Hukumu ya Mwanamke aliyeporwa mtoto, Mahakama imejiaibisha...!!

Huyo Jaji alijiridhisha kuwa mama wa mtoto kweli ni mgonjwa kiasi cha kutoweza kumlea mwanae?
Wabunge wa viti maalum wanawake -hasa wale wa UWT wanasemaji?
Hugo haiku Hana taaluma ya kufanya maamuzi hayo. Ustawi wa jammy na drs walipaswa kuhusika, lakini mama alipaswa kuhojiwa na kujiridhisha na kufanya maamuzi. Rushwa ya wazi kabisa:alien:
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hugo haiku Hana taaluma ya kufanya maamuzi hayo. Ustawi wa jammy na drs walipaswa kuhusika, lakini mama alipaswa kuhojiwa na kujiridhisha na kufanya maamuzi. Rushwa ya wazi kabisa:alien:
King'asti yule hakimu lazima atakuwa na taaluma ya kufanya maamuzi na ndio maana ameaminiwa na kukabidhiwa ofisi ya umma ili awatumikie wananchi.

Kinachoonekana hapa ni kwamba amekengeuka tu labda kutokana na kupewa bahasha, kwani hata mtu asiye na taaluma ya sheria alitakiwa ajiridhishe bila shaka yoyote kwamba ni kweli mama wa mtoto hana uwezo wa kumnyonyesha mwanae, na uthibitisho huo ulipaswa kuwa wa kitabibu (kutoka kwa daktari).
 
Last edited by a moderator:
Kusema ukweli jana niliangalia hiyo taarifa ya habari kweli niliuzunika sana yaani mtoto wa miezi mnne anatenganishwa na mama yake sababu ya pesa mbaya zaidi hakimu aliehukumu hiyo kesi ni mwanamke kweli kweli jamani! MWANAMKE unamnyanganya mwwenzio mtoto kisa pesa za wahindi nimejiuliza mambo mengi sana, kwanza inamaana huyu hakimu hajawai kuzaa hajui uchungu wa mwana.

Je! hii rushwa itakaa ije kuisha?
Je! hakimu kama huyu atachukuliwaje mbele ya jamii hususani majirani zake pale nyumbani kwake?

huyu hakimu ameidhalilisha tasnia yake kwahela za wahindi tumchukulie hatua gani.
kingine hakimu anatoaje hukumu bila vielelezo vya daktari kuthibitisha kuwa mama ni mgonjwa na haruhusiwi kumnyonyesha mtoto?
kwani hakimu ndio anayeamua mtoto anyonyeshwe au asinyonyeshwe? Nilikuw sijajua kama sikuhizi mahakimu nao pia ni madaktari??
BornTown Kuna baadhi ya watu huwa wanasema kwamba adui wa mwanamke ni mwanamke.
Kwa mazingira kama haya kauli hii inaweza kuwa na ukweli kiasi kikubwa, kwa hakimu mwanamke kutoa hukumu ya kikatili dhidi ya mwanamke mwenzake.
 
Last edited by a moderator:
Hakimu mtata hafikiri hata kigogo yaani ye angekuwa ndio kile kichanga agejisikiaje kuwa mbali na mama yake !
 
Mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu si mahakama ya kiislamu (mahakama ya kadhi) ndugu yangu,
sasa hizo sheria za kiislamu zinatoka wapi?

Ndugu wa mume amedai kwamba anataka kuongea na mwanamme mwenzake hamtaki
mama kwa kuwa yale ni mambo ya wanaume kwa mujibu wa sheria za
kiislamu.
Sina uhakika kama sheria za kiislamu ndivyo zilivyo, kama kuna
anayeifahamu vizuri sheria hiyo nitaomba afafanue hapa.

Kwa sheria za kiislamu hata mtoto huyo angekuwa 10 yrs asingepelekwa kwa baba maana hawakufunga ndoa.
 
