Hukumu ya Kwanza ya Jaji Kiongozi imetoa mwelekeo wa legacy yake. Tutarajirie haya...

😁😁😁
AIgmal.jpg
 
Kama kuna Mwana CCM yoyote mwenye akili timamu atakayefurahia hukumu ya kipuuzi namna ile basi nitamshangaa sana.

Juzi kwa Mara nyingine niliaminishwa kuwa Elimu haina maana yoyote ile, MTU anaweza kusoma kwa mateso na shida nyingi na akaja kufanya upuuzi ambao ungeweza kufanywa na mwendawazimu tu
Kwa kweli huyo Mustapha, katika jicho la kiimani, ni shetani katila bile la mwanadamu.

Kuna watu walipora kura ili waongeze muda wa kutawala zaidi ya muda uliotamkwa na katiba. Je, waliongeza? Mbona hawakumaliza hata ule muda halali wa kikatiba?

Huyu naye ameamua kuishi na shetani ndani mwake, kwa sababu shetani anamhadaa kuwa, achana na haki na taalum, litumikie tumbo lako, leo ni jaji kiongozi, bado kidogo utakuwa jaji mkuu. Lakini ni nani mwenye uhakika na kesho?

Wamekuwa kama yule tajiri mpumbavu kwenye biblia ambaye Bwana wetu alimzungumzia: Kulikuwa na tajiri, alivuna ngano nyingi, akaijaza kwenye maghala, kisha akajisemea, sasa nina kila kitu cha kutosha, kilichobakia ni kula na kunywa kwa miaka mingi. Lakini Bwana wa majeshi akasema, mpumbavu wewe maana usiku naihitaji roho yako.

Tuishi kwa kutenda haki, ili kama tunaishi au tunakufa, tunakuwa kwenye haki.

Mungu wetu waangalie hawa wapindishao haki kwa manufaa yao, wala wasimpe shetani wakati wa kujisifu kuwa ni mwenye nguvu mbele ya utukufu wako. Ukamtiishe shetani aishie katika mioyo yao ili wajue kuwa shetani ni takataka mbele ya ukuu wako. Ukuu na utukufu ni wako, duniani na mbinguni, milele na milele.
 
Haki huinua Taifa
 
Unawajua magaidi ndugu yangu?

Unajua namna gani tunawakandamiza hawa wapinzani.

Siasa za hovyo zimezaa wakimbizi wa kisiasa.

Tuyaepuke haya.
Acheni upuuzi nyie, kwa hiyo mtu akiwa mpinzani anakuwa malaika hafanyi makosa, msitumie kivuli cha upinzani kuficha madhambi yenu, acheni mahakama ifanye kazi yake Kama ilivyofanya kwa Sabaya.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Sura ya MAHAKAMA TANZANIA tayari inaonekana Wanafanya Kazi zao kwa MAAGIZO ya Muhimili mwingine na Wanaheshimu na Kutii MATAKWA ya WALIOWATEUA
 
Acheni upuuzi nyie, kwa hiyo mtu akiwa mpinzani anakuwa malaika hafanyi makosa, msitumie kivuli cha upinzani kuficha madhambi yenu, acheni mahakama ifanye kazi yake Kama ilivyofanya kwa Sabaya.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Unakumbuka kuna mbunge wa ccm alikamatwa na mitutu ya bunduki kule shinyanga???
Unakumbuka case ya ubakaji ya kapiga?
Unakumbuka case ya rushwa ya kugoma?
Kagoda
Escrow
Twin towers
Ndege
 
Hapana, siyo ujinga kujadili.
Hakuna aliyejuu ya sheria kamwe, lakini Jaji anaposoma hukumu bila kurelate vifungu vya sheria ni wazi kuna mbinumbinu hapo.

Kumbuka kwamba Jaji Siyani alisema yale yalikuwa maoni yake binafsi. sasa kama hukumu inayopaswa kuwa ya haki ipo based na maoni binafsi inawezekana kushawishi fikra kwamba haikuwa hukumu ya haki.
 
So what!!! Kwa hiyo unakubali kuwa Mbowe ni gaidi lakini unataka apate favour Kama waliyopata hao uliowataja au?!!

Acheni mahakama ifanye kazi yake, nyie siyo wanasheria, ni kosa kujadili kesi iliyo mahakamani, waachieni wanasheria wenu 9 wapambane huko mahakamani.

