HUKU JK akiuza sura, Kibaki kujenga reli mpya Nairobi na bandari Lamu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HUKU JK akiuza sura, Kibaki kujenga reli mpya Nairobi na bandari Lamu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, Apr 16, 2009.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Apr 16, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  Kenya wamezindua mradi mkubwa wa ujenzi wa mtandao wa reli ya umeme kuunganisha nairobi na vitongoji vya karibu na uwanja wa ndege ,mradi huu unakadiriwa kukamilika mwaka 2011.

  Sambamba na hilo wametumia pesa walizopata kwa kuuza hoteli yao ya kifahari ya GRAND REGENY kwa serikali ya Libya kuanzishia ujenzi wa bandari mpya ya LAMU,hii inatarajiwa kuwa kubwa kuliko ya mombasa na tarari pesa za kumalizia mradi huu zimepatikana,MELI YA KWANZA ITATIA NANGA LAMU MWAAKA 2012.

  Mradi wa bandari ya lamu unalenga soko la sudani kusini na sehemu ya kusini ya ethiopia...na pia reli zitajngwa kwenda huko sambamba.

  Tanzania chini ya jk wameshindwa kuendeleza bandari ya kusini ya mtwara kulenga soko kubwa la kusini na ile ya TANGA kulenda soko la uganda na kaskazini ya tanzania kupitia musoma....pia pesa walizopata kwenye EPA au wanazodai kupata wameshindwa kuzitumia kwenye miradi inayopimika ...badala yake wanadai kuzitumia kwenye mradi wa kufikirika wa mbolea ambao wala hatutaweza kuupima wanananchi wa kawaida....ingekuwa busara kama wangejengea vitu vya kuonekana kama wenzao walivyofanya....
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Huyo Kibaki miaka mitano ya kwanza alifanya nini?..
  Yawezekana kabisa haya yote yametokana na serikali ya mseto.. Sisi je tumejiandaa vipi?
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  wewe mbona una wasi wasi?
  sisi tuna mradi wa reli kwenda RWANDA itajengwa karibuni...

  tuna mradi wa kujenga INTERNATIONAL airport kule BAGAMOYO itajengwa karibuni

  tuna mradi wa refinery mpya itajengwa KARIBUNI

  Tuna mradi wa bomba la mafuta toka TANGA-RWANDA-BURUNDI..itajengwa karibuni inshaalah

  Tuna mradi wa kuvuna MVUA toka THAILAND inshaalah nayo itafanikiwa tuu

  Tuna mradi wa MJI MPYA kule mbele sijui kunaitwaje..wasomali tayari wako site

  Tuna mradi wa kujenga bandari BRAND NEW kule Bagamoyo itafanikiwa tuu ni uhai tuu mkulu

  mwisho zaidi tuna mradi wa kuziba ule mtaro mbele ya HAIDERY PLAZA ambao unatoa harufu na maji machafu tangu mwaka jana ...isipokuwa taarifa ni kuwa meya wa ILALA na KIMBISA bado wanafanya feasibility study kujua lile shimo litazibwaje

  at least for once you should be grateful kuwa nia TUNAYO,UWEZO TUNAO isipokuwa hatujajaaliwa tuu
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi mradi wa mvua ya Thailand bado umo vitabuni? Mimi nilidhani ulienda na Lowassa.
   
 5. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,809
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  The Keeping up With Joneses Syndrome imeshaanza.
   
 6. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimehamasika! Watanzania labda wauze mbuzi zao wajenge reli. Daraja la kigamboni tumeweka tenda ya wafanyabiashara binafsi! Kaka JK iga basi haya mazuri mazuri!
   
 7. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kijana umechambua sana, lakini mbona mahospital makubwa mapya hayajengwi na ya kisasa? Au ndo hizo za zamani zinatosha mfano Bugando ,muhimbili na kcmc tu! Watu wameongezeka mabadiliko yawepo.
   
 8. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Miradi ambayo inaweza kupimwa utekelezaji wake ama kuhojiwa na wananchi sio jambo la kipaumbele kwa viongozi wa Tanzania, wao wanachotaka ni miradi ya majukwaani na fedha zinzazotengwa zihamishiwe kwenye mambo yao binafsi, ukiuliza sana utaambiwa hilo/hayo hayamo kwenye ilani ya chama tawala!. "MUNGU IBARIKI TANGANYIKA"
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  duh.. tuna miradi mingi!
   
 10. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mkuuu...

  kuna miradi ya kugawia watu fedha yaani MABILIONI YA JK (KIBAKI AIGE AFE!!!)

  Utaratibu wetu ni wa pekee na wa kupigiwa mfano kwa wasiopenda kusonga mbele...
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Pia mmesahau mradi wa kupanda na kuvuna wa DECI!!!!!!!!!!!
   
 12. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  na ule wa JK kuzurura kila leo Je?
   
 13. A

  Adili JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 1,999
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Mbili za hizo tatu zina wenyewe. Bugando ni msaada wa Roma kwa Marehemu Cardinal Rugambwa wakati KCMC ni nguvu ya waLuteri. Bila ya hawa wawili tusingekuwa na hospitali ya rufaa yenye jina nchini.
   
 14. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Aacha bwana eeh, mimi nilijua tumejengewa na serikali yetu, kumbe loh ,kweli tuna matatizo sana ndio maana hata viongozi wanatibiwa nje, napata shaka pia na hawa madactari wetu na vyuo wanavyosomea.
   
