ANUNNAKI: Nadharia za Mungu, miungu, fumbo la sciencenscience na Teknolojia kubwa katika Dunia ya kale, kuanguka Kwa civilization na kuinuka Tena

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
4,064
8,231
Habari Wana JF na jukwaa la Intelligence natumaini mpo salama na tunasurvive chini ya jua kibishi,
Nimeona nilete hii mada ngumu kidogo kuhusu Accient civilization ya kale katika Dunia yetu,pamoja na nadharia mbali mbali za kuanguka na kupotea kwake,

Natumaini wale magreat thinkers watashashare idea zao kutoka vyanzo mbali mbali na natamani mjadala uwe endelevu na wale wenye watakaoweza kuweka rejea kutoka source mbali mbali wawe huru Ili mjadala uwe mpana kidogo hivyo uvumilivu unahitajika,
Note wafia Dini hamuhitajiki humu kama kitu hujui kaa kwa kutulia upate Somo na rejea mbali mbali,

Karibu!

Dunia ya kale ilipata kupitia katika ustaarabu mkubwa sana ambao Mpaka Leo unaacha utata mkubwa pamoja na fumbo kuu,
Wanasayansi,watu wa Dini,wanafalsa na wachunguzi huru wamejikuta kwenye sintofahamu juu ya ustaarabu ule uliopotea Huku wakibaki kwenye nadharia nyingi toka Hapo zamani,

Ushahidi kutoka maandiko ya kale ya Sumeria yaliyokutwa katika tablets za Mawe na michoro mbali mbali katika jamii nyingi za kale zimewataja viumbe walioitwa 'miungu'

"Miungu" au 'gods' tafsiri yake ikiwa na maana ya walioshuka kutoka 'mbinguni' au angani na Kushuka duniani,

Nadharia ya Miungu Katika Sumeria imewataja "ANUNNAKI"
Au Wana wa Annak
ANU =mtawala wa mbinguni na baba wa waanak na KI mother goddes mtawala wa Dunia,

Maandiko ya kale ya Wasumeria katika Mesopotamia yamewataja viumbe Anunak walipata Kuja duniani Miaka 450,000 BCE iliyopita,
Mtafiti wa mambo kale Zachariah Sitchin miaka ya 70's aliweza kutafsiri baadhi ya maandiko ya kale ya Wasumeria yanayodai Annunaki walipata Kuja pre human development yaani akiwa na maana Dunia ikikaliwa spicies ya Homo Elactus pekee,

Pia maandiko ya kale ya Sumeria yanadai Annunaki walitokea Sayari ya Nibiru ambayo huizunguka mfumo wetu wa Nyota ikiwa kwenye mhimili wake Kila baada ya miaka 3,600
Na maandiko hayo ya kale yanapata kuandika Annunaki ni intelligence being wenye high advanced science and technology na walipata kuja Duniani na Spaceships kwa lengo la kuchimba Dhahabu ikiwa kama metal ya mhimu huko kwenye sayari Yao ambayo waliitumia kurecover atmosphere ya anga lao,
Note hiyo ni according to Accient writings alizotafsiri Zachariah Sitchin,wanasayansi na Watafiti wa mambo kale kama Jesus Cediel,

Swali Wana jamii intelligence Inakuaje tablets kongwe na ya kale kuliko maandiko yoyote Yale yaani Sumerian iandike mambo kama hayo?

Fumbo!

Nitaendelea na mada karibuni Kwa mjadala!

ALALU:Mtangulizi wa mwanzo wa Annunaki
Katika accient tablets anatajwa Alalu huyu alikua ni agent kutoka Sayari ya Nibiru aliyepewa jukumu la kuzunguka Sayari mbali mbali kuangalia uwezekano wa kuwepo Kwa dhahabu,Alalu alifanikiwa kuifikia Dunia yapata miaka 450,000 BCE na kufanya tafiti mbali mbali Katika accient tablets anatajwa kama 'mungu' wa ugunduzi,Alalu alipata kutua Kush na akagundua hazina kubwa ya dhahabu,ugunduzi wa machimbo ya kale ya kush unathibitisha kugundulika Kwa dhahabu Kwa mara ya kwanza Katika uso wa Dunia ukifuatiwa ule wa South Africa na Maputo Msumbiji ambako miaka ya Hivi karibuni kuligundulika machimbo ya kale sana yalichimbwa Kwa ustadi Kwa kutumia vifaa vya kisasa unaoshangaza Dunia ya Leo,

