Huu ndiyo mkakati mzima wa CCM kuidhoofisha CHADEMA...

Wanaosema kukomboa nchi kwani imetekwa au ni ukombozi gani mnaozungumza!zungumzieni mageuzi sio ukombozi!!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Juzi wamekutana kwa siri maeneo fulani Ubungo.


Katika kikao cha jana ambacho ring leaders wote wawili walihusika,walilenga kufanya tathmini ya press conference ya juzi ile ya watu waliowakodi kutoka maeneo mbalimbali.

Kwanza wakasitika sana kwamba mkakati wao wa kukodi watu na kujifanya ni wajumbe halali wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ulikuwa umefeli vibaya kwa namna mbili.

1. Hawakupata coverage ya maana. Vyombo vyote makini vya habari vilijitenga na habari ile baada ya kugundua ni mkakati wa CCM kutumia mamluki, wasaliti na vibaraka kuharibu siasa nchini.

2. Hawakupata watu genuine. Kwamba kwenye tamko imeandikwa wako 78 lakini waliosaini ni watu 32.

Katika watu hao 32 wengine majina yao yalikuwa forged tena kwa kukosewa(mathalani yule kiongozi Khalid kutoka Tanga. Kuna wengine walisemwa wanatoka Singida lakini hawakubaliani nao na wengine wala majina yao hayapo
kabisa miongoni mwa viongozi wa Chadema achilia mbali kuwa wajumbe wa kikao chochote tena vikubwa kama Baraza Kuu na Mkutano Mkuu).

Pia wakalaumiana sana kwa jinsi tamko la juzi lilikosa 'radha' ya largeness kwa sababu fedha zilitafunwa vibaya sana na hivyo 'askari wa kukodiwa' kutoka Lindi ambao walipaswa kuwepo kwenye tamko hawakufika. Kwa sababu walikataa kupokea fedha kidogo walizopewa.

Mkakati ulikuwa kila atayekuja kwenye press ya juzi apate Tshs. 100,000; wao wa Lindi na Mtwara wakadhulumiwa sana. Wakagoma kuja.

Wakakubaliana fedha za kuhongwa ziongezwe. MM na M1 waongeze fungu la hela kwa ajili ya kuhonga na kununua viongozi genuine wa CHADEMA kwani kutegemea mamluki au watu wasiokuwa viongozi genuine kutawagharimu na kunaipatia ahueni CHADEMA kuwajibu na kushughulika nao!

Way forward

Naomba ni-summarize maana yaliyopo ni mengi, wakakubaliana kwamba leo waende kwa Msajili wa Vyama Vya Siasa ili eti wapeleke madai yao kwamba afanyie kazi tuhuma wanazotengeneza za madai ya ufisadi na kwamba Chadema
wasifanye kazi zao za siasa.

Pia waende kwa CAG kumtaka arudie tena ukaguzi kwenye mapato na matumizi ya CHADEMA. Hii inatokana na MM kuaibika baada ya CAG kushindwa kubaini tatizo lolote kwa CHADEMA alipofanya ukaguzi na kutoa ripoti hivi karibuni.

Sasa MM hataki kuumbuka kwa tabia yake ya unafiki na kusema uongo.

Ikumbukwe lengo kuu la mkakati huu ni mwendelezo wa ule Waraka wa Siri.
Safari hii viongozi wa CCM wako wazi wazi kabisa wakishiriki.

Lengo kuu ni ku-demobilize na ku-destibilize kabisa CHADEMA ili isifike au ifike mwaka kesho ikiwa hoi huku viongozi wake. Lengo jingine ni kupunguza au kumaliza kabisa nguvu za Mwenyekiti wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Slaa.

Kwa sababu watu hao mamluki wa CCM wanakiri kuwa CHADEMA chini ya viongozi wake hao makini na imara ikifika mwaka kesho itakuwa hatari sana na CCM itakuwa imeng'oka madarakani.

Hawako tayari kuona CHADEMA imara chini ya uongozi makini kama ilivyo leo ikifika kwenye uchaguzi mwaka huu na mwaka kesho! Maana itakuwa ni vigumu kuishinda na status quo kuendelea.

MM ameendelea kupewa majukumu ya kuleta pesa (maana tayari zipo nyingi sana wameshapewa). Yeye pia ndiye anayehusika na kuandika mchanganuo wa pesa hizo.

CCM itaizindua ACT Julai Mosi huko Kigoma.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Julius Malema.


