HUKU JK akiuza sura, Kibaki kujenga reli mpya Nairobi na bandari Lamu!

Game theory umenifurahisha sana kwa mnyumbulisho wako

infact, nia tunayo na uwezo tunao lakini tatizo kubwa ni hawa kizazi cha rushwa, naamini pindi kizazi hiki cha sasa kitakapokuwa kimeshika madaraka mambo yatabadilika. Dalili ya mvua ni mawingu.hawa jamaa wanaendekeza sana ufisadi wakithamini familia zao zaidi kuliko jamii yao, wanashndwa kuelewa hali hii haitowasaidia hata wao pia siku za usoni mambo yatakapoharibika kama nchi zingine, angalia somalia hali ilivyo mbaya.
 
Kwa ahadi tu, Kibaki hampati Kikwete hata chembe!..
Pamoja na yote haya wakuu zangu hivi kweli sisi wananchi tunaoongozwa pia wazima au?..

Hatuko wazima Kaka Bob. Na hii inatokana na kujikuta tuna ishi katika system ya watu wasiopenda mabadiliko. Kama tupo hivyo kibailojia, basi hili halitabadilika kamwe. Lakini kama kutokuwa na uzima huu inatokana na shinikizo fulani hivi externally, hakika kuna siku tunaoongozwa tutacharuka na kuonesha uzima wetu katika kuhitaji ahadi zinazotekelezeka.
 
Hatuna tatizo lolote la kibailojia hata kidogo. Sisi tu wazima kabisa, kabisa kwa kila maana ya neno. Tunauwezo wa kufikiri, kutenda na kufanya mabadiliko. Tatizo tulilonalo tunajifananisha na walioendelea - tunataka utashi wao na maendeleo yao. Huko ndiko tunakotafuta maendeleo ya kweli. Tunajidharau, tunajisahau, tunapoteza kumbukumbu kwamba ni utanzania nia wetu, weusi wetu ni msingi wa mabadiliko. Uzima wetu unaanza na utambuzi wetu kwamba sisi ni watanzania.
 
Hapa naona kila mtu anajaribu kuomyesha namna jk na serikali yetu tukufu inavyoshindwa kutekeleza majukumu yake jambo ambalo si la kweli ata kidogo.Utendaji wa serikali ya JK hauwezi kupimwa kwa vile Kibaki kajenga reli basi na sisi tujenge reli....ni ujinga kwa kweli.Kwa faida ya wasomaji wa hapa pengine niseme machache sana yaliofanywa na serikali ya Jk ili watu wote tuweze kuyapima.....kwanza ni ujenzi na upanuzi wa chuo kikuu cha dodoma....wanafunzi elfu alobaini wataingia hapo.....pili ni walter sector program inayotekelezwa kwa sasa ambapo kila mji utanufaika kwa maji safi kwa kiwango cha asilimia 94....kwa sasa tayari kigoma wameenza utekelezaji wa kuvuta maji toka mto malagalasina kusambazwa kigoma...wakazi wa maeeneo ya dar wanaona ujenzi wa mabomba mapya ya maji hususani maeneo ya tabata nimeshuhudia mwenyewe...ujenzi wa vyumba vya madarasa tayari kwawanafunzi wapya kuingia umefanyika nchi nzima...nani aliwapofusha mpaka yote haya hamuyaoni?

Kaka! kama kila mtu anaongea kwamba hamna maendeleo inamaanisha hamna maendeleo. Kama hayo maendeleo yote watu hawayooni lazima ujiulize tatizo likowapi? Haiwezekani watanzania wengi wapige makelele na ukali wa maisha halafu tuendelee kusema amefanya hiki na kile. Ni kweli amefanya, lakini yawezekana maslahi ya programu hizo hayajawagusa wengi.
 