Baada ya tafiti za Alalu walifuatia Wana wa Annak ENKI na ENLIL ambao walishuka na Spaceships s kubwa Wakiongozana na moja ya jamii ya Waanunaki waitwao IGIGI ambao waliotumika kama workers kwenye Migodi yote iliyoanzishwa huku wakiongozwa na ENKI na ENLIL kama viongozi,

Maandiko ya Sumeria yanadai baadae IGIGI walichoka kufanyishwa Kazi za machimbo ya dhahabu sababu ya brutality kitu kilichopelekea vita kubwa na ya kwanza Katika uso wa Dunia ikihusisha advanced weapons kama Nuclear weapons,
Baada ya resistance ya IGIGI
ENKI alikuja na Wazo la kumfanya Kiumbe awe replaced ndipo wakawafanya Nephilims (Wanefili) Hawa walikua ni Viumbe wenye mfanano na Annunak ila wakubwa na wenye nguvu,wakitumia Hybrid Nephilims walishindwa zaliana hivyo kuwapa mzigo ENKI kuwazalisha Kwa wingi kulingana na mahitaji na Kasi ya Kazi Katika Migodi maana walishindwa kuendana na Kasi sababu ya ukubwa na uzito wa miili Yao,

WAZO LA KUMFANYA BINADAMU,
Annunak Chronicles inaelezea mwanzo Dunia ilikaliwa na Viumbe waitwao Enkidu Katika Epic of Girgamesh wanamtaja Kiumbe Mtu Enkidu ambaye alikua spicies ya Homo Elactus walioishi duniani wakiwa hawana humanity waliishi pamoja na wanyama wa mwituni kama hayawani wengine,.
Enki alifikiria ni jinsi Gani atawafanya wale Enkidu wawe intelligence na akaja na Wazo la kuwaongezea vinasaba milini mwao Kwa kufanya DNA testing na walifanikiwa kufanya genre ya Homo sapiens wa kwanza,
Pia Maandiko ya Sumeria yanadai Annunaki walifanya human manipulation na cloning project na kumtengeneza mtu wa kwanza
ADAPA (Adamu)
Wakitumia DNA zao,manii na kupandikiza Kwa Kiumbe mke aliyekuja kuzaa genre ya Homo sapiens kamili iliyokamilika
(Sumeria tablets zinaelezea teknolojia ya Human cloning,human manipulation na sayansi nyinginezo kukamilisha Hilo)

Kwanini wamuumbe mtu Kwa mfano wao?
Ukisoma kitabu Cha Genesis kinadai Mungu alisema na tumfanye mtu Kwa mfano wetu
(Wale wa nadhari za Abrahamic Religion wajiulize ilikuaje Mungu aseme na tumfanye mtu Kwa mfano wetu)
Hiyo wetu inawakilisha uwingi ikiwa na maana ya "Gods"
(Walioshuka kutoka juu mbinguni na kuja Duniani)

NADHARIA ZA MUNGU NA MIUNGU/ KUUMBWA KWA BINADAMU WA KWANZA NA LOYAL BLOODLINE OF ADAM,

Mathalani umewahi sikia Nadharia kuhusu MUNGU au inawezekana ni mmoja unayeabudu nadharia hii ukiamini ni Supernatural power iliyoumba ulimwengu na vilivyomo,na nguvu hiyo Ipo ndani ya kiumbe aliyeketi kwenye kiti Cha enzi Cha Mbinguni na ni Mzee wa siku mwenye utukufu mkubwa akiwa kazunguka na wazee 24 wenye uhai,huko akihukumu Kwa haki jamii ya viumbe mbali mbali waliopewa majina ya Malaika,Maserafi,wanadamu nk

Nadharia hii ilitawala katika ulimwengu wa kale na wakisasa
Huko ikiwa na tofauti mbali mbali,

