Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

Kama kawaida ushahidi haujatosheleza kumdaka Zombe na wenzake.Tusubiri tena kuambiwa ushahidi haujatosha kwa Vijisenti,Mramba na Yona.Hii ndo Tz.
 
Bora tuanzishe mahakama ya kadhi tuu
Yaani Mahakama zinajidhalilisha zenyewe, Kuanzia sasa nakubali maneno ya Pinda ya kuwataka watu wanaoua maalbino wachukuliwe hatua mikononi
Bravo Waziri Mkuu Pinda You were absolute right in Tanzania Environment
 
Ndiyo maana watu wanajichukulia sheria mikononi mwao....... mmh
 
Mawakili wa Zombe walia na Koplo Lema

Na Hellen Mwango na Joseph Mwendapole

Mawakili wa utetezi kwenye kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva teksi mmoja, inayomkabili aliyekuwa Kaimu Kamanda na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake, wame onekana kuuhofia ushahidi uliotolewa na aliyekuwa mshitakiwa wa 11, marehemu Koplo Rashid Lema na wameisihi Mahakama Kuu isiutumie katika kufikia hukumu.

Kila wakili wa utetezi aliyesimama jana aliiomba mahakama isiutumie ushahidi huo wakidai kuwa mwenyewe hakusimama mahakamani hapo kuthibitisha alichoandika kwenye maelezo yake kwa Tume ya Jaji Mussa Kipenka.

Wa kwanza kuomba ushahidi huo usitumike mahakamani hapo ni wakili wa Zombe, Jerome Msemwa akifuatiwa na wakili Gaudionus Ishengoma anayemtetea Christopher Bageni ambaye ni mshitakiwa wa pili pamoja na Majura Magafu anayewatetea washitakiwa wa 3,5,7,9 na 10.

Lema ndiye aliyefichua siri ya mauaji hayo kwa kudai kuwa waliouwawa hawakupambana na polisi bali walichukuliwa wakiwa hai kutoka Sinza jijini Dar es Salaam na kupelekwa msitu wa Pande uliko Mbezi Louis ambako walipigwa risasi mmoja baada ya mwingine.

Magafu alimwomba Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Salum Massati kutupilia mbali ushahidi wa Koplo Lema kwani hakuna ushahidi mahakamani pale kwamba mauaji yalifanyika msitu wa Pande.

``Kama Lema kafa basi kaenda na maovu yake. Binadamu anarithi mali si maovu na kama kuna mali basi itarithi familia yake na si hawa washitakiwa,`` alidai Magafu.

Aliendelea kudai kuwa mahakama haitakiwi kukuzingatia ushahidi ambao mhusika hakusimama kizimbani na kuuelezea kama ilivyotokea kwa Koplo Lema.

Magafu alidai kuwa hilo linaweza kufanyika tu endapo itabainika kuwa upande mmoja kwenye kesi umefanya hujuma ili asihojiwe.

``Mtukufu Jaji kwa kuwa upande wa utetezi haujasababisha Lema asihojiwe, basi naiomba mahakama yako tukufu ushahidi huo utupwe ili wateja wetu wasihukumiwe kwa kosa ambalo si lao,`` alidai.

Alidai kuwa ushahidi wa Lema hauwezi kuisaidia mahakama kuthibitisha kuwa mauaji yale yalifanyika katika msitu wa Pande kama alivyodai Lema katika maelezo yake kabla hajafariki dunia.

Aliendelea kudai kuwa maelezo mengine yanayotaka kuonyesha kuwa mauaji yalifanyika msitu wa Pande na kwamba wateja wake ambao ni mshitakiwa wa 3,5 na 10 walikwenda kwenye msitu huo yalitolewa kama maelezo ya onyo ya mshitakiwa wa 12, Rajabu Bakari na hivyo akataka mahakama iyatupilie mbali.

Alidai kuwa hakuna ushahidi unaothibitisha bila shaka kuwa wateja wake walikwenda katika msitu huo ingawa wamekiri kuwa walihusika katika kuwakamata waliodaiwa kuwa majambazi.

Magafu alidai kuwa baada ya zoezi la kuwakamata waliodaiwa kuwa majambazi, mshitakiwa wa 3,5,9 na 10 waliendelea na maeneo yao ya doria.

Katika maelezo yake kwa Tume ya Kipenka, Lema alidai kuwa alikaa mafichoni, lakini aliamua kuibuka na kusema ukweli kwa sababu nafsi yake ilikuwa ikimsuta kutokana na mauaji yale.

Lema aliiambia Tume hiyo, kwamba wafanyabiashara hao walichukuliwa wakiwa hai na kupelekwa msitu wa Pande ambako waliuwawa mmoja baada ya mwingine wakiwa wamelazwa kifudifudi.

Lema alidai kuwa askari aliyekuwa akiwafyatulia risasi ni Koplo Saad, ambaye hadi leo anaendelea kutafutwa ili aunganishwe kwenye kesi hiyo.

Wakili Ishengoma anayemtetea mshitakiwa wa pili, Christopher Bageni, aliiomba mahakama itupilie mbali ushahidi uliotolewa na Koplo Lema kwa sababu zinazofanana na zile zilizotolewa na mawakili wengine.

Ishengoma alidai kuwa hakuna ushahidi wa uhakika kuwa mteja wake alikuwepo siku ya tukio la mauaji.
Alidai kuwa siku hiyo ya Jumamosi, Bageni hakuwa kazini na alikuwa shambani kwake Pugu.

Ishengoma alidai kuwa shahidi Juma Mussa aliyedai kuwa Bageni alikuwa kazini tarehe 14/1/2006 ni muongo.

Kwa upande wake, Magafu anayewatetea washitakiwa wa 3,5,7,9 na 10 alidai kuwa ushahidi unaojaribu kuwahusisha wateja wake na mauaji hayo si wa moja kwa moja na ni wa kuungaunga.

Alidai kuwa hakuna ubishi kuwa marehemu wote wanne walikamatwa wakiwa hai na hakukuwa na purukushani wala kurushiana risasi.

Magafu alidai kuwa maelezo hayo yanaungwa mkono na mashahidi walioshuhudia marehemu walipokuwa wakikamatwa kule Sinza Palestina.

Magafu alidai kuwa upande wa mashitaka umeleta mkanganyiko mkubwa kwenye kesi hiyo.

Alidai kuwa wapelelezi wa kesi hiyo hawakuwa makini na waadilifu, ndiyo sababu wamevuruga na kusababisha mkanganyiko.

Alidai kuwa jambo hilo inawezekana lilifanywa kwa makusudi au kwa uzembe na hivyo akasema: ``Hivyo (kutokana na mkanganyiko) hata haya mauaji haijulikani mpaka leo yalifanyika wapi,`` alidai.

