Huu sasa ni upendeleo wa wazi BBC

Huu sasa ni upendeleo wa wazi BBC

Ndani ya mwaka mmoja tu Kama Rais wa nchi hii na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama amefanikiwa kujenga uchumi unaomgusa kila mtanzania, angalia namna alivyogusa maisha ya wakulima kwa kuwahakikishia soko la uhakika na upatikanaji mzuri na kwa Bei nafuu pembejeo hasa mbolea baada ya kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini, amefanya mapinduzi ya huduma za Afya Elimu maji umeme na hata Miundombinu,

Balozi zetu zimeendelea kuheshimika Sana nje ya mipaka ya Tanzania, diplomasia yetu imekuwa na nguvu Sana wakati huu iliyopelekea kupata watalii na wawekezaji wengi Sana hapa nchini kutokana na ushawishi wa mh Rais wetu mpendwa kukubalika sana
We jamaa ni mtoto wake wa damu nini??
 
Acha ujinga wewe, Hivi Nani asiye Tambua kazi ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani katika ukanda huu wa Afrika mashariki na Kati? Unapozungumza Tanzania maana yake unamzungumza mama yetu Samia, Sasa utamkwepa vipi mama Samia katika kulinda amani ya ukanda huu na Afrika kwa ujumla?

Tanzania chini ya mama Samia imeendelea kuwa kimbilio la wanyonge na wanazohitaji kupumzika Kama ulivyoona Raila Odinga akina hapa Tanzania kupumzika,

Dunia inamtambua na unatambua mchango wa mh Rais wetu mpendwa kwa kupigania haki ya Elimu kwa mtoto wa kike, Hata ukienda Taasisi kubwa za kiharakati na haki za kibinadamu wanatambua Alama ya mama yetu Katika kumuwezesha mtoto wa kike kupata Elimu biila kikwazo

Dunia inatambua mchango wa mama Samia katika kupunguza vifo vya mama na mtoto baada ya juhudi zake za kuboresha huduma za Afya na kusogeza huduma karibu ya mwananchi

Dunia inatambua mchango wa mama yetu Katika kuhakikisha usalama wa chakula unakuwa imara na hata kuwalisha majirani zetu Kama Kenya wenye shida ya chakula kutokana na ukame kwao

Dunia inatambua mchango wa mama yetu Katika kupambana na mfumuko wa Bei, kuvutia wawekezaji na kuifanya Tanzania kuwa chaguo namba moja kwa mgeni yoyote atakaye kuja katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika

Mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani ndio kioo Cha Afrika kwa Sasa katika uongozi Bora na utawala wa sheria
Njaa mbaya sana aisee
 
Kweli wewe bado Sana kujuwa ulimwengu huu, Hivi wewe unawezaje kuizungumzia Afrika kiukombozi bila Tanzania? Unawezaje kuizungumzia amani ya ukanda huu bila Tanzania? Nenda kawaulize hata wachina juu ya Tanzania uone namna watakavyoizungumza kwa mambo makubwa ya kidiplomasia yaliyofanywa na nchi yetu, hata hicho kiswahili kupata ushawishi Afrika na dunia kwa ujumla Ni ushawishi na nguvu za diplomasia ya Tanzania yetu Hii imara na kimbilio la wanyonge,

Unazani hata hao wakimbizi wakinyarwanda na kiburundi walifika hapa na kukaa kwa bahati mbaya? Tanzania Ni ziwa na bahari ya matumaini, utakufa na wivu wako,

Tanzania Ni imara Sana chini ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani
AMANI

TANZANIA

NJAA

MARADHI
VIFO

HUDUMA MBOVU ZA MAJI...

ELIMU DUNI...

AMANI karume au amani Massawe .... Au amani yupi
 
Wewe kwa ndoto zako ndio wasema hayo lakini Dunia inamuangalia mama Samia Kama tumaini jipya la uongozi wenye kuleta matumaini kwa watu wote, ANaangaliwa Kama kiongozi wa kuigwa, anaangaliwa Kama kiongozi mwenye ushawishi mkubwa Sana hapa Afrika na hata nje ya Afrika kwa sasa
Anaweza kumshawishi nani huyo dikteta huko duniani ilihali ya huku kwake tu yamemshinda?
 
Tumepoteza ushawishi katika jumuia za kimataifa kwa kuamua kuwa vibaraka wa mabeberu.