Mosi ni Ile Mungu hapo zamani alishuka Moja Kwa Moja mpaka duniani akiounga upepo katika bustan ya Eden Pahali anapoishi binadamu wa kwanza kuumbwa Adamu,
Ukisoma maandiko ya kitabu Cha Mwanzo kinadai Mungu alishuka wakati wa alasiri bustanini kuongea na kiumbe wake
(Code nitaelezea hapa Kwa kina)

Pia hapo kale Wana wa Mungu Walishuka mpaka duniani na kukutana na watu wa kale na kuishi nao maisha ya kawaida
(Refer Watchers/Angels)
Hiyo ilikua swala la kawaida tu bila shaka,

Pili:Nadharia za kisasa
Hapa tunaona katika zama Fulani miungu walikndoka duniani ni kama waliitelekezwa vile,sababu ya kufanya vile hatujui ila inakuja ibuka nadharia ya watu wanaojita Mitume na Manabii ya hapo kale wakijifanya ni maajent wa Mungu na wasemaji wake Kwa watu katika mambo Fulani Fulani,
Je ilikuaje yule Mungu na wale Malaika wake wasije Tena mpaka Leo hii toka zama zile na hata wakija wanafikia Kwa jamii Fulani Tena watu wa blodline Moja?
(Fumbo)

Leo ninaenda kukupa majibu ya hilo fumbo hapa hapa!

Tuendeleee

Maandiko ya Biblia kwa asilimia 99% hasa agano la kale limecopy Maandiko ya Sumeria ambayo ni makongwe Sana Kuliko maandiko yoyote yaliyowahi rekodiwa hapa Duniani,
Hili linaungwa mkono na jamii nzima ya Leo maana sumerian tablets ndio msingi wa ustaarabu wote wa Mwanadamu katika Historia ya Dunia,
Sumeria ilikua ndio sehemu ya kwanza Alphabet yenye character 600 +
Ikiiacha mbali Alphabet tuitimiayo yenye character 26 tu
Yaani ABC to Z basi
Pia Sumeria walikua na Mathematical table ya kushangaza Sana,
Wataalamu wa mambo kale Wanakiri endepo tutaweza gundua calculation na njia ya kufanya Hisabati kama wao tutapiga hatua Kubwa sana katika science and technology
Refer wanasayansi kushindwa fanya calculation za accient civilization zilizotumika katika ujenzi wa majengo kama Pyramids na site mbali mbali
(Mifano mnayo)

Sasa basi Bible ilicopy maandiko hayo sababu waliyanakiri na kucopy visa vile walikosa Information kuhusu Accient civilization hivyo kuoelekea kuunga unga visa vilivyokaa bila mpangilio maalumu yakiwa Randomly
(Wanatheolojia watanielewa)

Baada ya ugunduzi wa Sumerian tablets miaka ya 1880's na baadhi kuyatafsiri ndio tukajua zile information zote tata zimeelezewa Kwa ufasaha na kupangiliwa visa kuhusu Accient gods waliokuja kutoka Nibiru planet kutafuta dhahabu na hatimaye kumuumba Binadamu kama man power!
 
Habari Wana JF na jukwaa la Intelligence natumaini mpo salama na tunasurvive chini ya jua kibishi,
Nimeona nilete hii mada ngumu kidogo kuhusu Accient civilization ya kale katika Dunia yetu,pamoja na nadharia mbali mbali za kuanguka na kupotea kwake,

Natumaini wale magreat thinkers watashashare idea zao kutoka vyanzo mbali mbali na natamani mjadala uwe endelevu na wale wenye watakaoweza kuweka rejea kutoka source mbali mbali wawe huru Ili mjadala uwe mpana kidogo hivyo uvumilivu unahitajika,
Note wafia Dini hamuhitajiki humu kama kitu hujui kaa kwa kutulia upate Somo na rejea mbali mbali,

Karibu!

