Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

Kiburi chanini wakati watoto wetu wanaanguka njaa mashuleni huku walimu wakipepesuka kwa njaa??

Wizara ipime kama Mchele hauna shida upelekwe mashuleni, Mchele wenyewe bei ghali shule gani inaweza kununua ikalisha watoto wake???

Waziri anakaa Dar anaamini watuwote tunakula Kila tunapojiskia...huku vijijini kunawatoto hupigwa kipigo kikali kisa kudokoa wali kutokana na njaa kali waliyonayo. Tunakula mlo mmoja tuu labda siku ya bahati ndiyo tule milo miwili.

Msiweke kiburi kisa ninyi mnakula mnashiba na kuvimbiwa, chamuhimu Mchele unaenda liwa shule ambamo hawawezi nunua Mchele wetu ambao bei ni yajuu.

Nilini tutapata viongozi wazalendo wenye akili nzuri na wanaojua nchi yao na watu wake wanavyoumia hasa huku vijijini??
Hopeless leaders kabisa!!
Unasema mchele upimwe? Kama hao jamaa wameweza kuuleta hadi umefika Bongo, unadhani kuna uwezekano wa kuukagua? Nani athubutu?

Kwa lugha rahisi tu ni kwamba Mmarekani anafanya anachotaka yeye; sie tutabaki wapiga-kelele tu.

Kifupi, viongozi wameshatuuza tayari.
 
Tena angekuwa uncle Magu viongozi wa hiyo NGO wangekula mboko, wanataka kutuulia kizazi chetu shupavu. Hii nchi ina watu wa hovyo sana, ilitakiwa wapewe masaa kadhaa huo mchele uwe umechomwa na TBS
Usihadaike na maneno ya huyo Msomali. Hii nimkshifa kubwa na inamhusu, uungwana ni Kujiuzulu tu tena haraka mno
 
Kwa uwezo wako wa kufikiria, unadhani tz tunahitaji msaada wa mchele, maharage n mafuta?? Vipi wasomali, palestines, Nigerians, Ukrainians...
Kwa fikra zako kwa stories za kuambiwa, kujisomea n uwezo wako wa kufikiria, unadhani America wana mapenzi hayo kweli ya dhati kwa watz?? Tukirudi kwenye historia, America amewahi kulisaidia taifa gani bila kuwa na agenda yeyote iliyojificha??
Hivi hujui uko Palestine kila kukicha sio chini ya watu 40 wanakufa kwa njaa? Kwanini asipeleke chakula chake kwenye taifa lenye uhitaji anatuletea uku ambapo tunategemewa na mataifa jirani tuwauzie mazao yetu ya ziada? Hatuna maendeleo kama yao, ila wasituone sisi maboya kiasi hiki.
Umesema vyema. Kuna watu akili zao ziko tenge tangu kuzaliwa.

Wameona Tanzania ndio nchi inayoweza kupokea misaada bila kuhoji.
 
Dar es Salaam. Saa chache baada ya kuibuka kwa mjadala katika mitandao ya kijamii juu ya mchele ulioongezwa virutubisho ulioletwa Tanzania kutoka nchini Marekani, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amefunguka akisema waagizaji hawakupaswa kuleta mchele huo kutoka nje, kwa kuwa Tanzania ina hazina ya mchele.

Akaongeza kuwa kama ni virutubisho, bado shirika lililoagiza mchele huo lingenunua mchele wa ndani na kuwaomba wafadhili wao wauongezee virutubisho hapahapa nchini, huku kila mtu akiona kuliko kuagiza kutoka nje ya nchi.

Mjadala wa mchele huo ulianzia katika mtandao wa X, baada ya ukurasa wa Ubalozi wa Marekani kuweka picha iliyokuwa ikionyesha viroba vya mchele huo, huku ikiambatisha na ujumbe uliosomeka:

"Chini ya mpango wa 'Pamoja Tuwalishe', Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, imetoa msaada wa kwanza wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani moja kwa moja hadi shuleni katika eneo la Dodoma nchini Tanzania."