Aidha, Magafu aliendelea kudai kuwa wakati upande wa mashitaka ukidai kuwa mauaji yalifanyika msitu wa Pande, baadhi ya mashahidi waliopelekwa mahakamani hapo na upande wa mashitaka walidai kuwa waliouwawa walikuwa wakipambana na askari katika Ukuta wa Posta.

Alidai kuwa hata shahidi wa 27 wa upande wa mashitaka ambaye ni ofisa wa juu katika Jeshi la Polisi alitoa ushahidi kuwa kulikuwa na mapambano.

Magafu alidai kuwa hata shahidi wa 22 ambaye ni askari alisema kulikuwa na mapambano ya kurushiana risasi.

``Afande Nikobai alikuja hapa akasema walikuta damu Ukuta wa Posta na waliokota mapande ya damu Ukuta wa Posta,`` alidai.

Alidai kuwa damu hiyo inadaiwa kuwa ilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini majibu yake hadi leo hayajawasilishwa mahakamani hapo.

Mkanganyiko mwingine kwa mujibu wa Magafu ni wa mashahidi wa 30,31 na 36 wa upande wa mashitaka waliodai kuwa mauaji yalifanyika msitu wa Pande.

``Hakuna ubishi kwamba watu waliuwawa tena kwa risasi, lakini Mtukufu Jaji, hadi leo kuna swali tunajiuliza. Hao watu waliouwawa ni wapi na nani aliyewaua... Upande wa mashitaka wangekuwa makini haya yote yasingetokea,`` alidai.

Magafu alidai kuwa upande wa mashitaka unataka kuishawishi mahakama iamini kuwa washitakiwa walikula njama za mauaji ya watu wanne wakati ushahidi wa kuonyesha kuwa kulikuwa na njama haujawasilishwa mahakamani hapo hadi jana.

\"Hivi hawa washitakiwa walikaa vipi pamoja wakapanga njama za mauaji? Ni dhahiri ushahidi huo haupo na ndiyo sababu mahakama hii ikaamua kuwaachia huru mshitakiwa wa 4, 6 na 8.

Alidai kuwa endapo kungekuwa na njama za mauaji hata washitakiwa ambao waliachiwa huru wasingeachiwa.

Alidai kuwa upande wa mashitaka ulipaswa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha kuwa mauaji yalifanyika kwa makusudi au kulikuwa na nia ya makusudi ya kusababisha mtu afe, jambo ambalo alidai wameshindwa kufanya.

Akitoa hoja za mwisho kuthibitisha kuwa mteja wake hana hatia, Wakili wa Zombe, Jerome Msemwa alidai kuwa hivi sasa wananchi wanamchukia mteja wake kutokana na vyombo vya habari kumhukumu kwa kumuandika vibaya.

Msemwa alidai kuwa vyomba vya habari vimekuwa vikiandika kuwa Zombe hachomoki lazima atanyongwa.

``Mtukufu Jaji, hata Yesu alihukumiwa na Pilato wakati hakuwa na kosa na watu wote wa Galilaya walimlilia wakisema ni mwana wa Mungu, lakini mwisho wake alifufuka na kudhihirisha kuwa ni mtu mwema kama Zombe. Naomba mahakama imuachie huru mteja wangu kwa sababu hahusiki na mauaji,`` alidai Msemwa.

Alidai kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kutoa ushahidi wa moja kwa moja kwamba Zombe amewaua wafanyabiashara wale.

Alidai hakuna shahidi aliyesema Zombe alishirikiana na wenzake kupanga mipango ya mauaji hayo na kwamba hata alipojitetea alieleza mahakama namna alivyopokea taarifa za matukio na mauaji yaliyotokea siku ya tukio hilo.

``Mtukufu Jaji, Zombe alipokea taarifa ya maandishi na barua ya tukio la mauaji hayo kwamba waliouawa walikuwa ni majambazi na ni utaratibu wa kawaida kwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa kupokea taarifa kwa njia ya maandishi kutoka kwa makamanda wa upelelezi wa eneo lake la kazi,`` alidai.

Wakili huyo alidai kuwa washitakiwa kudai kuwa walipewa vikaratasi vya maelekezo ya namna ya tukio lilivyokuwa ilielezwa kwenye maelezo ya marehemu Rashidi Lema, lakini hakuna shahidi wa upande wa mashitaka aliyeunga mkono maelezo hayo dhidi ya Zombe.

Aidha, alidai pia hatua ya Zombe kwenda Kituo cha Polisi Urafiki ni sehemu ya majukumu yake ya kazi ambayo alitekeleza siku hiyo baada ya kupigiwa simu na Mkuu wa Kituo cha Polisi Urafiki kwamba kuna tatizo la fedha za kielelezo zimepotea.

Alidai kuwa Zombe alitoa amri zipatikane na kweli siku ya pili yake mteja wake alikabidhiwa, lakini upande wa mashitaka haujaziwasilisha mahakamani hapo.

Msemwa aliongeza kuwa tukio hilo limeongelewa na upande wa mashitaka na washitakiwa wa pili, Christopher Bageni na wa tatu Ahemed Makelle ambao wameieleza mahakama.

``Mtukufu Jaji kuwapongeza washitakiwa ni kawaida kwa Jeshi la Polisi kwa wanaofanya vizuri, na sio wazo binafsi la Zombe. Hizi ni taratibu za kiofisi,`` alidai.

Alidai kuwa mteja wake amelalamikia mahakama huhusu hatua ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) aliyestaafu Godfrey Shaidi, kumshitaki baada ya kufanya mawasiliano na washitakiwa wenzake wakiwa gerezani ambapo alizitumia kama kigezo cha kumfungulia mashitaka.

``Bila kuacha shaka, mteja wangu hakushiriki kupanga wala kufanya mauaji hayo na naiomba mahakama hii isimtie hatiani, imuachie huru,`` alidai Msemwa.

Naye wakili Denis Msafiri anayemtetea Rajabu Hamis alidai kuwa mteja wake alikuwa muungwana na kwamba alieleza jinsi ukweli na mtiririko mzima wa tukio hilo akiwa na kiongozi wake Bageni.

Upande wa mashitaka uliomba shauri hilo liendelee leo ili watoe hoja zao dhidi ya washitakiwa.

Hata hivyo, Jaji Massati alisema kesi hiyo haiwezi kuendelea leo kwani ilikuwa imepangwa isikilizwe hadi jana tu na itaendelea tu pale Jaji Mkuu wa Tanzania atakapotoa kibali.