...au pia ni mithili ya maslahi ya mtoto kunyonyeshwa. Je katika hili napo wanataka credit?
 
wewe mbona una wasi wasi?
sisi tuna mradi wa reli kwenda RWANDA itajengwa karibuni...

tuna mradi wa kujenga INTERNATIONAL airport kule BAGAMOYO itajengwa karibuni

tuna mradi wa refinery mpya itajengwa KARIBUNI

Tuna mradi wa bomba la mafuta toka TANGA-RWANDA-BURUNDI..itajengwa karibuni inshaalah

Tuna mradi wa kuvuna MVUA toka THAILAND inshaalah nayo itafanikiwa tuu

Tuna mradi wa MJI MPYA kule mbele sijui kunaitwaje..wasomali tayari wako site

Tuna mradi wa kujenga bandari BRAND NEW kule Bagamoyo itafanikiwa tuu ni uhai tuu mkulu

mwisho zaidi tuna mradi wa kuziba ule mtaro mbele ya HAIDERY PLAZA ambao unatoa harufu na maji machafu tangu mwaka jana ...isipokuwa taarifa ni kuwa meya wa ILALA na KIMBISA bado wanafanya feasibility study kujua lile shimo litazibwaje

at least for once you should be grateful kuwa nia TUNAYO,UWEZO TUNAO isipokuwa hatujajaaliwa tuu

Miradi yote hiyo 'itajengwa karibuni'

Unaamini unachosema mkuu? karibuni ni lini?
 
...au pia ni mithili ya maslahi ya mtoto kunyonyeshwa. Je katika hili napo wanataka credit?
Yap,
Unajua kama watanzania lazima tuwe na haki zetu za kuwa watanzania. Sisi kama watanzania haki yetu ni nini? Kuwa maskini? La hasha! Serikali inapaswa kutuwekea miundo mbini ili nguvu kazi zetu itumike. Kujenga barabara sio kazi ya wananchi ni ya serikali. Shule sio kazi ya wananchi ni serikali. Sasa serikali inapofanya wajibu wake isitafute kupewa pongezi, iniambie mimi - nimejenga barabara, shule, na miundo mbinu natako usome, ulipe kodi na uwe na afya kujenga taifa hili - uone kama sitatimiza wajibu wangu!
 
Petu Hapa,
Hatuna tatizo lolote la kibailojia hata kidogo. Sisi tu wazima kabisa, kabisa kwa kila maana ya neno. Tunauwezo wa kufikiri, kutenda na kufanya mabadiliko. Tatizo tulilonalo tunajifananisha na walioendelea - tunataka utashi wao na maendeleo yao. Huko ndiko tunakotafuta maendeleo ya kweli. Tunajidharau, tunajisahau, tunapoteza kumbukumbu kwamba ni utanzania nia wetu, weusi wetu ni msingi wa mabadiliko. Uzima wetu unaanza na utambuzi wetu kwamba sisi ni watanzania.
Mkuu wangu shukran sana kwa maelezo mazito lakini nadhani kinachofuata hapa ni kujiuliza sisi wenyewe - Maendeleo ni nini?.
Kusema kweli kila siku tunalonga kuhusiana na Uongozi wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa na leo hii Kikwete.. viongozi wote hawa wanasifa zao na kuna malalamiko mengi sana, na hakuna kati yao ambaye anadaiwa kuleta maendeleo na wananchi wengi isipokuwa sifa zetu ni kwa ALOPENDWA sana..Huko kupendwa hata siku moja sijafahamu kunatokana na sifa zipi..Hizo sifa zinahusiana vipi na maendeleo ya jamii yetu au nchi..
Jamani reli ya Uhuru inamong'onyoka, bandari hata kuitazama mara mbili inachusha na nadhani kuna maradhi makubwa yatokanayo na toxic. Uwanja wa ndege ati JKN International unafanana na Soko la Kariakoo kwa kila kitu hadi huduma zake. Majumba yetu ndio usiseme, Maji, Umeme, Hospital, kila kitu leo hii bila misaada ya NGos sijui nchi ingefanana vipi..Kisha tunafikiria kujenga Belt na mji mpya wa Dar ambayo hata mifereji haina.
Kodi zetu ni kubwa kupita nchi zote za kusini mwa Afrika, population yetu kubwa kuliko nchi nyingi kusini mwa sahara, mali asili ndio hata usigusie, tazama ramani tu utaona nchi nzuri!.. katikati yake ndio tumebarikiwa sisi..Lakini sisi ndio tumeshika mkia..Something is very wrong!.. sidhani kama ni swala la Kikwete kuna siri yetu sisi ambayo intakiwa wataalam wa biologia na saikologia kutufanyia uchunguzi..Haiwezekani tukawa wazima!
 
