivu Konstebo (DC) Abel na DC Lukas walipeke gari hilo na nyaraka hizo katika kituo cha Polis Chang’ombe, Dar es Salaam kwa upelelezi wa kesi hiyo.

Aliiomba mahakama hiyo ikapokea hati ya ukamataji mali pamoja gari hilo lililoegeshwa katika kituo cha Chang’ombe kuwa vielelezo vya ushahidi wa upande wa mashtaka.

Baada ya maelezo hayo ndipo leo akahojiwa na mawakili wa utetezi na kutoa majibu hayo. Sehemu ya mahojiano hayo kwa baadhi ya maswali aliyoulizwa shahidi huyo na majibu yake ni kama ifuatavyo:

Wakili Kibatala: Unafahamu Kuna special form ambazo zinatumika kubadilishana vielelezo?
Shahidi ACP Katabazi: Sikumbuki
Kibatala: Unaifahamu Police form number 145?
Katabazi: Sizikumbuki
Kitabatala: Ijumaa tulikwenda Chang'ombe Polisi na kule ukakabidhi kielelezo (gari ya Range Rover aliyoikaitoa ikapokewa na mahakama kama kielelezo cha Saba cha upande wa utetezi – PE7), unakumbuka ulimuonesha Jaji exhibit label (kitambulisho cha kielelezo) inayohusiana na hicho kielelezo?
Katabazi: Sikumuonesha
Kibatala: Ni kweli kuna register (rejesta – kitabu cha kumbukumbu za vitu) inayoonesha utunzaji vilelezo mpaka kinatolewa mahalani?
Katabazi: Sikumbuki
Kibatala: Baada ya kuikamata ile gari ni kweli ilifikishwa Polisi Arusha?
Katabazi: Ofisini kwangu
Kibatala: Kwani ofisini kwako ni nyumbani kwako?
Katabazi: Kituo cha Polisi
Kibatala: Shahidi Unafahamu PGO 229(18) (Police General Order – Mwongozo wa utendaji kazi wa Jeshi la POlisi) inasema kielelezo kitarekodiwa kwenye Polisi fomu namba 16 na mkuu wa kituo au afisa yeyote wa Polisi aliyekasimishwa na mkuu wa kituo?
Katabazi: Sikumbuki
Kibatala: Unakumbuka ulimpa jaji nakala ya exhibit register ambayo ulilitumia kuweka kumbukumbu za (gari hilo) kielelezo hicho?
Katabazi: Sikumbuki
Kibatala: Wakati unawakabidhi wale askari (DC Abel na DC Lukas) kile kielelezo (gari) kulileta Chang'ombe, kuna fomu ya makabidhiano uliitoa?
Katabazi: Sikumbuki
Kibatala: Ijumaa tarehe 16/6/2023 ulitoa kielelezo mahakamani, mpaka unakitoa uliieleza Mahakama kuwa awali kilikuwa kinatunzwa na nani?
Katabazi: Sikusema
Kibatala: Shahidi, ulitoa hiki kielelezo hapa mahakamani certificate of seizure (hati ya ukamataji mali), lengo la kukitoa ilikuwa nini?
Katabazi: Sikumbuki
Katabazi: Sasa shahidi wewe hii gari uliikamata kutoka kwa nani?
Katabazi: Meneja wa hotel ya SG, Omari
Kibatala: Mpaka leo unatoa ushahidi wewe uliyeikamata Unafahamu hii gari ni mali ya nani?
Katabazi: Sifahamu
Kibatala: Sasa shahidi hebu soma kielelezo hiki (hati ya ukamataji) mwambie Jaji wewe umeikamata hiyo gari kutoka kwa nani?
Katabazi: Anasoma maelezo ambayo ni tofauti na swali
Kibatala: Uliijaza wewe mwenyewe hiyo fomu?
Katabazi: Sikumbuki
Kibatala: Nakuuliza tena kwa mujibu wa hiyo karatasi ulii-seize (uliikamata) kwa nani?
Katabazi: Kwa Omar,sababu ndiye aliyekuwa meneja wa hoteli ile.
Kibatala: Nani alikuwa anashuhudia hilo zoezi (upekuzi na ukamataji mali)? Nani walikuwa mashahidi huru?
Katabazi: Alikuwa Omari Mfangabo, Karimu Mkuruma na Winston Laizer
Kibatala: Huyu Omari Mfangabo ndiye yuleyule ambaye gari lilikuwa kwenye custody yake?
Katabazi: Kama nilivyosema maana yule ndiye meneja wa hotel na akaja kuwa shahidi.
Kibatala: Afande Katabazi, unafahamu umuhimu wa kisheria wa mashahidi huru kupekua au kukamata mali?
Katabazi: Nafahamu.
Kibatala: Hapo katika hiyo karatasi kuna majina Miriam Steven Mrita na mwenye gari humfahamu hayo majina ya Miriam kisheria yana mantiki gani hapo?
Katabazi: Mantiki ya hayo majina wanaoielewe ni wale wanapeleleza kesi ya mauaji.
Kibatala: Sasa shahidi huku ndani mmechukua nyaraka nyingi za maisha ya kibiashara za mteja wangu,mmechukua nyaraka za usimizi wa mirathi, barua ya mauziano ya shamba na za benki, hizi nyaraka ziko wapi?
Katabazi: Nilizikabidhi kwa askari wazipeleke Chang'ombe.
Kibatala: Zilikuwa na mahusiano na maelekezo ya DCI kuzichukua hizo nyaraka zikiwemo za usimamizi wa mirathi?
Katabazi: Maelekezo aliyonipa ni kwamba mikamate gari,
Kibatala: Hizi nyaraka zina uhusiano na hiyo gari?
Katabazi: Zina uhusiano kwa sababu zilikuwa ndani ya hiyo gari.
Kibatala: Ijumaa pale Chang'ombe (wakati akikabidhi gari kwa mahakama kuwa kielelezo cha upande wa mashtaka) ulizionesha hizo nyaraka kwamba ndizo nilizozikamata ndani ya gari?
Katabazi: Sikuonesha
Kibatala: Shahidi ulitoa ufafanuzi kwa Jaji kwamba kwa nini hiyo gari haina namba (plate number) za usajili?
Katabazi: Sikutoa.
Kibatala: Ni kweli au sio kweli namba za usajili wa gari zina mfumo wake wa usajili ambao unaanzia TRA ambazo zinatofautisha gari moja na kingine?
Katabazi: Sikumbuki.
Kibatala: Ulito ufafanuzi kuwa awali uliwakabidhi Afande Lukas na mwenzake gari ile bila namba?
Katabazi: Sikutoa
Kibatala: Wewe kama RCO Uliwahi kufahamu gari hilo tarehe 25 Mei, 2016 lilikuwa wapi wewe kama Kachero?
Katabazi: Hapana Sikumbuki.
Kibatala: Ulipokwenda SG hotel ukamuona Omari Mfangabo alikwambia kuwa Miriam Mrita yuko wapi?
Katabazi: Sikumbuki
Kibatala: Huyu Karim Unafahamu ndiye dereva wa hilo gari?
Katabazi: Sikumbuki.
Kibatala: Shahidi ukiwa chini ya kiapo nakuuliza, huyu Karimu Mruma siye aliyeendesha gari kutoka Arusha mpaka Polisi Chang'ombe?
Katabazi: Sikumbuki
Kibatala: Na Karimu Mruma ndiye aliyeendesha kwa sabu si kila.mtu anweza kuendesha Range Rover, Unafahamu?
Katabazi: Sifahamu.
Kibatala: Wakati DCI wa kipindi hicho Diwani Athuman, anakupa maelekezo ya kukamata hilo gari alikutajia namba za usajili wa gari hilo?
Katabazi: Alinitajia.
Kibatala: Wewe unafahamu alizipata wapi hizo namba?
Katabazi: Sifahamu