Mbali na Zombe washitakiwa wengine ni Christopher Bageni, Ahmed Makelle, Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Chonza, Abeneth Saro, Rajabu Hamis na Festus Chenge.

Katika kesi hiyo, washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka manne ya mauaji, Januari 14, mwaka 2006 wanadaiwa kuwa waliwaua wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, Ephraimu Chigumbi, Mathias Lukombe na dereva teksi Juma Ndugu.
 
Waandishi wa habari si walikuwepo full time? Natumaini wataitoa muda si mrefu.
Ninataka nione Jaji alijikwamua vipi wakati alishasema inaonekana hawakuuliwa kwa kutupiana risasi kama Polisi walivyodai, wote walikua executed (Wamepigwa risasi kichogoni wote).

Kwa hiyo alishasema polisi walidanganya, sasa iweje leo wote hawana hatia? Niko confused sana.


,,,,,Mkuu KANG si ndo JUDGE kesha sema kwamba POLISI watafute wauaji halisi,ambao yeye JUDGE kutokana na ushahidi uliopelekwa pale anawaona ni Pc SAADI na mwingine sijui nani huyo.
 
Ni upumbavu mtupu, sasa serikali ijiandae kumlipa fidia na kumrudishia kazi yake aliyokuwa anafanya. Hii serikali ya JK ni upuuzi mtupu, subiri na kesi ya Mramba, Yona na wengine. Utasikia kesi imefutwa hakuna ushahidi huku watu wamelamba pesa za walipa kodi. Mtasikia tu hata Mzee wa Gari Nyekundu pia kafutiwa kesi............hakuna ushahidi wa kutosha. Hii ndiyo Tanganyika.
 
Pamoja na kwamba kuna utawala wa sheria, lakini kwa hali halisi ya mazingira ya kesi iliokua ikimkabili Zombe na kwa kuzingatia ripoti ya kamati ilioundwa kuchunguza suala hili, kweli naona kuna uwalakini mkubwa sana kwa Zombe kuwa huru.

Swali ni Je, nani aliewaua hao watu...? Nashauri upande wa walalamikaji yaani serikali wakate rufaa mara moja kuelekea mahakama ya Rufani, kule hakuna mchezo na ndiko wanasheria halisi walipo...!

Tatizo lililojitokeza katika sakata hili la mauaji wa 'wafanyibiashara' nguvu nyingi ilielekezwa kwa Zombe ilhali ukiangalia mazingira ya kiutendaji unakuta Zombe hana uzito wowote katika kesi hii kama mtu muhimu. Hili lilikuwa linajulikana wazi kisheria. Waandishi wa Habari na wanaharakati wengine waliupotosha umma kwa kumuhukumu Zombe nje ya mahakama na ndiyo maana hadi leo baadhi ya watu hawaamini kwamba Zombe angeweza kutoka huru katika mahakama kuu.
Kesi hii itupe fundisho la kuacha kuongea na hisia zetu, kuacha ushabiki na badala yake kuwekeza katika fikra yakinifu zenye kuangalia mambo kwa mapana na marefu, vinginevyo tabia zetu ndiyo zitakazoendelea kutufanya waandishi wa habari watuandikie kitu gani kwa maslahi ya biashara zao.
Kwangu mimi, Zombe alikuwa siyo mshtakiwa muhimu katika kesi hii na kosa la Prosecution ni kufuata ushauri wa kisiasa uliotolewa na kamati maalum ya uchunguzi, vinginevyo Zombe ndiye ambaye alitakiwa kuwa shahidi muhimu katika kesi hii na si mshitakiwa.
 
,,,,,Mkuu KANG si ndo JUDGE kesha sema kwamba POLISI watafute wauaji halisi,ambao yeye JUDGE kutokana na ushahidi uliopelekwa pale anawaona ni Pc SAADI na mwingine sijui nani huyo.

King Zenj,
Ukiangalia kwa makini hata ingelikuwa Judge wa mahakama ya Dunia, ingemuwia vigumu kuhukumu kesi hii ya mauaji wakati kuna watuhumiwa wengine hawajapatikana. Itakuwaje baada ya jaji kupitisha hukumu halafu wanatokea wale waliotoroka na kubainika ndiyo waliouwa?
Nadhani hawajamaa wasimlaumu Judge, amefanya kazi yake viliivyo kwa mujibu wa sheria.
 
Tatizo lililojitokeza katika sakata hili la mauaji wa 'wafanyibiashara' nguvu nyingi ilielekezwa kwa Zombe ilhali ukiangalia mazingira ya kiutendaji unakuta Zombe hana uzito wowote katika kesi hii kama mtu muhimu. Hili lilikuwa linajulikana wazi kisheria. Waandishi wa Habari na wanaharakati wengine waliupotosha umma kwa kumuhukumu Zombe nje ya mahakama na ndiyo maana hadi leo baadhi ya watu hawaamini kwamba Zombe angeweza kutoka huru katika mahakama kuu.
Kesi hii itupe fundisho la kuacha kuongea na hisia zetu, kuacha ushabiki na badala yake kuwekeza katika fikra yakinifu zenye kuangalia mambo kwa mapana na marefu, vinginevyo tabia zetu ndiyo zitakazoendelea kutufanya waandishi wa habari watuandikie kitu gani kwa maslahi ya biashara zao.
Kwangu mimi, Zombe alikuwa siyo mshtakiwa muhimu katika kesi hii na kosa la Prosecution ni kufuata ushauri wa kisiasa uliotolewa na kamati maalum ya uchunguzi, vinginevyo Zombe ndiye ambaye alitakiwa kuwa shahidi muhimu katika kesi hii na si mshitakiwa.

Nimepatwa na butwaa kuona kuwa JF ambao tunasema ni GREAT THINKERS tukihukumu kwa Hisia.watu hawajasoma hukumu ya jaji,hawajahudhuria mahakamani kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili,mara nyingi wamekuwa wakinukuu msemo wa MAO no research no right to Speak, lakini leo wamekuwa majaji na wanasheria.

Criminal Law kwa waendesha mashtaka wa Tanzania sio rahisi kumtia hatiani mtuhumiwa.nchi za Ulaya bado sio rahisi kuwatia watu hatiani kwenye Murder.

nimesoma Tanzania Daima wao kidogo wameweza kuonesha Jaji kasema nini?kwenye sheria hii ya CRIMINAL ni jukumu la waendesha mashitaka kudhibitisha au kupeleka ushahidi kwa Jaji na si kazi ya Jaji kutafuta ushahidi wa kumtia hatiani mtuhumiwa.kazi ya jaji ni kutafisiri sheria.