Dunia ya kale ilipata kupitia katika ustaarabu mkubwa sana ambao Mpaka Leo unaacha utata mkubwa pamoja na fumbo kuu,
Wanasayansi,watu wa Dini,wanafalsa na wachunguzi huru wamejikuta kwenye sintofahamu juu ya ustaarabu ule uliopotea Huku wakibaki kwenye nadharia nyingi toka Hapo zamani,

Ushahidi kutoka maandiko ya kale ya Sumeria yaliyokutwa katika tablets za Mawe na michoro mbali mbali katika jamii nyingi za kale zimewataja viumbe walioitwa 'miungu'

"Miungu" au 'gods' tafsiri yake ikiwa na maana ya walioshuka kutoka 'mbinguni' au angani na Kushuka duniani,

Nadharia ya Miungu Katika Sumeria imewataja "ANUNNAKI"
Au Wana wa Annak
ANU =mtawala wa mbinguni na baba wa waanak na KI mother goddes mtawala wa Dunia,

Maandiko ya kale ya Wasumeria katika Mesopotamia yamewataja viumbe Anunak walipata Kuja duniani Miaka 450,000 BCE iliyopita,
Mtafiti wa mambo kale Zachariah Sitchin miaka ya 70's aliweza kutafsiri baadhi ya maandiko ya kale ya Wasumeria yanayodai Annunaki walipata Kuja pre human development yaani akiwa na maana Dunia ikikaliwa spicies ya Homo Elactus pekee,

Pia maandiko ya kale ya Sumeria yanadai Annunaki walitokea Sayari ya Nibiru ambayo huizunguka mfumo wetu wa Nyota ikiwa kwenye mhimili wake Kila baada ya miaka 3,600
Na maandiko hayo ya kale yanapata kuandika Annunaki ni intelligence being wenye high advanced science and technology na walipata kuja Duniani na Spaceships kwa lengo la kuchimba Dhahabu ikiwa kama metal ya mhimu huko kwenye sayari Yao ambayo waliitumia kurecover atmosphere ya anga lao,
Note hiyo ni according to Accient writings alizotafsiri Zachariah Sitchin,wanasayansi na Watafiti wa mambo kale kama Jesus Cediel,

Swali Wana jamii intelligence Inakuaje tablets kongwe na ya kale kuliko maandiko yoyote Yale yaani Sumerian iandike mambo kama hayo?

Fumbo!

Nitaendelea na mada karibuni Kwa mjadala!
Ndio maana watu weusi tunakufa mapema. Wewe una kitu unacho lakini umejaa kiburi kusema. Kwanini usifunguke yakaisha?
 
Anunnaki walijuaje kuwa kuna dhahabu inapatikana duniani na ingeweza kurecover atmosphere ya anga lao?
Nalog off Z
mkuu kwema ukisoma SUMERIAN tablets zinasema Annunaki waliwatuma watangulizi wa kufanya research.

ANUNNAK anayeitwa ALALU Ndie alikua wa kwanza kushuka duniani Miaka mingi sana akaichunguza Dunia na kugundua Uwepo wa dhahabu na Ndie aliyewatumia ujumbe Juu ya ugunduzi wa Dunia baadae wakaja ENKI na ENLIL Wana wa ANU kutoka Nibiru wakiwa na spaceship kubwa sana pamoja na Viumbe wanaoitwa Igigi kama workers kwenye machimbo ya mwanzo kabisa kabla hawajaweka Makazi rasmi.

SUMERIAN tables zinataja sehemu kama Nippur kama sehemu ya kwanza spaceship ya Annunak kutua baadae wakajenga ground kubwa huko Baarbek Lebanon ambao watafiti wa mambo kale wamesema ndio ulikua wanja mkubwa wa Meli za angani wa Annunak mpaka Leo ukienda Baarbek Lebanon utaona mabaki yake!
 
mkuu kwema ukisoma SUMERIAN tablets zinasema Annunaki waliwatuma watangulizi wa kufanya research
ANUNNAK anayeitwa ALALU Ndie alikua wa kwanza kushuka duniani Miaka mingi sana akaichunguza Dunia na kugundua Uwepo wa dhahabu na Ndie aliyewatumia ujumbe Juu ya ugunduzi wa Dunia baadae wakaja ENKI na ENLIL Wana wa ANU kutoka Nibiru wakiwa na spaceship kubwa sana pamoja na Viumbe wanaoitwa Igigi kama workers kwenye machimbo ya mwanzo kabisa kabla hawajaweka Makazi rasmi,
SUMERIAN tables zinataja sehemu kama Nippur kama sehemu ya kwanza spaceship ya Annunak kutua baadae wakajenga ground kubwa huko Baarbek Lebanon ambao watafiti wa mambo kale wamesema ndio ulikua wanja mkubwa wa Meli za angani wa Annunak mpaka Leo ukienda Baarbek Lebanon utaona mabaki yake!
Ahsante sana
Z
 
Enhe, hao anunaki watakuja lini tena?
hakuna hakika Juu ya Hilo mkuu maana mara ya mwisho habari zao kurekodiwa ni kule Mesoamerica hasa kwenye Maandiko ya wamaya na Aztec nk

Ukisoma baadhi ya vyanzo inadai Annunaki waliokua duniani walitofautiana wao Kwa wao sababu kubwa Ilikua ni jinsi ya kuwahandle binadamu Kuna baadhi Yao walitaka binadamu aendelee kua mtumwa wao Kuna wengine walidai binadamu anastahili kupewa ujuzi na maarifa makubwa afanane na wao,tofauti Ile ilikuja kuzaa vita kubwa kati ya pande mbili maana Enki aliyewafanya binadamu alitaka wakubalike na watambuliwe Katika jamii ya wanibiru ila ENLIL alikataa akidai lengo la binadamu ilikua ni kuwa vijakazi Katika Migodi Yao na baada ya mission kukamilika wanastahili kuondoshwa na kutoweshwa Katika tofauti zao wakakubaliana kuwaacha huru ila Kwa sharti wasipewe access ya advanced technology Bali wapate elimu ya ujuzi wa kawaida kama
Engineering, Music, uchimbaji madini mbali mbali, kufua vyuma nk yaani Ile nyepesi tu na baada ya hapo waliondoka kurudi Kwao Nibiru planet na hawajawahi rejea Tena baada ya kukaa duniani Kwa Miaka maelfu nyingi sana,huo ndio ukawa mwisho wa accient civilization za kale kama Sumerians, Assyrian, Babylon, Egyptian, Kush, Aztec, Maya, Peru, Indus valley kuanguka na binadamu Kuanza survive Katika Hali ya kawaida huku akibakia na dhana ya Mungu, Miungu kutoka juu akitumainia ipo siku watarudi kuwakomboa kwa shida zao,

Mfano kule mexico kwenye jamii ya Aztec na Maya walitoa kafara za binadamu Ili kutuma maombi Kwa Miungu hiyo irudi itatue shida zao mbali mbali

Angalia movie ya Apocalypto ya Mel Gibson utapata idea kidogo kwanini wale watu wanatoa kafara kwa Miungu jua au star gods ambao ndio hao ANNUNAKI!
 
Napata tabu kuamini hivyo vitu maana wanaotuletea wenyewe wanadai ni tafsiri ya kutokana na michoro ya kale! Sasa unajuaje labda ni watoto wa zamani walukuwa wanachezea udongo na kupigiana hadithi?

Lakini pia kingine ni watu kutokuelewa baadhi ya vitu tu. Labda walitembelewa na watu wa kabila/race nyingine ya hapahapa duniani yenye ujuzi ndo wakawaona ni miungu. Na hata kama wakitoka nje ya dunia bado wanakuwa sio mungu ni viumbe tu. Mfano aje mzungu na jet za kupaa za kuvaa halafu mimi nimuite mungu kwa sababu anapaa hewani na kutengeneza mawingu. Atakuwa mungu

Mungu yeye yupo sema haonekani, sasa wanadamu kwa kutamani kujaza hilo gepu ndio wamekuwa wakijitungia miungu na kubambika uungu vitu vingine kwa sababu tu ya kutomjua Mungu wa kweli
 
mkuu wangu ukitumia akili za kawaida huwezi sema michoro ya kale ya watu wenye mbawa ilichorwa na watoto wakati katika nadharia za Dini za kale hao waliitwa miungu ukienda kule Peru kwenye temple of condor pamoja na pyramids za Cholula,great stone of Costa Rica, Stonehenge, pyramids za Giza,Angkor wat kule Cambodia,Rama setu bridge huko kote utakuta picha za hao wings being waliopewa majina mbali mbali ,
Mesopotamia waliwaita ANUNNAKI,huko Mesoamerica waliwaita Kwa majina mbali mbali
Ukienda Kwa Israelites waliwaita Nephilims/Watchers/Angeles

Hayo yote yanakubalika katika Dini kongwe na za kale hasa huko India wakimtaja Mungu Brahma kama ndie deit mkongwe kuliko wote.

Nadharia za miungu Katika SUMERIAN na Akkadians imewataja hao viumbe kama 'gods' ikiwa na maana ya walioshuka kutoka juu mbinguni na kuja Duniani huko.

'GOD' kama mtawala wa mbinguni
Na watu wa kale waliwaabudu sababu ya ukuu wao hasa kutokana kuwa high advanced science and technology,
Pia.

Unapodai Kuna Mungu jua upo kwenye chain Ile Ile maana hiyo maana ya Mungu na dhana nzima kumhusu walianzisha wao wakimtaja mkuu wa Sayari Yao Nibiru!
 
Unajua maana ya neno Mungu kwanza?
Unapodai Kuna Mungu ila haonekani unaleta utata sababu huwezi Thibitisha uwepo wake,

Nikupe SoMo Leo kijana
Maana ya
'GOD' ni master of high chamber katika accient civilization ya Mesopotamia walitumia
'ANU' wakimuwakilisha mtawala wa Sayari ya Nibiru kwasababu ya watoto zake kuja Duniani kutafuta gold watoto zake wakaitwa wa Annak au
'gods' ikiwa na maana walioshuka kutoka juu mbinguni au mawinguni na kuja Duniani kutafuta dhahabu

'Miungu' ni watoto wa Mungu mkuu wa Mbingu sababu wanae walikuja duniani hivyo ni mkuu wa mbinguni na Duniani hapa ndipo Siri na nadharia ya Uungu ilipoanzia na Mungu Sio jina ni cheo Cha mtawala wa Dunia na mbingu
ANU alikua Mtangulizi wa kale wa miungu aliyekua na mamlaka kuu baadae walifuatia miungu Wengine mfano

Kuna Mungu Elohim/YHW huyu watu wengi humwabudu katika Dini za kisasa huko waabuduo hawajui ni Moja ya Miungu wa kale wa ANNUNAKI na Aliabudiwa na Abraham aliyetokea Uru ya Ukaldayo Mesopotamia ambako Ndio nadharia za Mungu na miungu zilianzia sababu ya uwepo wa ANUNNAKI

Soma historia utajua ujinga wa kuwaita viumbe Mungu ndio utajua utapeli wa Dini mlizoletewa waafrika na mkazimeza nzima nzima!
 
Soma historia utajua ujinga wa kuwaita viumbe Mungu ndio utajua utapeli wa Dini mlizoletewa waafrika na mkazimeza nzima nzima!

Hatuko tofauti sana ukichunguza wala huhitaji kuniweka sawa saana kwenye historia labda tu niziweke uchi facts zilizopo;

Ni kwamba watu/viumbe kuamua kwamba mfalme wao ndio mungu wao sio jambo geni. Wachina/japan walifanya hivyo wa Egypt walifanyaga sana na propaganda zinadai wakorea sijui hadi leo ila nahisi ni propaganda tu. Hata hao anunaki watakuwa walifanya hivyo. Hilo linaonesha tu ule uhitaji wa kumuona mungu[na kumthibitisha kimaterial].

Lakini moja kwa moja huyo ANU hawezi kuwa mungu kwa sababu anahitaji dhahabu - kitu material. Kwa hiyo kama kuna dini mtu anaitangaza ikiwa na mungu mwenye kuhitaji material basi anakuwa bado hajamjua Mungu wa kweli.

Sasa kuthibitika kwa hiyo historia hakuwezi kutufanya sisi kuacha kumuabudu Mungu ila tutaacha kumuabudu huyo wa uongo na kuendelea kumtafuta wa Kweli. Kwa kifupi tu historia yako ikithibitika kuwa ni kweli basi tutajua tu kuwa tulipigwa na tutaendelea kumtafuta Mungu wa Kweli katika namna yoyote haibadilishi kuwa Mungu yeye yupo.