USA walioleta sheria ya ugaid wenyewe hajawahi kuhukumu mtu kwa ugaidi kutukana na ugumu wake kwenye ushahidi.
Itakuwa wewe mtanzania na mapolisi wako wa div 4 wasiojuwa hata Tafsiri yenyewe tu ya gaidi?
Wapo wapi wale wa UAMSHO?
Yupo wapi ponda?
Rwakatare
 
hebu tulia basi wakati unaandika.
soma hoja, ielewe kisha andika yako.

unachokifanya hapa ni kudemka na umepanic
 
USA walioleta sheria ya ugaid wenyewe hajawahi kuhukumu mtu kwa ugaidi kutukana na ugumu wake kwenye ushahidi.
Itakuwa wewe mtanzania na mapolisi wako wa div 4 wasiojuwa hata Tafsiri yenyewe tu ya gaidi?
Wapo wapi wale wa UAMSHO?
Yupo wapi ponda?
Rwakatare
Kwani tatizo lenu ni nini nyie Chadema, mmeweka wanasheria 9 kwa ajili ya kesi ya Mbowe, so tulieni wanasheria wenu wapambanie kesi yenu.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kuapishwa kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania, Mhe. Jaji Kiongozi Mustapha Siyani ametoa mwelekeo wake kupitia Hukumu yake ya Kwanza kama Jaji Kiongozi.

Nimesema mwelekeo nikimaanisha aina ya legacy yake. Kwa mtazamo wangu ninaona mwelekeo au mguu aliouanza Jaji Kiongozi katika hukumu yake ya Kwanza haukuonesha uongozi wa Kimahakama kuonesha haki inatendeka.

Mimi siyo Shabiki wa Mbowe wala CHADEMA hata kidogo. Ukipitia posts zangu za nyuma unaweza kuthibitisha hili. Lakini siwezi kuwa shabiki wa udhalimu, dhulma na ubaguzi mkubwa unaofanywa na CCM yangu kwa Watanzania hususani Wapinzani.

Hukumu hii ya kwanza kama Jaji Kiongozi iwaalike wanazuoni wa Sheria kuitazama sura ya Mahakama ya Tanzania iwapo inasimama kama hekalu la haki au hekalu la kuwapa kinga ya kisheria wezi, wauaji, wanyang'anyi na nasaba hizo.

Tujipe fursa sasa ya kuanza kuokota ama kukusanya vipande vinavyoweza kupelekea upatikanaji wa Katiba Mpya yenye kutoa haki, kuwajibisha na kuimarisha misingi yetu kama Taifa moja bila kubaguana.

Jaji Kiongozi ameonesha mwelekeo wake kama msimamizi mkuu wa judicial caucus yenye dhamana kubwa kwa Taifa hili.

Hapa sijamtaja Jaji Mkuu ambaye bado anaamini Jamhuri ina makamu wawili wa RaisView attachment 1981914View attachment 1981915
Naona umetoa lawama tu wewe ulitaka hukumu iwe vipi na kwa mtazamo wako wapi umeona amekosea?
 
In short mijadala ya huku JF kuhusu kesi ya Mbowe haina msaada wowote, acheni mahakama na wanasheria wenu wafanye kazi yao.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Hapa hatujadili mwenendo wa kesi bali tunaijadili HUKUMU ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Angalia sana usichanganye mlenda kwenye pilau.

Mahakama inaheshimiwa na inaheshimika sana hata kama Executives hawaiheshimu na kuipa uhuru wake.

take your stand fellow
 
Naona umetoa lawama tu wewe ulitaka hukumu iwe vipi na kwa mtazamo wako wapi umeona amekosea?
Ukisoma hoja yangu kwa umakini, nimejiweka mbali na hicho unachosimamia yaani LAWAMA.

Haki kutendeka inajumuisha pia eneo ama hali ya kuonesha haki inatendeka. Ushawishi huo haupo kwa mwingine bali anayetoa hukumu.

Hukumu hii imeshazalisha zama mpya za kutoheshimu utu na haki za binadamu kwa sababu polisi ama watu wa dola wanaofanya hivyo wanapewa kinga na mahakama.

tunahitaji sana kuelewa hizi moves kuliko kujitia upofu wa mahaba ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom