Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,578
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huwaletea makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa. Mada ya leo ni a bit abstract, ambapo Nimesikia sauti ya Voices From Within ikiniambia JPM yuko Mbinguni kwa Baba, hivyo nauliza swali, jee wajua kuwa JPM yuko peponi, Mbinguni, Kwa BABA YAKE?

Why watu wengine waendelee kumshutumu, kumsakama na kumsimanga?. Kwa nini asiachwe ajipumzikie zake kwa amani!. Mtu ameisha tangulia mbele ya haki, kwanini watu waendelee kumsema sema kwa ubaya.

Mimi mwana jf mwenzenu ni Mzee wa Sauti za Ndani "the inner voice", unafanya kitu fulani na mara unasikia sauti from within ikikuambia jambo fulani.

Angalizo kuhusu Abstract Topics.

Issues na mtu akiisha kufa, we all knows what happens to the body, but roho huwa inakwenda wapi, no one knows for sure, hivyo tunategemea mafundisho ya dini zetu.

Kuna sisi dini za wana wa Nabii Ibrahim, Wakristo na Waislamu tumefunzwa kuhusu mbinguni, peponi, ahera, jehanam ya moto wa milele, na kuna siku ya mwisho siku ya hukumu ya mwisho ya kiama atakapo rudi Mwana wa Adamu, ambapo kutakuwa na ufufuko wa miili na uzima wa milele.

Kuna wenzetu wa Buddhism na Hindu ambao ni waumini wa karma, wao wanaamini kwenye after life na incarnation.

Hakuna yeyote awaye yote aliwahi kufa akayashudia hayo na kurejea duniani kututhibitishia mbingu ipo, peponi kupo na motoni kupo, wala waumini wa reincarnation no one can say for sure alikuwa nani before, zaidi ya ushahidi wa deja vu, hakuna uthibitisho wowote wa reincarnation Ila kwa vile na mimi niliishi India, I know for sure karma ipo and it's for real!

Hivyo hii mada ni mada ya imani, kama wewe huamini, please keep your faith nakuomba usibeze imani za wengine, ukijiona huamini, nakuomba jipitie zako kimya kimya, tuache sisi waumini.

Leo asubuhi nilikuwa nasoma michango ya wachangiaji wa bandiko langu hili. "Mimi ni Mwenzenu Hapa, Sijabadilika ni Yule Yule "KaJoni" - Ni Maneno Simple, Humble and Down to Earth Yenye Maana Kubwa!

Sasa ni wakati nasoma bandiko lenyewe, na naomba nililete hapa bandiko lenyewe lote kwa faida ya wavivu to follow links.
Wanabodi,
Hili ni bandiko la hoja ngumu zinazoitwa abstract, na zinahusu kitu kinachoutwa psychoanalysis, mtanisamehe, sikijui Kiswahili cha abstract wala psychoanalysis, lakini inahusu kumsikiliza mtu kauli na kuibaini kama inatoka moyoni au mdomoni. Ili uweze kuibaini kauli ni ya kutoka moyoni lazima na wewe uwe na jicho la roho, hivyo kwa uzoefu wangu humu jf, issues za psychoanalysis zinachangiwa na watu wachache kwasababu ni abstract.

Sisi binadamu tumeumbwa na uwezo tofauti wa uelewa kuanzia kwenye kusoma maandishi hadi kwenye kusikiliza na kuelewa maneno yanayotamkwa na mzungumzaji kama ni ya kweli, yanatoka mdomoni tuu au moyoni, kumaanisha one just speaks to say something or one's speaks and real mean what he/she says.

Kwenye kusoma maandishi utaalamu wa kubaini psychological state of a writer wakati anaandika, unaitwa graphology, zamani kwenye barua za kuomba kazi sehemu nyeti, waombaji walitakiwa kuandika barua kwa mkono, na wataalamu wa graphology, walizipitia barua hizo na kuamua wamuite nani kwenye interview, na siku ya interview hatua ya kwanza ni kuandika jina lako kwenye karatasi kujisajili, mwandiko usipofanana, unaishia hapo hapo mlangoni.