Ujumbe huo uliendelea kueleza kuwa msaada huo unalenga zaidi kutoa milo yenye lishe kwa wanafunzi wa shule zaidi ya 300 zinazoshiriki, huku ukieleza kuwa mbali na mchele huo, pia wataanzisha bustani za shule na kufunza mbinu za kuvuna.

Alichosema Bashe

Akizungumzia suala hilo wakati akielezea miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na yale aliyoyafanya katika sekta ya kilimo, Bashe amesema Tanzania inazalisha mchele na maharagwe kwa kiwango cha kutosha.

"Tumewaambia ile NGO, waambieni Wamarekani kuwa mchele upo maharagwe yapo nchi hii, zile fedha wanazotumia kuwapa wakulima wa Marekani wawape Watanzania. Tununue mchele kutoka Tanzania, maharage kutoka hapa Tanzania, halafu hivyo virutubisho mnavyotaka kuweka muwekewe hapahapa Tanzania wote tunaona," amesema Bashe na kuongeza kuwa ameieleza NGO hiyo kuwa Tanzania inajitosheleza kwa chakula.

Maoni mtandaoni

Elisha Mbise alitoa maoni yake katika ujumbe ulio katika ukurasa wa Ubalozi wa Marekani akiandika: "Tanzania tuna chakula cha kutosha...mchele umejaa kila mahali. Walete vitu vya maana, wajenge maabara, walete vifaa vya hospitali, vifaa vya kufundishia, vyuo vya ufundi. Hivi ndivyo vitu vinavyoweza kugusa elimu na afya kama kweli wana nia na kusaidia hayo maeneo.’’

Naye Dani Zayumba aliandika: "Tanzania hatuhitaji chakula cha misaada bali tunahitaji mabadiliko ya mitalaa ya elimu, ili tuweze kujilisha wenyewe. Mnaweza kufananisha mchele wa Mbeya na Marekani kweli?’’

Credit: Mwananchi digital

View attachment 2936741

Hapo awali Balozi wa Marekani ukiandika kwenye Mtandao wa X Kwamba, "Chini ya mpango wa 'Pamoja Tuwalishe', Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, imetoa msaada wa kwanza wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani moja kwa moja hadi shuleni katika eneo la Dodoma nchini Tanzania. Zaidi ya kutoa milo yenye lishe, wanafunzi katika shule zaidi ya 300 zinazoshiriki, pia wataanzisha bustani za shule, na kujifunza mbinu za kuvuna maji ya mvua. Ikiwa ni mfano kamili unaoweza kuigwa, programu hii inaakisi ahadi na dhamira ya dhati ya Marekani ya kukuza afya, elimu, na fursa kwa watoto kote ulimwenguni."
View attachment 2936743View attachment 2936744
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alikuwa wapi vyakula hivi vikigawanywa huko Dodoma hadi lilivyoibuliwa Jf?
 
Mkuu umeshatembea huko vijijini ukawaona watoto wanavyoteseka na njaa na walivyodumaa. Lishe duni ni tatizo kubwa Tanzania. Kama wewe na watoto wako mnajitosheleza hapo ulipo shukuru Mungu, kuna watu huko hawajui mchana watakula nini. Cha msingi hapo Serikali ijiridhishe usalama wa hicho chakula kama Kipo Sawa mm sioni shida. Mchele na chakula kilichopo tz ni Kwa wanaojiweza Tu.
Serikali ijiridhishe? Mpaka imeruhusu mchele umeingia nchini, unadhani nini kitabadilika?

Nani mtaalamu atakayekuwa tayari kulitia dosari taifa la Marekani, iwapo kuna uwalakini kwenye huo mchele?
 
Ulipitia wapi hadi umefika Dodoma? Kwani Tanzania inaruhusu kuingiza Mchele? Changa la macho baada ya kuona reactions za watanzania.
 
