LiFe 2-point-0
JF-Expert Member
- Mar 22, 2024
- 4,452
- 12,235
Very painful.Kuna wanawake kama wanakuamini sana ukiwasaliti hata akisema amekusamehe bado roho itaendelea kumuuma daima milele amina. Kuna ndoa fulani ambapo mke na mume wote ni rafiki zangu, mke classmate, mume roomate wa chuo, mke alikuwa anamuamini sana mume wake kiasi aliwahi kuniambia hata angeambiwa mwamba ameonekana anatoka guest house na demu, asingeamini. Siku alipofuma msg mumewe amemtumia ela mchepuke atoe mimba, ni mwaka wa tano ila things have never been the same again.
Wanaishi wote, wana kazi nzuri wote, mke anatimiza majukumu yote, wanatengeneza miradi wanasomesha watoto, yani wote wako vizuri sana kila moja ana take home si chini ya 4mls, lakini ni kama wanaishi kwa mazoea. Mume kajaribu sana weeka mambo sawa lakini wapi. Mke anasem yuko sawa na kamsamehe lakini mtu anayewajua anaona tu wanaigiza.
Sitaki tena haya masuala ya ndoa. Sitaki tena hata kuyasikia