Wataalamu wa kubaini genuineness ya kauli, kama mtu akitamka maneno fulani yanatoka moyoni au mdomoni tuu inaitwa intuition, hii intuition kila mtu anayo, ila wanawake wanakuwa more sensitive kuliko wanaume, ndio maana ukiwatokea, unapigwa kwanza kalenda ili wajiridhishe, na kusema ukweli, kwa sisi wanaume wa off side tricks, kuna wake zetu wengi wanajua tuu, tunavyopiga mipira ya kona ila hawasemi.

Ukimtamani msichana mrembo kwa tamaa tuu za mwili ili kumtumia, yaani lust and infatuation, utamwambia "I love you" na mtu ukimpenda msichana huyo kwa upendo wa kweli, true and genuine love, pia utamwambia "I love you"

Kati ya wawili hao kuna mmoja ni mkweli na mmoja ni muongo, huyu mrembo anayependwa, how will she know, kama anapendwa kweli au anatamaniwa tuu atumike na kutoswa?.
Kitu kinachoitwa female intuitive kitamhulisha huyu mwanamke nani ni mkweli na nani ni muongo.

Utabaini kwa kusikiliza sauti kutoka ndani yako, yaani listening to yourself ili usikie, the voices from within, the voices from inside by listening to yourself. Hata hivyo dada zetu wengi hupotea maboya ukiingia kwa gia kubwa, kwa kutumia universal language, wengi hukubali kulainika na kuingia kingi kirahisi japo moyoni wanaisikia kabisa sauti ikiwaambia wanadanganywa!. Na kwa wale mangurubange wa danga chee, wao wanaangalia tuu usawa wa salio na sio mapenzi hivyo hapendwi mtu bali.

Kutamka kitu kinachotoka mdomoni na sio moyoni kinaitwa paying lip services, unapofika mwaka wa uchaguzi wanasiasa wengi wanazungumza mengi kutoka mdomoni tuu na sio moyoni. Wanazungumza kile ambacho wananchi watapenda kusikia hata ikibidi kutoa ahadi za uongo ili kupata kura.

Elimu ya kufanya uchambuzi wa kauli za viongozi kama wanasema kweli au just paying lip services, inaitwa psychoanalysis scrutiny ya baadhi ya kauli za viongozi wetu.

Mimi ni miongoni mwa wana jf wachache ambao from time to time, huwa nawaletea psychoanalysis scrutiny ya baadhi ya kauli za viongozi wetu, miongoni mwa issue niliyoifanyia scrutiny kubwa humu ni issue ya makinikia, nikisema zile tume mbili zilifanya lip services ya kitu bwana mkubwa alichotaka kusikia, tukaja na bili ya ajabu ya dola bilioni 190 za kutosha Noah ya kila Mtanzania, ukweli ulipobainika, deni hilo liliyeyuka, tukaambulia kile kile kushika uchumba cha dola milioni 300 kinacholipwa ndani ya miaka 7!.

Leo nimeisikia kauli hii

"Mimi ni mwenzenu hapa, sijabadilika ni yule yule "KaJoni". Kauli hii japo ni maneno machache simple, lakini yamebeba maana kubwa sana, hii kauli ni kutoka moyoni, ambayo inaonyesha humbleness, simplicity and down to earth ambayo ina maana kubwa sana kwa mustakabali wa nchi yetu.

Kufuatia baadhi ya makabila kuwa na mijitu yenye miili mikubwa, mijitu ya miraba minne, akitokea mtu mwenye umbo dogo, jina lale linatanguliwa na neno "ka", "kapasiko", hivyo zamani enzi za utotoni, udogoni, kule kijijini Chatto, kumbe rais Magufuli alikuwa anaitwa "KaJoni" kujulisha kuwa jina lake ni Joni, lakini kutokana na kuwa na umbo dogo akawa anaitwa KaJoni.

Mtu anaye kuwa kwa kuitwa kwa prefix ya neno ambalo ni deamining kuonyeshea udogo au kudogoshwa akiukwaa ukubwa hadi kuwa ni rais wa nchi....

Kwa muda mrefu humu mimi nimekuwa nikichambua baadhi ya kauli za viongozi, kwenye kauli nzuri nazipongeza na kaulu mbaya nazikosoa.

