Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Combative

Member
Apr 19, 2014
58
103
Hili ni andiko la Hussein Bashe:

Bashe:

Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi

Membe amekuwa Waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.

Hoja kuwa Serikali haijapungua ama kubwa or ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .

Membe amekuwa sehemu ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa. Amefaidika na safari za nje yy binafsi bila manufaa kwa nchi. Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake Magufuli believes matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya Hovyo na yasiyo ya lazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.

Ni muhimu Membe afahamu Magufuli ana style yake tutampima kwa matokeo as of now hatujaona athari za safari labda Membe kama yy binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kuli muathiri yy binafsi kwa kukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Common wealth that's why leo anakosoa.

Tunafahamu maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka ktk Awamu ya nne. Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serikali ya awamu ya Tano.

Hoja ya kutokuwa na mabalozi magufuli hana siku 100 yy amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwa na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .

Amekuwa mmoja wa mawaziri walokuwa foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu yx mis use of funds ktk wizara yake. Kipindi chake safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.

Ni muhimu Membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathiriki directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.

Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya Magufuli ya uongozi aliwahi kusema Sankara "You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"

Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliyekuwa akinyonywa hapo awali tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakuwa style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wa kuwanyonya wengi na wachache kufaidika.

Wassalaam
 
Wakuu sijamuelewa bashe, anamaanisha rais ni mwendawazimu kidogo au anaigiza uendawazimu kidogo? Asiigize style za watu wengine mwisho wa sankara haukuwa mzuri.
 
Bashe kaa chonjo huko Bungeni yaelekea kuna akina membe wengine watakaojaribu kukosoa na kwa namna moja au nyingine kutaka kukwamisha juhudi za Rais wetu Magufuli. Twamshukuru sana Allah kwa Membe kuukosa urais kumbe angeendeleza yale yale kwa staili ile ile. Wasipewe nafasi watu aina ya Membe!
 
Mhesh.Bashe nakuunga.mkono 100%.You have made a case. Tusimame ktk misingi ya ukweli. Hatua anazochukua Magufuli ni kwaajili ya kuwanufaisha watanzania wa kawaida. Membe ni msemaji wa mfumo uliokubuhu kuwanyonya watanzania ktk awamu ya 4. Mfanyabiashara ambaye halipi kodi ni mnyonyaji. Afunge biashara zake/aondoke. Ni hoja ya kipuuzi eti kulinda wafanyabiashara. They must pay tax, otherwise they are useless to th welfare of th wananchi. Nchi zinazoongozwa na mafisadi huwa hazikusanyi kodi kwasababu wao ni beneficiaries wa ukwepaji kodi huo. Nina mashaka makubwa sana na "uadilifu" wa Membe. Huyu angekuwa raisi nchi ingeuzwa kwa wafanyabiashara wasiolipa kodi. Membe anawakilisha kundi lenye ajenda mbaya dhidi ya watanzania na raisi wao Magufuli. Vyombo vya dola vichukue tahadhari ktk hili. Magufuli songambele. Wewe ndo tulikuchagua. Una dhamana ya nyoyo zetu. Who is Membe?Atuambie juu ya fedha za Gafaffi. Kidumu chama cha mapinduzi!!!!!!
 
Hongera bashe
Bashe ana akili timamu anajua uchaguzi umeisha na Rais ni Magufuli. Wakati wa mchakato wa uchaguzi kunakuwa na kambi za wagombea. Mchakato ukiisha watu makini wanaungana na team ya ushindi. Huu ndio ukomavu ws kisiasa. Majeraha huwa yanapona kwa waliojeruhiwa its time to heal na kumsaidia Rais mteule afanye kazi. Membe naye anatakiea apone majeraha na sio kukokosoa hata vitu ambavyo ni vya msingi. Nchi bila kukusanya kodi itakuwa si nchi endelevu.
 
Kila mtatanzania ana uhuru wa kutoa maoni ila asivunje katiba.

sasa wanasiasa wana hofu nini mtu akitumia uhuru wake, au kwa sababu wameathiliwa na NDIOOOOOO.

Nchi haiwezi kuendelea kama kutakuwa na watu wanaowazuia wenzao kufikiri nje ya boksi.
 
Back
Top Bottom