Wakili Nehemia Nkoko: Ni nini katika fomu hiyo kinaonesha kuwa gari uliyoikamata inahusiana na kesi ya mauaji KGB/IR/2849/2016?
Katabazi: Hakuna.
Nkoko: Utakubaliana na mimi mshtakiwa wa kwanza na wa pili huwafahamu na hujawahi kujihusisha na jambo lolote linalowahusu?
Katabazi: Sawa

Baada ya maswali ya dodoso kutoka kwa mawakili wa utetezi, shahidi huyo ameulizwa tena mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali, Maguta, maswali ya kusawazisha na kufafanua hoja zilizoibuliwa katika maswali ya dodoso.Sehemu ya mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili Maguta: Shahidi umeulizwa kama unawafahamu washtakiwa ukajibu kuwa huwafahamu hebu tufafanulie.
Katabazi: Ni kwamba jukumu langu lilikuwa ni kukamata mali nilizoelekezwa kwa maana hiyo kesi ya msingi ilikuwa inapelezwa na watu wengine.
Maguta: Pia umeulizwa kama uliwakabidhi gari Lukas uliwakabidhi kwa kutumia fomu ukasema hukumbuki hebu elezea chain of custody (mnyororo wa utunzaji vielelezo)
Katabazi: Chain of custody ni kwamba nilivyowakabidhibwao nao wao waliwakabidhi wengine
Maguta: Pia umeulizwa maswali kuhusiana na kielelezo PE6 (kielelezo cha 6 cha upande wa mashtaka ambacho ni hati ya ukamataji mali) ukaulizwa kwanini hakuna jina la suspect wala saini yake, hebu eleza kwa nini hakuna jina la suspect
Katabazi: Mimi jukumu langu lilikuwa ni kukamata mali nadhani wapelelezi wengine wanajua hilo.
Maguta: Pia uliulizwa kama wewe ndiye ulijaza kielelezo hiki (hatia ya ukamataji mali) ukasema hukumbuki, hebu eleza kama sasa unakumbuka.
Katabazi: Mimi ndiye niliye-search na ndio niliyejaza

