Hussein Tuwa vs Eric Shigongo (Riwaya)


Naomba ukasome "No Orchid for Miss Blandish"ya J.H.Chase,halafu rudi kwa "Mkimbizi" ya H.Tuwa na rejea maelezo(ushabiki?) wako.
 
Wanaotaka kusoma hadithi za hussein tuwa. nenda ka-like ukurasa unaitwa "kona ya riwaya reloaded" hukoo facebook. Mpaka sasa hivi ameandika hadithi 2.
- mtafiti
- miss tanzania.... ambayo inaendelea sasa hivi.
 
Hussein Tuwa ni mtunzi mahiri sana! Ametunga hadith chache na zina msisimko wa ajab...


Shigongo ni mtunzi mzuri pia, tatizo hadith zake zinafanana sanaaa na zina usuper man sana (hazina uhalisia)
 
Wakati najifunza kusoma riwaya miaka ya 80 mwishoni ,nilisoma nyingi za kiswahili,na nilifurahi.90's nilianza kusoma za kiingereza nikapata tofauti kubwa.Hasa za J.H.Chase.Changanya zote ili upate ladha tofauti.
 
Shigongo ni sio muandishi bali ni mkalimani anayecopy kazi za watu na kutafsiri kwa kiswahili kisha huweka jina lake kama yeye ndo kaandika riwaya hiyo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

una uhakika?tafuta novel hata 1 dunian ambayo ameikop coz alishatangaza dau,the guy z talented jaman
 
Shigongo ni sio muandishi bali ni mkalimani anayecopy kazi za watu na kutafsiri kwa kiswahili kisha huweka jina lake kama yeye ndo kaandika riwaya hiyo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

thibitisha kauli ako kwa mfano wa hadith ake ambayo amecopy
 
Naomba ukasome "No Orchid for Miss Blandish"ya J.H.Chase,halafu rudi kwa "Mkimbizi" ya H.Tuwa na rejea maelezo(ushabiki?) wako.

Chase si wa kumfananisha na Tuwa,ni disrespecf kwa James Hadley Chase.But between Tuwa ns Shigongi i agree riwaya za Tuwa zina msisimko mno.
 
Nikikumbuka ile riwaya ya utata duuuh, mh. Tuwa namnyoshea mikono asee
 
hivi ukitaka vitabu vya riwaya vya husen tuwa utavipata wapi?
 
Shigongo ndo habar ya mjini. fatilia hata mauzo ya vitabu vyake utagundua jamaa anauza sana
 
dharau hizo Tuwa kumfananisha na Shigongo .Tuwa yuko juu!
 
Me namjua Shigongo,huyo mwingine simjui.Nachojua mimi ni kwamba Shigongo ni mtunzi mahiri wa hadithi kuliko wote niliowahi kuwajua bongo

Umenifurahisha sana yaani hujui watunzi wengine lakini unasema shigongo ndio best
 

Unakosea sana kusema Tuwa alibahatisha,hii inatokana na kuwa labda hujafuatilia sana riwaya zake.

Jamaa sio mmiliki wa gazeti lolote so huwa anatoa kwenye gazeti la kiu kwa kupokezana either na Beka Mfaume au Amri Bhawji.

Mfano wa riwaya ambazo nimezisoma za Tuwa ni
1.Mkimbizi
2.Mtuhumiwa
3.Utata wa 9/12
4.Mdunguaji
5.Bondia
6.Mfadhili (tena hiki kitabu kilichukua hadi tuzo ya MacMillan na kikawa kinatumika mashuleni kwa wale wa wanaosoma Kiswahili advance)

Nimesoma hadithi za Shigongo nyiingi saana ila uwezo wa Hussein Issa Tuwa upo juu sana.Tafuta kitabu chake hata kimoja nakuhakikishia hutojuta na nnauhakika utajiunga katika chama cha Tuwa ktk riwaya

Ahsante.
 
Hadithi za Hussein Tuwa kwa kweli zinamsisimko ukiwa unazisoma mfano ile ya Miss Tanzania au Mkimbizi ukisoma hadi unapata mdadi..
 
Me namjua Shigongo,huyo mwingine simjui.Nachojua mimi ni kwamba Shigongo ni mtunzi mahiri wa hadithi kuliko wote niliowahi kuwajua bongo

Ulishahi kusoma hadithi za Musiba, kama sanda ya jambazi, kikomo no 1 na no 2 na vingine vingi alivokua akitunga kabla ya kuzuiwa na serikali, ama wewe ni kizazi kipya?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…