Kauli hii niliyousikia leo, ya "Mimi ni mwenzenu hapa, sijabadilika ni yule yule "KaJoni", ni kauli yenye maana kubwa sana ya self realization of going back to his roots. Japo rais Magufuli alikuwa akizungumza na Wana Chato, kuwaeleza kuwa japo kwa sasa mimi ni rais wa JMT, ni mtu mkubwa sana, mwenye nguvu nyingi na mamlaka na madaraka makubwa kama rais wa nchi na Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, lakini kwa nyinyi wana Chato, mimi ni mwenzenu yule yule KaJoni, huu urais wa JMT, vyeo, madaraka, mamlaka, ni vitu vya kuja tuu na kupita, lakini mimi ni yule yule KaJoni ka Chato.

Katika baadhi ya analysis zangu kwa kauli za viongozi, niliwahi kusema baadhi ya viongozi wana kauli za kujiinua mno, kauli hizo za kujiinua zilizoanzia juu, zikapelekea viongozi wa chini nao kujiinua wakiwemo ma RC hadi vi DC navyo vimejiinua hadi masikio kutaka kuzidi kichwa kwa kuongea kwa vitisho, ukali, kugomba na kusweka watu ndani ikiwemo kutukana watu hovyo hata waliowazidi umri!.

Kitendo cha rais Magufuli kuwaeleza wana Chato, yeye ni yule yule KaJoni, inatuma ujumbe mzito wa kujishusha na kujinyenyekeza, humbleness, being down to earth, na kuongea kwa humility ambazo ni changes for the better ambazo nimekuwa nikizisema kwa mtu huyu kuwa "This man is changing for the better" tunaweza kushangaa kuja kufikia 2025, rais Magufuli aka end up kuwa the best president this country had ever had.

Mwelekeo wa kauli kama hizi kwa mwaka wa uchaguzi, they are expected, kwasababu huu ni mwaka wa viongozi kuwarudia wananchi kujinyenyekeza kuombea kura, wanasiasa wenye kauli za maudhi na majigambo ya jeuri ya mamlaka, wanapojinyenyekeza kuomba kura, ndiko paying lip services kwenyewe ninako kuzungumzia, lakini kwa kauli hii ya rais Magufuli, mimi kwa kuisikiliza nimeibaini, kuwa ni bonafide genuine imetoka moyoni na sio lip services, hivyo haitegemewi mtu ambaye ni humbleness hii na down to earthiness hii akaja kujiinua tena na urais kumpanda tena kichwani!

Once KaJoni, always KaJoni!,
Hongera sana rais Magufuli, kujishusha kutoka Joni hadi KaJoni, utabarikiwa sana na Tanzania itabarikiwa.

Pasaka Njema
Pasakali.
Rejea za kauli mbalimbali za viongozi
Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!. - JamiiForums

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais Magufuli!, Alimaanisha Nini?!. - JamiiForums

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje? - JamiiForums

Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii? - JamiiForums

Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba! - JamiiForums

Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?. - JamiiForums

Awamu ya tano: Kuweni Wakali, msionee! Tangulizeni utu na ubinaadamu kwanza! - JamiiForums

Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani! - JamiiForums

Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The Better!. Hongera Sana! - JamiiForums

Tusilalamike tuu, kulaumu na kulaani kila kitu, kwenye mazuri tupongeze! Rais Magufuli is changing for the better!. - JamiiForums

This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea? - JamiiForums

Je, kuna ukweli watu wafupi wana inferiority complex hivyo kukasirika sana wanapohisi kudharauliwa? - JamiiForums

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu. - JamiiForums

Psychoanalysis: Je, wajua dress code ya mtu ina represent the soundness of his mind? - JamiiForums

Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity - JamiiForums

Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni asili tuu ya wasukuma, sio udikteta! - JamiiForums

Ndipo nikaisikia sauti, voices from within kuwa JPM yuko peponi, ahera, mbinguni kwa Baba!

Kwa kawaida ya sauti, huwa inakuambia tuu kitu na haikupi sababu, hivyo naomba msiniulize sababu, hapa kazi yangu ni moja tuu kuwaeleza kile nilichosikia Leo ni JPM yuko peponi!

