Muda wa kuamka ni sasa

Muda wa kuamka ni sasa

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
16,046
Reaction score
9,540
(Emancipate from mental Slavery)

Watanzania kwa ujumla wetu bado tumelala usingizi mzito tukiota ndoto za jinamizi kuhusu mustakabali wa Taifa letu.

Mambo nayoyasoma na kuyasikia yakitoka vinywani na maandishi kusema kweli ni aibu kwa taifa ambalo waasisi wetu walitujengea misingi bora ya Taifa letu. Leo hii tumezama katika ombwe la Ubaguzi ambao tunaivunja misingi hiyo makusudi kama kwamba tumechoka, liwalo na liwe.

Kuna haya mambo mawili nayasoma na kuyasikia sana yakinadiwa bila hekima chini ya mwanvuli wa UDINI na UKANDA katika majukwaa ya mihadhara mbali mbali ya Kijamii tena wazi kabisa huhitaji elimu ya saikologia.

Leo hii kuna watu hawaoni aibu kabisa kuzungumzia Uzanzibari na Utanganyika, wala hawana uso wa soni kutuonyesha wazi chuki zao kwa Waislaam ama Wakristu kama kwamba ni jambo la kheri kabisa kwa ulinzi wa jamii zao ama Taifa hili.

Binafsi kuna wakati hudhani pengine mimi ndiye naota ndoto hizi kwa sababu misingi tuloachiwa na Waasisi wetu ilikuwa thabiti haiwezekani kabisa ikavunjwa kupitia Ubaguzi wa aina yeyote.

Niseme hivi, kama kweli sababu ya migongano yote hii ni rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwanamke, Mzanzibar na Muislaam basi yawapasa Wanawake, Wazanzibar na Waislaam wote wasimame naye kwa sababu ni mwenzao, ama iwe Wanaume, Watanganyika na Wakristu wasimkubali rais huyu kwa sababu sii mwenzao!

Basi huu utakuwa ni Upumbavu mkubwa ulopita vipimo vyote vya mapana na marefu. Ni Upumbavu uso kifani ambao mwalimu Nyerere alituasa mapema kabisa katika moja ya hutuba zake. Tunachotakiwa ni kumlaani shetani alochukua nafsi zetu kwa ahadi hizi za kutupeleka Jahanam hapa hapa duniani tukiwa hai ndotoni kabla hata ya Kiyama!

Kibaya zaidi, leo tunashuhudia baadhi Viongozi ama Wanasiasa wakizungumzia Uzanzibar wakidai nchi yao sii kwa sababu nyingine ya maana isipokuwa kuwakana Watanganyika na Wakristu! Vile vile Upande wa Bara pia kuwakana ndugu zao kwa sababu ni Wazanzibar na Waislaam - Heeee!

Mimi nitoe rai yangu kwa watu wote wanaotumia Dini na Ukanda kutaka kutugawa Watanzania kwa sababu ya nia na dhamira zao chafu ambazo aidha wanadhani hili ndio koti lilowabana, nawashauri wajipime wenyewe upya isije kuwa wao ndio wamenenepa sana ama wamekondeana kiasi cha kuhatarisha afya zao.

Yawezekana kabisa rais Samia ana mapungufu mengi kama kiongozi wa nchi, lakini inapotumiwa sababu za Udini na Ukanda kuashiria ndio sababu za mapungufu yake, basi haya mapungufu sii yake yeye bali ya wale wanao mshutumu. Vile vile kwa wale wanaomsifia Samia wasiyaone mapungufu yake kwa sababu hizo hizo nao pia wamepikwa chungu kimoja.

Amkeni, amkeni Watanzania toka usingizi wa pono unatesa ndoto zetu tukifukuzwa na jinamizi baya lilojaa hasada mpaka tunapaa hewani na ufagio bado likiwa nyuma yetu.

Maasalaam
 
Watanzania wanakoroma na usingizi wa porno.

Kama taifa hakuna kitu kinacho tu unganishwa...

Kuna dini na michezo tu ambavyo havina uhusiano wowote na mustakabali wa maendeleo ya kijamii.
 
