Hukumu ya Mwanamke aliyeporwa mtoto, Mahakama imejiaibisha...!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hukumu ya Mwanamke aliyeporwa mtoto, Mahakama imejiaibisha...!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyahende Thomas, Jun 28, 2012.

 1. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
  Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
  Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
  Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.

  MY TAKE:
  Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Mahakama Tanzania ni kichaka cha rushwa na dhuluma ya haki, wanaangalia upande wenye chapaa na kuhamia huko na kusahau sheria zao
   
 3. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wametumia SHERIA ZA KIISLAM,kuamua hiyo kesi mkuu!si unajua zilivyonamagumashi
   
 4. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dah Mahakama,
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ana miez 3 si mi 4, inaonekana hakimu kahongwa pesa mingi kiasi cha kuona ni haki kumtenganisha na mama yake kiumbe huyo anayehtaji mapenzi ya mama yake, ROHO MBAYA NA UKATILI WA HALI YA JUU
   
 6. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika mazingira kama ya kesi hii sina shaka kabisa kwamba hakimu atakuwa amelambishwa chochote kitu.
   
 7. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu si mahakama ya kiislamu (mahakama ya kadhi) ndugu yangu, sasa hizo sheria za kiislamu zinatoka wapi?

  Ndugu wa mume amedai kwamba anataka kuongea na mwanamme mwenzake hamtaki mama kwa kuwa yale ni mambo ya wanaume kwa mujibu wa sheria za kiislamu.
  Sina uhakika kama sheria za kiislamu ndivyo zilivyo, kama kuna anayeifahamu vizuri sheria hiyo nitaomba afafanue hapa.
   
 8. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kilichonisikitisha zaidi ni kwamba hakimu mwenyewe ni mwanamke lakini katika hili haonekani kutambua umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyo Jaji alijiridhisha kuwa mama wa mtoto kweli ni mgonjwa kiasi cha kutoweza kumlea mwanae?
  Wabunge wa viti maalum wanawake -hasa wale wa UWT wanasemaji?
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  uislam unasemaje hapo mdau,,,,,kwani mahakama hiyo ni ya kiislam????
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hapana si jaji huyo alotoa hukumu mdau,,,,,,,
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kilichonichosha zaidi hakim mwenyewe ni mwanamke mwenzake pia mtoto ni wa miezi miwili. Tz tumekwisha kwa sasa hakuna shm ya haki wala usalama!
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nani katoa hukumu? hebu soma tena mada.
   
 14. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,063
  Trophy Points: 280
  Siyo Jaji ni hakimu ila kiukweli inauma maamuzi mengine kwani hati ya dharula ndio inamwongoza hakimu? hapa amekurupuka huyu hakimu
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine basi ficha Upumbavu wako kidogo, sasa Uislam umeingiaje apo nyie ndio mnaipa picha mbaya JF wewe JF kwako ni uwanja wa kejeli dhidi ya Uislam wakati sie wengine JF ni shule.
   
 16. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,063
  Trophy Points: 280
  Kuna mbaba ndugu wa mwanaume alionekana akisema kwenye camera ya ITV kwamba kwa sheria ya kiislamu mwanamume ndio mwenye sauti katika jambo hilo, sasa nikajiuliza mbona hilo suala wamelipeleka kwa mahakama ya serikali (Kisutu)
   
 17. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ndo mahakama za kadhi zijianza sijui itakuwaje kwa haki za wakina mama
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mdau fjm,nimeangalia habar huyo mama alohojiwa ni HAKIMU si jaji,,,,,,,
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ngoja tuangalie gol la barotel
   
 20. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Hili liko wazi Mkuu!

  Tanzania yetu ndio hii!
   
Loading...