Hukumu Kesi ya Kikatiba ya Jamii Media: Mahakama yakiri Sheria Makosa ya Mitandao inahitaji kanuni

15 Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
16 Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
 
23 Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema.
24 Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia.
 
Yapo mengine wanayafanya kinyume kabisa na sheria. Mfano ni kusudio la kukata rufaa dhidi ya dhamana kwenye kesi ya lema lilielezwa kwa mdomo tu. Sheria inataka wawasilishe kwa utaratibu na hakimu angeendelea kutolea uamuzi baada ya kupokea "submissions" za upande wa mashitaka na utetezi...


Okay, kwa nini hakimu alikubali oral submission ya Jamhuri kama sheria inakataa?

Hilo ni kosa la Jamhuri au la mahakama?
 
Kama ni kweli mahakama kuu imeamua kuwa polisi hawana automatic right ya kupata taarifa toka JF au media nyingine yoyote mpaka wapitie court, basi ni ushindi mkubwa ktk kuzuia udikteta nchini. Naomba hata court of appeal wa affirm hiyo point
 
Mahakama inawaonya AG na DPP kwa misingi ipi?

Wao mahakama ndio wame rubber stamp kila anachotaka DPP. Kosa sio la DPP.

Kwa sababu, labda ngoja nitoe elimu kwa umma hapa, ever so briefly.

Mfumo wa sheria wa Tanzania ni adversarial judicial system. Pande mbili zinazokutana mahakamani zinapingana kwa nguvu zote, hakuna kuchekeana wala huruma, ubaya ubaya!

DPP na state attorneys wake wamekula kiapo cha kitaaluma na cha kiajira cha kutetea na kupigania interest za Jamhuri mbele ya mahakama kwa nguvu zao zote, akili zao zote, jasho, mbinu, hila, sarakasi, technicalities, na kila aina na namna ya figisu inayokubalika kisheria kutafuta ushindi. Ukishindwa jukumu hilo una makosa yanayoitwa incompetent representation of counsel.

Sasa ni jukumu la Mahakama kukwamisha hila ya wakili wa Jamhuri ambayo haikubaliki kisheria.

Kwenye kesi ya Lema, kwa mfano, hakimu alitia rubber stamp, alikubali taarifa ya mdomo ya Jamhuri ya kunuia kukata rufaa ya dhamana. Akamsweka Lema ndani wakisubiri shauri. Siku ya shauri la dhamana Jamhuri ikaondoa kesi asubuhi! Lema kashakaa ndani miezi! Jaji akatoa machozi!

Such a brilliant, shrewd, legal maneuvre by the state attorney which takes advantage of the inept magistrate handling the case along with the gaping loopholes in the criminal procedure laws.

Jaji unalalamika nini? Kwani DPP ndio alimsweka Lema ndani? Jaji alitakiwa kum lambast hakimu aliyemkubalia DPP kila anachoomba.

Halafu sasa kibaya zaidi, Freeman Mbowe, leader of the opposition akaenda mbele ya microphone kuitangazia dunia kwamba upinzani tulikuwa tunadhani kimakosa kwamba mahakama is compromised.

Badala ya kusema karipio la jaji limedhihirisha kwamba Mahakama was compromised Mbowe essentially anasema tulikuwa tunakosea kuilaumu mahakama. Amerudisha nyuma miaka na miaka ya juhudi na vilio vya upinzani kwamba the judiciary is a rubber stamp of the government.
Nadhani hii comment yako ungeifungulia thread kabisa nadhani wangepatikana watu ambao wangejibu na kuzua mjadala ambao ungeleta manufaa!
Nilichojifunza ni kuwa DPP ana mamlaka fulani mahakamani so hakuna common ground kati ya mawakili wa serikali na wa watu binafsi!Nadeclare sina taaluma ya sheria ila kwa mtazamo nimeona hivyo!Ndio maana nikashangaa jamhuri kuwaombea dhamana watuhumiwa wa dawa za kulevya akina TID,wakati ni hao hao serikali iliyowashitaki!Fungua uzi tafadhali tuulize haya ili wengine tupate elimu kidogo!
 