Tangu zamani tangu kuumbwa tumekuwa tukimtafuta Mungu kwa namna mbalimbali ndo zinazoitwa Dini
 
Hatuko tofauti sana ukichunguza wala huhitaji kuniweka sawa saana kwenye historia labda tu niziweke uchi facts zilizopo;
Ni kwamba watu/viumbe kuamua kwamba mfalme wao ndio mungu wao sio jambo geni. Wachina/japan walifanya hivyo wa Egypt walifanyaga sana na propaganda zinadai wakorea sijui hadi leo ila nahisi ni propaganda tu. Hata hao anunaki watakuwa walifanya hivyo. Hilo linaonesha tu ule uhitaji wa kumuona mungu[na kumthibitisha kimaterial].

Lakini moja kwa moja huyo ANU hawezi kuwa mungu kwa sababu anahitaji dhahabu - kitu material. Kwa hiyo kama kuna dini mtu anaitangaza ikiwa na mungu mwenye kuhitaji material basi anakuwa bado hajamjua Mungu wa kweli. Sasa kuthibitika kwa hiyo historia hakuwezi kutufanya sisi kuacha kumuabudu Mungu ila tutaacha kumuabudu huyo wa uongo na kuendelea kumtafuta wa Kweli. Kwa kifupi tu historia yako ikithibitika kuwa ni kweli basi tutajua tu kuwa tulipigwa na tutaendelea kumtafuta Mungu wa Kweli katika namna yoyote haibadilishi kuwa Mungu yeye yupo. Tangu zamani tangu kuumbwa tumekuwa tukimtafuta Mungu kwa namna mbalimbali ndo zinazoitwa Dini
Mungu wa kweli ni nani?

Kumbuka Mungu Sio jina ni cheo haya nambie Mungu unaemdai ni WA ukweli ni Mungu Gani?
 
Mungu wa kweli ni nani?

Kumbuka Mungu Sio jina ni cheo haya nambie Mungu unaemdai ni WA ukweli ni Mungu Gani?
Angalizo: kutaka kumuweka Mungu katika tafsiri fulani ni jambo lisilowezekana. Yaani ni kama unataka tumucondense awe kakidonge tumuweke kwenye kikombe juu ya meza tuseme ndio huyu. Haiwezekani. Kwa akili zetu zenye mwisho wa kuelewa[finite] hatuwezi kumutafsiri yule ambaye hana mwisho [infinity].

Ndio, mungu sio jina ni cheo. Na huyu mungu kwa sisi viumbe kila mmoja huwa anamuelewa relatively na kile anachokijua hadi wakati huo. Yeye anabaki kuwa vyote katika yote. Top.
Mfano sisimizi anaweza kuwa anajua mwisho mtaa anaozuriria - Kwa hiyo atajua mungu kwake ni aliyeumba huo mtaa na vyote vilivyomo na yupo juu ya mtaa na pote katika mtaa

Binadamu wa kale akawa anaijua dunia tu so mungu akawa ni yule aliyeumba dunia yote, yeye yupo juu ya dunia yote na anadhihirika pote katika dunia yote. Ndio maana walipokuja viumbe kutoka nje ya dunia hao watu wakajua anhaa mungu ndo huyu hapa sasaa! kumbe bado inaendelea bhana. Tena inawezekana labda hao viumbe walitoka tu kisiwa fulani labda who knows

Binadamu wa sasa akaangalia na darubini akashangaa akasema Mungu ni aliyeumba ulimwengu wote so viumbe wote wapo chini yake yeye yupo juu ya vyote na anamanifest pote.

Binadamu tena huyohuyo wa sasa akanza kutengeneza mahesabu, manadharia, na mengineyo ya maulimwengu ameanza kusema oooh! kuna ulimwengu nyingi, sayari nyingine kuna viumbe wengine wana akili sana. Mungu atabaki kuwa yule aliye juu ya hayo maulimwengu yote na anamanifest pote ameyaumba au yapo chini yake. SIKU ZOTE BINADAMU ATAENDELEA KUMJUA MUNGU KADRI AKILI YAKE INAVYOPANUKA. Na huku kupanuka namaanisha vyote kwa ukuuuubwa na udoooogo. Kama juu ya vyote mbali, na ndani ya vyote karibu.
 
Unakwepa swali eee nakuuliza huyo Mungu wa kweli anaitwa nani na unamtambuaje?
 
Back
Top Bottom