Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,752
Baada ya kuapishwa kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania, Mhe. Jaji Kiongozi Mustapha Siyani ametoa mwelekeo wake kupitia Hukumu yake ya Kwanza kama Jaji Kiongozi.
Nimesema mwelekeo nikimaanisha aina ya legacy yake. Kwa mtazamo wangu ninaona mwelekeo au mguu aliouanza Jaji Kiongozi katika hukumu yake ya Kwanza haukuonesha uongozi wa Kimahakama kuonesha haki inatendeka.
Mimi siyo Shabiki wa Mbowe wala CHADEMA hata kidogo. Ukipitia posts zangu za nyuma unaweza kuthibitisha hili. Lakini siwezi kuwa shabiki wa udhalimu, dhulma na ubaguzi mkubwa unaofanywa na CCM yangu kwa Watanzania hususani Wapinzani.
Hukumu hii ya kwanza kama Jaji Kiongozi iwaalike wanazuoni wa Sheria kuitazama sura ya Mahakama ya Tanzania iwapo inasimama kama hekalu la haki au hekalu la kuwapa kinga ya kisheria wezi, wauaji, wanyang'anyi na nasaba hizo.
Tujipe fursa sasa ya kuanza kuokota ama kukusanya vipande vinavyoweza kupelekea upatikanaji wa Katiba Mpya yenye kutoa haki, kuwajibisha na kuimarisha misingi yetu kama Taifa moja bila kubaguana.
Jaji Kiongozi ameonesha mwelekeo wake kama msimamizi mkuu wa judicial caucus yenye dhamana kubwa kwa Taifa hili.
Hapa sijamtaja Jaji Mkuu ambaye bado anaamini Jamhuri ina makamu wawili wa Rais