Hukumu Kesi ya Kikatiba ya Jamii Media: Mahakama yakiri Sheria Makosa ya Mitandao inahitaji kanuni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,464
Wakuu,

IMG_3500.JPG


Nimeona kupitia Twitter ya JamiiForums wakitoa taarifa kuwa kesho ndiyo siku ya hukumu ya Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Jamii Media dhidi ya Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa matumizi mabaya ya Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Sababu za kufunguliwa kesi ziliandikwa hapa: Jamii Media yafungua Kesi ya Kikatiba kupinga Vifungu vya Sheria ya Makosa ya Mtandao







F6A70B74-205E-489F-894F-710433E44134.jpeg

4B09060B-3BEF-41A0-AA0E-765510509807.jpeg


Kwa maana hiyo, tarehe hii itaingia kwenye historia ambapo aidha watumiaji wa mitandao watarejeshewa uhuru wao na Mhimili wa Mahakama au ndiyo utazikwa rasmi na hatma ya watumiaji wa mitandao kubaki katika hali ya mashaka.

=======
UPDATES:

Hukumu ya Kesi ya Sheria ya Makosa ya Mtandao iliyofunguliwa na Jamii Media yashindikana kusomwa.

Sababu za msingi kushindikana kusomwa kwa hukumu hiyo hazijaelezwa.

Aidha sababu nyingine ya kushindikana kusomwa kwa Hukumu hiyo ni kutokana na mmoja wa Majaji waliokuwa wakisimamia kesi hiyo Jaji Koroso amehamishwa na kupelekwa katika Mahakama mpya ya Mafisadi.

Hukumu imepangiwa tarehe rasmi ya kusomwa kuwa MACHI 8, 2017 asubuhi saa 4.

========
HUKUMU:





3BC100C5-83BE-4233-8E2F-19CFAB493051.jpeg


Mahakama Kuu imesema Vifungu vya Sheria vilivyopingwa na Jamii Media, vipo sawa kikatiba ila imekiri sheria kutumiwa bila kanuni ni changamoto. Pamoja na kusema vifungu vipo sawa, imezitupilia mbali hoja zote za Serikali
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Hoja za Upande wa Jamii Media zilikuwa ni:

1) Sheria inaendeshwa bila kanuni, hivyo inavunja haki za binadamu

2) Vifungu vya 32 na 38 vinatumika visivyo; hivyo vitangazwe kuwa kinyume cha Katiba

⁠⁠⁠⁠Mahakama Kuu imetoa mwongozo kuwa kesi chini ya kifungu cha 32 ya Sheria ya Mitandao, Polisi walitakiwa waende mahakamani endapo Mtoa Huduma(kama JamiiForums) amekataa kutoa taarifa ili itolewe "court order".
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mwanasheria Ben Ishabakaki kaeleza kuwa kwa tafsiri ya kauli hii ya Mahakama Kuu kisheria, ina maana kesi za jinai zilizofunguliwa dhidi ya [HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG] hazijafuata sheria kwa sababu polisi walitakiwa waende kwanza mahakamani badala la kukamata na kufungua mashtaka moja kwa moja.

Wamesema kifungu kipo kinachowataka Polisi kwenda mahakamani endapo watanyimwa data kabla ya hatua wanazochukua dhidi ya Jamii Media kama mtoa huduma.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mahakama Kuu imeionya Jamhuri kuacha kuhoji Mamlaka ya Mahakama katika kutafsiri sheria.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mahakama imesisitiza kuwa sheria zilizopo zinahitaji kuzingatia maendeleo ya teknolojia na Haki ya Faragha(privacy).

Mahakama imeongeza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na Kanuni za kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Makosa ya Mitandao.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠"Ni muhimu wananchi kujua nani wako nyuma ya msukumo huu wa kupata data za watumiaji. Hatupambani na Dola" - Maxence Melo
 
Hii ni hukumu yenye kugusa mustakbali wa nchi, inahusu mustakbali wa watu katika dhima na juhudi za kujenga taifa la watu huru, demokrasia ya kweli lililo well informed.

Hii hukumu ni muhimu sana kwetu wananchi kwa sababu century hii ni century ya digital information, hukumu hii tukishindwa tu basi tutarudi nyuma mno ktk stone age
 
Hakuna siku hata moja giza liliwahi kuishinda nuru....

Kama watu wanahitaji kujifunza hata kwenye historia wanaweza kuwa binadamu bora kabisa kwenye maisha yao na maisha ya wengine na kamwe hawataweza kusahaulika....

Siyo jambo dogo hata mara moja unakuta mtu alishaondoka duniani miaka mingi lakini anashindwa kusahaulika na binadamu wenzake alioishi nao hapa duniani kwasababu yoyote ile,pia siyo jambo dogo kwa binadamu kuweza kujulikana na wanadamu wengi duniani....

Haya maisha siyo jambo la maana kiasi hicho hadi uanze kusababisha mazingira magumu kwa binadamu wengine kuishi hapa duniani.Ishi maisha yako kwa nidhamu maana hujawahi hata siku moja na hata hukuwaza kupewa maisha haya unayoishi leo,umejikuta tu unaishi....

Tuishi maisha ya amani sote hapa duniani na yenye upendo wa hali ya juu maana iko siko siku tutamanani leo hii ijirudie lakini haitawezekana.....
 
Uhuru kamili uko njiani ni suala muda msifadhaike mioyoni mwenu mtakapo kuwa kwenye mapambano na nguvu zangu zitakuwa juu yenu.

Nitawapa ujasiri nguvu na mbinu ya kumshinda yule muovu. Nitawafuta machozi mtapata furaha na kuukumbatia furaha ile ya kwanza. Ndani ya ardhi yangu mtaneemeka kwa makuu yale nitakayowatendea. Nasema tena nitawafuta machozi.
 
Mungu ibariki JF, kama VIPI taarifa zote Kule mahakamani ziungue moto
 
Tanzania ya viwanda kesho tusitishe shughuli za viwanda muda wa hukumu au tuendelee na Tanzania ya viwanda??
 
Daaah patamu hapo..
Huku makonda na siro kikaangoni..
Na huku jf na polisi..
Hii haina uchama kwa kweli kwani watumiaji wa jf ni wakutoka vyama vyote
 
Back
Top Bottom