Huko Mbinguni tutaonana na Mungu uso kwa uso au atakuwa bado anajificha?

Huwa nawashangaa sana wakristo wanaosema kuwa Mbinguni watakwenda kuimba na kumsifu bwana tu .Hakuna kula wala kunywa ilihali biblia yao inapingana na wao....Biblia inasema hivi


Mathayo 8:11 BHN​

Basi, nawaambieni kwamba watu wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbinguni.

LUKA 14:15

Mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja naye aliposikia maneno haya akamwambia, “Ana heri mtu atakayepata nafasi ya kula katika karamu ya Ufalme wa Mbinguni!


Hivyo basi maisha ya peponi misosi mitamu ipo kama kawaida. We hapa duniani ukiambiwa ukae nusu saa tu unamsifu na kumtukuza Mungu utaona shida ndio uende ukakae milele huko mbinguni unasifu tu?!!!!
 
Mkuu Vipi kwa hao wanawake ndo watakua hawahawa wa huku duniani, kwamba watafanywa upya kua bikra na kugewa kwa kila mwanaume au watakua wapya ambao hawajawai kuwepo duniani?

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Siku ya kufufuliwa, wanaume wote tutafufuliwa hali ya kuwa tupo uchi na tukiwa hatujatahiriwa. Mungu atarudisha hadi vile vipande vya govi vilivyokatwa na kutupwa.Hapa wale waliokadhibisha kuwa hawatafufuliwa ndio watatamani ardhi ipasuke watumbukie chini.


Wanawake nao watafufuliwa uchi wa mnyama na bikra zao. Wote tufafufuliwa tukiwa katika umri wa ujana mithili ya umri ambao masihi Isa mwana wa maryam aliokuwa nao kipindi anapaishwa kwenda mbinguni. Miaka 33.

Wanawake wa peponi watakuwa wapya wataongezewa uzuri zaidi ya huu waliokuwa nao duniani na wataozeshwa kwa wanaume watakaoingia peponi. Ikiwa mtu mume ameingia na mkewe peponi basi wataendelea kuwa pamoja ama ikiwa ni mume tu ndio kabahatika kuingia peponi basi ataozeshwa mwanamke aliyeingia peponi na pia kuna wanawake wa ziada ambao wameumbwa makhsusi kwa wanaume watakaoingia peponi. Hawa wanaitwa Hoor al ayni
 
Naam Mola wetu ataonekana kiasi ambacho hakuna atakae mwambie sogea nimuone yaani kama vile uonapo jua la saa mchana.

Hii ni kwa wale waja wema tu kwani watalipwa Pepo na ziada ambayo ndiyo kumuona Mola muumba.
Mtamuona ila atakuwa amebadili umbile ambalo hamlijui na mtamkataa badae atarudisha umbile lake mnalolijua ndio mtamkubali
Nukuu
Hadith Sahih al-Bukhari 6573 ......Allah will come to them in a shape other than they know and will say 'I am your Lord.' They will say, 'We seek refuge with Allah from you ...... ,Then Allah will come to them in a shape they know and will say, "I am your Lord.' They will say, '(No doubt) You are our Lord.
 
Mungu yupo ndugu na hajawahi kujificha hata mara moja, inawezekana wewe ndie umemficha Mungu uso wako ndio maana humuoni ila wengine tunamuona.
 
Amekupa uhuru utende unavyotenda ili mwisho wa siku akija kukuliza kwann ulitenda jambo fulani usiwe na pa kusingizia kuwa ulionewa. Hutakuwa na kumlaumu ila nafsi yako tu..upo?!
yeye si ameshapnga kila kitu au mtoa mada ni muongo
 
Katika maisha haya ya Duniani hakuna kiumbe kilichowahi kumuona Mungu, iwe ni malaika,jini,binadamu,ndege au mdudu yeyotwle yule.

Mtume Musa alijaaliwa kuwa anaongea na Mungu moja kwa moja na ilifika kipindi akaomba amuone macho kwa macho ila Mungu hakumkubalia ombi lake

Quran inaelezea tukio hili katika sura ya 7 aya nambari. 143

"Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahala pake basi utaniona. Basi alipo jionyesha Mola Mlezi wake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema: Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini."
Nimependa kisa cha musa, japo kwa upande wa ukristo limepindishwa kidogo ila upande wa uislam haina walakini.


Lakini kuna mahali umesema hata malaika hawajawahi kumwona Mungu, sasa mimi najua Mungu na malaika zake wote huishi mbinguni sasa iweje hawaonani
 
Pia ameliweka jambo la kumuamini bila ya kumuona kuwa ni mtihani wa kiimani kwa wanaadamu na majini.