Hivyo baada ya kuisikia hiyo sauti nikamsikiliza tena JPM kwa makini sana katika video hii
Nimejiridhisha bila chembe ya shaka, huyu mtu yuko mbinguni, peponi kwa Baba yake!, yuko na Baba yake!.

Hapa simaanishi kuwa JPM yuko peponi kwasababu he is perfect kama malaika, no!. JPM was a human being hivyo he is not perfect and no one is perfect, kilichofanya hiyo sauti ni despite his human mistakes JPM alitubu kabla ya umauti na kusamehewa dhambi zake zote na makosa yake yote, na ndio maana nimeambiwa, sasa he is in heaven now!.

Kwa bandiko hili, sasa ningewaomba watu humu, kutoendelea kumsakama, kumshutumu, kumsimanga na kuendelea kumsema vibaya, na badala yake tumwache apumzike kwa amani. Kama Mungu mwenyewe amemsamehe na kumuita kwake, who are you kuendelea kumsema sema vibaya?

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
 
PASKALI nimesoma andiko lako kwa tafakuri kubwa sana! Unaweza kuwa sahihi kwa sauti yako ya ndani ambayo iko juu ya uwezo wako kuweza kui control.. Lakini tukija kwenye uhalisia wa maandiko kwa imani ya mhusika ni kwamba wafu bado hawajafika peponi bali wote wako kaburini wakisubiri kiama ama mwisho wa dunia ambapo kila mtu atapewa hesabu yake
Niliwahi kuandika hapa kwamba zana ya pepo/peponi na Jehanum kuzimu iko pale kaburini, kwamba wale waliotenda mema roho zao ziko pale zimelala kwa utulivu lakini wale waliotenda mabaya (kwa tafsiri yoyote ya ubaya) roho zao zinahamanika na kuhangaika huko na huko, hiyo ndio tafsiri ya kuzimu/jehanum

Kwa upande wa karma.. Hii sote tunajua haikopeshi.. Tendo kwa tendo ..ubaya kwa ubaya na wema kwa wema.. Hivyo inategemea nani anaamini kwenye nini ndio atamuweka mhusika huko..

Kuna hili la mizania ya haki.. Hili hupimwa kwa matendo ya mtu mabaya na mazuri..Asili ndio huhukumu., hapa si dini bali ni asili, asili itakuchagulia njia yako kutokana na maisha uliyoishi kabla ya kifo

Hapa kuna ishu ya uumbaji ambayo kupitia mikono yake kwa tafsiri yoyote ile uumbaji huo uliumia, uliteseka na pengine kudhulumiwa haki ya kuishi.. Hapa ishu ni zile sauti zinazolia na kusononeka kwa namna yoyote ile.. Hapa ndio muunganiko wa mizania ya haki na asili hutokea... Kuna vitu viwili ambavyo kiimani vinapaswa kutendewa kwa tahadhari kubwa mno navyo ni uumbaji/uhai na ardhi.. Kwa waamini vitu hivi tumeonywa tusivichezee..!

LA mwisho ni hili la kuonya wadau wasiendelee kumsakama marehemu kwakuwa tayari alishafanya kitubio na yuko peponi..brother sidhani kama maneno yao yatakuwa na athari zozote kwenye hili.. Japo sasa kama ni kweli bado hata baada ya kufa watu wanaendelea kumsema vibaya basi lazima tutambue kuna tatizo kubwa mahali kuhusiana na yeye..!
 
NI sahihi kwa Jinsi alivyokuwa mzalendo naimani kaitendea haki nafasi aliyopewa ingawa Kuna mapungufu yaliyosababishwa na chama chake na watendaji wake aidha makusudi kumchafulia au na yeye akawa directly Masterminder...mfano lisu kushambuliwa na risasi why Kama Rais asitoe tamko zito kulaani
 
NI sahihi kwa Jinsi alivyokuwa mzalendo naimani kaitendea haki nafasi aliyopewa ingawa Kuna mapungufu yaliyosababishwa na chama chake na watendaji wake aidha makusudi kumchafulia au na yeye akawa directly Masterminder...mfano lisu kushambuliwa na risasi why Kama Rais asitoe tamko zito kulaani
Ah ah, mzalendo hasiwe Mamako aje awe uyo mwizi?? Kojoa ukalale
 
Uko sahihi mleta mada. Marehem anapaswa kuachwa apumzike kwa amani. Ila matendo machafu au masafi yaliyogusa watu sio rahisi kuacha kusemwa kwa hisia tofauti tofauti.