Zombe akingeshitakiwa kwa makosa mengine kama uzembe kazini au kujua kosa lililofanyika chini ya dhamana yake, lakini sio mauaji kwani sheria ya Criminal inatonya nafasi kubwa kwa mtu kushinda.
Hivi hapa JF hatuna wanasheria? waje kutufundisha sheria kama hizi.hatuna tofauti na watu wanashinda vijiweni.
 
King Zenj,
Ukiangalia kwa makini hata ingelikuwa Judge wa mahakama ya Dunia, ingemuwia vigumu kuhukumu kesi hii ya mauaji wakati kuna watuhumiwa wengine hawajapatikana. Itakuwaje baada ya jaji kupitisha hukumu halafu wanatokea wale waliotoroka na kubainika ndiyo waliouwa?
Nadhani hawajamaa wasimlaumu Judge, amefanya kazi yake viliivyo kwa mujibu wa sheria.

Nimefikiria kwa makini sana na kupata conclusion kuwa serikali na waendesha mashitaka wake ama kwa makusudi au kwa kuwa na uwezo mdogo ni chanzo cha kushindwa kwa kesi hii na nyingine nyingi za ufisadi huko mbeleni.

Haingii akilini watu 12 kuua watu 4 kwa risasi moja moja ya kisogoni wakati bunduki ina trigger moja. mashitaka yaliandaliwa kwa kukurupuka ili kufuata maelezo ya IKULU kwa kuwa tume ya Kipenka imebaini kuwa waliouwawa si majambazi sheria ifuate mkondo na huu ndiyo mkondo. Kesi ingekuwa na matokeo tofauti kama mashitaka yangefunguliwa kwa mujibu wa yalivyotakiwa kuwa. counts zingekuwa

1. Kuwaua raia wema kwa kukusudia

2. Kula njama za kuwauwa raia wema na kuwaibia

3. Kudanganya umma ukweli kuhusu mauji ukiwa ni mtumishi wa umma mwenye dhamana ya kuuambia ukweli umma juu ya kilichojiri

4. Kupanga njama za kuzuia sheria isichukue mkondo wake kwa kutumia cheo chako kuwalazimisha watuhumiwa kusema ukweli mbele ya Tume ya rais na mahakamani

5. Kumuacha mtuhumiwa wa mauji "Saad Alawi" kutoroka wakati ukijua kuwa ni dhahiri ameshiriki mauaji na wewe ukiwa ni mwenye dhamana ya kukamata wakalifu ukamtorosha

6. Kutumia nafasi yako kutisha raia wema kwa kuwapiga vibao na kuwadhalilisha kwa kuwaweka ndani wakati ukijua kuwa hawakuwa na hatia yoyote
.
.
.
.
.
30. ........

Nina hakika kuwa Zombe na wenzake wasinge futa counts zote hizi ila kwa kuwa waendesha mashitaka kwa ufinyu wa akili zao ama kwa makusudi au kwa ukilaza wao wamempatia Zombe Kicheko.

" Hongera Zombe, unastahili na kurudishiwa wadhifa wako wa RPC wa Rukwa" na kulipwa malupulupu yako yote na kurudishwa kazini ufanye kazi yako.

Haya wale ndugu za wa UDSM pale Faculty of law mmepata nondo mpya ya kujibia mtihani wa "Criminal law". Zombe et al Vs URT by Salum Massati jaji wa mahakama kuu.
 
Nimepatwa na butwaa kuona kuwa JF ambao tunasema ni GREAT THINKERS tukihukumu kwa Hisia.watu hawajasoma hukumu ya jaji,hawajahudhuria mahakamani kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili,mara nyingi wamekuwa wakinukuu msemo wa MAO no research no right to Speak, lakini leo wamekuwa majaji na wanasheria.

Criminal Law kwa waendesha mashtaka wa Tanzania sio rahisi kumtia hatiani mtuhumiwa.nchi za Ulaya bado sio rahisi kuwatia watu hatiani kwenye Murder.

nimesoma Tanzania Daima wao kidogo wameweza kuonesha Jaji kasema nini?kwenye sheria hii ya CRIMINAL ni jukumu la waendesha mashitaka kudhibitisha au kupeleka ushahidi kwa Jaji na si kazi ya Jaji kutafuta ushahidi wa kumtia hatiani mtuhumiwa.kazi ya jaji ni kutafisiri sheria.

Zombe akingeshitakiwa kwa makosa mengine kama uzembe kazini au kujua kosa lililofanyika chini ya dhamana yake, lakini sio mauaji kwani sheria ya Criminal inatonya nafasi kubwa kwa mtu kushinda.
Hivi hapa JF hatuna wanasheria? waje kutufundisha sheria kama hizi.hatuna tofauti na watu wanashinda vijiweni.

I agree na wewe kabisa kuwa kumtia mtu hatiani katika CRIMINAL case hasa kesi za mauaji ni jambo gumu sana. Mimi ni mpenzi sana wa Crime Scene Investigations; Forensic Files na vingine vingi kama hivyo. Pamoja na teknolojia na maendeleo makubwa katika nchi zilizoendelea, lakini suala la maamuzi ya kesi za mauaji linabaki kuwa gumu na nyeti. Nchi hizi zimeshashuhudia mara kadhaa watu waliopatikana na hatia wakirudishwa mahakamani kufutiwa mashtaka kwa sababu ya makosa yaliyojitokeza na kutoa wrong judgment.

Mfano sasa hivi kuna suala la Troy Davis ambaye amehukumiwa kifo kutokana mauaji aliyoyafanya miaka 20 iliyopita. Huyu jamaa hadi leo hii mahakama za Marekani zinasuasua kuidhinisha kunyongwa kwake.
http://news.aol.com/article/supreme...e/supreme-court-orders-new-hearing-for/454596
 
I agree na wewe kabisa kuwa kumtia mtu hatiani katika CRIMINAL case hasa kesi za mauaji ni jambo gumu sana. Mimi ni mpenzi sana wa Crime Scene Investigations; Forensic Files na vingine vingi kama hivyo. Pamoja na teknolojia na maendeleo makubwa katika nchi zilizoendelea, lakini suala la maamuzi ya kesi za mauaji linabaki kuwa gumu na nyeti. Nchi hizi zimeshashuhudia mara kadhaa watu waliopatikana na hatia wakirudishwa mahakamani kufutiwa mashtaka kwa sababu ya makosa yaliyojitokeza na kutoa wrong judgment.

Mfano sasa hivi kuna suala la Troy Davis ambaye amehukumiwa kifo kutokana mauaji aliyoyafanya miaka 20 iliyopita. Huyu jamaa hadi leo hii mahakama za Marekani zinasuasua kuidhinisha kunyongwa kwake.