Katika kikao hicho wajumbe walionekana kusikitishwa sana na kushindwakupata brains za CHADEMA hasa watu kama Tundu Lissu, John Mnyika, EzekiaWenje, Peter Msigwa na watu wengine wakiwemo wabunge makini. Kwamba kushindwa huko kuwapata watu kama hao ni pigo kubwa sana kwao.

Wakasema kuwa wabunge wanaoonekana kuwa na MM ni Viti Maalum (majina yalitajwa) ambao wengi wanaonekana hawana impact yoyote.

Wakalalama sana kumkosa Halima Mdee. Wakasema amekuwa akimwambia MM kuwa wako wote kumbe anawang'ong'a masikio. Wameishia kumtamani.

Sasa leo wanaweza kufanya press conference tena.

Lakini tunaomba kuwaambia Watanzania sasa mchawi wao ambaye anataka kukwaza ndoto zao mabadiliko ya mfumo na utawala kujikomboa mikononi mwa mafisadi na ufisadi, anajibainisha zaidi.

Wanyonge wa Tanzania sasa semeni basi kwa unafiki huu wa genge la akina Zitto, Kitila na wenzao ambao wameamua kufanya kazi ya CCM kwa nia ovu kabisa ya kutaka kuua upinzani nchini kwa kupitia janja janja ya ACT...chama fake cha upinzani.

Naomba nisisahau jambo moja kwamba wamepanga kuzunguka nchi nzima kununua na kuhonga viongozi wa CHADEMA kwa kutumia mabilioni ya fedha ambayo hadi sasa wanaojua zinakopatikana ni MM na M1 pekee!


...TAARIFA FUPI YA KIKAO CHA ACT CHA TAR 22/06/2014...

Kilichojiri juu ya kikao cha ACT kilicho fanyika j2 ya tarehe hiyo....,Dr Kitila Mkumbo ndie aliyekuwa M/kiti wa Kikao tajwa.Kikao hicho kiliwashirikisha viongozi kadhaa walio simamishwa uongozi CHADEMA katika jimbo la Kinondoni akiwepo aliye kuwa M/kiti wa Jimbo la Kinondoni PAULO WAZIRI na KALAMA KAILA ambao hawa wote walisimamishwa uongozi kulingana na utendaji mbovu ndani ya chama. Katika kikao hicho pia kilia wachagu watajwa hapo juu kuwa viongozi wa ACT kwa Jimbo la Kinondoni...na walikabidhiwa kadi za ACT kama wanachama halali.Pia MOSES RAYMOND aliteuliwa kuwa mwenezi na ndie mratibu mkuu wa Vikao vyote na mikutano ya ACT itakayo fanyika DsM.

Wajumbe walioshiriki hawapungui 16 ila nisiwataje kwa sababu maalumu za kiuchunguzi.Jimbo la Kawe amekabidhiwa MANASE BUSA ambae alimuhakikishia Dr Mkumbo kuwa Jimbo hilo halitarudi CHADEMA..wapo baadhi ya wajumbe ambao
hawakupenda kujionesha mapema ilawamesema watatoa ushirikiano wa kutosha pale utakapo hitajika....Mfano Mzee Kayombo aliyekuwa M/kiti wa Kata ya Makumbusho na Mateleka aliyekuwa kiongozi wa Kata ya Ndugumbi.....

MAAZIMIO YA KIKAO
- Kuhakikisha chama kina kuwa kwa kasi kwa kuanzia na jimbo la Kinondoni

- Kutafuta ofisi ya jimbo na kwa kuanzia wamepanga ofisi ya Kata ya Tandale ya CHADEMA kuilipia mara tu kodi itakapo kwisha

- Kupeperusha bendera za ACT katika vijiwe vya CDM walivyo jenga kwa nguvu zao.mfano MAPESA ambae ni M/kiti wa kata ya tandale ameahidi kutoa kijiwe kimoja.

- Kumshawishi Zitto agombee jimbo la Kinondoni.

- Kufanya ziara nchi nzima kuanzia tar2 mwezi wa9 siku ambayo Zitto atarudisha kadi ya CHADEMA.....swala la Ubunge wake litajadiliwa kikao kijacho cha tarehe 29 mwezi huu....

Watashindwa vibaya wasaliti hawa
 
Naona watu wengi mmeweka siasa pembeni na kumpa Dr Kitila ushauri wa kumsaidia yeye na Familia yake.

Ni vigumu sana kuangamiza upinzani nchini kama anavyotamani iwe.Nyakati hizi ni zama nyingine kabisa.

Yaan kafilisika mpaka anatia kinyaa. Majina mengine ni hatari sana "MKUMBO" hata udokta wake ni wa mkumbo tu ndo maana CHADEMA walipofanya scanning wakadetect virus... Halafu bila aibu eti anapambana na waliomlea
 
Yaan kafilisika mpaka anatia kinyaa. Majina mengine ni hatari sana "MKUMBO" hata udokta wake ni wa mkumbo tu ndo maana CHADEMA walipofanya scanning wakadetect virus... Halafu bila aibu eti anapambana na waliomlea

Mkuu umeongea mambo mazito sana.Niishie tu hapo!
 
Uwongo na uzushi ndio silaha ya wajinga duniani kote. Fanyeni kazi ya kujenga chama chenu. Acheni kujitungia uwongo na kuzusha mambo. Hatuna muda huo wa kijinga. Nchi hii ni nchi huru yenye kufuata mfumo wa vyama vingi, hakuna namna unayoweza kulazimisha mtu kupenda au kuchukia chama chako au cha mtu mwingine.

Daktari,
Ukitlia maanani kuwa aliyoyaandika crashwise yametokea kweli (nazungumzia habari ya "wana CHADEMA" kwenda kwa msajili na CAG), uongo na uzushi unaousema wewe hapa ni upi? Nakubaliana na wewe kuwa mtu halazimishwi kupenda chama, lakini mbona kila unachokiandika tangu ufukuzwe CHADEMA kinaonekana kuhusu CHADEMA zaidi ya chama chako kipya (ACT)?
 
ubinadamu bora ni kulinda heshima na kuwa na misimamo thabiti Dr Kitila mkumbo plz rudi ktk taaluma kwani ni HESHIMA zaidi//

What if huyo unaemshauri anajua kuwa kwenye taaluma ni misfit? Mwenye taaluma ambae ni competent asingefika hapo alipofika in the first place!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu crashwise,
Umenifurahisha sana, ni kama vile wewe ulikuwa mjumbe kwenye kikao vile!!!!! kazi kweli kweli.
 
Kitu cha kujiuliza hivi Zitto ataendelea kutegemea pesa za kuhongwa na CCM hadi lini?
 
Wabongo wengi wanafiki,kila mtu anatafuta nafasi ya kula pesa za nchi.Sidhan kama hao chadema wakichukua nchi hawatakuwa mafisadi kama hawa wengine.Sihitaji mtu wa kupigania maisha yangu ntajipigania mwenyewe.
Poor Politics

You are missing the point here! Mabadiliko tunayoyataka sio ya CHADEMA kuchukua nafasi ya ccm halafu status quo ikabaki. Tunataka uwajibikaji ambapo walio madarakani watawajibika kwa wananchi na wakishindwa watolewe madarakani. We need functional internal controls ili chama kiwacho chote kikiwa madarakani kisi-act with impunity kama genge hili la kina kikwete!

Unajidanganya unapoamini kuwa utaweza kujipigania mwenyewe na kufanikiwa kama mfumo wa utawala wa sheria haufanyi kazi yake inavyotakiwa. Kama kila mtu atajipigania mwenyewe public goods zitatoka wapi? Ungana na sisi katika mapambano ya kudai mabadiliko ili kila mtu apate fursa sawa ya kutumia uwezo wake kujiletea maendeleo!
 
Daktari,
Ukitlia maanani kuwa aliyoyaandika crashwise yametokea kweli (nazungumzia habari ya "wana CHADEMA" kwenda kwa msajili na CAG), uongo na uzushi unaousema wewe hapa ni upi? Nakubaliana na wewe kuwa mtu halazimishwi kupenda chama, lakini mbona kila unachokiandika tangu ufukuzwe CHADEMA kinaonekana kuhusu CHADEMA zaidi ya chama chako kipya (ACT)?

Mkuu wangu nikurekebishe kidogo.Walioenda kwa msajili siyo wanachadema bali ni wanachama wa CCM kupitia ACT ambao ni waganga njaa na wachumia Tumbo.
 
Kitu cha kujiuliza hivi Zitto ataendelea kutegemea pesa za kuhongwa na CCM hadi lini?

Muda wake umefika. Hata ccm wenyewe watagundua kuwa zito hana influence waliyokuwa wanam-credit nayo. Wote (ccm na zito) wali underestimate fact kuwa nguvu na umaarufu wa zito ulitokana na yeye kuwa ndani ya CHADEMA, nje ya CHADEMA zito si lolote wala chochote!
 
Back
Top Bottom