Huu hapa Ukweli uliojificha kumhusu Mlalamikaji Mnafiki Fiston Mayele na Lawama zake za Kurogwa na Waganga wa Yanga SC

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
Fiston Mayele yuko sahihi kwa 100% kwani Waganga Wawili Wakubwa wa Yanga SC mmoja akitokea Kisiwani Zanzibar na mwingine akitokea Kusini ( Mtwara na Lindi ) ni tatizo na sababu ya Kinachomkuta.

Taarifa za uhakika ambazo GENTAMYCINE nimepewa na Mmoja wa Wachezaji wa Ndani ( Mzawa ) wa Yanga SC na Kiongozi Mwandamizi Mmoja wa Yanga SC ni kwamba Fiston Mayele alikubali Mwenyewe kuwa Mbeba Majini ya Ufungaji kwa Sharti Kuu kuwa kila akifunga tu Goli awe anaomba na analazimisha Kutoka ili aingie mwingine asiharibu Utaratibu wa Kiushirikina.

Taarifa zaidi zinasema kuwa alichokisahau na kinachomtesa sasa Fiston Mayele ni kwamba Ushirikina aliofanyiwa na hao / hawa Waganga Wawili Wakubwa wa Yanga SC ulikuwa ni kwa ajili ya Nyota ya Yanga SC tu pekee na hilo Jini lake Lilinuiwa kuifanikisha Yanga SC kwa Magoli yake mengi na ya Ajabu Ajabu aliyokuwa Akiyafunga kwa msaada mkubwa wa Majini aliyobebeshwa.

GENTAMYCINE nimeendelea Kujulishwa kuwa kumbe hata Jezi ya Fiston Mayele na Viatu vyake ( Njumu ) vilikuwa vinalala kwa Waganga ili Wazitengeneze Kiushirikina na awe na Nguvu za Ajabu, Atishe Mabeki na Aogopwe nao na awe Anafunga mno Kitu ambacho Kilifanikiwa kwa 99.9%

Kwa sasa anachotakiwa Kukifanya Fiston Mayele ni ama kuja Tanzania ili Ategue Uchawi / Ishirikina mkubwa Alioufanya na Aliofanyiwa kisha kama Uwezo wake wa Kiuchumi unamruhusu basi aondoke na Mmoja wa hawa Waganga Wawili ili akaishi nae huko nchini Misri na aweze Kumsaidia kwani hata akifanyiwa kutokea Tanzania hatofanikiwa kwakuwa kamwe Uchawi hauvuki Bahari.

Mwishoni nikamaliziwa kuambiwa kuwa karibia 99% ya Timu Kubwa za Simba na Yanga huwa zinategemea mno Majini ya Kutuma na Kutekeleza huku Majini ya Yanga SC yakiwa ni ya Kike yanayopenda Kutumia Damu za Hedhi za akina Dada / Mama huku Simba SC ikiwa inatumia zaidi Majini ya Kiume ambayo hupenda sana Kuua na Kujeruhi vibaya ( Wachezaji Kupasuka na Kuumia vibaya kwa kutokwa na Damu ) kama sehemu yao Kafara.

Nimedokezwa kuwa hata Magoli ya mbali na ya Mashuti makubwa ya Balama Mapinduzi, Bernard Morrison, Zawadi Mauya, Feisal Salum 'Feitoto' na lile la karibuni la Kibu Denis yote yalitokana na Nguvu ya Msaada wa Jini / Majini.

Hivyo basi Kiherehere cha Fiston Mayele cha kujifanya anaipenda sana Yanga SC na Kukubali kubeba Makombora makubwa ( Majini ) ili Afunge Magoli na Ateteme kusudi Umaarufu wake usipotee ndiyo Kimemponza na huu Ukweli anaujua japo nimeshangaa kusikia / kuiba kuwa Analalamika Mitandaoni.

Na kama kuna Mtu ambaye Kamponza na Kumharibia Fiston Mayele juu ya haya Malalamiko yake na Kiwango chake Kushuka ni aliyekuwa Rafiki yake mkubwa ambaye ni Haji Manara.

Nyota Kali aliyokuwa nayo Fiston Mayele baada ya kuondoka rasmi Yanga SC na kwenda huko Pyramid FC ni kwamba Haji Manara kapita nayo mazima ( kaichukua ) na sasa anaitumia kiasi kwamba Nyota yake inawaka na anafanikiwa japo ndani ya miaka Mitatu Minne ijayo atashuka Kiumaarufu, Kufilisika na kuwa Mtu wa Kawaida ( Ngumbaru ) tu kama Mimi GENTAMYCINE.

Na sababu kubwa ya Haki Manara kujifanya kumsihi na kumshauri Fiston Mayele ni kwamba hataki Alichomfanyia ( kupitia Nyota ya Mayele na Majini ) kijulikane kwa sasa na Mtetemaji Fiston Kalala Mayele.

ANGALIZO

Sijamlazimisha Mtu yoyote Kuusoma na Kuuamini huu Uzi wangu japo nina uhakika nao ( tena kwa Kujiamini kabisa ) kwa 100% kwani Wanyetishaji wangu ni Wachezaji na Viongozi kadhaa kutoka Yanga SC yenyewe.

Hivyo basi unajua / unajijua kabisa kuwa kwa Ujuha wako hunipendi na unanichukia GENTAMYCINE hapa JamiiForums nakuomba acha kabisa kusoma Threads zangu na niachie wale Members Wanaonielewa na Wanajitambua Kichwani / Kiakili pia..

Soma tu Threads za Uwapendao Ok?


Haya na wale mnaopenda Kukopi Taarifa zangu mbalimbali na za Kipekee hapa JamiiForums na Kujifanya ni zenu na mmezitafuta nyie mkiitumia huko katika Blogu zenu na Kurasa zenu za Mitandao na hata katika Redio na Runinga tafadhali msiache na msione Wivu kusema kuwa mmeitoa Kwangu GENTAMYCINE The only SPORTS NEWS KING hapa Jamvini.

Kula Chuma hiki / hicho Kudadadeki.
 
Fiston Kalala Mayele acheza mpira, hii mambo ya kusingizia sijui majini ohoo mara kutukanwa hayatamsaidia katika carrier yake na atashindwa kufikia malengo yake. Muda ni mwalimu wacha ninyamaze.
 
Hamtaki kuamini ila kwenye hizi mechi uchawi upo, mchezaji anabaki na kipa nafasi kubwa ya kufunga inaonekana halafu anapaisha shuti au inaenda nje ,mashabiki wanaanza kulalamika ni mbovu anakosaje pale kumbe kuna mengine yanaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamtaki kuamini ila kwenye hizi mechi uchawi upo, mchezaji anabaki na kipa nafasi kubwa ya kufunga inaonekana halafu anapaisha shuti au inaenda nje ,mashabiki wanaanza kulalamika ni mbovu anakosaje pale kumbe kuna mengine yanaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
Mchezaji kukosa goli la wazi ni kimuhemuhe na wala si uchawi.

Uchawi ni dhana ambayo ni ya kufikirikika tu haina uhakika wowote
 
Back
Top Bottom