Huku Russia vs Ukraine, kule Israel vs Palestina

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Ehe bwana ehe, mimi kama Muhaya original kabisa, na thubutu kusema Dunia mpaka sasa bado inaupiga mwingi kabisa.

Mambo kama haya tuliyazoea kipindi kile cha Ofisa Bin Laden Mwamba kabisa aliyeitikisa Dunia na Marekani kwa mapigo yake na akili yake ya kipekee ambae kwa karne hii hakuna mtu aliyethubutu kuitikisa Dunia kama Bin Laden, kupelekea kwamba mpaka jina lake tu ukilisikia unaona limekaa kibabe.

Kiukweli Dunia haijawai kupoa na haitokuja kukaa na kupoa hata siku moja. Kama uliwahi kufikiri Dunia itakuja kuacha mapiganao umejidanganya sana. Mambo haya ya vita yalianza tangu enzi na enzi hata kabla ya wakoloni ambapo tuliweza kuona falme, Koo, kabila, na familia mbalimbali zikipigana vita zidi ya koo, kabila, familia, falme nyingine wakinyanganyana ardhi, mifugo, na kadharika kitu kilichopelekea pia koo na makabila kuwa yana hama hama kutafuta sehemu salama.

Vita vya kwanza na vya pili vya Dunia ni marudio tu ya matukio ya vita ambayo kidogo yalihusisha maneno makubwa ya Dunia, na idadi kubwa ya wapiganaji kuwahi kutokea.

Baada ya vita ya kwanza na ya pili Dunia,nchi zilikaa na kukataza matukio kama hayo ya vita vya Dunia kujirudia ili kuepusha maafa.

Lakini hata hivyo bado Nchi mbalimbali zimeendelea kufuana na kutishiana mabavu, kila nchi ikionesha umwamba dhidi ya mwenzake.

Hivi karibuni tumetoka kushuhudia vita kati ya Russia na Ukrein ambapo mpaka sasa vita inaendelea na tumeshuhudia watu na wanajeshi wengi wakifariki huku kila vikao vikifanyika kutoa suluhu dhidi ya vita hivyo. Hata hivyo vikao hivyo ni kama vile watu walienda kukaa kupokea posho tu na kunywa Alikasusu na kupiga kura ambazo hazina madhara. Maana vikao vimefanyika huko Umoja wa Mataifa ila hakuna suluhu iliyopatikana huku Ukrein akiendelea kuchezea Kwenzi za kutosha kutoka Ukrein. Huku Marekani na nchi za ulaya waakizidi kuchochea vita kwa kugawa mawe ili Ukrein amponde nayo Russia, Russia nae anaendelea kumkoa kwenzi Ukrein.

Hatujakaa sawa, huku vugu vugu la Israel na Palestina likiendelea chini chini, naona dogo naye Palestina kachoka kuchezea Mitama kutoka kwa pacha mwenzake Israel. Palestina kaamua kurudisha mapigo kwa kaka yake, na sasa hivi huko Israel ni kivumbi, watu wamejifungua ndani. Kundi la Hamas la wapalestina wameingia mpaka kwenye miji ya Palestina na kumimina Njugu kwa kila muisrael anayekatiza kwenye anga zao. Jeshi la Israel limetoa hali ya dharua na kila mtu kujifungia ndani huku ving'ora vya tahadhari vikilia kila chocho, na makombora ya wapalestina yakinwagika kama mvua huko Israel.

MY TAKE: Husijekutegemea vita vitaisha hata kidogo hapa Duniani. Hata Tanzania ilitaka kufuana na Malawi kisa mpaka wa ziwa Nyasa. Uganda iliwahi kupokea kichapo kitakatifu dhidi ya Tanzania baada ya Dada Idd kutaka kuchukua ardhi ya Tanzania huko mkoani Kagera. Uenda kesho Kenya nayo ikaleta mdomo tukaifua. Tuendelee kuomba mungu hatuepushe na Vita, vita isikie kwa jirani, raha ya vita uisikie kwa jirani. Ikikutokea wewe ni shida tupu. Tupendaneni tuwe wamoja.
 
Back
Top Bottom