Mimi naomba mnisaidie kuelewa hili, hivi mjadala kama huu kwenye JF hausomwi na maafisa wa serikali yetu bongo na kama wanasoma kwa nini wasichukue baadhi ya challenges wakazifanyia kazi??

Kwa mfano tulishaongea humu JF kuwa kwa nini pesa ya vitambulisho isifanye kazi nyingine (kununua mtambo ya umeme) kwa sababu national IDs siyo dharula! Je serikali wanaonaje wazo hili??

Ofcourse, hatuwezi kufanya maamuzi yetu kwa kufuata eti kibaki kafanya hili lakini nacho jiuliza je viongozi wetu wana nini akilini mwao kushindwa kuona mazuri ya kusaidia wanananchi kwa baadaye??
 
Something is very wrong!.. sidhani kama ni swala la Kikwete kuna siri yetu sisi ambayo intakiwa wataalam wa biologia na saikologia kutufanyia uchunguzi..Haiwezekani tukawa wazima!

Matokeo ya ukandamizaji ni kujiona sisi kama watanzania tunatatizo kiakili ama kibiologia. Hizo ni siasa za kikandamizaji, ambazo tunaendelea kuzibeba mpaka tunawapa watoto wetu leo. Kwamba kuwa msomi ni kusema kimombo, kuwa mstaarabu ni kuwa kama mzungu, maendeleo ni umeme na barabara. Sisi kama watanzania, maendeleo yanaonekana pale tu ambapo tunaondoka katika utanzania wetu kufuata tamaduni za kigeni. Leo wakulima wetu hawajui kulima mpaka walime kilimo cha kisasa, taifa halijui kujiongoza mpaka tuige utawala wa nje, maendeleo ya wanachi hayaji mpaka wataalamu wa maendeleo wayapanga, hata misamihati ya lugha imekuwa mgeni. Mzee wa miaka 50 anaambiwa miaka yote aliyoishi haina maana na anahitaji kujifunza upya.

Hatuna matatizo ya kisokolojia, tatizo ni kwemba tumetupa taratibu zetu za kila siku za jamii na kuamua kuchukua zingine ambazo hatuzielewi. Leo hii mikopo inachukuliwa katika mfumo wa kibepari ambapo utamaduni wake ni lazima utunze faida ili ulipe deni. Watanzania bado hatujatenganisha maisha yetu na biashara - mama akiumwa, ada ikupungua tunakata humo humo kwenye mradi! Huku sio kutokujua utaratibu wa biashara, ila miradi kushidwa kutambua mahitaji halisi ya jamii.

Tatizo letu, sisi wasomi wa kati tunataka kuibadilisha jamii wakati jamii inaendelea na tamaduni zake. Mpaka tuelewe tamaduni zetu za kila siku ni zipi, na zinamuwezeshaji mwanakijiji anendelee kuwepo hata bila misaada ya serikali ndipo tutaendelea.
 
Petu Hapa,

.........katikati yake ndio tumebarikiwa sisi..Lakini sisi ndio tumeshika mkia..Something is very wrong!.. sidhani kama ni swala la Kikwete kuna siri yetu sisi ambayo intakiwa wataalam wa biologia na saikologia kutufanyia uchunguzi..Haiwezekani tukawa wazima!

