Hukumu ya Mwanamke aliyeporwa mtoto, Mahakama imejiaibisha...!!

Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.

MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.

Kwa Tanzania, Pesa ndiyo hakimu. Huna pesa huna haki.
 
Nani katoa hukumu? hebu soma tena mada.

Hukumu imetolewa na hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Ni mwanamke lakini nimeshindwa kuelewa ilikuwaje akatoa ruling bila uwepo wa mama wa mtoto ama uthibitisho wa kitabibu kwamba mama hawezi kumnyonyesha mwanae?
 
Katika Taasisi nisizo ziamini Nchini Tanzania Mahakama ni ya Pili ikiongozwa na Polisi
 
Ipo haja ya wana jf kupita maeneo ya makahama kujua kesi zilizopoambazo zina utata utata,ili kuziweka wazi humu jamvini,naamini kwa kiasi fulani mahakimu na majaji wakijua kesi hizo ziko jamvini itakuwa vigumu kupinda sheria!mimi naamini mla rushwa ukimbaini mapema kabla hajafanya maamuzi ya kumsaidia mtoa rushwa na kumuweka wazi kwa jamii,hawezi kupinda sheria(kwa kiasi fulani itasaidia)
 
hakimu katokota akubali tu hata kama mama hakuwa na uwezo wa kumnyonyesha mtoto bado mama alikuwa na haki ya kumlea mtoto kulingana na umri wa mtoto alio nao.
 
Uwezi amini hii kitu inatokea Tanzania hii,anyway sasa inadhihirisha kuwa mahakama zetu zinasimamia udhalimu kwa kutumiowa na watu wachache wenye hela zao.
 
...Tamwa? Wizara na NGO zinazodai kutetea na kusimamia haki za watoto na akina mama?????
 
Huyo Jaji alijiridhisha kuwa mama wa mtoto kweli ni mgonjwa kiasi cha kutoweza kumlea mwanae?
Wabunge wa viti maalum wanawake -hasa wale wa UWT wanasemaji?

Wewe huna akili kweli! Wabunge viti Maalum wa nini? Wao kazi yao kugonga meza bungeni kupongeza upuuzi wa magamba. Hawana kitu hao, wanakula tu kodi za watanzania na kuwaburudisha wazee. Angalia michango yao mjengoni utakinai. Hizi nafasi zao za kufuta. Hapa ungesema kituo cha haki za binadamu, tgnp kule ndio kuna majembe ya ukweli
 
Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.

MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.

Huwa mahakimu hawagomi, kazi ni moja tu kwa wale wasio waadilifu.........mzigo upoooo! dismisss case! big shame!! tena Mhindi yule alimwaga dharau ya wazi eti wanawake hawana haki ya kukaa na wanaume wakati aliyeamua case hiyo ni mwanamke. Mhindi anasingizia sheria za kiislam!!! sasa wakipata hiyo mahakama ya kadhi inabidi wanawake wa kiislam wahame dini vinginevyo wamekwisha!!!
 
Wametumia SHERIA ZA KIISLAM,kuamua hiyo kesi mkuu!si unajua zilivyonamagumashi

sheria ya kiislaam inaruhusu mwanamke kukaa na mtoto mpaka umri wa miaka saba. uislam sio nani amefanya nini. uislam ni quran na hadithi za mtume. je ulishawahi kusoma hivyo au unakurupuka kwa sababu una chuki na uislam.
 
Mahakama ni vijiwe vya kujiingizia vipato binafsi,pesa ndiyo msahafu wenye aya za maamuzi
majaji,mahakimu,waendesha mashtaka,mpaka mawakili lao moja..yaani siku hizi kila mahakama nje kuna vijiwe kama vya madalali au kama wale vishoka wanaojazana TRA au wapiga debe wa feri na ubungo wako standby na hati feki na vitambulisho feki vya udhamini na pia wana namba zote za watendaji niliowataja hapo juu...Hamna haki pale
 
Njaa mbaya jamani. Hili halihitaji TAKUKURU. Mbaya zaidi Hakimu ni ama, hivi kweli huyu mama anaujua uchungu wa mama? shame
 
Kusema ukweli jana niliangalia hiyo taarifa ya habari kweli niliuzunika sana yaani mtoto wa miezi mnne anatenganishwa na mama yake sababu ya pesa mbaya zaidi hakimu aliehukumu hiyo kesi ni mwanamke kweli kweli jamani! MWANAMKE unamnyanganya mwwenzio mtoto kisa pesa za wahindi nimejiuliza mambo mengi sana, kwanza inamaana huyu hakimu hajawai kuzaa hajui uchungu wa mwana.

Je! hii rushwa itakaa ije kuisha?
Je! hakimu kama huyu atachukuliwaje mbele ya jamii hususani majirani zake pale nyumbani kwake?

huyu hakimu ameidhalilisha tasnia yake kwahela za wahindi tumchukulie hatua gani.
kingine hakimu anatoaje hukumu bila vielelezo vya daktari kuthibitisha kuwa mama ni mgonjwa na haruhusiwi kumnyonyesha mtoto?
kwani hakimu ndio anayeamua mtoto anyonyeshwe au asinyonyeshwe? Nilikuw sijajua kama sikuhizi mahakimu nao pia ni madaktari??
 
Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.

MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.

mlungula huo
 
Back
Top Bottom