Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Membe ni moja ya mawaziri wa awamu ya nne ambaye alikuwa mzigo balaa, hukuwa na msaada na Watanzania wanaoteseka huko nje ya Nchi, mfano kule China na Hongkong jina la Tanzania limechafuka sana kutokana na wageni kununua passport za Tanzania hasa wanaijeria na kuingia huko wakiaminika ni Watanzania kisha kufanya uhalifu mwingi sana, matokeo yake Tanzania imechafuka sana lakini hakuwahi kwenda huko kusafisha jina la Tanzania badala yake alikwenda china kuomba pesa za kampeni tu, huku akiacha Watanzania wakinyanyaswa sana China kwa kubambikiwa kesi kuporwa pesa wengine wamefungwa kwa uonevu kisa amekutwa na mtu anayeuza Unga na yeye anabambikiwa hata kama alikuwa hajui kuwa mwenzake ni muuza unga, police wa China wanavuna pesa nyingi za wafanyabiashara wa Tanzania wanaokamatwa kwa kuunganishwa na watu wasiowajua kisha pesa zao kutaifishwa, Membe hakufanya lolote kutetea Uovu kwa Watanzania huko Hongkong na China, lakini kenya na Uganga wao wamesimama kidete kutetea Raia wao wanaoonewa na police huko.membe kaa kimya tu maana miaka 10 hujasaidia nzuri hata moja zaidi ya kulitia hasara taifa.
 
Kiukweli CCM ni mchanganyiko wa vyama vingi tofauti ndani yake

kinachowaunganisha ni kuwa madarakani tu
siku wakitoka watabaki vipandevipande....

ndo maana kuna vision tele
kila mtu na yake.....na wafuasi nao kila mtu na kundi lake....
Kundi la Membe ni Mwenyekiti wa ccm, makamu wake, katibu mwenezi( Nape) January Makamba, Mwigulu na wahindi akina sumaiya, manji na wenzao
 
Mimi sielewi...ina maana mtu ukimkosoa Magufuli ndo hutaki afanye kazi yake?

Ukimkosoa ndo unamzuia kufanya kazi yake?

Huyo Magufuli yuko juu ya kila kitu hata kukosolewa/ kujadiliwa?
The same same principle mnayotumia kumtetea bwana Membe kwamba ana haki ya kutoa maoni yake km mwananchi bila ya kuvunja katiba muitumie pia kwa hawa watanzania wenzenu wanaomkosoa Membe...maana wao kwa maoni yao wanaona Membe kaongea mambo kinafiki..wala haina haja ya kuanza kustaajabu as long as kila mtu anatoa maoni yake....hata wewe leo ukiamua kumkosoa JPM kuna watu watakuunga mkono na kuna watakaokupinga mkuu so haina haja ya kuwashangaa wanaompinga bwana Membe na pia haina haja ya kuwashangaa wanaomuunga mkono bwana Membe...personally naona Membe ni mnafiki tu,hakuna kitu productive alichokisema zaidi ya kutafuta cheap popularity ya kwenye media
 
  • Thanks
Reactions: nao

Kwani kuna mtu kasema kwamba wanaomkosoa Membe hawana haki ya kufanya hivyo?
 
Kwani kuna mtu kasema kwamba wanaomkosoa Membe hawana haki ya kufanya hivyo?
Umeandika mwenyewe jinsi unavyoshangaa watu wanaopingana na anti-JPM....mie pia nilikua sioni sababu ya wewe kushangaa maana kila mtu yuko kwenye uhuru wa maoni...toa maoni yako na wengine watoe yao..
 
M
The same same principle mnayotumia kumtetea bwana Membe kwamba ana haki ya kutoa maoni yake km mwananchi bila ya kuvunja katiba muitumie pia kwa hawa watanzania wenzenu wanaomkosoa Membe...maana wao kwa maoni yao wanaona Membe kaongea mambo kinafiki..wala haina haja ya kuanza kustaajabu as long as kila mtu anatoa maoni yake....hata wewe leo ukiamua kumkosoa JPM kuna watu watakuunga mkono na kuna watakaokupinga mkuu so haina haja ya kuwashangaa wanaompinga bwana Membe na pia haina haja ya kuwashangaa wanaomuunga mkono bwana Membe...personally naona Membe ni mnafiki tu,hakuna kitu productive alichokisema zaidi ya kutafuta cheap popularity ya kwenye media
membe ni bonge la mnafiki hana lolote.
 
Membe sasa kajawa na wivu pia anaona Kama Magufuli kamsahau haraka kwa kazi ya fitna alizowafanyia Ukawa, alitegemea Magufuli atamwona ni mungu mtu , sasa anajuuta kumfahamu Magufuli
 
Wale waganga wa kienyeji Utitiri toka Gambia na kwingineko Duniani sasa wanamdai Membe pesa nyingi mpaka kapagawa maana aliwaahidi pesa nyingi pindi Magufuli akiingia ikulu watalipwa pesa ndefu lakini imekuwa kinyume baada ya Magufuli kudai ni nguvu za Mungu zilimuingiza ikulu hivyo hayupo tayari kutoa pesa za kuwalipa. Membe sasa anahaha kusaka pesa za kuwalipa ndiyo maana kaamua kumsakama Magufuli ili akimuuliza amjibu kuwa kapagawa kwa sababu karogwa na ile kamati ya Ufundi ambayo inamdai chao .
 
