Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Nimependa aya ya tatu,Bashe anasema Membe amekua sehemu ya mfumo dhaifu uliotufikisha hapa!!! Anataka kuungana na mnyika kwamba ba riz alikua dhaifu na kusababisha mfumo dhaifu?
Kwani anayemtetea hakuwa sehemu ya mfumo huo? Mbona rais akihutubia bunge alisifu awamu iliyopita na kusema anaendeleza ilipoishia hasa kwenye sera ya mambo ya nje?
nashauri wasiongee sana wajue kuhifadhi maneno
 
Jamani Membe tuachie serikali yetu ya Magufuli kwa nini usikae kimya na uangalie utekelezaji wa awamu ya tano. Ya kwenu yalishapita waacheni nao wenzenu wachape kazi.
 
Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi.

Membe amekua waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.

Hoja kuwa serekali haijapungua ama kubwa or ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .

Membe amekua sehem ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa,Amefaidika na safari za nje yeye binafsi bila manufaa kwa nchi, Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake Magufuli believes matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya Hovyo na yasiyoyalazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.

Ni muhimu membe afahamu Magufuli ana style yake tutampima kwa matokeo as of now hatujaona athari za safari labda Membe kama yeye binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kuli muathiri yeye binafsi kwa kukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Commonwealth thats why leo anakosoa.

Tunafaham maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka ktk Awamu ya nne, Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serekali ya awamu ya Tano.

Hoja ya kutokua na mabalozi magufuli hana siku 100 yeye amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwa na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .

amekua mmoja wa mawaziri walouwa foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu ya mis use of funds katika wizara yake, kipindi chake Bernad Membe safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.

Nimuhimu membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathiriki directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.

Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya Magufuli ya uongozi aliwahi kusema Sankara " You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"

Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliekuwa akinyonywa hapo awali tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakua style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wakuwanyonya wengi na wachache kufaidika.


Wassalaam.

Bashe

Mupe mupe maembe kavu kavu! Mpuuzi mwili mzima!
 
Kiukweli CCM ni mchanganyiko wa vyama vingi tofauti ndani yake

kinachowaunganisha ni kuwa madarakani tu
siku wakitoka watabaki vipandevipande....

ndo maana kuna vision tele
kila mtu na yake.....na wafuasi nao kila mtu na kundi lake....

Mimi sielewi...ina maana mtu ukimkosoa Magufuli ndo hutaki afanye kazi yake?

Ukimkosoa ndo unamzuia kufanya kazi yake?

Huyo Magufuli yuko juu ya kila kitu hata kukosolewa/ kujadiliwa?
 
Ombi langu Magufuli aangalie mbele aachane na hawa waathirika wa Urais.
 
Mimi sielewi...ina maana mtu ukimkosoa Magufuli ndo hutaki afanye kazi yake?

Ukimkosoa ndo unamzuia kufanya kazi yake?

Huyo Magufuli yuko juu ya kila kitu hata kukosolewa/ kujadiliwa?


Sio culture ya CCM kumkosoa Rais

Sababu hata Magufuli mwenyewe hakupatikana katika open contest

Sasa sababu wanajua ile mandate ya Magufuli sio genuine
kila anaemkosoa wanaona 'kuna hatari' ya kuinfluence uasi...

hilo ndo linalowasumbua.....na sio Magufuli tu
kina Kolimba walimkosoa Mkapa....Kambona alijaribu kumkosoa Nyerere
Mrema kumkosoa Mwinyi...the list is endless.....kukosoa sio culture ndani ya CCM
 
Hivi bashe mbona hamuiti Magufuli raisi, anamuita ndugu magufuli, au na yeye ni kama wale ambao hawamtambui?
 
Ndugu Bashe, ile kamati ya bungeni kuhusu mambo Foreign Affairs SI yalikuwa Chini ya Lowasa. JEE aliyakemea madudu hayo uyajuayo?
 
Back
Top Bottom