Kikwete ni mmoja kati ya matatizo makubwa ya nchi hii kama hukujua. Ofcourse yeye ndiye anayeturithisha na blames zote lazima abebeshwe yeye. Kidogodogo kaka, RUSHWA ndio tatizo kubwa la nchi hii. Hizo raslimali na mali zoooote za nchi hii haziwezi kuendeshwa kwa rushwa zikaendelea. Mkuu wa nchi akiwa na ujasiri wa kukemea rushwa ndipo wa chini yake watafanya the same. Unafikiri wale matrafiki polisi wanaokudai rushwa ya sh 2000 barabarani, wanato wapi huo ujasiri? All the way up to mkuu wa polisi anapata mgawo. Obviously otherwise angesaidiana na wasaidizi wake kuwa-track. Na mkuu wa nchi hawezi kumwajibisha mkuu wa polisi kisa polisi kadai rushwa, maana anamtumiaga kumfichia marushwa yake kuanzia wizi wa kura mpaka raslimali. All other sectors likewise.

Tukianza na kudhibiti wizi, tutakusanya za kutosha kuwalipa hao polisi wapate mlo halali wa kutosha na ziada ya kutosha madawa, walimu na mashule, barabara, nk.

Narudia tena, tatizo la hii nchi ni Kikwete for now! Baada ya hapo ndio sisi. Uongozi wake tu ndio unaweza kutukomboa. Uongozi wa rais unaweza kuharibu kabisa watu wake. Mbona unasahau kirahisi hivyo? Enzi za Mwinyi watu waliacha kwenda shule, walicha kazi maofisini wakahamia kijiweni, etc. Hudhani ile ilikuwa kwa sababu ya uongozi wa wakati ule? kwaheri.
 
Kijana umechambua sana, lakini mbona mahospital makubwa mapya hayajengwi na ya kisasa? Au ndo hizo za zamani zinatosha mfano Bugando ,muhimbili na kcmc tu! Watu wameongezeka mabadiliko yawepo.

Hospitali!! ya nini? HAkuna waziri atakayeshindwa kupelekwa Ulaya au sauzi.

Hawa wanannchi wa Kawaida hapo Dar, Mikocheni, Amana, Temeke, M'nyamala na Muhimbili zinatosha ila tu tutawaomba manesi wapunguze matusi.
 
hahahhahaahhaha.... Angalieni wenzetu hao. Wanajenga. Japokuwa wanaiba lakini wanajenga nchi yao sio kama viongozi wetu wanajua kujishibisha wao tu.
 
Kaka! kama kila mtu anaongea kwamba hamna maendeleo inamaanisha hamna maendeleo. Kama hayo maendeleo yote watu hawayooni lazima ujiulize tatizo likowapi? Haiwezekani watanzania wengi wapige makelele na ukali wa maisha halafu tuendelee kusema amefanya hiki na kile. Ni kweli amefanya, lakini yawezekana maslahi ya programu hizo hayajawagusa wengi.
Sasa hapo ni ukosefu wa shukrani kwa serikali yetu,kwani hio reli inagusa maslai ya watu wengi kuliko chuo kikuu kinachochukua watu elfu alobaini?ukelini kuwa kweli nchi yetu ni masikini tena sana na wananchi wana haki ya kulalamika...lakini umasikini huu haujaletwa na serikali yetu bali ni tatizo la kihistoria...wakoloni hawakuijenga nchi yetu kama walivyofanya kwa kenya na uganda..matokeo yake ni kuwa wakati tunapata uhuru Tanganyika ilikuwa kati ya nchi kumi na sita ambazo ni masikini zaidi duniani,kwa sasa kungi hili limeonezeka na nchi pekee ilioweza kujikomboa hapa ni Botswana tu.matokeo ya uchumi mbovu uloachiwa na wakoloni ni pamoja na kukosa moyo wa kujituma.Watz tuko wavivu by nature,tukifanya kazi kidogotu tunataka ujira mkubwa.ukienda hotelini ukamkuta waitre wa kikenya ni tofauti na wa kitz.wasomi wetu wanadahani serikali ndio ina wajibu wakuwakwamua,hawataki kwenda kufanya kazi vijijini kwa madai maisha mabaya,lakini kwenye maisha yko kwa nini ushindwe kijitolea ata miaka mitano tu kufanya kazi kwa ajiri ya watanzania wenzako....tunazaliana kama ndege kuliko uwezo wa serikali kumudu.nchi kama namibia na botswana zani watu pungufu ya miilioni tano.sie tuko wangapi...watanzania wote hatuwajibiki kwa wastani.
 
