Huu ufa kwenye hii ndoa unazibika?

Huu ufa kwenye hii ndoa unazibika?

Furaha haipo tena wakuu nimedaiwa talaka na mke wangu usiku wa kuamkia leo, mimi mke bado namuhitaji. Chanzo cha yote(tatizo) ni mimi haihusiani na usaliti na tulishakaa vikao na familia tukayamaliza lkn mara zote toka hapo haijawahi kuisha wiki bila kununiana furaha siku 3 nne zillizobaki ni sintofahamu pamoja na kuwa anatimiza majukumu yake yote kama mke.

Usiku wa kuamkia leo baada ya kuniomba talaka yake alimpigia mama yake simu by 7 kasoro usiku kumueleza kuwa hana furaha tena! mama alikuwa na hamu ya kujua nini tatizo lkn binti alisisitiza siioni ndoa yangu tena na kukata simu ila kabla ya kukata alimuahidi kesho ntakuambia kila kitu.

Kwa hili sikuwa na namna sababu nilisharuhusu simu kupigwa japo baada ya kupiga simu nilimuomba usizungumze chochote na mama yako kuhusu hili wewe utajua namna ya kuongea ili kutuliza hali na ameniitikia kwa kunielewa, lkn sijui kichwani anawaza nini!

Nilimuahidi mimi pia nitazungumza na mama yake, jambo jingine nimemuomba nimuache peke yake kwanza nisafiri ili angalau upatikane muda wa utulivu kwanza lkn sio kumpa talaka.
Talaka ni jambo la kheri. Mruhusu aende.

Mapenzi yanaisha. Unapaswa kukubali. Utaumia lakin utazoea, maisha yataenda. Ni kheri kuumia akiwa mbali kuliko akiwa karibu.

Kuendelea kumkumbatia ni kujitafutia magonjwa na kifo.

Pole sana. Ila mpe talaka
 
Sio rahisi kihivyo wanawake wengine ni mgodi unaotembea. Unakuta mwanamke ni mchapakazi, anakupa heshima ya mume, hana makorokoro ya kando, mzuri na mtamu, hana tabia ya kuomba pesa hovyo anasolve mambo yake. Halafu wewe unakuwa mlevi pesa yake ya malengo unapigia liquor. Akikuambia anataka kusepa lazima kichwa kiwake moto
Uko sahihi kwa asilia mia mkuu
 
Yangu macho tu ya kusomea uzi na vidole vya kuandikia reply, ila hisia na akili za kushauri juu ya utoe Tanaka au usitoe wakati umeombwa talaka.. au pia niseme uzoefu Sina.
 
Uko sahihi mkuu na sababu inayonifanya nakuwa na ugumu kwenye kuamua pmj na kuwa mimi ndio tatizo ni aina ya mwanamke niliyenaye hakika ni mtu sahihi sijawahi kunusa usaliti kwake wa mapenzi yake kwangu hayajawahi kuwa na kipimo kubwa zaidi ana khofu ya Mungu
Wanao sema ww ni marioo hawapo mbali na ukweli.
 
Furaha haipo tena wakuu nimedaiwa talaka na mke wangu usiku wa kuamkia leo, mimi mke bado namuhitaji. Chanzo cha yote(tatizo) ni mimi haihusiani na usaliti na tulishakaa vikao na familia tukayamaliza lkn mara zote toka hapo haijawahi kuisha wiki bila kununiana furaha siku 3 nne zillizobaki ni sintofahamu pamoja na kuwa anatimiza majukumu yake yote kama mke.

Usiku wa kuamkia leo baada ya kuniomba talaka yake alimpigia mama yake simu by 7 kasoro usiku kumueleza kuwa hana furaha tena! mama alikuwa na hamu ya kujua nini tatizo lkn binti alisisitiza siioni ndoa yangu tena na kukata simu ila kabla ya kukata alimuahidi kesho ntakuambia kila kitu.

Kwa hili sikuwa na namna sababu nilisharuhusu simu kupigwa japo baada ya kupiga simu nilimuomba usizungumze chochote na mama yako kuhusu hili wewe utajua namna ya kuongea ili kutuliza hali na ameniitikia kwa kunielewa, lkn sijui kichwani anawaza nini!

Nilimuahidi mimi pia nitazungumza na mama yake, jambo jingine nimemuomba nimuache peke yake kwanza nisafiri ili angalau upatikane muda wa utulivu kwanza lkn sio kumpa talaka.
Relax mpe talaka baadaya hapo jenga empire yako kuwa busy ili umsahau mapem
 
Shida hasa ilikuwa pombe kiasi sikuwa nazingatia familia na hapo alikuwa mkoa mwingine kikazi hii ilileta shida kiasi hta nikashindwa kuheshimu amana zake sababu kunq wakati alipata eneo shamba nimnunulie na alinitumia milioni moja lkn sikuitimiza hii ahadi na ulitokea mzozo wa kudai talaka pia lkn tulikaa na familia tukamaliza hili kwa kuahidi kumrejeshea kiasi chake.Wakati huo mimi ni misheni town tu yy ni mujiriwa familia ikashauri itabidi ukaungane na mwenzio pmj nilikubalina na wazo hili nikajichukulia hakiba yangu kwanza nikamlipa kiasi chake nikabaki km na m hv ukiondoa maswala ya nauli na mahitaj mengine nikabakiwa km na laki 7 hivi so toka nimefika huku ni mwezi wa 4 sasa vtu havijaenda vile inavyotakiwa au ilivyopngwa.
Wiki iliyopita Kuna kiasi chake km 200000 hiv niliichukua na kumuahidi ntamrejeshea jna lkn sikutimiza hii ahadi, mara ghafla naona usiku vilio nauliza nini tatzo majibu ndio km hayo
Hapo shida ni wewe mkuu. Siwezi sema exactly ni ipi but kwa hayo maelezo yako inaonesha wewe sio mpambanaji (mvivu), hutumii akili ya ziada kwenye utaftaji bali upo upo tu, huna future plans nzuri inayoonesha mwanga mzuri kwenye maisha mbeleni, na sie wanawake hua tunawaza mbele watoto wetu wataishije, so ameona atakwenda kuteseka sana na wewe na familia huko mbeleni.

Anza kwa kumtia moyo kwa wewe kupata ajira au husle ya maana itakayomuonesha mwanga mbeleni, akifurahi hapo tu basi hatoomba taraka tena.
 
Ni dhahiri unampenda na kuachana naye nafsi inakusuta kwa sababu ni wewe umemkosea.

Fanya kile moyo wako unakusukuma kufanya, kama matatizo yanasuluhishika jaribu kutafuta busara ya kuyamaliza ila kumbuka siku zote mapenzi hayalazimishwi.
 
Mkuu,mbona humu kuna nyuzi kibao tu za wanawake wanaotafuta waume?

Au mimi ndio hua sizielewi hizo nyuzi?
Zipo nyingi ndio. Na ni kwasababu wameaminishwa kwamba bila kuolewa hawataheshimika. Ila ukweli ni kwamba ndoa inampa feva zaidi mwanaume. Mwanamke ni kijakazi tu kama sheria za ndoa ya kiafrika zaitafuatwa kisawasawa.
 
Back
Top Bottom