Nakubaliana na wewe mtu akiisha nyongwa ni irreversible na ndiyo maana Jamaa kesi yake inabidi kusikilizwa upya

US Supreme Court Orders New Hearing for Troy Davis

By Jonathan Springston, Senior Staff Writer, The Atlanta Progressive News (August 17, 2009)
(APN) ATLANTA -- The Supreme Court of the US, in a 6-2 decision, ordered a federal judge in Georgia on Monday, August 17, 2009, to consider and rule on innocence claims brought by Georgia death row inmate Troy Anthony Davis.
The majority opinion, written by Justice John Paul Stevens, calls on the U.S. District Court for the Southern District of Georgia to "receive testimony and make findings of fact as to whether evidence that could have been obtained at the time of trial clearly establishes [Davis'] innocence."
"The substantial risk of putting an innocent man to death clearly provides an adequate justification for holding an evidentiary hearing," Stevens wrote.
A jury sentenced Davis to death in 1991 for the murder of Savannah police officer Mark Allen MacPhail in a Burger King parking lot in 1989.
Chatham County prosecutors used only eyewitness testimony to obtain a conviction. Since that time, seven of nine state witnesses have either changed or recanted their testimonies in sworn affidavits.
The other two, Stephen Sanders and Sylvester "Red" Coles, have not recanted.
Sanders was hanging with Air Force friends at the Burger King at the time of the incident. He told police two hours after the incident he could only recognize those at the scene by their clothes but implicated Davis two years later at trial.
Coles, who told police he possessed a .38 caliber revolver on the night of the murder and who was with Davis at the time of the shooting, always maintained Davis was the killer. Yet three witnesses now say Coles confided to them on different occasions that he in fact pulled the trigger.
Davis supporters applauded Monday’s Court decision.
"We are grateful the nation’s highest court has seen the wisdom in granting a new evidentiary hearing to Troy Davis," Laura Moye, Director of Amnesty International USA’s Death Penalty Abolition Campaign, said in a statement. "For years, Amnesty International has maintained that this man’s compelling case of innocence needs to see the light of day. Finally it will."
Moye, who previously served as Atlanta-based Deputy Director in Amnesty USA's Southern Regional Office, recently moved to Washington, DC, to accept the new position.
As previously reported by Atlanta Progressive News, Davis has narrowly avoided execution three times since July 2007 while seeking relief from the Georgia Board of Pardons and Paroles, the Georgia Supreme Court, and the Eleventh Circuit Court of Appeals.
A three-judge panel of the Eleventh Circuit in April denied Davis’s request for an evidentiary hearing, arguing they were bound by procedural requirements of the Anti-Terrorism and Effective Death Penalty Act of 1996.
Justice Antonin Scalia, writing the dissent, called Monday’s Court order "a fool’s errand," and "a confusing exercise."
"The Court proceeds down this path even though every judicial and executive body that has examined petitioner’s stale claim of innocence has been unpersuaded, and (to make matters worst [sic]) even though it would be impossible for the District Court to grant any relief," Scalia wrote.
"Transferring this case to a court that has no power to grant relief is strange enough," he added. "It becomes stranger still when one realizes that the allegedly new evidence we shunt off to be examined by the District Court has already been considered (and rejected) multiple times."
However, in APN's analysis of the legal history of this case, this news service found that no court actually considered the evidence in the context of innocence claims, even though it was presented to them.
Stevens argued it "would be an atrocious violation of our Constitution and the principles upon which it is based to execute an innocent person."
"Imagine a petitioner in Davis’s situation who possesses new evidence conclusively and definitively proving, beyond any scintilla of doubt, that he is an innocent man,” Stevens wrote. “The dissent’s reasoning would allow such a petitioner to be put to death nonetheless. The Court correctly refuses to endorse such reasoning."
Justices Stephen Breyer and Ruth Ginsberg joined Stevens in his opinion while Justice Clarence Thomas joined Scalia in dissent. Justice Sonia Sotomayor, who was only confirmed in recent weeks, played no role in Monday’s decision, Stevens noted.
Attorneys for Davis filed what was considered at the time a long-shot writ of habeas corpus, a lawsuit that allows an inmate to bring a constitutional claim with the Supreme Court, in May 2009.
Later that month, 27 former judges and prosecutors, including former Georgia lawmaker Bob Barr and FBI Director William Sessions, filed an amicus brief in support of Davis.
The Court surprised many in June 2009 when it remained quiet on the Davis writ as its previous term expired. Legal groups had expected the Court to wait until at least later this fall when it returned for a new session to make a decision.
"Given the lack of hard evidence tying Davis to Officer MacPhail’s murder, it would be nothing short of unconscionable to put him to death as a means of conveniently tying up loose ends," Moye said Monday. "Finally there is an opportunity for justice to truly be served."
Due to efforts by groups like Amnesty International and Georgians For Alternatives to the Death Penalty, support for the Davis case has garnered international attention. Former President Jimmy Carter, Pope Benedict XVI, and Archbishop Desmond Tutu are among the noted figures calling on clemency for Davis.
EDITOR'S NOTE: Many of our readers will recall that back in 2007, within the days and weeks leading up to Davis's first scheduled execution, Atlanta Progressive News was the only media organization to have reported on the 7 out of 9 recanted witnesses in Davis's case.
 
h.sep7.gif
master.gif

Zombe ashinda kesi
• Asema serikali imeshindwa kuthibitisha kesi

na Happiness Katabazi na Deogratius Temba


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana ilitoa hukumu ya kushtusha baada ya kumwaachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe na wenzake wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja.

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya saa sita, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati, alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, amebaini kuwa serikali imeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo.

"Katika kesi hii upande wa mashitaka licha ya kuleta mashahidi 37 na vielelezo 23, umeshindwa kuithibitishia mahakama kuwa ni kweli washitakiwa wote ndio waliowaua marehemu na kwa sababu hiyo nawaachia huru washitakiwa wote.

"Na kwa kuwa mahakama hii imewaona washitakiwa si wauaji, hivyo kuanzia sasa naliagiza Jeshi la Polisi liende kuwasaka wauaji wa marehemu wale, na Zombe na wenzake waachiliwe huru," alisema Jaji Massati na kuuacha umati wa watu ukiwa umeshangaa.

Jaji Massati, alisema kamwe mahakama haiwezi kumhukumu mshitakiwa kwa ushahidi dhaifu na wa kusikia kama uliowasilishwa mahakamani hapo, kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria.

"Mahakama haipo kwa ajili ya kuonea mtu kwa kumhukumu kwa ushahidi wa kusikia, ambao haukubaliki kisheria,"

alisema Jaji Massati huku akionekana kujiamini.