hapa naona kila mtu anajaribu kuomyesha namna jk na serikali yetu tukufu inavyoshindwa kutekeleza majukumu yake jambo ambalo si la kweli ata kidogo.utendaji wa serikali ya jk hauwezi kupimwa kwa vile kibaki kajenga reli basi na sisi tujenge reli....ni ujinga kwa kweli.kwa faida ya wasomaji wa hapa pengine niseme machache sana yaliofanywa na serikali ya jk ili watu wote tuweze kuyapima.....kwanza ni ujenzi na upanuzi wa chuo kikuu cha dodoma....wanafunzi elfu alobaini wataingia hapo.....pili ni walter sector program inayotekelezwa kwa sasa ambapo kila mji utanufaika kwa maji safi kwa kiwango cha asilimia 94....kwa sasa tayari kigoma wameenza utekelezaji wa kuvuta maji toka mto malagalasina kusambazwa kigoma...wakazi wa maeeneo ya dar wanaona ujenzi wa mabomba mapya ya maji hususani maeneo ya tabata nimeshuhudia mwenyewe...ujenzi wa vyumba vya madarasa tayari kwawanafunzi wapya kuingia umefanyika nchi nzima...nani aliwapofusha mpaka yote haya hamuyaoni?

kumbe ndo maana saudia imempa medali kubwa kiasi hicho!
 
Kikwete ni mmoja kati ya matatizo makubwa ya nchi hii kama hukujua. Ofcourse yeye ndiye anayeturithisha na blames zote lazima abebeshwe yeye. Kidogodogo kaka, RUSHWA ndio tatizo kubwa la nchi hii. Hizo raslimali na mali zoooote za nchi hii haziwezi kuendeshwa kwa rushwa zikaendelea. Mkuu wa nchi akiwa na ujasiri wa kukemea rushwa ndipo wa chini yake watafanya the same. Unafikiri wale matrafiki polisi wanaokudai rushwa ya sh 2000 barabarani, wanato wapi huo ujasiri? All the way up to mkuu wa polisi anapata mgawo. Obviously otherwise angesaidiana na wasaidizi wake kuwa-track. Na mkuu wa nchi hawezi kumwajibisha mkuu wa polisi kisa polisi kadai rushwa, maana anamtumiaga kumfichia marushwa yake kuanzia wizi wa kura mpaka raslimali. All other sectors likewise.

Tukianza na kudhibiti wizi, tutakusanya za kutosha kuwalipa hao polisi wapate mlo halali wa kutosha na ziada ya kutosha madawa, walimu na mashule, barabara, nk.

Narudia tena, tatizo la hii nchi ni Kikwete for now! Baada ya hapo ndio sisi. Uongozi wake tu ndio unaweza kutukomboa. Uongozi wa rais unaweza kuharibu kabisa watu wake. Mbona unasahau kirahisi hivyo? Enzi za Mwinyi watu waliacha kwenda shule, walicha kazi maofisini wakahamia kijiweni, etc. Hudhani ile ilikuwa kwa sababu ya uongozi wa wakati ule? kwaheri.

Ni kweli tatizo ni kikwete na nadhani wananchi wengi tunajuta "why we voted for the guy?". Mategemeo yetu yote kumbe ilikuwa ni bure, jamaa naye mwizi tu kwa sababu analea wezi halafu yeye ni kutembea tu. Hana tofauti na baba mlevi anayeshinda kwenye pombe ili asikutane na watoto wake akirudi, yeye ni usuku kwa usiku.
 