Inauma sana unatoka nyumbani unaenda mahakamani ukitarajia unapata haki yako badala yake ndo mahakama inakunyima haki yako inauma sana ..pesa inanyima mtu haki jaman tunaelekea wapi ...nimehuzunishwa xana hicho kitendo
 
Una ushahidi?
Ila kwa jinsi yule muhindi alivyokuwa anaongea ameonyesha dharau kubwa sana kwa wazazi wa binti na mahakama yenyewe.

btw, hujambo lakini? umeoptea!!:peep:

ushahid wa kimazingira,,,,,,mahakama ilipaswa walau kujiridhisha na taarifa ya daktari basi,au kwa sababu wamegoma????
 
Ninashauri na kupendekeza mahakama ngazi ya juu iitishe faili la kesi hiyo na kiliptia.Pia weneye weledi wa kisheria kama chama cha sheri cha wanamwake waingilie na kuomba utekelezaji wa hukumu ile usimamishwe kwanza. Nawakilisha.:spy:
 
Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.

MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.

Huyo mwanamke ni mzima wa akili na afya na hakuna kipimo chochote hata cha kucha walichomfanyia....huyo MWANAMKE (HAKIMU) kashakunja zake.....waswahili tunasema LIWALO NA LIWE.......
 
Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.

MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.
kula chako usepe ndio iliyotumika hapo.....
 
Kilichonichosha zaidi hakim mwenyewe ni mwanamke mwenzake pia mtoto ni wa miezi miwili. Tz tumekwisha kwa sasa hakuna shm ya haki wala usalama!

Namuomba huyo mama aende Sumbawanga! Mbona wengine tulishaachana hizi mahakama za mafisi! Ukinidhulumu naenda Mpanda au Sumbawanga, radi inakupiga mchana bila kuwepo hata wingu, lol.
 
Alicho fanyiwa mama huyo ni kitendo kisichovumilika hata kidogo! Kuna kila sababu mashirika ya kutetea haki za binadamu kuingilia kati, ndugu zangu watanzania kama kweli imefikia hali hii katika mahakama zetu tumekwisha sisi walalahoi. mama ambebe mwenyewe tumboni miezi 9, leo sababu tu ya pesa akose haki ya kumlea mwanae! Kama ni mgonjwa na kwa kuwa kila mzazi anamatamani mwanaye awe na afya njema angeelezwa akashauriwa na wataalamu wa kada hiyo angeelewa. Ndugu zangu watanzania kuna mambo ambayo atuyafanyi sasa tukiona hayana umuhimu lakini baadaye tutatamani tungeyafanya hayo kuliko tunayo yafanya sasa.
 
MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.[/QUOTE]

Kwa mahakama za bongo si ajabu. mimi nawashaangaa mnaoshangaa haya maanuzi ya hakimu. Nchi hii ukitanguliza rupia hukumu unapanga wewe.
 
Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.

MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.

Mimi nasema kila siku kuwa serikali ndiyo inayohamasisha watu kujichukulia sheria mkononi watu wanabisha na kuuliza kivipi? mimi ningekuwa ndio mjomba wa huyo mtoto baada ya maamuzi yale ningempasua na kitu kati ya Hakimu au huyo aliyemchukua mtoto.

cha ajabu zaidi yule Kama mama akigoma kumnyonyesha mtoto wake mchanga,anashitakiwa na jamhuri kwa kuhatarisha haki ya msingi ya kuishi ya mtoto. Jiulize hapo kichanga hakijahatarishiwa haki yake ya msingi ya kuishi na huyo hakimu anayenuka rushwa? dawa yao ni kuwapasua kabla ya kwenda mahakamani ukijua wanapesa zaidi yako.
 
Wametumia SHERIA ZA KIISLAM,kuamua hiyo kesi mkuu!si unajua zilivyonamagumashi

Haaa una maana waislamu huwa hawalelewi na mama zao? Na hawa wanaolelewa na mama zao inakuwaje? Mahakama ya kisutu ni ya kiislamu?
 
Back
Top Bottom