Swali jee utafiti umefanywa kuhakikisha hivyo virutubisho ni vizuri kwa watoto wetu, visine kuwa na Virutubisho vya kujenga marekebisho ya JINSIA ya Vijana kuwa vinginevyo. Maana siku hizi kuna hila za kupunguza idadi ya watu, haswa barani Africa
Au inawezekana ni virutubisho vya majaribio.

Watanzania wanageuzwa kuwa Guinea Pigs!
 
Hata vifaru na zana za kijeshi vinapitisha nchini .

Jana nimekutana na msafara wa magari ya Uganda ukitokea bandari ya Tanga, kupitia huko Arusha na Kilimanjaro kuelekea Uganda.

Mizigo iliyokuwa imebebwa ni mungu anajua, tena escort ya police wa TANZANIA ilikuwa mbele kulinda na kusindikiza huu mzigo.
 
Kwa uwezo wako wa kufikiria, unadhani tz tunahitaji msaada wa mchele, maharage n mafuta?? Vipi wasomali, palestines, Nigerians, Ukrainians...
Kwa fikra zako kwa stories za kuambiwa, kujisomea n uwezo wako wa kufikiria, unadhani America wana mapenzi hayo kweli ya dhati kwa watz?? Tukirudi kwenye historia, America amewahi kulisaidia taifa gani bila kuwa na agenda yeyote iliyojificha??
Hivi hujui uko Palestine kila kukicha sio chini ya watu 40 wanakufa kwa njaa? Kwanini asipeleke chakula chake kwenye taifa lenye uhitaji anatuletea uku ambapo tunategemewa na mataifa jirani tuwauzie mazao yetu ya ziada? Hatuna maendeleo kama yao, ila wasituone sisi maboya kiasi hiki.
Mbali ya hicho chakula, mbona kuna miradi lukuki inayofadhiliwa na USA na hatujaona serikali ikijishaua hivyo. Bashe aache uswahili, tatizo si uwepo wa mchele, tatizo ni uwezo wa kaya (purchasing power) nyingi kuafford huo mchele, na hii ni dalili ya jamii iliyojaa ufukara..
 
Kwani imewahi kutokea mzungu akampenda mtu mweusi??? Tukienda huko kwao wanatuita nyani na kutunyanyapaa kila kona. BTW mzungu anatafuta kila namna kumpoteza mtu mweusi kwenye uso wa dunia.

Tunalindwa na Mungu tu
 
Tena angekuwa uncle Magu viongozi wa hiyo NGO wangekula mboko, wanataka kutuulia kizazi chetu shupavu. Hii nchi ina watu wa hovyo sana, ilitakiwa wapewe masaa kadhaa huo mchele uwe umechomwa na TBS
Tungekuwa na rais mwenye akili huo mchele usingeingia kabisa. Bashe na mamake hamnazo kabisa
 
Lakin pamoja na Yote maabara zetu zinashindwa kbsa kupma huo mchele una nn ndan , Watu wanapng tuu utazan n story za vijiwen
 
Sehemu chakula kinapotoka lishe ni duni. Shida ni elimu sio uhaba
Elimu juu ya lishe sahihi inaweza kuwa sehemu ya tatizo, lakini yapo matatizo lukuki mbali ya hiyo elimu. Mojawapo ni uwezo wa kumudu hicho chakula kwa mwaka mzima, sana sana wakati wa mavuno inawezekana ila baada ya hapo ni maisha ya kubangaiza.
Matatizo ya kijamii inaweza pia kuwa tatizo jingine, wakati wa mavuno anayekwenda kuuza mazao ni baba wa familia, akishauza matumizi yanakuwa si mazuri, baada ya muda hakuna pesa ndani, wanaotaabika ni mama na watoto kwa kuanza kuokoteza vyakula mashambani.
Kwa umasikini huu si rahisi kaya nyingi zikapata lishe bora kwa msimu mzima, hata ukizipa elimu ya kutosha mabadiliko yatakuwa kidogo hasa kwa zile kaya zenye kujiweza kwa msimu mzima.
 
Back
Top Bottom