(Emancipate from mental Slavery)

Watanzania kwa ujumla wetu bado tumelala usingizi mzito tukiota ndoto za jinamizi kuhusu mustakabali wa Taifa letu.

Mambo nayoyasoma na kuyasikia yakitoka vinywani na maandishi kusema kweli ni aibu kwa taifa ambalo waasisi wetu walitujengea misingi bora ya Taifa letu. Leo hii tumezama katika ombwe la Ubaguzi ambao tunaivunja misingi hiyo makusudi kama kwamba tumechoka, liwalo na liwe.

Kuna haya mambo mawili nayasoma na kuyasikia sana yakinadiwa bila hekima chini ya mwanvuli wa UDINI na UKANDA katika majukwaa ya mihadhara mbali mbali ya Kijamii tena wazi kabisa huhitaji elimu ya saikologia.

Leo hii kuna watu hawaoni aibu kabisa kuzungumzia Uzanzibari na Utanganyika, wala hawana uso wa soni kutuonyesha wazi chuki zao kwa Waislaam ama Wakristu kama kwamba ni jambo la kheri kabisa kwa ulinzi wa jamii zao ama Taifa hili.

Binafsi kuna wakati hudhani pengine mimi ndiye naota ndoto hizi kwa sababu misingi tuloachiwa na Waasisi wetu ilikuwa thabiti haiwezekani kabisa ikavunjwa kupitia Ubaguzi wa aina yeyote.

Niseme hivi, kama kweli sababu ya migongano yote hii ni rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwanamke, Mzanzibar na Muislaam basi yawapasa Wanawake, Wazanzibar na Waislaam wote wasimame naye kwa sababu ni mwenzao, ama iwe Wanaume, Watanganyika na Wakristu wasimkubali rais huyu kwa sababu sii mwenzao!

Basi huu utakuwa ni Upumbavu mkubwa ulopita vipimo vyote vya mapana na marefu. Ni Upumbavu uso kifani ambao mwalimu Nyerere alituasa mapema kabisa katika moja ya hutuba zake. Tunachotakiwa ni kumlaani shetani alochukua nafsi zetu kwa ahadi hizi za kutupeleka Jahanam hapa hapa duniani tukiwa hai ndotoni kabla hata Kiyama!

Kibaya zaidi, leo tunashuhudia baadhi Viongozi ama Wanasiasa wakizungumzia Uzanzibar nankudai nchi yai sii kwa sababu nyingine ya maana isipokuwa kuwakana Watanganyika na Wakristu! Vile vile Upande wa Bara pia kuwakana ndugu zao kwa sababu ni Wazanzibar na Waislaam.

Mimi nitoe rai yangu kwa watu wote wanaotumia Dini na Ukanda kutaka kutugawa Watanzania kwa sababu ya nia na dhamira zao chafu ambazo aidha wanadhani hili ndio koti lilowabana, nawashauri wajipime wenyewe upya isije kuwa wao ndio wamenenepa sana ama wamekondeana kiasi cha kuhatarisha afya zao.

Yawezekana kabisa rais Samia ana mapungufu mengi kama kiongozi wa nchi, lakini inapotumiwa sababu za Udini na Ukanda kuashiria ndio sababu za mapungufu yake, basi haya mapungufu sii yake yeye bali ya wale wanao mshutumu. Vile vile kwa wale wanaomsifia Samia wasiyaone mapungufu yake kwa sababu hizo hizo nao pia wamepikwa chungu kimoja.

Amkeni, amkeni Watanzania toka usingizi wa pono unatesa ndoto zetu tukifukuzwa na jinamizi baya lilojaa hasada mpaka tunapaa hewani na ufagio bado likiwa nyuma yetu.

Maasalaam
kweli kabisa.
 
Nyerere ndio essence ya matatizo yote haya.Kwani angeiacha Zanzibar kando Tanganyika haya mauza uza yangetokea wapi.