Beberu keshatuweka mfukoni hatuna tena cha kuwaambia bali sisi tunayo ya kuambiwa na wao na shurti tuyafuate.
Beberu an mfuko mkubwa kiasi gani kiasi wote tuingia na kukaa mfukoni humo?
 
Nimefuatilia matangazo ya bbc kutoka London. Naona wanajitahidi kuwafanyia mahojiano viongozi wa kike akiwemo waziri mkuu wa Bangladesh na PM wa New zealand.

Ila sijaona mama yetu ambaye ni Rais kabisa akitafutwa na kuhojiwa. Isitoshe ameingia London mapema sana jana huku. Je huu sio upendeleo wa wazi? Kweli mawaziri wakuu ni muhimu kuliko Rais tena mwanamke?
Kapeto ni wa hapahapa nyumbani
 
Kama ubalozi wenu haukufanya pr ya kutosha na maandalizi ya interview hilo haliwezi kutokea. Maandalizi yanafanyika kabla. BBC hawa google kujua nani kaja, nani ana muda na nani yuko tayari kuulizwa nini
 
Nimefuatilia matangazo ya bbc kutoka London. Naona wanajitahidi kuwafanyia mahojiano viongozi wa kike akiwemo waziri mkuu wa Bangladesh na PM wa New zealand.

Ila sijaona mama yetu ambaye ni Rais kabisa akitafutwa na kuhojiwa. Isitoshe ameingia London mapema sana jana huku. Je huu sio upendeleo wa wazi? Kweli mawaziri wakuu ni muhimu kuliko Rais tena mwanamke?
Kila mtu na nyota yake hio sio TBC, some of those interviews are pre arranged self initiative of interviewees, visibility has to be fought for, if you care and value you will look for the journalists. But what for it depends any way!!
 
Hakuna amayekutawala wewe mtu mweusi ngedere unatawaliwa na udumavu WA akili , ubinafsi , tamaa , wivu ,majungu , uvivu , ukosefu WA maono , uzezeta , wizi na lundo la tabia nyingi mbovu ulizonazo .
Inauma ila ndio ukweli halisi, hailazimu kuwa PhD holder kulijua hilo
 
Huyo mama yenu hakualikwa official, ni kiherehere tuu. Marais walioalikwa ni watatu Ghana, Gabon na SA.
 
Alienda kufanya nini nani alimuambia aende.!?

Kuna ishu zingine ni za kuzipotezea tu kama wahusika hawajaamua kukushirikisha.

Tuachage viherehere.

We have to be proud of ourselves.
 
Kwenye misiba hata hapa kwetu huwa kuna yale mapaka ambayo yanazunguka tu kuvizia chakula, saa nyingine huwa yanaachwa tu...anyway sijui hata nilitaka kusema nini
 
Acha ujinga wewe, Hivi Nani asiye Tambua kazi ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani katika ukanda huu wa Afrika mashariki na Kati? Unapozungumza Tanzania maana yake unamzungumza mama yetu Samia, Sasa utamkwepa vipi mama Samia katika kulinda amani ya ukanda huu na Afrika kwa ujumla?

Tanzania chini ya mama Samia imeendelea kuwa kimbilio la wanyonge na wanazohitaji kupumzika Kama ulivyoona Raila Odinga akina hapa Tanzania kupumzika,

Dunia inamtambua na unatambua mchango wa mh Rais wetu mpendwa kwa kupigania haki ya Elimu kwa mtoto wa kike, Hata ukienda Taasisi kubwa za kiharakati na haki za kibinadamu wanatambua Alama ya mama yetu Katika kumuwezesha mtoto wa kike kupata Elimu biila kikwazo

Dunia inatambua mchango wa mama Samia katika kupunguza vifo vya mama na mtoto baada ya juhudi zake za kuboresha huduma za Afya na kusogeza huduma karibu ya mwananchi

Dunia inatambua mchango wa mama yetu Katika kuhakikisha usalama wa chakula unakuwa imara na hata kuwalisha majirani zetu Kama Kenya wenye shida ya chakula kutokana na ukame kwao

Dunia inatambua mchango wa mama yetu Katika kupambana na mfumuko wa Bei, kuvutia wawekezaji na kuifanya Tanzania kuwa chaguo namba moja kwa mgeni yoyote atakaye kuja katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika

Mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani ndio kioo Cha Afrika kwa Sasa katika uongozi Bora na utawala wa sheria
Hivi hujui kuwa kuna nchi ukienda hawajui hata kuna nchi inayoitwa Tanzania hapa duniani???!!! Sembuse kumfahamu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan!!!!!
 
Back
Top Bottom