Huu Wimbo wa "Kuchapiwa ni SIRI ya Ndani"

Huu Wimbo wa "Kuchapiwa ni SIRI ya Ndani"

wimbo huu hata kuusikiliza ni kwa sauti ndogo huwezi kushabikia kuchapiwa kwamba ni siri ya ndani ingawaje mamlaka zimeshachelewa wimbo ushachuja.....Yamsondo mumpe Ngurumo hayo mengine hayafai

napenda tukichangia hoja namna hii
 
Naomba nieleweshwe vizuri

  1. Ni kweli haya maneno walisema wazee wa zamani?
  2. Huu wimbo una maadili hasa kuimbwa na watoto?
  3. Ni kweli kuchapiwa ni SIRI ya Ndani? kivipi?
  4. Wapi mamlaka?

Mitungii blantiii mikasiii ooyeaa.vp huo nao?
 
Mkuu concern yako inaeleweka kabisa-najiuliza siku mwanangu ananiuliza nini maana ya kuchapiwa sijui nijibu nini!
 
Kwangu mimi huu ni moja ya nyimbo za kijinga nilizo pata kusikia.

Siupendi kabisa na unatia aibu kusikiliza hasa ukiwa na watu wako wa heshima.

Kuna bar fulani tulikuwa tumekaa ukapigwa huu wimbo niliona watu wana angaliana kwa aibu.

Alafu unaweza kukuta kwenye function watoto wanaimba huu wimbo wote hadi yale maneno na kufurahi kakini aibu inabaki kwa wazazi wao.

Kwa kweli huu wimbo unatia aibu sana kusikiliza.
 
Kuna mdau aliyetangulia ametumia nguvu nyingi sana kuutetea wimbo huo na kutuwekea lyrics zote, lakini hajatufafanulia baadhi ya beti tata za wimbo huo zina maana gani. Hii ni mifano miwili tu:

Ukiwa Mjanja kuchapiwa ni siri ya ndani
Mmh muji musingi Kiuno ukishatendwa ndio byebye
 
Mkuu concern yako inaeleweka kabisa-najiuliza siku mwanangu ananiuliza nini maana ya kuchapiwa sijui nijibu nini!

huenda umwambie ni kuwekewa plasta kwenye nyumba......................
 
naona amepotea labda atarudi baadaye
Kuna mdau aiyetangulia ametumia nguvu nyingi sana kuutetea wimbo huo na kutuwekea lyrics zote, lakini hajatufafanulia baadhi ya beti tata za wimbo huo zina maana gani. Hii ni mifano miwili tu:

Ukiwa Mjanja kuchapiwa ni siri ya ndani
Mmh muji musingi Kiuno ukishatendwa ndio byebye
 
tujadili kama hivi bial kuonekana kana kwamba tunamzibia riziki, achukue kama changamto kwa sababu najua ame invest sana hadi ukatoka
Kwangu mimi huu ni moja ya nyimbo za kijinga nilizo pata kusikia.

Siupendi kabisa na unatia aibu kusikiliza hasa ukiwa na watu wako wa heshima.

Kuna bar fulani tulikuwa tumekaa ukapigwa huu wimbo niliona watu wana angaliana kwa aibu.

Kwa kweli huu wimbo unatia aibu sana kusikiliza.
 
Ili serikali isiwe kigeugeu, kwa kuifungia ile nyimbo ya wale waliokuwa wakijiita Ngoni Tribe, ya "Wanawake wazuri wameolewa wamebaki MANUNGAYEMBE wanahangaika" basi waifungie na hii, kwani angalau ile ilikuwa ikiwakataza wanawake kuwa wahuni. Pia ile nyimbo ya "MAMBO KWA SOKSI" ya hayati DR REMMY ONGALLA ilikuwa ni ya maana zaidi katika vita dhidi ya ukimwi lakini ilifungiwa. Hii ya KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI inahamasisha watu kuvumialia wake/waume zao wanapotoka nje ya ndoa, iwe siri. Hata kama mashairi yangeongea vinginevyo hayasikiki/hayajulikani kama hicho kibwagizo cha kuchapiwa ni siri ya ndani. Lazima uwe mtaalamu wa lugha ya kiswahili uweze kutofautisha dhana, maudhi ya ndani na nje, nk. Kwa ufupi huo wimbo japo midundo na melodi yake ni yakuvutia lakini haufai...!!!
 
Nami pia nimekuwa nikisikiliza wimbo huo lakini siuelewielewi. Kwa hiyo ukichapiwa ukatunza siri ndio ujanja au?
 
Pia jamaa anamwonea sana samaki anaposema"Nimekuwa kama samaki kutamani nisivyoviweza" samaki anatamani vitu gani asivyoviweza
 
Huu wimbo ni takataka tu, generally sipendi bongo fleva, ni chache sana zenye maana mengine ni matakataka tu, melody mbovu, message uozo, yani kwa kifupi sifagiliii. lakini mavitu kama haya ndo waswahili wengi hupenda.

Poleni na wale mnaopenda manyimbo kama hayo...
 
Mnajisikiaje wimbo huu unapopigwa, tena kwa sauti kubwa, mkiwa ndani ya daladala?
 
Nami pia nimekuwa nikisikiliza wimbo huo lakini siuelewielewi. Kwa hiyo ukichapiwa ukatunza siri ndio ujanja au?

nikitafakari sana kuna igizo niliona kaka mtu akimwambia mdogo wake atembee na mkewe kwa kuwa yeye si rijali na wakasema iwe siri yao, lakn katika uhalisia mpana tafakuro tunduizi inakataa kabisa, hapa hata matumizi ya neno kuchapiwa yana taathira fulani ya uzinzi eti halafu utajua na kuifanya iwe siri.......mimi nawaza tu unaimbwa uko na wakwe zako mathalani au watoto wako wakubwa wenye uelewa na wamekuja na wake zao au hata kukawa na kesi ya kufumaniwa inaendeshwa halafu huu wombo unapigwa..........dah........pengine hata umealika wageni wako wa maana.....
 
Kupenda wimbo so lazima uelewe maana. Unaweza vutiwa na beat,rhythm n.k. Acha ubwege
aaaaaaaaaaaaaaahhhh, umeharibu mwishoni, mjibu tu kwa hoja.......
 
na kweli bhana, uswahilini unapendwa sana
Huu wimbo ni takataka tu, generally sipendi bongo fleva, ni chache sana zenye maana mengine ni matakataka tu, melody mbovu, message uozo, yani kwa kifupi sifagiliii. lakini mavitu kama haya ndo waswahili wengi hupenda.

Poleni na wale mnaopenda manyimbo kama hayo...
 
kama ulishasikiliza nyimbo za taarabu wewe unaweza kuja na tafsiri yako wenyewe wakaja na tafsiri yao sasa hapa ni bora atafutwe muimbaji atupe tafsir ya huu wimbo
 
Back
Top Bottom