Baada ya Jaji Massati kutamka kuwaachia huru washtakiwa hao, Zombe na Christopher Bageni (aliyekuwa mshitakiwa wa pili) walikumbatiana kizimbani kwa furaha na wananchi waliokuwa wamefurika katika ukumbi namba moja mahakamani hapo wakionekana kushangilia na wengine kuhuzunika.

Baada ya Jaji Massati kutoka mahakamani hapo, Zombe na wenzake walitolewa kwa mlango wa nyuma huku wakiongozwa na wanausalama.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata, zinaeleza kuwa baada ya Zombe na wenzake kutolewa mahakamani hapo, walipelekwa Kituo cha Polisi Kati na baada ya muda kila mmoja aliondoka.
Habari hizo zinaeleza kuwa kuanzia leo, Zombe na wenzake wanaweza kwenda gereza la Keko kuchukua vifaa vyao.

Awali, akiuchambua ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo, Jaji Massati, alisema ushahidi wa upande wa mashtaka ni dhahifu na ulijikita katika ushahidi wa kusikia.

Alisema kati ya mashahidi waliofika mahakamani hapo, hakuna hata mmoja aliyeiambia mahakama kwamba alikuwa eneo la Msitu wa Pande na kushuhudia washitakiwa hao wakiwaua marehemu hao.

Jaji Massati alisema hoja ya upande wa mashitaka kwamba hatua ya Zombe kwenda Kituo cha Polisi Urafiki Januari 14,

2006 ilidhiirisha kwamba alikuwa akijua nini kilikuwa kikiendelea kuhusu mauaji hayo, haina nguvu kwani kwa mujibu wa Police General Order (PGO), inampa mamlaka Mkuu wa Upelelezi (RCO) kufika eneo lolote pindi litokeapo tukio la uhalifu, hivyo akasema mshitakiwa huyo alikwenda kituoni hapo kwa mujibu wa sheria za Jeshi la Polisi.

Akipangua hoja kwamba Zombe alitoa mkono wa pongezi kwa baadhi ya washitakiwa wenzake, Jaji huyo alisema kwa mujibu wa PGO pia inamruhumu kiongozi wa Jeshi la Polisi kutoa zawadi au mkono wa pongezi kwa askari wake wa chini pindi apatapo taarifa kuwa wamefanya vizuri.

Hata hivyo, alisema licha ya baadhi ya washitakiwa kudai kuwa walipongezwa na Zombe, upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kama ni kweli alitoa mkono wa pongezi.

Akimzungumzia mshitakiwa wa 12, Rajabu Bakari, alisema pamoja na kwamba katika utetezi wake alikiri kwenda Msitu wa Pande na kueleza kuwa alimshuhudia mshitakiwa wa 14, Saad (hajakamatwa hadi sasa) kuwa ndiye aliyewaua marehemu hao kwa risasi, Jaji Massati alisema utetezi huo hauna msingi wowote kwa kuwa mshitakiwa huyo hajakamatwa.
"Ushahidi wa Bakari hauna msingi wowote kwa sababu alimtaja Saad ambaye hayupo mbele ya mahakama hii, na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mtu ambaye bado hajafikishwa mahakamani," alisema Jaji Massati.

Pamoja na hayo, Jaji Massati alisema hakubaliani na hoja za upande wa mashitaka iliyowahi kutolewa na wakili Mgaya Mtaki, kwamba mahakama hiyo imwone Zombe na Festus Gwasabi kuwa wana hatia ya mauaji, na endapo mahakama haitawaona na hatia katika mashitaka hayo, basi iwatie hatiani na kosa la kujua tukio hilo.

Alisema kimsingi washitakiwa hao walishitakiwa kwa kesi ya mauaji, hivyo si kazi ya mahakama kubadilisha hati ya mashitaka na kuwashitaki kwa kosa jipya.

Mbali na Zombe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Christopher Bageni, Ahmed Makele, WP 4593 PC Jane Andrew, D 1406 Koplo Emmanuel Mabula, D 8289 DC Michael Shonza, D. 2300 Abeneth Saro, D.4656D/Koplo Rajabu Bakari na D.1317D/XP Festus Gwasabi.

Washitakiwa hao walidaiwa kuwa Januari 14, mwaka 2006 waliwaua wafanyabiashara watatu wa madini wa wilayani Ulanga, mkoani Morogoro; Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi na Mathias Lukombe pamoja na dereva teski Juma Ndugu, mkazi wa Dar es Salaam kwa madai kuwa walikuwa majambazi.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, maelfu ya wananchi walianza kumiminika katika viwanja ya mahakama hiyo kuanzia saa 12 asubuhi, ili kushuhudia Zombe na wenzake watakapofika mahakamani hapo. Zombe na wenzake waliwasili mahakamani hapo, majira ya saa 2:30 asubuhi wakiwa kwenye basi la mahabusu na kusindikizwa na magari madogo aina ya Land Cruiser STK 4479 na STK 4478, yaliyokuwa na askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza waliokuwa na silaha nzito.

Ndani ya Mahakama Kuu

Kutokana na umati mkubwa wa wananchi waliomiminika kusikiliza kesi hiyo, Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Lameck Mlacha, alitaka watu wasijae mahakamani hapo kwani vitafungwa vipaza sauti ukumbini hapo na kwenye varanda za mahakama hiyo. Hata kabla ya kuanza kusomwa kwa hukumu hiyo, watu walionekana kuchoka kutokana na kufika mahakamani hapo muda mrefu.

Kijana akamatwa mlangoni kwa Jaji

Katika tukio lisilo la kawaida majira ya saa 5:20 asubuhi, kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Fabric Msami (20), alikamatwa na Jeshi la Polisi, akiwa amejiegesha kwenye uchochoro mdogo ambao Jaji anapitia kuingia na kutoka mahakamani.
Kijana huyo, aliyekuwa na kitambulisho cha Shule ya Sekondari Jitegemee ya jijini Dar es Salaam, ambacho kilimalizika muda wake mwaka 2007, aliwaeleza polisi katika mahojiano kuwa alikuwa ametumwa na askari polisi ambaye hakumtaja kwa jina.
Bila kueleza alikotokea, alipozidi kuulizwa hakuweza kueleza lengo la kujibanza katika mlango huo ambao hauruhusiwi kuingilia mtu yeyote au kusimama, na sababu za kuwepo mahali hapo zaidi ya kueleza kuwa alikuwa ametumwa na askari. Askari polisi walimkabidhi kijana huyo mahabusu ndogo ya mahakama, ambapo baadaye haikujulikana alikopelekwa baada ya kuchukuliwa maelezo.
Ulinzi waimarishwa kila kona

