Huu Utitiri Wa Gesti Mjini Songea Unaashiria Nini?!!

Huu Utitiri Wa Gesti Mjini Songea Unaashiria Nini?!!

hajatembeatembea Msamvu morogoro pale karibu na chuo cha kiislam, mtaa mzima kuna lodge hakuna nyumba ya familia hata moja, na mitaa ya sabasaba.. Huwa wanaboa kweli watu wanaojifanya wametembea nchi nzima then kufanya comparison

sijatembea nchi nzima mkuu lakini kile nilichokiona huku Songea siyo hali ya kawaida,.

Unajiuliza wenyeji nao wanaishi gesti pia?
 
Hmmmm we mtoa mada ni mgeni kabisa na Songea..tuulize wenyeji tukuambie,mpaka tunakariri guest/lodge zote ujue zipo za kuhesabika

sijakataa kuwa hazihesabiki mkuu,.

Ila ni nyingi kupita maelezo,.
 
hajafika makambi, matogoro, ruvuma, mahilo, mateka kwa mama sabena, mateka ya wayao, chemchemu, luhira iliko songea boyz, kipera n.k poor analysis.. ni sawa na mimi niende Msamvu pale Morogoro then nije nianzishe mada kuwa Morogoro kuna lodge nyingiii

mkuu kujua maeneo kwa kuyataja majina tu haiashirii kwamba unachosema ni cha kweli,.

Kote huko unapopasema hali ni hiyohiyo
 
Mleta uzi hakika huijui Songea!!! Nadhani wewe unapajua hapo stand kuu tu ndo unakuja na uzi wa guest kibao!! Umetembea wapi wewe hapo Songea? Umefika Msamala,Mshangano,Shule ya Tanga,Mlilayoyo,Hanga,Mtyangimbole,Gumbiro huko kote kuna gest utitiri?

mkuu mji wa Songea upo stendi tu?
 
wewe jibu unalotaka umeshapewa "kuwa sis wakaz wa songea ni wazinz" hilo ndio jambo unalolichokonoa indirect ili lijadiliwe hapa..je nikuulize ulifanya research ktk gest zote ukaambiwa hawataki kufanya booking ya siku nyingi? Kama hukufanya basi nawe ni mmoja ya wazinzi na wateja wa hizo gest..nahisi wewe ni mwanafunzi either wa St. augustine au st. Joseph na wengi wanafunzi wanaishi mfaranyaki, majengo, na lizaboni tu na ndio maeneo yenye gest nyingi, lakini sio songea yote, usitudanganyeee, wewe uko songea miaka miwil? Mi mwenzio tokea 2003 hadi leo na wala sitaraji kuondoka

miaka miwili Songea ni mingi sana kwa mtu mwenye kuzunguka na haichukui muda kuyafahamu maeneo mengi maana huu mji ni mdogo.

Nakushangaa sana wewe kuishi muda wote huo Songea halafu huijui,..
 
Pole sana mkuu huenda hata kufika Songea hujawahi,.
we acha mambo yako... Songea haina gesti nyingi kama unavyodai... Halafu kwa taarifa yako machimbo ndogondogo zimepelekea hata hizo chache zikawepo
 
mimi ni mkazi wa songea, gesti ni chache tu ila bodaboda{pikipiki} ndo kila kona, ukipiga hesabu kila nyumba 1 inatoa pikipiki 5
 
mimi ni mkazi wa songea, gesti ni chache tu ila bodaboda{pikipiki} ndo kila kona, ukipiga hesabu kila nyumba 1 inatoa pikipiki 5

mbona mimi sijazungumzia bodaboda mkuu,..
 
hizo nyingine zitakua nyumba za wageni na sio guest house.

Please serikali fungia viroba..:suspicious:
 
sijatembea nchi nzima mkuu lakini kile nilichokiona huku Songea siyo hali ya kawaida,.

Unajiuliza wenyeji nao wanaishi gesti pia?

acha uongo wewe. Unataka kunambia songea kati ya nyumba 3, moja lazima iwe gest. Au unataka nikutafute ili tufanye research ya mji mzima tutafute idadi gest ukiringanisha na nyumba zote..Niko songea miaka kumi, naujua huu mji kaka kama machinga, gest nyingi zipo mfaranyaki, hicho ni kitongoji kimoja tu kati za zaidi ya vitongoji 20..sasa wewe unakuja kusema eti gest ni nyingi kiasi kwamba hujui wenyeji tunaishi wapi?
 
mimi ni mkazi wa songea, gesti ni chache tu ila bodaboda{pikipiki} ndo kila kona, ukipiga hesabu kila nyumba 1 inatoa pikipiki 5

Unanikumbusha kuna jamaa alisema kuna mkutano mmoja wa chama cha siasa ulikuwa na magari mengi kuliko watu, ni sawa na hiyo ya nyumba moja boda boda 5.
 
mbona mimi sijazungumzia bodaboda mkuu,..

km ndo hivyo unawadanganya watu hakuna gesti nyingi kuzidi sehemu nyingine mfano moro,mafinga. Wewe unaonekana hujawahi kusafiri. NB: comment zako zimezidi yaani mtu asicomment na wewe unataka ucomment ndo maana post inajaa kumbe wewe mwenyewe unajaza
 
Back
Top Bottom