Sasa hapo ni ukosefu wa shukrani kwa serikali yetu,kwani hio reli inagusa maslai ya watu wengi kuliko chuo kikuu kinachochukua watu elfu alobaini?ukelini kuwa kweli nchi yetu ni masikini tena sana na wananchi wana haki ya kulalamika...lakini umasikini huu haujaletwa na serikali yetu bali ni tatizo la kihistoria...wakoloni hawakuijenga nchi yetu kama walivyofanya kwa kenya na uganda..matokeo yake ni kuwa wakati tunapata uhuru Tanganyika ilikuwa kati ya nchi kumi na sita ambazo ni masikini zaidi duniani,kwa sasa kungi hili limeonezeka na nchi pekee ilioweza kujikomboa hapa ni Botswana tu.matokeo ya uchumi mbovu uloachiwa na wakoloni ni pamoja na kukosa moyo wa kujituma.Watz tuko wavivu by nature,tukifanya kazi kidogotu tunataka ujira mkubwa.ukienda hotelini ukamkuta waitre wa kikenya ni tofauti na wa kitz.wasomi wetu wanadahani serikali ndio ina wajibu wakuwakwamua,hawataki kwenda kufanya kazi vijijini kwa madai maisha mabaya,lakini kwenye maisha yko kwa nini ushindwe kijitolea ata miaka mitano tu kufanya kazi kwa ajiri ya watanzania wenzako....tunazaliana kama ndege kuliko uwezo wa serikali kumudu.nchi kama namibia na botswana zani watu pungufu ya miilioni tano.sie tuko wangapi...watanzania wote hatuwajibiki kwa wastani.

---Kuzaliana ni jambo la neema iwapo viongozi tunaowachagua kwa matumaini makubwa wangelikuwa wanatekeleza yale wanayoahidi kwenye majukwaa ya siasa.

---Duuh, mkuu kwenye hilo la ukoloni umeniacha hoi kwa kweli. Kwa hiyo ni bora tukubali, tuwarejeshe maana yametushinda, au?

---Vijana wanakimbilia mijini kwa sababu, kodi wanazokatwa wananchi vijijini zinazidi kutumika vibaya mijini, zinazidi kuibiwa mijini na hamna anayefikishwa mahakamani na tukaona amefungwa kwa kosa hilo. Kilimo ni uti wa mgongo kama tunavyoamini, na inatakiwa iwe hivyo. Nchi nyingi zinategemea kilimo. Sisi maisha ya mission town ndiyo imekuwa uti wa mgongo wetu. Ni nani huyu ambaye anatakiwa kuwa anatusimamia? Wakoloni au chama kilichopo madarakani? Sisi wenyewe. "Kivipi" ndiyo swali.
 
Petu Hapa,
Mkuu binafsi nina imani kubwa sana na maelezo yako na ndio dini yangu..
Matatizo ya kibilogia na Kisakologia yanakuja pale unapoacha yako ukachukua ya mwingine. Kama wewe ni mweusi na unaukataa weusi wako hivi kweli tatizo ni mzungu? tena vishawishi hivi vya kuacha utamaduni wetu, Utanzania wetu umekuja baada ya Uhuru!..
Najiuliza sana mkuu wangu. Sisi wakati tunapigania Uhuru weusi ulikuwa cake, Utanzania ulikuwa ndani ya damu yetu na tuliweza kupata Uhuru wetu kwa viamsho kama hivyo vya kizalendo lakini imekuwaje leo hii sisi tunapenda Uzungu na kuacha yaliyo yetu..
Tukisema Elimu, sidhani kwani leo hii tuna wasomi wengi sana kuliko enzi zile tena basi hakuna watu wanopenda uzungu kama wasomi wetu. Tukisema ni exposure, then tunarudi kujiuliza hivi Maendeleo ni kitu gani.. kama hatufahamu maendeleo ni yapi, kitu gani - bila shaka tuna matatizo ya kiakili au kimwili..
Nakuomba anzisha mjadala wa nini Maendeleo.. Yaani mtu akisema Tanzania imeendelea huwa ana maanisha vitu gani kisha tazama tutakavyojigonga!..
 
Back
Top Bottom