Askari polisi, askari kanzu, na wale wa usalama wa taifa zaidi ya 200, walifurika mahakamani hapo kwa lengo la kuimarisha ulinzi wakati hukumu ya kesi ikisomwa.
Askari hao, waliokuwa wamechanganyika na maofisa wa majeshi hayo hususani wale wenye vyeo vya warakibu na wakaguzi wasaidizi, walionekana wakizunguka kila kona ya jengo la mahakama wakiwa na redio za mawasiliano.
Mbali na askari hao wa vyeo vya juu kufurika katika mahakama hiyo, askari wengine wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU), waliokuwa kwenye magari sita aina ya Land Rover, wenye silaha nzito na mabomu ya machozi, mbwa na gari la maji ya kuwasha, walionekana wakiwa umbali wa mita 30, kutoka jengo la mahakama.
Mbali na polisi, askari wa Jeshi la Magereza, nao jana walionekana wamevalia kininja, wakiwa wametanda ndani ya uzio wa mahakama hiyo wakiwa na silaha. Taarifa ambazo zilipatikana kutoka kwa vyanzo vya kuaminika ndani ya Jeshi la Polisi, zilieleza kuwa amri ya kuwepo kwa askari polisi wengi mahakamani hapo ilitoka makao makuu ya jeshi hilo tangu asubuhi, kwamba uongozi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, udhibiti wananchi kusogelea lango la Mahakama Kuu.

Hukumu inatolewa

Mara baada ya Jaji Massati kumaliza kusoma hukumu, nyuso za watu wengi waliokuwapo eneo la mahakama zilibadilika na baadahi yao kuanza kukimbia huko na huko. Wengine wakishuka ngazi kwa kuhofia vurugu, wengine wakipiga makelele kuwa hakuna haki iliyotendeka.
"Hawana kosa! Hawana kosa! Wameachiwa wote!'' ni sauti za mikato zilizokuwa zikisikika kutoka kwa baadhi ya watu waliokuwapo mahakamani hapo huku wakielekea kutoka nje ya mahakama hiyo.
Katika ngazi za jengo la Mahakama Kuu, kutoka ghorofa ya kwanza, ambako hukumu ilikuwa ikisomwa, ndugu wa Zombe waliokuwa wamekaa katika viti vya mapokezi, walipopata taarifa, walianguka chini na kuzimia, huku baadhi ya watoto ambao hawakufahamika wametoka wapi walionekana wakilia na wengine wakiruka ruka kushangilia.
Wakati huo, wananchi wengi walioonekana wenye hasira, walianza kupiga kelele na kuziba lengo la mahakama wakitaka Zombe atolewe nje, ili wamshambulie kwa mawe, kitendo kilichofanya askari kanzu kuzingira lango hilo na kudai kuwa hatatolewa hadi wananchi wote watakapoondoka eneo hilo.

Huku magari ya askari kanzu yasiyo na namba za polisi yakiwa yamezingira lango la mahakama, ghafla saa 9:47 adhuhuri, Zombe na wenzake walipakizwa katika gari ndogo aina ya RV4 ya rangi ya fedha, kwa mlango wa nyuma huku wakisindikizwa na askari zaidi ya 20, wenye silaha waliokuwa kwenye magari maalumu yaliyokuwa yakipiga ving'ora vya tahadhari. Wakati Zombe na wenzake wakiondolewa kwa kasi katika eneo hilo, wananchi wengi walikuwa wakipiga kelele na kuyafukuza magari hayo kwa nyuma, wakitukana na kutoa maneno hovyo wakidai kuwa hakuna haki.

Wakili wa Zombe anena

Wakili wa kujitegemea, aliyekuwa upande wa utetezi, Gaudiosus Ishengoma, alisema ushahidi wa kosa la jinai ni tofauti na watu wanavyotarajia, kwani hakukuwepo na ushahidi wa moja kwa moja, kati ya ule wa mahakama na polisi, kwani hawakuweza kuwasilisha ushahidi wa mauaji.
"Polisi haikuweza kuleta ushahidi wa moja kwa moja juu ya mauaji, haikutoa vielelezo ni nani aliyeua, sasa sheria imeshachukua mkondo wake, afadhali kuachia watu 100, kuliko kumtia hatihani mtu mmoja asiye na hatia," alisema Ishengoma.
Alisema serikali inalo jukumu la kufikiri kama inakata rufaa, ifanye hivyo ndani ya muda iliyopewa ambao kisheria ni siku 14, baada ya hukumu kutolewa.

Akizungumzia suala la Zombe na wenzake kudai fidia kwa kushitakiwa kwa makosa ambayo si ya kwao, Ishengoma, alisema wanayo haki ya kufanya hivyo wakitaka, na kama wataona kama wanahitaji kulipwa fidia kutokana na kupotezewa muda na kuchafuliwa majina yao.
Mwanasheria huyo, alibainisha anayetakiwa kulipa fidia kama Zombe na wenzake watakwenda mahakamani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani ndiye aliyeunda tume ya kuchunguza tukio hilo na kuwafikisha mahakamani na si familia ya marehemu waliouawa.
"Mtu anayeachiwa na mahakama kwa kutokuwa na kosa, hasa kwa kesi kama hii, anamshitaki aliyempeleka polisi na kusababisha kupandishwa mahakamani. Hapa ni rais ambaye aliunda tume ya kuwachunguza na baadaye kuwapelekea polisi taarifa ambapo waliwakamata watuhumiwa hao," aliongeza. Wakili wa Serikali, Kaishozi, alisema katika kesi hiyo Jaji ndiye aliyekuwa na maamuzi ya mwisho, ila wataenda kukaa na kuangalia kama watarudi mahakamani kukata rufaa au la.

Wananchi walalamika

Umati wa wananchi uliokuwa umefurika nje ya mahakama, ulianza kutoa maoni yao, wengi wao wakionekana kuilaumu mahakama kwa kutoa hukumu hiyo.
"Wazee wa baraza walishasema kuwa anayo hatia, leo mahakama inasema hawajaua, sisi raia tunajiuliza haki ipo wapi? Tunaiomba serikali kukata rufaa la sivyo serikali imeshindwa kazi, na hatuitaki tena," alisema Ramadhan Abdallah, huku akishangiliwa na mamia ya wananchi wenzake. Pia baadhi ya wananchi walionekana kukerwa na kitendo cha washitakiwa hao kuachiwa huru na kupewa ulinzi wa polisi wa kuwatoa mahakamani na ving'ora wakati mwananchi masikini hapewi ulinzi wala msaada hata wa kumpeleka hospitali.
 