Hongereni sana Wakuu kwa ushindi huu mkubwa sana dhidi ya Serikali katika uhuru wa kupashana habari nchini.

kui

Wakuu,

View attachment 473062

Nimeona kupitia Twitter ya JamiiForums wakitoa taarifa kuwa kesho ndiyo siku ya hukumu ya Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Jamii Media dhidi ya Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa matumizi mabaya ya Sheria ya Makosa ya Mtandao.







Kwa maana hiyo, tarehe hii itaingia kwenye historia ambapo aidha watumiaji wa mitandao watarejeshewa uhuru wao na Mhimili wa Mahakama au ndiyo utazikwa rasmi na hatma ya watumiaji wa mitandao kubaki katika hali ya mashaka.

=======
UPDATES:

Hukumu ya Kesi ya Sheria ya Makosa ya Mtandao iliyofunguliwa na Jamii Media yashindikana kusomwa.

Sababu za msingi kushindikana kusomwa kwa hukumu hiyo hazijaelezwa.

Aidha sababu nyingine ya kushindikana kusomwa kwa Hukumu hiyo ni kutokana na mmoja wa Majaji waliokuwa wakisimamia kesi hiyo Jaji Koroso amehamishwa na kupelekwa katika Mahakama mpya ya Mafisadi.

Hukumu imepangiwa tarehe rasmi ya kusomwa kuwa MACHI 8, 2017 asubuhi saa 4.

========
HUKUMU:





Mahakama Kuu imesema Vifungu vya Sheria vilivyopingwa na Jamii Media, vipo sawa kikatiba ila imekiri sheria kutumiwa bila kanuni ni changamoto. Pamoja na kusema vifungu vipo sawa, imezitupilia mbali hoja zote za Serikali
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Hoja za Upande wa Jamii Media zilikuwa ni:

1) Sheria inaendeshwa bila kanuni, hivyo inavunja haki za binadamu

2) Vifungu vya 32 na 38 vinatumika visivyo; hivyo vitangazwe kuwa kinyume cha Katiba

⁠⁠⁠⁠Mahakama Kuu yatoa mwongozo wa kesi yoyote chini ya kifungu cha 32 ya Sheria ya Mitandao, polisi lazima waende mahakamani kuomba mahakama ishurutishe mtoa huduma kutoa taarifa.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mwanasheria Ben Ishabakaki kaeleza kuwa tafsiri ya kauli hii ya Mahakama Kuu kisheria ina maana kesi za jinai zilizofunguliwa dhidi ya [HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG] hazijafuata sheria kwa sababu polisi walitakiwa waende kwanza mahakamani badala la kukamata na kufungua mashtaka moja kwa moja.

Wamesema kifungu kipo kinachowataka Polisi kwenda mahakamani endapo watanyimwa data kabla ya hatua wanazochukua dhidi ya Jamii Media kama mtoa huduma.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mahakama Kuu yamwonya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutohoji Mamlaka ya Mahakama katika kutafsiri sheria.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mahakama yasisitiza kuwa sheria zilizopo zinahitaji kuzingatia maendeleo ya teknolojia na Haki ya Faragha

Mahakama imeongeza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na Kanuni za kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Makosa ya Mitandao
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠"Ni muhimu kujua nani wako nyuma ya msukumo huu wa kupata data za watumiaji. Hatupambani na Dola" - Maxence Melo
 
  • Thanks
Reactions: kui
Baada ya kuona taarifa kupitia ITV usiku huu ndio nimejua kuwa hii hukumu imetoka leo.Niliona hii thread mapema leo ila nikaona ya mwezi February hivyo sikuhangaika kuisoma kumbe ina update.

Hata hivyo, nawapongeza sana Jamii Media kwa huu ushindi ambao ni wetu sote.
 
Hongera Jaji Winnie Koroso kw kutetea wananchi kupitia Jamii Media hongereni sana Justice has prevailed
 
Nimefarijika sana leo. Siamini kama ni Tanzania hukumu hii yaweza kutoka. Ila tutegemee sarakasi nyingi sana katika kutetea uhuru wa habari. Vita ndiyo imeanza. Hatari ni kwa wale wasiojua sheria na wananyanyasika kila kukicha
 
Mungu akulinde na kukupa hekima zaidi,umetuwezesha watanzania wengi kujifunza mengi hapa JamiiForums hakika maxence mello shujaa wetu
 
Back
Top Bottom