Mungu amejidhihirisha katika uumbaji wake na matendo yake, ila suala la kumuamini ameliweka liwe ni la hiyari kwetu sisi. Ukitaka umuamini usipotaka mkufuru ila mwisho wa siku utakwenda kukutana nae baada ya kufa na utaulizwa kwa yote yale uliyoyafanya.

Maisha haya tumeumbiwa kuwa ni mtihani tu ili Mungu aangalie nani atatenda matendo mema. Yaani tumewekwa katika uliimwengu wenye mchanganyiko wa mambo mema mengi na mabaya mengi ,kisha Mungu anataka kuona katika kuishi kwetu humu duniani tutarejea tukiwa na mema au mabaya.Na akatanabahisha wazi kuwa wale watakaorudi na mema watalipwa mema na wale watakaokusanya uovu nao watalipwa uovu vilevile
Umejitahidi sana maelezo yako yananipa matumaini ya nitake kumjua zaidi Mungu.

Nakuja dm kwako nitakuomba namba yako ya what'sapp nitakuwa nakutumia maswali ya kiimani ili nijifunze zaidi naona una madini yanayonishawishi
 
Kwa mujibu wa Uislamu, Ni kweli tutamuona Mwenyezi Mungu baada ya kufa na kufufuka na kulipwa kwa tuliyoyatenda. lakini watakao muona ni wale watendao mema tu, watu waovu hawataweza kumuona.

QURAN 75 20-25
20." La! Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,

21. Na mnaacha (hamshughulikii) maisha ya Akhera.
22. Zipo nyuso siku hiyo zitang'ara,

23. Zitamwona Mola wao Mlezi.

24.Na zipo nyuso siku hiyo zitakunjamana.

25.Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo. "
 
Nimependa kisa cha musa, japo kwa upande wa ukristo limepindishwa kidogo ila upande wa uislam haina walakini.


Lakini kuna mahali umesema hata malaika hawajawahi kumwona Mungu, sasa mimi najua Mungu na malaika zake wote huishi mbinguni sasa iweje hawaonani
Malaika wana mwisho wao wa kufika huko mbinguni. Ukimaliza mbingu saba kuna uwanda mkubwa zaidi kuliko hizi mbingu saba ili ufike alipo Mungu. Juu ya mbingu saba kuna kursiy,then kuna Arsh (kiti cha enzi), juu zaidi huko yupo Mungu.

narrated by Muslim in his Saheeh (4136) from ‘Abd-Allaah ibn ‘Abbaas who said: A man from among the companions of the Prophet (peace and blessings of Allaah be upon him), one of the Ansaar, told me that the Messenger of Allaah (peace and blessings of Allaah be upon him) said: “… But when our Lord, may His name be blessed and exalted, decrees something, the bearers of the Throne glorify Him, then the people of the heaven that is closest to them glorify Him, until the tasbeeh reaches this lowest heaven (al-sama’ al-dunya). Then those who are closest to the bearers of the Throne say to the bearers of the Throne: ‘What did your Lord say?’ So they tell them what He said. Then the people of the heavens ask one another until the news reaches this lowest heaven.’” This very clearly indicates that the Throne and its bearers are above all the heavens.

Malaika huko mbinguni wanapokea taarifa/maagizo tu kutoka kwa Mungu hawaonani nae ana kwa ana ila yeye anawaona.

Sehemu ya mwisho ambayo malaika anaweza kufika inaitwa Sidrat al muntaha ( the lote tree/mkunazi) ni sehemu ya mwisho huko juu ambayo malaika anaweza kufika , hawezi kuvuka zaidi ya hapo. Mtume Muhammad alipelekwa na malaika mkuu (jibril) kwenda kukabidhiwa amri ya swala tano. Alifikishwa mahala na malaika Jibril kisha akaambiwa asonge mbele zaidi, alimuuliza Jibril kwanini asiende nae, Jibril akamjibu kuwa hawezi kuzidi zaidi ya hapo huko mbele zaidi kuna nuru kali ya Mungu. Ila Mtume Muhammad ndie alipewa kibali asonge zaidi akafunikwa na pazia, licha ya kusonga mvele zaidi bado hakumuona Mungu zaidi alipewa hizo amri azishike na malipo yake ni pepo kwa yule atayeshikamana nazo
 
It was narrated that ‘Aa’ishah (may Allaah be pleased with her) said: “Whoever told you that Muhammad (peace and blessings of Allaah be upon him) saw his Lord was lying. He said that no vision can grasp him [cf. al-An’aam 6:103]…”

(Narrated by al-Bukhaari, al-Tawheed, 6832).


Quran 6:103

"Vision perceives Him not, but He perceives [all] vision; and He is the Subtle, the Acquainted."



"Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari"

So hakuna jicho linaweza kumtazama Mungu katika ulimwengu huu.Ila baada ya kufufuliwa macho yataondolewa pazia na tutamuona Mungu waziwazi.
 
Back
Top Bottom