Last edited:
Nimefikiria kwa makini sana na kupata conclusion kuwa serikali na waendesha mashitaka wake ama kwa makusudi au kwa kuwa na uwezo mdogo ni chanzo cha kushindwa kwa kesi hii na nyingine nyingi za ufisadi huko mbeleni.

Haingii akilini watu 12 kuua watu 4 kwa risasi moja moja ya kisogoni wakati bunduki ina trigger moja. mashitaka yaliandaliwa kwa kukurupuka ili kufuata maelezo ya IKULU kwa kuwa tume ya Kipenka imebaini kuwa waliouwawa si majambazi sheria ifuate mkondo na huu ndiyo mkondo. Kesi ingekuwa na matokeo tofauti kama mashitaka yangefunguliwa kwa mujibu wa yalivyotakiwa kuwa. counts zingekuwa

1. Kuwaua raia wema kwa kukusudia

2. Kula njama za kuwauwa raia wema na kuwaibia

3. Kudanganya umma ukweli kuhusu mauji ukiwa ni mtumishi wa umma mwenye dhamana ya kuuambia ukweli umma juu ya kilichojiri

4. Kupanga njama za kuzuia sheria isichukue mkondo wake kwa kutumia cheo chako kuwalazimisha watuhumiwa kusema ukweli mbele ya Tume ya rais na mahakamani

5. Kumuacha mtuhumiwa wa mauji "Saad Alawi" kutoroka wakati ukijua kuwa ni dhahiri ameshiriki mauaji na wewe ukiwa ni mwenye dhamana ya kukamata wakalifu ukamtorosha

6. Kutumia nafasi yako kutisha raia wema kwa kuwapiga vibao na kuwadhalilisha kwa kuwaweka ndani wakati ukijua kuwa hawakuwa na hatia yoyote
.
.
.
.
.
30. ........

Nina hakika kuwa Zombe na wenzake wasinge futa counts zote hizi ila kwa kuwa waendesha mashitaka kwa ufinyu wa akili zao ama kwa makusudi au kwa ukilaza wao wamempatia Zombe Kicheko.

" Hongera Zombe, unastahili na kurudishiwa wadhifa wako wa RPC wa Rukwa" na kulipwa malupulupu yako yote na kurudishwa kazini ufanye kazi yako.

Haya wale ndugu za wa UDSM pale Faculty of law mmepata nondo mpya ya kujibia mtihani wa "Criminal law". Zombe et al Vs URT by Salum Massati jaji wa mahakama kuu.

Waendesha mashitaka wengi wamemaliza OPEN UNIVERSITY OF TZ hawana uelewa wa sheria nimeshuhudia wengi wameajiriwa na wanasimamia kesi kubwa kubwa cha ajabu hata uzoefu hawana.kesi kama hii wangemkodisha Professor Abdallah Saffari toka kwenye kuandaa mashitaka hadi mahakamani.

kuna mmoja wa waendesha mashitaka anayesimamia kesi kama hizi nilikuwa naongea nae masuala haya ya sheria nikaona uoni wake ni mdogo sana nilitaka anisadie masuala ya sheria, niikajikuta mimi namsaidia yeye.

hata vitendea kazi alikuwa hana anatumia kitabu cha Criminal Law cha Professor Saffari ambacho ni muongozo kwa wasio wanasheria, mwanasheria yule wa serikali hata kondakta wa daladala ambaye mjanja ni ngumu kumtia hatiani.mshahara wao ni shilingi laki tatu.alinimaliza kuniambia ana masters ya sheria.
 
Last edited:
Ukistaajabu ya musa utaona ya firauni!!!! Hukumu ya zombe inaniashiria yafuatayo katika kesi zilizo mahakamani na zijazo kama itafanywa rejea na hukumu zijazo:
1. Wauaji wote wa albino wataachiwa maana hakuna aliyeshikwa anamuua albino ila watuhumiwa wanakutwa na viungoi vya albino-kama alivyosema masati itakuwa ni ushahidi wa kimazingira
2. Polisi akikutoa nyumbani kwako kama mtuhumiwa kesho ukakutwa umekufa, hana hatia maana hakuna aliyeona anakupiga risasi- ushahidi wa kimazingara tutegemee vifi vingi
3. Polisi wataua sana kwa hukumu kama hii- atakuchukua, atakuua vyumba vya sero, hakuna aliyemuona anafyatua risasi-hana hatia
4. Mwisho naomba kujua wasifu wamasati na ikiwezekana baadhi ya kesi zilizopitia mikononi mwake for refrence
5. Kama hukumu zake ndio hizi, basi kesi zilizopitia kwake tangu aingie kwenye nafasi za kutoa haki ni questionable
6. Mungu ziweke roho za wote peponi-amen
 
Jaji ameshindwa kutetea damu za marehemu. Hivyo basi, mikono yake naye imejaa damu za marehemu. Mpaka wakati wake ukifika akumbuke hilo
 
Habari ndy hiyo kaachiwa huru off all suggestions. Tanzania hakuna haki hata siku moja. Tumuombe Mungu atutangulie katika kila jambo. kwa utaratibu huu tumekwisha.
 
Kwani Zombe na wenzake walishtakiwa kwa kosa MOJA tu? Kama hawakutiwa hatiani kwenye kosa la kuua, hayakuweko makosa mengine?

Hakukuweko na kosa la kuwabambikizia watu kosa la wizi wa silaha? Maana walikuwa wamewabambikizia marehemu kosa la kuiba kwa silaha, na badaye alitokea mtu aliyesema ndiye aliyeiba na akapanga na Bageni akimbilie Zanzibar.

Hakukuweko na kosa la kuficha ushahidi? Hakukuwepo na perjury? Maana ushahidi ulitolewa kuonyesha Zombe na Bageni walidanganya mahakama kuhusu yaliyotokea Sinza.

Walishtakiwa kosa kosa moja tu? Au wameshinda yote?
 
Last edited:
Kesi imekwisha jamani tugeukie uchaguzi na iundwe tume huru ya uchaguzi.
 
Jaji ameshindwa kutetea damu za marehemu. Hivyo basi, mikono yake naye imejaa damu za marehemu. Mpaka wakati wake ukifika akumbuke hilo

Mkuu ulitaka Jaji afanyeje, awe nje ya sheria? Maamuzi ya sheria hayaendani na utashi wa wananchi wanataka maamuzi yawe vipi.

Ukiniambia kwamba waendesha mashitaka wa serikali ndio wamechemka hapo tutakuwa pamoja lakini sio Jaji.
 
Back
Top Bottom