 15. B

  Bobby JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Phillemon ahsante sana tunashukuru ila kuna kitu unaoneaka unakiovalUku, sisi miradi yetu ni safari nje kwa sana. Mpaka sasa tumevunja record na tutaendelea kuivunja mpaka ikome si unaona saa hizi tuko Saudia kwa raha zetu?!?

  The game unapoint sana lazima uwe genius kwa kweli umenivunja mbavu. Ila miradi ya harufu ni mingi, mingine hukuitaja, kuna ubungo karibu na urafiki na maeneo ya magomeni/jangwani. Pia kuna miradi ya mifereji ya maji machafu kama maeneo ya May Fair na shoppers plaza. Sina hakika kama Kimbisa na mwenzie watakuwa wamemaliza feasibility study kama Yesu hajarudi.

  ILA TANZANIA NAKUPENDA LAKINI PIA NAKUONEA HURUMA SANA KWA KUKOSA UONGOZI TAIFANI MPAKA MTAANI KAMA SIO HADI NGAZI YA FAMILIA.
   
 16. N

  Nchimbi J Senior Member

  #16
  Apr 16, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa naona kila mtu anajaribu kuomyesha namna jk na serikali yetu tukufu inavyoshindwa kutekeleza majukumu yake jambo ambalo si la kweli ata kidogo.Utendaji wa serikali ya JK hauwezi kupimwa kwa vile Kibaki kajenga reli basi na sisi tujenge reli....ni ujinga kwa kweli.Kwa faida ya wasomaji wa hapa pengine niseme machache sana yaliofanywa na serikali ya Jk ili watu wote tuweze kuyapima.....kwanza ni ujenzi na upanuzi wa chuo kikuu cha dodoma....wanafunzi elfu alobaini wataingia hapo.....pili ni walter sector program inayotekelezwa kwa sasa ambapo kila mji utanufaika kwa maji safi kwa kiwango cha asilimia 94....kwa sasa tayari kigoma wameenza utekelezaji wa kuvuta maji toka mto malagalasina kusambazwa kigoma...wakazi wa maeeneo ya dar wanaona ujenzi wa mabomba mapya ya maji hususani maeneo ya tabata nimeshuhudia mwenyewe...ujenzi wa vyumba vya madarasa tayari kwawanafunzi wapya kuingia umefanyika nchi nzima...nani aliwapofusha mpaka yote haya hamuyaoni?
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145

  --- Mradi wa kupanua New Bagamoyo Road bado uko vitabuni tangu early 2000s, feasibility study bado inafanyika, hata jana watu wenye vijizibao vya kung'ara walikuwepo mabarabarani wakihoji wananchi. Utamalizika KARIBUNI.

  --- Dar Rapid Transport (DART) umeandikwa weee tangu ukiwa chini ya kina Sykes, mwongo mmoja sasa unapita. Utamalizika KARIBUNI.

  --- Mradi wa vitambulisho UTAMALIZIKA 2010 baada ya uchaguzi kufanyika, utakuwa umetekelezeka kwa jimbo moja tu la Dar. Kisha feasibility study nyingine itaibuka kujua kama tuendelee nao au tuutose na ku-revert to alternative paper based ID, hivyo kuweza kumalizika miaka michache baada ya hapo KARIBUNI.

  --- Dar Ring Road utamalizika KARIBUNI.

  --- Daraja la Kigamboni (hatimaye litamalizika karibuni)

  --- Kesi zote za wahujumu uchumi zitamalizika KARIBUNI!

  Inasikitisha. Iwapo nchi ikiwa katika amani kama ilivyo yetu inashindwa kuwa na maendeleo ya chapchap; M.Mungu atuepushe nayo - itakuwaje pale machafuko yatakapotokea? Hamna namna nyingine ya kuelezea hii situation tuliyo nayo sisi. Siasa zetu under CCM zina incubate machafuko ya kisiasa, kwani paka huyu anayegandamizwa kwenye kona kila kukicha kwa kutumia kivuli cha utulivu na amani ipo siku atageuka chui. Dua zetu zinatofautiana, wengine wanaomba isitokee kabisa, wengine wanaomba itokee KARIBUNI.
   
 18. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #18
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hii ndo tz,"hata baba akimpeleka mwanae shule anataka ashukuriwe"
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yaguju ,feza ya kukwiba wataipata wapi wakianzisha hisia za kujenga mambo hayo ,ikiwa tuna reli ya kati miaka zaidi ya 90 ,tumeshindwa kuiendeleza reli ambayo ilitakiwa iwe ya kisasa kabisa kuvuna feza za wanyarwanda na Waburundi na kule Tazara ,yaani wezi hawa wanakwiba benki kuu halafu unawaletea mawazo mchovu ya kuwavunja moyo ,wacha watafune ,ndio maana wanakula chao hawali cha nchi nyengine ,endeleeni kukwiba shamba la babu wa Taifa kwani hawa wezi ukiwapima miaka yao ni wajukuu wa Nyerere tu ,so shamba la babu wa Taifa.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa ahadi tu, Kibaki hampati Kikwete hata chembe!..
  Pamoja na yote haya wakuu zangu hivi kweli sisi wananchi tunaoongozwa pia wazima au?..
   
Loading...