Wakili Kibatala anasimama na kupinga swali hilo akisema: Mheshimiwa tuna concern moja. Nilimuuliza shahidi swali hilo akasema hakumbuki lakini sasa anasema anakumbuka, kwa hiyo hio ni jipya.

Jaji Edwin Kakolaki:
Nimeelewa swali (la mwendesha mashtaka) kwamba sasa baada ya kuoneshwa tena (hiyo hati) kama anakumbuka.
Kibatala: Hata sisi tulimuuliza akiwa na hicho kielelezo.

Hata hivyo Jaji Kakolaki, amesema kuwa hiyo siyo hoja mpya na kwamba na wakili Kibatala akakubaliana naye kisha wakili Maguta akaendelea

Maguta: Shahidi pia umeulizwa swali kuwa aliyesafirisha gari mpaka Dar ni Karim na kwamba Range haiendeshwi na kila mtu hebu ieleze Mahakama nani aliyeendesha gari
Katabazi: Mimi ninachokumbuka niliwakabidhi hao (askari DC Abel na DC Lukas) pale sasa kama aliyeendesha nani mimi sijui.
Maguta: Pia uliulizwa kama lilitoka Arusha bila namba na kama ulimfafanulia Jaji, hebu ieleze Mahakama.
Katabazi: Hiyo gari ilikuwa na namba na iliendeshwa mpaka Dar ikiwa na namba.

Wakili Kibatala anasimama kupinga jibu hilo akisema: Mheshimiwa hiyo ni hearsay (uvumi kwamba ililetwa mpaka Dar ikiwa na namba maana yeye hakuwepo.

Jaji: Labda mpaka pale alipoikabidhi.
Kibatala: Sawa Mheshimiwa jaji
Maguta: Umeulizwa kama kwenye kielelezo hicho kinahusika na kesi ya KGB/IR/2849/2016, hebu ieleze Mahakama.
Katabazi: Kwa mujibu wa hili kielelezo kimeitaja hiyo gari kuwa ni Range Rover T429 BYY.

Huo ndio ulikuwa mwisho wa maswali ya Wakili Maguta na mwisho wa ushahidi wa shahidi huyo.

Hivyo Jaji Kakolaki aliahirisha kesi hiyo mpaka kesho Jumanne Juni 20, 2023 asubuhi baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa ulikuwa umeandaa shahidi mmoja tu kwa kuwa walikuwa angetumia siku zima ya leo kulinga na maelzo ya upannde wa utetezi Ijumaa kuwa wangekuwa na maswali mengi kiasi kwamba leo wasingemaliza

CREDIT: MWANANCHI

View attachment 2662834

Noma sana Babu yangu ameshinda kesi ya mauwaji Kwa mazingira hayo hayo wakajichanganya mpaka ikaonekana Babu Hana kesi.
 
Jaji Edwin Kakolaki: Nimeelewa swali (la mwendesha mashtaka) kwamba sasa baada ya kuoneshwa tena (hiyo hati) kama anakumbuka.
Kibatala: Hata sisi tulimuuliza akiwa na hicho kielelezo.

Hata hivyo Jaji Kakolaki, amesema kuwa hiyo siyo hoja mpya na kwamba na wakili Kibatala akakubaliana naye kisha wakili Maguta akaendelea

Maguta: Shahidi pia umeulizwa swali kuwa aliyesafirisha gari mpaka Dar ni Karim na kwamba Range haiendeshwi na kila mtu hebu ieleze Mahakama nani aliyeendesha gari
Katabazi: Mimi ninachokumbuka niliwakabidhi hao (askari DC Abel na DC Lukas) pale sasa kama aliyeendesha nani mimi sijui.
Maguta: Pia uliulizwa kama lilitoka Arusha bila namba na kama ulimfafanulia Jaji, hebu ieleze Mahakama.
Katabazi: Hiyo gari ilikuwa na namba na iliendeshwa mpaka Dar ikiwa na namba.

Wakili Kibatala anasimama kupinga jibu hilo akisema: Mheshimiwa hiyo ni hearsay (uvumi kwamba ililetwa mpaka Dar ikiwa na namba maana yeye hakuwepo.

Jaji: Labda mpaka pale alipoikabidhi.
Kibatala: Sawa Mheshimiwa jaji
Maguta: Umeulizwa kama kwenye kielelezo hicho kinahusika na kesi ya KGB/IR/2849/2016, hebu ieleze Mahakama.
Katabazi: Kwa mujibu wa hili kielelezo kimeitaja hiyo gari kuwa ni Range Rover T429 BYY.

Huo ndio ulikuwa mwisho wa maswali ya Wakili Maguta na mwisho wa ushahidi wa shahidi huyo.

Hivyo Jaji Kakolaki aliahirisha kesi hiyo mpaka kesho Jumanne Juni 20, 2023 asubuhi baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa ulikuwa umeandaa shahidi mmoja tu kwa kuwa walikuwa angetumia siku zima ya leo kulinga na maelzo ya upannde wa utetezi Ijumaa kuwa wangekuwa na maswali mengi kiasi kwamba leo wasingemaliza

CREDIT: MWANANCHI

Inavyoonekana Mtaala wa Kufundishia Maafisa wa Polisi nchini Tz uko hovyo, wao wanachojua ni matumizi ya nguvu tu bila akili.
Ni maoni yangu kwamba Masomo yanayotolewa katika Vyuo vya Upolisi kule Moshi. Kurasini (Dsm) na Kidatu Kilombero yajikite kwenye skills mbalimbali zinazomhusu Polisi katika utendaji wake wa kazi huku ikitilia mkazo zaidi na zaidi somo la Sheria.
Iwe ni sharti au kigezo cha lazima kwamba mtu yeyote hawezi kuajiriwa kama Afisa wa Polisi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tz bila ya kuwa na angalau Elimu ya Cheti cha Awali cha Sheria (Basic Certificate in Law, or Legal Practices or Jurisprudence). Angalau Taaluma ya Sheria kwa ngazi ya Cheti kwa Maafisa wa Polisi liwe ni suala la Lazima kwa Mapolisi wote.
Aidha, kwa hapa Tz tutunge Sheria ya kuwataka Wataalamu wa Afya ya Akili au Madaktari wa Tiba ya Binadamu kuwapa Nasaha au Tiba-ushauri kwa Maafisa wa Polisi kuhusiana na Masuala ya Afya ya akili pamoja na Kuwasisitizia/Kuwakumbusha mara kwa mara hao Mapolisi juu ya UMUHIMU WA UHAI KWA BINADAMU(Haki ya Kuishi). Hili ni jambo muhimu sana kulizingatia kwa sababu katika utafiti wangu binafsi nimegundua kwamba Mapolisi wengi tulionao HAWAJUI THAMANI YA UHAI ALIONAO BINADAMU, jambo hili ni hatari sana katika nchi. Uhai wa mtu una thamani kubwa sana kuliko kitu kingine chochote kile hapa duniani, vifo vingi vya watuhumiwa vinavyotokea kwrnye vituo vya Polisi vinasababisha maumivu makali sana kwa umma, tena vinasababisha chuki kubwa kati ya wananchi na Jeshi la Polisi.
Nje ya Mfumo wa Mahakama, na ndani ya utendaji wa Jeshi la Polisi, Uhai wa mtu ufupishwe tu pale ambapo ni lazima kufanya hivyo ili kulinda uhai wa Polusi mwenyewe au wa raia wema/watu, na ithibitike wazi kwamba hapakuwa na namna nyingine yoyote ile ya kufanya zaidi ya kufupisha uhai wa muhanga/mtu aliyeuawa. Hii ithibitike pasipo kuacha shaka, kusiwepo na mauaji ya kiholela yanayofanywa na Polisi.
 
Ifikie wakati hili jeshi la polisi lifumuliwe. Litoke kwenye huu mfumo wa sasa wenye maudhui ya Jeshi la Kikoloni, na kuwa Jeshi la kulinda raia na mali zao.

Halafu lianze sasa kuchukua vijana wasomi ambao wataweza kuendana na mfumo mpya wa matumizi makubwa ya akili kwenye kutatua changamoto mbalimbali za kihalifu, kuliko haya matumizi yao ya nguvu nyingi, kuliko akili.
 
Inakuwaje mnaoa wachaga wakati wanawake wamejaaa tele Tanzania kuna mmoja amempiga kisu mwenzake kisa hela ya umeme ila wachaga wana roho mbaya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IQ zao zipo kwenye misuli ya mikono na miguuni... swali la kutumia akili wao hawana. Huko nyuma ili ujiunge na chuo cha upolisi hata na jeshi ni urefu na kama hauna michoro au makovu mwilini.

Issue ya uwezo wa kiakili haipimwi.. ndiyo huyo sasa yupo kizimbani akihoniana na mawakili wasomi...

Ni lazima uone utopolo
 
Back
Top Bottom