Hivi unafikiri yule mwanachi aliyaefanyiwa jema akajengewa nyumba pale Mapipa utaweza kumnyamazisha vipi kumsema Marehem?

Ama yule mwingine aliyepotezewa mwanae hajui hata mwili wake uliko, au yule aliyetumikia Taifa kwa miaka mingi alafu miaka michache tu kabla ya kustaafu, anakuja mtu anamtumbua na kutaifisha mafao yake yoote kisa alitumia cheti Cha mjomba wake kujielimisha na kupata kazi, unadhani anaweza kujizuia kumtaja taja huyo Marehem?
 
Suala la wapi mtu anaenda baada ya kifo ni la kiimani zaidi. Ni kati ya Muumba wake na mhusika. Sio ndugu, Rafiki, jamaa Wala mpenzi wa marehem anajua au anaamua marehem anaenda wapi au anakua wapi baada ya kifo.

Cha msingi ni angalizo ulilolitoa tu kwamba Mtu akishafariki, aachwe apate kamisheni sawasawa na matendo yake.
 
PASKALI nimesoma andiko lako kwa tafakuri kubwa sana! Unaweza kuwa sahihi kwa sauti yako ya ndani ambayo iko juu ya uwezo wako kuweza kui control.. Lakini tukija kwenye uhalisia wa maandiko kwa imani ya mhusika ni kwamba wafu bado hawajafika peponi bali wote wako kaburini wakisubiri kiama ama mwisho wa dunia ambapo kila mtu atapewa hesabu yake
Niliwahi kuandika hapa kwamba zana ya pepo/peponi na Jehanum kuzimu iko pale kaburini, kwamba wale waliotenda mema roho zao ziko pale zimelala kwa utulivu lakini wale waliotenda mabaya (kwa tafsiri yoyote ya ubaya) roho zao zinahamanika na kuhangaika huko na huko, hiyo ndio tafsiri ya kuzimu/jehanum

Kwa upande wa karma.. Hii sote tunajua haikopeshi.. Tendo kwa tendo ..ubaya kwa ubaya na wema kwa wema.. Hivyo inategemea nani anaamini kwenye nini ndio atamuweka mhusika huko..

Kuna hili la mizania ya haki.. Hili hupimwa kwa matendo ya mtu mabaya na mazuri..Asili ndio huhukumu., hapa si dini bali ni asili, asili itakuchagulia njia yako kutokana na maisha uliyoishi kabla ya kifo

Hapa kuna ishu ya uumbaji ambayo kupitia mikono yake kwa tafsiri yoyote ile uumbaji huo uliumia, uliteseka na pengine kudhulumiwa haki ya kuishi.. Hapa ishu ni zile sauti zinazolia na kusononeka kwa namna yoyote ile.. Hapa ndio muunganiko wa mizania ya haki na asili hutokea... Kuna vitu viwili ambavyo kiimani vinapaswa kutendewa kwa tahadhari kubwa mno navyo ni uumbaji/uhai na ardhi.. Kwa waamini vitu hivi tumeonywa tusivichezee..!

LA mwisho ni hili la kuonya wadau wasiendelee kumsakama marehemu kwakuwa tayari alishafanya kitubio na yuko peponi..brother sidhani kama maneno yao yatakuwa na athari zozote kwenye hili.. Japo sasa kama ni kweli bado hata baada ya kufa watu wanaendelea kumsema vibaya basi lazima tutambue kuna tatizo kubwa mahali kuhusiana na yeye..!
Umeelewa babu Pascal Mayalla sio kuyomba yomba hovyo kama 🐒 siku ingine ukileta nyuzi za aina hii tunakupiga
 
Kusikia Voices from Within, hii hali hunipata pia. Nimewahi kusikia sauti ya mwimbaji maarufu (marehemu) akilia kwa uchungu, wakati huo nilikuwa nasikiliza moja ya wimbo wake. Ndipo nikajua nyimbo za kidunia zinaunguza kila aimbaye Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom