Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Nchi inayomwangalia tu rais kwa
Mkuu Shetani na wamarekani wanaishangaa CCM
Nchi inayomwangalia tu rais kwa maendeleo yake ina tatizo kubwa japokuwa rais ana nafasi pekee. Kinachotakiwa ni utaratibu wa utawala ambao unaweza kuhojiwa. utaratibu uanaofuatwa na watu wote na anayekiuka kupewa kisago. rais anaweza kuwa mzembe miaka 10 si itakuwa balaa?
Wengine wanafiki watupu. wanaomsema Kikwete sasa ndio hao walimtetea 2010 . sasa wanadiriki kusema serikali yake ilikuwa dhaifu kwa miaka 10. Nauliza ni kiitu gani kiliwafanya washindwe kumwondoa kikatiba baada ya miaka 5 kama kweli alikuwa dhaifu? hao hao wanaomshutumu Kikwete watajamshutumu Magu akija rais mwingine ili tu wapate kula. tuwe objective.
 
Hapo ndipo utamu wa siasa ulipo!ni kama upepo haujulikani unatoka wapi unakwenda wapi!ha ha ha ha
 
haa haa bashe bwanaaa duh. kumkosoa maghufuli ni dhambi. membe yuko sahihi sana kwa hili....
 
ukiachana na nyumbu lazima akili ikurudie... sasa bashe akili imerudi .....
 
Na JK ndio alitaka kumpa Membe uraisi,huyu jamaa angetuuza,kuna watu waliiba sana hela za walalahoi sasa mirija imekata wanaanza kuweweseka.MUNGU endelea kumlinda Magufuli aendelee kutumbua majipu
 
Karibu Mkuu ila sis hapa Lumumba tumevurugwa na huyu jamaa tulio muweka madarakani kimagumashi. Tunashikana uchawi sis wenyewe. Pengine tunaona ni bora tungemuacha mamvi kuliko huyu tuliomuweka.
 
Wafu wameanza kuzika wafu wao.he
Nape Nnauye ataweza kumziba mdomo mshenga wake Membe?
Bashe ninakupongeza sana sana, kwa kuamua kuwa msemaji wa Serikali katika eneo hilo binafsi ninajua kwa uhakika Membe alikua anapelekewa kila asubuhi, sijui kama bado, dola 5,000 cash toka kwa Ghalis Salim Mohamed, boss wa Alosco kila siku iendayo kwa mungu dereva wa myemen anahakikisha zinafika kwa dada pale ofisni kwa Membe, ndio maana hata zile hela zilizokamatwa airport na kuandikwa front page Nipashe zilirudishwa ofisini kwao pale Lumumba, mahali ambapo baba wa taifa alianzisha TANU, wanausalama wakaingina na kutoka na vikapu vya hela tukivionoa, Membe ni wa kukaa nae mbali sisi kama taifa hatuhitaji ushauri toka kwake, awamu yao imekwisha kale hela za Gadafi kama ulizitunza, tafadhali tusisikie Magufuli kamchagua kwenye lolote, kwanza hana ujuzi wowote zaidi ya kutesa watu na majungu
 
Membe Ni mnafiki Kama unavyosema na msanii anaenda na upepo unavyovuma. Mwanzo alisifu raisi kuzuia safari kwa kusema walikuwa wanapishana angani! Sasa amekuja tena na mpya! Anaweweseka
Extra time yake ilikuwa kwenye ukatibu mkuu.Pombe kammwaga.Ndio maana unaona Povu linamtoka,Haamini kama leo sio mh.ni raia kama wengine."Panic
 
Ombi langu Magufuli aangalie mbele aachane na hawa waathirika wa Urais.
Ushauri mzuri sana.

Nimeshangaa bado kuna Friends of Membe wakati walituambia wamevunja makundi ya kusaka Urais ndani ya CCM.
 
Membe tunamjua toka kitambo na uzaifu wake katika utendaji tunaufahamuuu...
Hoja ya msing hapa n kujua hatima ya zanzbar na mawazo yake kawapa kwamba kufutwaa kwa uchaguz sio sahihi....
Kusikia ukweli huu Ccccm mmehamaki na kuja juu na uozo wa mwenzenu ndani ya chama.. sasa jibuni hojaaa hiyo ya zanbar sio hayo makandokando yenu.. kila mtu anayajuaaa.
 
Wakuu sijamuelewa bashe, anamaanisha rais ni mwendawazimu kidogo au anaigiza uendawazimu kidogo? Asiigize style za watu wengine mwisho wa sankara haukuwa mzuri.
Utamwelewa utakapoacha ushabiki wa aliyemtangulia Magufuli
 
Hili ni andiko la Hussein Bashe:

Bashe:

Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi

Membe amekuwa Waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.

Hoja kuwa Serikali haijapungua ama kubwa or ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .

Membe amekuwa sehemu ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa. Amefaidika na safari za nje yy binafsi bila manufaa kwa nchi. Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake Magufuli believes matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya Hovyo na yasiyo ya lazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.

Ni muhimu Membe afahamu Magufuli ana style yake tutampima kwa matokeo as of now hatujaona athari za safari labda Membe kama yy binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kuli muathiri yy binafsi kwa kukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Common wealth that's why leo anakosoa.

Tunafahamu maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka ktk Awamu ya nne. Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serikali ya awamu ya Tano.

Hoja ya kutokuwa na mabalozi magufuli hana siku 100 yy amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwa na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .

Amekuwa mmoja wa mawaziri walokuwa foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu yx mis use of funds ktk wizara yake. Kipindi chake safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.

Ni muhimu Membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathiriki directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.

Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya Magufuli ya uongozi aliwahi kusema Sankara "You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"

Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliyekuwa akinyonywa hapo awali tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakuwa style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wa kuwanyonya wengi na wachache kufaidika.

Wassalaam
Membe alikuwa Waziri mzembe kupita kiasi hasa huku Zanzibar sisi wafanya biashara tunaokwenda China na Hongkong tunamchukia sana, maana pale Hongkong na Viwanja vingine vya China mamia ya wazanzibar na Watanzania wamerejeshwa viwanjani wakiwa na pesa zao walizokwenda kununulia bidhaa kisa wamesahau hotel watazofikia na vijisababu vya kijinga jinga tu, lakini Membe hakuthubutu kukemea huo Unyama wa kukosa huruma wanaotendewa Watanzania akawa busy kuwa omba omba misaada tu na huyo boss wa NIDA rafiki yake mkubwa aitwae Jack Gotham ambaye ameficha mali na pesa nyingi za Membe, Magufuli chapa kazi lakini tunakuomba Umwambie balozi wa china na ujumbe utumwe kwenda Hongkong kuwalalamikia kwa usumbufu wanaowafanyia watanzania, Nchi zingine kama kenya, Uganda nk wao tayari walipiga mkwara kuwarejesha watu wao pasipo na sababu za msingi.
 
Statement imekaa kishabiki, imejaa hasira na chuki..., Bado maumivu yapo kutokana na yale makundi ndani ya CCM...,
Yanawaathiri wahusika!
Ukweli unauma hapa hakuna ushabiki wala hasira kilichokuwepo ni Ukweli tu.
 
Back
Top Bottom