Burundi na Rwanda ambazo zilikuwa sehemu ya Germany east colony hakuziona?.Wazanzibar tofauti na lugha ya kiswahili kitu gani kinatuleta pamoja.Wenyewe hawana na hawajawahi kuwa na furaha na huu muungano kwanini tuwalazimishe.

Kama ni muungano mbona Zanzibar inatambulika lakini Tanganyika inabaki tu kuwa Tanzania bara(kitu ambacho sijui kilitokea wapi hiki,hakuna taifa lolote linaloitwa Tanzania bara).

Nyerere alikuwa mshenzi na ndio chanzo lakini kwa haya ya sasa Magufuri namba moja,Kikwete namba mbili na Mkapa anafuata.Mwinyi anaweza kuwa na haueni
 
Ndio nasema ondokeni katika ndoto hizi kwa sababu hiyo Tanganyika ni mipaka ya Wakoloni. Historia yetu Hapakuwa na nchi yenye mipaka ya Tanganyika wala Zanzibar kwa sababu neno Zanzibar limetokana na wageni Waajemi waloita ardhi hii 'NCHI ya WEUSI' Sasa ikiwa Zanzibar ni nchi ya weusi wewe umewezaje kujua mipaka yake kama sio ile ulivyofunzwa na Wakoloni? Please know your History first..

Je unajua kwamba pwani yote ya Bara ilikuwa sehemu ya Zanzibar KABLA kabisa ya wakoloni Wajarumani na Waingereza kuja? Hili jina Tanganyika limekuja itwa na Waingereza tena baada ya vita ya kwanza ya dunia. Je, hii nchi iliitwaje au haikuwepo kabla ya vita kuu ya kwanza? Hapakuwa na nchi za Tanganyika, Rwanda na Burundi wakati wa Mjarumani, unaongopewa!

Wewe kama Mtu mweusi, unawezaje kuitenga Zanzibar kwa sababu ya mipaka hiyo kama hufanani na Wasouth Afrika ambao leo wanatuona Watanzania kama foreigners! Unadhani haya ni mawazo yao wao ama wamepikwa! Hizi Siasa za aina hii mnazotupeleka wapi?

Jiulize kwa nini nchi zote za Ulaya leo, zinaweka sheria kali kwa wahamiaji wote kutoka Afrika na wengine wanasakwa na kufukuzwa hadi wajumbani warudi Afrika! Je, trend hii sisi tutapona kweli maana wenzatu tayari wameshakula nyama za watu. wee pia unataka kuonja nyama ya mtu?
 
Ndio nasema ondokeni katika ndoto hizi kwa sababu hiyo Tanganyika ni mipaka ya Wakoloni. Historia yetu Hapakuwa na nchi yenye mipaka ya Tanganyika wala Zanzibar kwa sababu neno Zanzibar limetokana na wageni Waajemi waloita ardhi hii 'NCHI ya WEUSI' Sasa ikiwa Zanzibar ni nchi ya weusi wewe umewezaje kujua mipaka yake kama sio ile ulivyofunzwa na Wakoloni? Please know your History first..

Je unajua kwamba pwani yote ya Bara ilikuwa sehemu ya Zanzibar hata baada ya wakoloni Wajarumani na Waingereza kuja? Hili jina Tanganyika limekuja itwa na Waingereza teba baada ya vita ya kwanza ya dunia. Je, hii nchi iliitwaje au haikuwepo kabla ya vita kuu ya kwanza?

Wewe kama Mtu mweusi, unawezaje kuitenga Zanzibar kwa sababu ya mipaka hiyo kama hufanani na Wasouth Afrika ambai leo wanatuona Watanzania kama foreigners! Unadhani haya ni mawazo yao wao ama wamepikwa!

Jiulize kwa nini nchi zote za Ulaya leo, zinaweka sheria kali kwa wahamiaji wote kutoka Afrika na wengine wanasakwa na kufukuzwa hadi wajumbani warudi Afrika! Je, trend hii sisi tutapona kweli maana wenzatu tayari wameshakula nyama za watu.l, wee pia unataka kuonja nyama ya mtu?
Safi kabisa tuondokane na mipaka ya wakoloni na historia zao.Sasa naomba nirudishiwe Buhaya kingdom maana hata hiyo Tanganyika sio kitu tena.

Hivyo hivyo makabila mengine yadai tawala zao maana haya yote ya sasa ni ubatili mtupu(si unasema nijue historia yangu)

Sasa waafrika kama hawatakiwi ulaya unataka wabaki kufanya nini huko?yani mwenye nyumba anakwambia ondoka kwangu unaanza kuuliza maswali ya kwanini ulijenga nyumba.Ulishasema ni waafrika sasa huko Ulaya wameenda kufanya nini?
 
Haya wewe umeongeza na UKABILA. Je ukiambiwa Wahaya walitokea Uganda utasema wakurudishe Uganda au wakupe Uganda yako? M7 anasubiri jibu😂😂😂
 
Unajua jina la Afrika limetokana na nini? Ndugu yangu ebu punguza munkhar maana majina tunapewa na watu sii UTU wa binadamu.
Hata Yesu, anaitwa Issa na Waislaam wengine wakuita Jesus ila nakuhakikishia kama huyo Yesu angekuwa leo mtaani na watu wakamwita majina hayo asinge geuka maana sii majina yake halisi alopewa na wazazi wake!
- Sijui tunaelewana?
 
Huu sio ukabila ni utambulisho wangu.Hilo neno ukabila yule babu wa Butihama alilitumia vibaya sana kwa sababu alikuwa anajua kwamba alikuwa na mapungufu mengi kukalia nafasi aliyokuwa nayo.

Wahaya sio sehemu ya Uganda.Buhaya kingdom na Buganda kingdom kweli zilikuwa mwingiliano lakini mipaka ilikuepo na watawala walikuwa tofauti kabisa
 
Kabila sii Utambulisho labda kama unataka kutambika! Utu wako hauna kitambulisho zaidi ya maumbile yako ambayo kwa mantiki ya kisayansi ni tofauti na hata ndugu pacha wako wa tumbo moja.
 
Kiongozi kuanza ku-trace neno Africa limetoka wapi na linaenda wapi unataka kunipa kazi ya kurudi darasani sasa.Hoja ya msingi ni hao wanaofukuzwa ulaya wametoka wapi?walipotoka ndiko warudi acha janja janja
 
Kabila sii Utambulisho labda kama unataka kutambika! Utu wako hauna kitambulisho zaidi ya maumbile yako ambayo kwa mantiki ya kisayansi ni tofauti na hata ndugu pacha wako wa tumbo moja.
Kaka ujue wewe ni mkongwe humu nilitakiwa niwe najifunza kwako lakini sasa hapa umenichosha kabisa

Kabila sio utambulisho wangu?How?
Kwanini kabila langu lisiwe utambulisho wangu?.Utu na maumbile yangu ni mada nyingine hapa umezalisha.Mada ya msingi ilikuwa kujua historia yangu.

Historia yangu inaanza kueleza mimi ni nani pia inafuata historia ya familia yangu,ukoo wangu na kabila langu(Hii ndio historia uliyosema nijue)
 
Huu sio ukabila ni utambulisho wangu.Hilo neno ukabila yule babu wa Butihama alilitumia vibaya sana kwa sababu alikuwa anajua kwamba alikuwa na mapungufu mengi kukalia nafasi aliyokuwa nayo.

Wahaya sio sehemu ya Uganda.Buhaya kingdom na Buganda kingdom kweli zilikuwa mwingiliano lakini mipaka ilikuepo na watawala walikuwa tofauti kabisa
Buhaya na Buganda kama ulivyosema ni kingdom yaani tawala sii asili ya watu hao, isitoshe Buhaya Kingdom haikuwa utawala kwa Wahaya wote!
 
Mhaya ambaye hayuko ndani ya Buhaya huyo sio mhaya.Ukianza kutafuta chimbuko la kila mtu utarudi either kwenye jamii za nyani au kwa Adam(mada itakuwa ndefu hii)
 
Back
Top Bottom