Nasikitika kuwa Bungeni bado tunapeleka Wajinga..

Mbunge anaandika bandiko la Kijinga namna ile... Ni kwamba hajui Kiswahili ama Kiswahili hakijitoshelezi hadi Achanganye na Kiingereza.????!.

Bandiko limepoteza Maana kabisa.
 
Hawastahili heshima ya u girlfriend hao uliowaita ma girlfriends. Ni MAKAHABA kama Wengine. Tofauti yao na hawa wa Mori na Kona Bar ni kuwa hawajisimamishi barabarani tu, ila wote wanajiuza,sasa tuondoe double standards za kuwaita hawa wa Mori makahaba na hao wengine ma girlfriends! Mbaya zaidi, kodi yangu imetumika kusafirisha na kutunza makahaba ilihali barabara mbovu.
Kweli tofauti yao hawa makahaba wana diplomatic passport nakusifu hukuremba kwani kahaba ni kahaba tu.Kuhusu kauli ya bashe naiona imekaa vizuri kwa macho mawili ila ukiangalia kwa jicho la tatu ndo itakukumbusha mambo ya kambi zao na grudges zao.
Pana mengi tutayasikia hizo figisufigisu na majeraha ya uchaguzi yanauma jamaniiii.
 
Kw
Nasikitika kuwa Bungeni bado tunapeleka Wajinga..

Mbunge anaandika bandiko la Kijinga namna ile... Ni kwamba hajui Kiswahili ama Kiswahili hakijitoshelezi hadi Achanganye na Kiingereza.????!.

Bandiko limepoteza Maana kabisa.
kwani kuchanganya lugha ( kiswanglish ) ni ujinga? Kumkosoa Membe ni ujinga? Mbona yeye kamkosoa Magufuli alichanganya Lugha kwa kuweka Maneno ya Kingereza, Sidhani kama kukosoana ni ujinga hakuna binadamu aliye kamili kila mmoja ana udhaifu na mapungufu yake.
 
Kila mtatanzania ana uhuru wa kutoa maoni ila asivunje katiba.

sasa wanasiasa wana hofu nini mtu akitumia uhuru wake, au kwa sababu wameathiliwa na NDIOOOOOO.

Nchi haiwezi kuendelea kama kutakuwa na watu wanaowazuia wenzao kufikiri nje ya boksi.
Ni kweli kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo, na pia azingatie na kuelewa kuwa awe tayari kuwa huru kukosolewa mawazo yake; ndio moja ya sifa za wanazuoni (kutoa mawazo hadharani na kusubiri kujadiliwa na kukosolewa iwe ni chanya au hasi) - Huo ndio ukomavu wa kimawazo
 
Membe si alimpigia debe magufuli Lindi sasa analalamika nn ? Walimchagua wenyewe.

Ha haa alidhani atamlinda Kama ndugu yake. Magu ni mwiba mchungu kaanza kumchoma amebaki kuropoka tu.
 
Kwani huyu mmwera ana cheo gani serikalini? Maana anaropoka kila siku yeye atuachie rais wetu akale mamilioni ya Gaddafi huko wala hatumuhitaji kawa waziri kwa kipindi kirefu kashindwa kufanya chochote cha maana leo analeta porojo hapa? Ameumia Sana kuukosa urais na ndo basi tena maana mpaka 2025 atakuwa ashapotea kwenye ramani ya siasa.
 
Hongera sana Bashe, kwani ni kweli kwa wanaopinga mtazamo na mwelekeo wa utawala wa rais JPM ni wazi kwamba na wao ni majipu yaliyokuwayamejificha na sasa yanaanza kujitokeza. Dawa yake ni kuyatumbua kwa "screw driver" za moto. Manake hatuna namna namna nyingine. Membe anabanwa na magirl friend wake kwa ahadi alizowahidi kuwapeleka nje ya nchi kununua lip stick na rangi za kucha, imekula kwake. JPM hili jipu (membe) usilipe nafasi litumbuliwe lipone mapema.
 
Hili ni andiko la Hussein Bashe:

Bashe:

Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi

Membe amekuwa Waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.

Hoja kuwa Serikali haijapungua ama kubwa or ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .

Membe amekuwa sehemu ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa. Amefaidika na safari za nje yy binafsi bila manufaa kwa nchi. Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake Magufuli believes matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya Hovyo na yasiyo ya lazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.

Ni muhimu Membe afahamu Magufuli ana style yake tutampima kwa matokeo as of now hatujaona athari za safari labda Membe kama yy binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kuli muathiri yy binafsi kwa kukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Common wealth that's why leo anakosoa.

Tunafahamu maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka ktk Awamu ya nne. Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serikali ya awamu ya Tano.

Hoja ya kutokuwa na mabalozi magufuli hana siku 100 yy amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwa na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .

Amekuwa mmoja wa mawaziri walokuwa foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu yx mis use of funds ktk wizara yake. Kipindi chake safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.

Ni muhimu Membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathiriki directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.

Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya Magufuli ya uongozi aliwahi kusema Sankara "You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"

Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliyekuwa akinyonywa hapo awali tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakuwa style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wa kuwanyonya wengi na wachache kufaidika.

Wassalaam
Bashe kachanganyikiwa huyo ana matatizo sana maana hawataki kukoselewa.
 
Back
Top Bottom